Dreamliner yaanza safari kwa kishindo: Tiketi za Mwanza na KLM tayari zimeisha mpaka tarehe 18 Agosti 2018

Dreamliner yaanza safari kwa kishindo: Tiketi za Mwanza na KLM tayari zimeisha mpaka tarehe 18 Agosti 2018

Mkuu ni kwasbb ya ugeni wa hiyo ndege bombardiers ni watu 76 lkn hakuna wateja mpk flight inaahirishwa itakuwa hiyo wa 200+
mhn ni kweli pia inawezekana lakini ifike wakati hebu turudi ile miaka ya 80s ndege kupanda kwa watu wakati halikuwa jambo la ajabu tuanze kusave japo kwa miaka miwili tupande ndege mara moja.
ifike wakati tuviangalie vipato vyetu tulazimishe kusafiri vizuri japo kwa mwaka mara moja.
nilikuwa napiga hesabu kwa mtu ambaye anategemea kwenda kilimanjaro mwezi wa disemba akiamua kupunguza mafuta kwa shiling elfu tatu kila siku kutoka shillingi 20,000 ambazo watu wengi wa dar wanaweka kwa mwezi anaweza kuwa amesave shilingi 90,000 na kwa miezi kumi 900,000/- sasa akichanganya na nauli ya likizo anaweza kumudu kupande ndege yeye, mkewe na watoto wawili.
uwezo tunao fikiria tu gharam za kusafiri na gari binafsi moshi natugharimu kiaisi gani toka dar halafu utatjua kuwa sehemu kubwa ni mind set tukifanyiwa marketing vizuri tutapanda tu.
 
Siku zote uzinduzi hujaza watu hasa wenye shauku ya kujionea tukio lakini safari inapopamba moto mnaanza kupungua mwisho mtafika wachache.
itakapofika hapo bei lazima ishuke ili kupunguza gharama za uendeshaji na sisi wengine tutaiona fursa ya kuzipanda.
 
Biashara ya ndege ni hasara90% kwa Tanzania ni hasara zaidi mana atcl haina hata business plan so far poor you
hili la business plan mpaka sasa sikubaliani nalo hiyo bodi iliyowekwa mpaka sasa inafanya nini haijatengeneza business plan? hakuna ubishi kuwa hii biashara haiweze kutengeneza faida ila tunachokitegemea ni faida zisizo za moja kwa moja kwa uchumi kwa impact itakayoletwa kwa kuwa na ndege.
shirika la reli halipati faida kwa kusafirisha abiria ila linatoa tu huduma kwa hasara. inategemea mizigo zaidi kwa kutengeneza faida. hivyo tunapoongelea swala la ndege inabidi ufikirie mbali zaidi sio hapa karibu vinginevyo huwezi kuona moja kwa moja la sivyo umeamua kubisha na kwamba lazima ushinde kama ikiwa hivyo nimekuelewa na ifike wakati nikubaliane na wewe sawa.
 
mhn ni kweli pia inawezekana lakini ifike wakati hebu turudi ile miaka ya 80s ndege kupanda kwa watu wakati halikuwa jambo la ajabu tuanze kusave japo kwa miaka miwili tupande ndege mara moja.
ifike wakati tuviangalie vipato vyetu tulazimishe kusafiri vizuri japo kwa mwaka mara moja.
nilikuwa napiga hesabu kwa mtu ambaye anategemea kwenda kilimanjaro mwezi wa disemba akiamua kupunguza mafuta kwa shiling elfu tatu kila siku kutoka shillingi 20,000 ambazo watu wengi wa dar wanaweka kwa mwezi anaweza kuwa amesave shilingi 90,000 na kwa miezi kumi 900,000/- sasa akichanganya na nauli ya likizo anaweza kumudu kupande ndege yeye, mkewe na watoto wawili.
uwezo tunao fikiria tu gharam za kusafiri na gari binafsi moshi natugharimu kiaisi gani toka dar halafu utatjua kuwa sehemu kubwa ni mind set tukifanyiwa marketing vizuri tutapanda tu.

Hujaweka gharama baada ya kushuka KIA hadi kijijini, vipi kuhusu convenience???
Hesabu za kwenye makaratasi huwa tamu kuliko uhalisia..

Twende kwenye uhalisia:
Bei zinazotozwa na ATC kwa sasa ni promotional for August only...bei zao baada ya hapo zitapanda kama kawaida...
Nimeangalia endapo nikikata/book ticket leo DAR kwenda KIA Dec 20 na kurudi Jan 05 2019, bei itakuwa Tsh 381,980 kwa abiria mmoja. Hiyo 900k bado inatosha mke na watoto wawili???

