DSTV yalamba hasara ya bilioni 122, gharama za vifurushi zawakimbizia wateja 486,000

DSTV yalamba hasara ya bilioni 122, gharama za vifurushi zawakimbizia wateja 486,000

Kampuni ya Multichoice inayomiliki visimbuzi maarufu vya DSTV imelamba hasara ya Tshs bilioni 122 kwa miezi sita iliyoishia Septemba mwaka jana sababu kuu ikiwa kupungua kwa wateja wake huku Afrika kusini pekee ikipoteza wateja zaidi ya laki nne.

Multichoice imedai kutekeleza malengo yake yote iliyoyapanga lakini mazingira inayofanyia kazi yametawaliwa na kukatika katika kwa umeme, presha kwenye gharama za kuishi na kushuka kwa thamani ya pesa katika nchi walizopo dhidi ya dola.

Mwaka huu channel maarufu ya michezo ya supersport itashindwa kuonesha michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza January 13 nchini Ivory Coast. Mwezi uliopita shirikisho la mpira wa miguu Afrika liliingia mkataba wa haki za matangazo kwa miaka miwili na kampuni kutoka nchini Togo ya New World TV iliyoanzishwa mwaka 2015.

Ni mwanzo wa mwisho wa utawala wa DSTV kusini mwa Afrika? Bado DSTV ni moja ya nguli wa kurusha matangazo barani Afrika huku kampuni zake mbili za DSTV na GoTV zikiwa na visimbusi milioni 23 vilivyo hai kwenye nchi 50 barani Afrika.
Du! ujinga huu waliofanya DSTV ni zaidi ya ule ujinga wa Magufuli kuwakamia wafanyabiashara hadi wakafunga biashara na kupelekea uchumi kudorora. Na baada ya uchumi kudorora akaamua kukimbilia kukopa matrioni ya pesa hivyo kuiingiza nchi kwenye mzigo mkubwa wa madeni unaotuumiza vichwa hadi sasa. Mungu anamuona.
 
Wafanye Compact 40,000/- waone wateja watavyoongezeka.
Mimi nilikuwa nalipia Shangwe 34000/- walivyopandisha 37000/- huku hawaonyeshi CAF SUPER LEAGUE WALA CAF CHAMPIONS LEAGUE, nikawana matapeli tu. Sasa nalipa 24000/- ili wife aangalie HUBA nami LA LIGA tu.
Kwanza Arsenal inavyofungwa hata hamu ya EPL sina
 
Na bado, cha maana hakuna wamebaki na EPL tu.
Nilikuwa siikubali Azam ila nitahamia, kama ni EPL nitastream live basi.
Azam quality ya picha itatuhamisha DStv naona kuna low quality picture,DStv Wana HD,pia azamu Wana mavipindi ya hovyo nje ya mpira,DStv Wana documentary za utafiti baharini,upishi 175 na 174 hii na zile animal channels na TNT movie na multchoice movie zote na African magic zote,Azam wakaze boot,quality is a number one factor.
 
Ukiwa na Dstv ni ngumu Sana kuhamia Azam, DStv Wana option ya kulipia kidogokidogo Hadi siku ya mwisho wa kifurushi chako kuisha ndani ya mwezi.
Kwangu Mimi nitaendelea kutumia Tu DStv mwanzo mwisho
Mzee acha uongo hiyo option unaipata wap maana wote tuna DStv au Yako ni special kuhusu Azam tunaopenda mpira wa bongo tunalipia na kufaid burudan
 
Azam quality ya picha itatuhamisha DStv naona kuna low quality picture,DStv Wana HD,pia azamu Wana mavipindi ya hovyo nje ya mpira,DStv Wana documentary za utafiti baharini,upishi 175 na 174 hii na zile animal channels na TNT movie na multchoice movie zote na African magic zote,Azam wakaze boot,quality is a number one factor.
Azam Wana vipind vizuri na documentary zipo Mzee lipia Cha 35000 unapata kuhusu Quality ya picha labda tv Yako tu mbona tunapata kitu Bora
 
Azam quality ya picha itatuhamisha DStv naona kuna low quality picture,DStv Wana HD,pia azamu Wana mavipindi ya hovyo nje ya mpira,DStv Wana documentary za utafiti baharini,upishi 175 na 174 hii na zile animal channels na TNT movie na multchoice movie zote na African magic zote,Azam wakaze boot,quality is a number one factor.
Ile HD ya DStv inaitwa HD proper hii ni zaidi ya HD za kawaida kama Azam
 
Azam quality ya picha itatuhamisha DStv naona kuna low quality picture,DStv Wana HD,pia azamu Wana mavipindi ya hovyo nje ya mpira,DStv Wana documentary za utafiti baharini,upishi 175 na 174 hii na zile animal channels na TNT movie na multchoice movie zote na African magic zote,Azam wakaze boot,quality is a number one factor.
Channel zote hizo zipo azam tv, na ishu ya quality ni kwa channel zinazomilikiwa na azam tv tuu na inategemea na aina ya tukio husika mfano ufunguzi wa AFL ilikuwa ni HD. Hizo channel zingine ambazo unaona sio HD bc sio kosa la azam bali ni kutoka kwenye channel husika
 
Back
Top Bottom