Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Naona Western Bloc wanataka kubaki peke yao wanapiga propaganda vita ya Urusi na Ukraine ambapo Multichoice Afrika maarufu kwa kisimbusi chake cha DSTV imeiondoa chaneli ya Urusi ya Russia Today(RT) ambapo kwenye tamko lake wakisema hatua hiyo wamelazimika kuichukua kutokana na vikwazo vilivyowekwa na umoja wa Ulaya.
Mwanahisa mkubwa Multchoice Afrika ni kampuni mama ya Naspers ambayo asilimia 49 inamilikiwa na waholanzi wa Prosus. Mapema wakati vita inaanza EU ilipiga marufuku RT kuonekana barani Uropa.
DSTV ina visimbuzi milioni 20 vilivyo hai na kulipiwa barani Afrika, hata hivyo inawezekana uono kuwa mkubwa zaidi kutokana na vingi kuangaliwa kwenye ngazi ya familia au jamii kama bar na vibandaumiza.