Harrier 2.4 ukiweka full tank 60L kwa Tsh150,000 unafika hadi kijijini kwenu!!

Usafiri wa ndege Tanzania bado uko gharama ya juu sana hata baada ya ujio wa Bombardier.....Dreamliner yetu hizi domestic route ni za muda tu, huwezi ukatumia mabus kama ya Shabiby kwa towntrip and so is our Dreamliner.
 
TRA watakapokuwa wabakufata ofisini kwako pia usiwakimbie mpe Hongera Rais Magufuli, maana hilo dude linaingiza hasara, na ili kufidia itabid mwananch wa chini Aumie,

Kwahiyo sitarajii kuona Ukileta uzi humu kuwa TRA inakubana na kodi zimeongezeka
Mimi naona ni KICHAA kabisa maana biashara IPO demand kubwa faida IPO tu were unachuki binafsi na serikali na wivu was kihasara hasara tu ujinyonge tu hakuna jinsi !
 
Imeshasemwa wazi kuwa, mipango ni kuifanya Dreamliner iende Guangzhou (China), Bangkok (Thailand) na Mumbai (India). Kuna mambo ya vibali, kujitangaza na logistics kwa ujumla. Ndiyo maana inaanza hapa Bongo Viwanja vya KIA na Mwanza.
Sawa Mkuu lakini ATCL walijua kuwa Dreamliner unakuja kwa nini hawakufanya "preliminary arrangements" kama vile kupata vibali cha IATA, Kutafuta "landing slots" nk. Kuliko kusubiri mpaka ndege imefika ndiyo waanze michakato! Haya mambo ya "baadaye itaenda Guanzhou" ni ubabaishaji. Ilitakiwa ikitua tu inaanza route ya Dar-Guanzhou. Ukiangalia pale Emirates Engineering Centre hata ndege zilizopo matengenezo huwa already zimepangiwa routes, sembuse na hii ambayo ilijulikana mwaka mmoja kabla? Ndiyo efficiency inayotakiwa.
 
Bei zinazotozwa na ATC kwa sasa ni promotional for August only...bei zao baada ya hapo zitapanda kama kawaida...
Nimeangalia endapo nikikata/book ticket leo DAR kwenda KIA Dec 20 na kurudi Jan 05 2019, bei itakuwa Tsh 381,980 kwa abiria mmoja. Hiyo 900k bado inatosha mke na watoto wawili???
teh..teh...teh.. inatosha sana ukichanganya na anuli uliyolipwa ya watoto wanne ambao wawili watatangulia na dereva wa kukodi au mdogo wako utakaye mtoa 100,000/- kwa safari ili uweze kutumia hiyo gari ukiwa huko!
ni kweli ni gharama lakini kiukweli natamani (binafsi ) tuweze kuanza kukabiliana na hizi changamoto za kuogopa ndege binafsi sijapanda siku nyingi sana na kiukweli sioni kama nastahili kuwa hivyo mwishoe utapanda ndege yule muhudumu wa ndege akikuchekea utauona kama anakutaka kumbe ndo kawaida yao.
ngoja tuone siku zinavyokwenda itakuwaje zinaweza kushuka siku zijazo.
 
hili la business plan mpaka sasa sikubaliani nalo hiyo bodi iliyowekwa mpaka sasa inafanya nini haijatengeneza business plan? hakuna ubishi kuwa hii biashara haiweze kutengeneza faida ila tunachokitegemea ni faida zisizo za moja kwa moja kwa uchumi kwa impact itakayoletwa kwa kuwa na ndege.
shirika la reli halipati faida kwa kusafirisha abiria ila linatoa tu huduma kwa hasara. inategemea mizigo zaidi kwa kutengeneza faida. hivyo tunapoongelea swala la ndege inabidi ufikirie mbali zaidi sio hapa karibu vinginevyo huwezi kuona moja kwa moja la sivyo umeamua kubisha na kwamba lazima ushinde kama ikiwa hivyo nimekuelewa na ifike wakati nikubaliane na wewe sawa.

Business plan hawana. Ndio mana wana tafuta consultant mkuu awatengenezee
Ukweli mchungu hii biashara ngumu zana

Lengo liwe kuifanya dar kia iwe hub and transit route lakin sio kutegemea faida kwa ndege haipo hiyo cha msingi faida yetu itokee kwenye utalii na biashara inayotegemea air transport sio kutegemea nauli ilete faida
 
Kunyanyua hilo dege from Dar na kutua KIA au MWZ ni matumizi mabaya ya resources; inabidi likageuzie South Sudan kuitafuta runway. Dude ambalo uwezo wake wa "wese" ni lita 126,210 yaani zile semi-trailer tanker za mafuta zinamimina mle 3 na bado halijai. Sio mchezo.

