DSM kwa sasa inahitaji treni na sio mwendokasi

DSM kwa sasa inahitaji treni na sio mwendokasi

Kinachonishangaza,hawa planner wetu wanaona kabisa bado adha ya usafiri iko vile vile au imeongezeka zaidi.

Baada ya kuja na solution ndo kwanza wanazidi kuzijenga hizi barabara za mwendo kasi,
Yani kweli kwa dar kwa sasa tunahitaji sana tram.
Ndo ushangae ss
Ila jmn Africa 🙌
Acha watu wakimbie tu
 
Nakazia 📌
Mji kama Düsseldorf, Germany una watu 650k tu ila kuna trams,
Dar yenye watu zaidi ya 7m bado raia wanategemea mabasi yasiyo na ufanisi ya daladala na mwendokasi, huo ni utani na kukosa maarifa
Maendeleo ya Dsm yanakimbia kwa kasi sana
 
Fungua nchi watu watawanyike. TZ sio DSM tu. Hata treni ziende kila kona kama influx ya watu itaendelea miundombinu itazidiwa tu.
Nchi imefunguliwa serikali kuhamia Dodoma lakini bado tu watu wanazidi kumiminika DSM
 
Kwenye njia hizo za mwendokasi wanaweza wakaongeza njia za trams kuelekea hayo maeneo uliyoyataja. Mixing ya bus na trams ndiyo itakuwa mwarobaini wa public transport hapo mkoani kwenu.
Njia za mwendokasi wamezibana sana kama nyoka. Huwezi kuongeza chochote
 
Dar bado ina watu wengi sana yaani hata yote yawe active barabarani bado , tena yanaleta uchafu zaidi na foleni .....Dar kuna watu wengi sana tena wanaoenda sehemu moja kwa wakati mmoja kama soko kubwa ni kariakoo na ofisi nyingi zipo posta , hilo ndio tatizo .

Ukiona pale Mbezi mwisho abiria kama wapiga kura walivyojipanga kitu ambacho ni hatari sana maana mpaka wanasukumana kweny barabara ni huruma kwa kweli .
Hapo Mbezi nilikuta foleni ya watu zaidi ya 200 wamesimama wanasubiri basi lifike kutoka mjini. Nikasema huu ni utumwa kwa namna nyingine
 
Mkuu Nafikiri Hilo ni Wazo Zuri.Tunaweza Tengeneza Tram Trains ambzo ni tofauti n Train za kawaida na zinweza kufuata Network ya Barabara iliyopo
Tena hizo train zipige kazi asubuhi kumi na moja hadi saa nne zipumzike. Zianze tena jioni saa tisa hadi tano usiku. Hapo itaondoa au kupunguza tatizo la usafiri
 
Nchi imefunguliwa serikali kuhamia Dodoma lakini bado tu watu wanazidi kumiminika DSM

Mpiga mwingi mwenyewe anaishi DSM nani atahamia Dom? Hakuna mtu yupo serious na kuhamia Dom.

Kupunguza watu Dar sio serikali inabidi bandari za Tanga na Lindi ziwezeshwe kupunguza msongamano DSM.

Soko lingine liwezeshwe kucompete na kkoo.

Hospitals na huduma zingine as well. Cha msingi ziganywe ziguse kila pembe ya nchi. Vinginevyo watu watazidi kumimimika Dar.
 
Hapo kwenye soko uko sahihi kabisa. Mtu aweze kununua bidhaa za jumla Mwanza kama bei ya Kariakoo. Ili wafanyabiashara kanda ya ziwa wasilazimike kufata mzigo kariakoo
 
Njia za mwendokasi wamezibana sana kama nyoka. Huwezi kuongeza chochote
Hizo hizo zinatosha maana watatumia ratiba hivyo hakutakuwa na mgongano. Modern infrastructure kwa ajili ya public transport hazihitaji kutenga njia bali unaweka infrastructure ambazo mabasi na trams zinapita bila shida.
 
Back
Top Bottom