DStv badilisheni mtangazaji na utangazaji wa Kiswahili kwenye mechi za Kombe la Dunia

Huyu mtangazaji wenu anapayukapayuka na hata haieleweki anaongea nini. Kila wakati anapaza sauti na kuongea vitu visivyoeleweka wala kuhusiana na mechi iliyopo mubashara.
Yaani nilivosikia wachambuzi wa bongo tu nkapata kichefu chefu.,uswahili mwingi....ndio maana siku zote naangalia tv yenye wazungumzaji wa kiingereza...jamaa wako vizuri...wanatema reality na facts...ukija wa bongo Sasa no fact ,utumbo mtupu...siasa za Simba na Yanga zimeharibu Sana akili za wachambuzi .

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Watangazaji walikuwa Radio Tanzania,na External ,idhaa ya nje,
Jocob Tesha,Jurious Nyaisanga,Maria chipungahelo,Aboubakar liongo,nk,
Siku hizi ni kupayuka tu,
Wasafi walikuwa na mpayukaji mmoja,Zembwela,wakaona hatoshi,wakamuajiri Ktenge Ili apayuke zaidi,baade akakimbilia Efm,kwenda kupayuka zaidi!!
Efm pale,Kitenge,Gerald hando,Musa Kipanya,na Mdada mmoja,ukisikiliza Cha maana wanachoongea hakuna,ni utumbo mtupu!!
 
Huyu mtangazaji wenu anapayukapayuka na hata haieleweki anaongea nini. Kila wakati anapaza sauti na kuongea vitu visivyoeleweka wala kuhusiana na mechi iliyopo mubashara.
🀣🀣🀣🀣🀣🀣

Tumepigwa
 
Hawapo live uwanjani kivipi,si nimeskia wapo qatar jamn kila mechi watakua live au[emoji848][emoji848][emoji848]
 
Kwa Sasa Kuna Gharib Mzinga wa azam, yule jamaa anajitahidi
Akiwa anatangaza mechi anakua na taarifa za wechezaji wote, sio kama wale WA TBC hawajui hata mchezaji anaeingia sub, shwaini zao
Huyo gharib Yuko well informed yani,dogo anajianda Sana na mechi anayoenda kuitangaza...
 
Kama unatazama DSTV, pale ni VISUAL sasa sauti hata sio lazima.

Hata kwa anayetangaza kupitia TV halazimiki kuelezea kila kitu maana Watu wanaona, hiyo sio Redio.

Kazi ya Mtangazaji sanasana ni kwa ajili ya kufafanua mambo madogomadogo kama sheria za soka ili Mtazamaji asiyejua aelewe baadhi ya maamuzi ya Refa, au mara moja moja kutoa wasifu wa Mchezaji n.k.

Otherwise sio lazima kumsikiliza Mtangazaji.
 
Hawapo live uwanjani kivipi,si nimeskia wapo qatar jamn kila mechi watakua live au[emoji848][emoji848][emoji848]

Quatar ya wapi? Wamejifungia kwenye kachumba hapa hapa na wao wanaangalia kwenye Tv kama sisi.
 
Yule mwamba wa TBC anaitwa Nazareth nadhani anajua sana
 
Huyu mtangazaji wenu anapayukapayuka na hata haieleweki anaongea nini. Kila wakati anapaza sauti na kuongea vitu visivyoeleweka wala kuhusiana na mechi iliyopo mubashara.
Atakuwa Juma Nkamia huyo kama siyo Denis Mpagaze
 
Wapo watangazaji wa kiswahili wanaotangaza kwa data na ufundi mkubwa mfano mzuri ni Gharib Mzinga wa Azam tv
 
Kuna wa TBC yeye hutaja tu nchi yoyote

Utamsikia "ni free kick kuelekea Portugal.....anapiga kule unababatiza mabeki wa Brazil unakuwa ni kona...anaenda kupiga kona nambari kumi wa Croatia...anapiga kona go go gooo...la la inatoka juu ya lango...ni goal kick kuelekea Poland...wakati huo huo Wachezaji wa Ecuador wanamlalamikia Refa kwamba Kipa aliugusa mpira ule".
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Huyo jamaa kaua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…