Malizia uchanganuzi mkuu. Hizo lita 126,210 ni shilingi ngapi, mbali na mafuta gharama zingine ni shilingi ngapi, itabeba jumla ya abiria wangapi, watakaolipa shilingi ngapi kisha utoe gharama za uendeshaji utuambie tunapata hasara ya shilingi ngapi.

Pia naomba kufahamishwa maana ya runway ili nielewe unaposema ndege inaenda kugeuzia South Sudan kutafuta runway. Ina maana ikishatua Mwanza itanyanyuka kwa muujiza ili iende Sudan kutafuta runway ili iruke kurudi Dar ama? Runway ni nini?
 
Hamuwezi kuendesha hili shirika kwa faida kwa kutegemea mauzo ya ticket tu hasa tukianza route za kimataifa.

Gharama za kuhudumia ndege,mafuta, mishahara ya wafanyakazi, chakula kwa abiria, hoteli kwa abiria panapotokea matatizo, charge za kupaki/kutua katika viwanja vya ndege,kulipa mainjinia wa kuihudumia, n.k kamwe haviwezi kubebwa na mauzo ya ticket tu.

Wanaofanikiwa katika hii biashara hawategemei mauzo ya ticket tu vinginevyo mashirika mengi yasingekuwa yanatangaza hasara.

Pia, eleweni tu Bombardier zilizokuwa zinatumia hiyo route sasa zinakosa abiria na ni hasara kuzipaki kwa huo mwezi mzima.
Vitu kama hivi hakuna mtu anafikiria, na kimsingi hiyo machine sio ya route fupi kiasi hicho, wacha tusubire
 
Jamaa yangu kakata leo tiketi Mza- Dar Dreamliner na kapata tiketi bila shida!!!! Hili la "Nafasi zimekwisha" ni uongo mtupu!!!!!
Hivi amesema zimekwisha au amesema tarehe aliyotaka ndo zimekwisha??? Muongo wewe!!!!
 
Kijana ulishaona ndege kama fastjet imejaa inaelekea Mwanza au basi ngapi zinatoka dar kenda mwanza na abiria jumla ya basi zote wanafikia idadi gani ndio uje ujaze hilo dude watu 200 kwa siku moja
Kumbe hili dude litakuwa linaenda Mwanza kila siku na kukatisha tiketi kwa siku moja kama Kigumo Express? Nilifikiri hii safari ya Mwanza inakwenda kwa ajili ya matangazo tu kisha itaendelea na mpango wa kununuliwa kwake ambao ni kwenda nje na kwa kuanzia ni India. Naona niko nyuma sana.
 
Kunyanyua hilo dege from Dar na kutua KIA au MWZ ni matumizi mabaya ya resources; inabidi likageuzie South Sudan kuitafuta runway. Dude ambalo uwezo wake wa "wese" ni lita 126,210 yaani zile semi-trailer tanker za mafuta zinamimina mle 3 na bado halijai. Sio mchezo.
Katibu wa uenezi na propaganda. Ndege hujazwa mafuta kulingana na safari yake; iwapo inakwenda mwanza itawekwa mafuta chini robo tanki mradi yaifikiseha Mwanza; siyo kuwa kila mara lazima ndege ijazwe mafuta full tank. Nadhani hata gari lako huwa hujazi mafuta full tank kila siku. Angalia hata Uganda nayo sasa inachangamkia kijimilikisha ndege zake halafu eti watanzaia sisi tunapinga. Angalia hii
Uganda Airlines signs deal to buy 4 Bombardier jets, two
 
Safi sana,nakumbuka Mwz-Dar kwa Bombadier ni kama saa 1.45 hivi,kwa hilo mashine itachukua muda gani..?
Itakuwa ni kama dakika 40 hivi; hata enzi zile za Boeing 737 tulikuwa tunatumia dakika 45 tu
 
watu ukiwaambia kuwa hizi ndege zinajaa hawakubali sijui wanatakaje?

hivi katika tanzania yenye watu zaidi ya millioni 50 hakuna watu wenye uhitaji wa kupanda ndege 3000 kwa siku? hii ni hesabu rahisi tu wakati ndege zote zikijaza za shirika hilo hawafiki watu 1000?

tumekazana kuwa watapata wapi wateja kweli? yaani unazaa mtoto lakini sala zako unaomba mtoto afe haraka do! sijatembea na kuvuka mpaka lakini tujifikirie upya kwa maslahi ya taifa vinginevyo tusema kuwa tunayopinga tuna furahisha ubongo kupunza stress zetu.
Mkuu wangu umeongea wazi kabisa
 
Back
Top Bottom