Dua yangu kwa Paulo Makonda

Dua yangu kwa Paulo Makonda

Saalaam kwenu WanaJamvi

Baada ya pilikapilika nyiIngi kupita, pilika za kutangaza nia, kuchukua fomu, kampeni na hatimaye Uchaguzi mkuu hatimaye sasa Jahazi la nchi yetu limeanza kutulia kabla MZEE hajatangaza baraza lake la mawaziri na kuanza kusonga mbele rasmi kwa pamoja.

Kwangu mimi binafsi, ni wiki sasa inatimia tangu nianze kumuweka Rasmi kwenye Maombi ya Viongozi wangu Bwana Paulo Makonda aliyekua kamanda wetu hapa jijini, hasa baada ya MZEE kusisitizia katika hotuba zake za hivi karibuni kuwa kwa asilimia kubwa hatafanya uteuzi mpya hasa mikoani na wilayani, nikamkumbuka huyu kiongozi wangu shupavu na jasiri Bwana Paulo.

Kiongozi aliyekua bado ana ndoto za kufika mbali kiuongozi akifuata nyayo za mwenyewe MZEE za kuwatetea na kuwapigania wananchi hasa wale wa chini kabisa wasio na mtetezi, huyu Bwana Paulo alijitahidi kuwapigania bana, mara huku akina singo mama, mara kule bodaboda, sijui waliimu bila kuwasahau viongozi wa Dini aliojitahidi sana kuwaleta pamoja ili wafanye kazi kwa Umoja bila kuchukiana wao kwa wao kugombania kondoo. Tunazijua vita nyingi alizozianzisha na kuzipigania mpk mwisho 'field marshal' huyu mpk sasa jiji hili na nchi kwa ujumla imekaa salama kwa upande wa madawa ya kulevya.

Namuombea sana Bwana Paulo aweze kuonwa tena katika nafasi ya uongozi wa nchi yetu hii yenye kuhitaji watu wa aina yake ukiachilia mbali madhaifu yake ya kibinadamu ambayo tumeumbiwa nayo, alikua muwajibikaji mzuri sana kusimamaia vitu vinavyomuhusu yeye binafsi au mkoa wake kama kiongozi. Hakuwa muoga huyu jamaa wengi aliwashangaza kwa hilo, hata nchi nzima ilipomsema na kumnanga bado huyu jamaa alisimama imaara inaonesha hata mabeberu atawakazia sana huko mbele kama dua zangu zikikubalika mbele za Mungu na MZEE.

Tunamjua MZEE kwa misimamo yake anaweza sana kumkazia na kutompa tena hata wilaya LAKINI MZEE unazo zile nafasi za wabunge wa kuteuliwa (nafikiri zinakua 10) tafadhali tunakusihi, jicho lako limgeukie tena huyu Bwana Paulo sio kama utakuwa unarudisha mpira kwa kipa hapana ila kijana wako Paulo alikua mtiifu sana kwako achilia mbali ndoto zake mwenyewe kama kiongozi za kuhakikisha anakusaidia wewe kufikia ile nchi ya ahadi, basi ikikupendeza umuweke tena katika wale 'wanao' kumi wa ziada pale mjengoni ili wakati anapigania kutimiza ndoto zake hizo na sisi tunufaike na uongozi wake na kusonga mbele Pamoja.

Wako mtiifu!
Bwana alimkataa Sauli...kama Bwana amemkataa maombi yako ni makelele...halafu huyo makonda siyo spiritual kivilee...anyway kila mtu ashinde mechi zake kama mdau mmoja anavyosemaga humu
 
ndo la msingi hilo mkuu kila mtu kushinda mechi zake, kama ni upande wake tuache aendelee kushinda tu!
 
Saalaam kwenu WanaJamvi

Baada ya pilikapilika nyiIngi kupita, pilika za kutangaza nia, kuchukua fomu, kampeni na hatimaye Uchaguzi mkuu hatimaye sasa Jahazi la nchi yetu limeanza kutulia kabla MZEE hajatangaza baraza lake la mawaziri na kuanza kusonga mbele rasmi kwa pamoja.

Kwangu mimi binafsi, ni wiki sasa inatimia tangu nianze kumuweka Rasmi kwenye Maombi ya Viongozi wangu Bwana Paulo Makonda aliyekua kamanda wetu hapa jijini, hasa baada ya MZEE kusisitizia katika hotuba zake za hivi karibuni kuwa kwa asilimia kubwa hatafanya uteuzi mpya hasa mikoani na wilayani, nikamkumbuka huyu kiongozi wangu shupavu na jasiri Bwana Paulo.

Kiongozi aliyekua bado ana ndoto za kufika mbali kiuongozi akifuata nyayo za mwenyewe MZEE za kuwatetea na kuwapigania wananchi hasa wale wa chini kabisa wasio na mtetezi, huyu Bwana Paulo alijitahidi kuwapigania bana, mara huku akina singo mama, mara kule bodaboda, sijui waliimu bila kuwasahau viongozi wa Dini aliojitahidi sana kuwaleta pamoja ili wafanye kazi kwa Umoja bila kuchukiana wao kwa wao kugombania kondoo. Tunazijua vita nyingi alizozianzisha na kuzipigania mpk mwisho 'field marshal' huyu mpk sasa jiji hili na nchi kwa ujumla imekaa salama kwa upande wa madawa ya kulevya.

Namuombea sana Bwana Paulo aweze kuonwa tena katika nafasi ya uongozi wa nchi yetu hii yenye kuhitaji watu wa aina yake ukiachilia mbali madhaifu yake ya kibinadamu ambayo tumeumbiwa nayo, alikua muwajibikaji mzuri sana kusimamaia vitu vinavyomuhusu yeye binafsi au mkoa wake kama kiongozi. Hakuwa muoga huyu jamaa wengi aliwashangaza kwa hilo, hata nchi nzima ilipomsema na kumnanga bado huyu jamaa alisimama imaara inaonesha hata mabeberu atawakazia sana huko mbele kama dua zangu zikikubalika mbele za Mungu na MZEE.

Tunamjua MZEE kwa misimamo yake anaweza sana kumkazia na kutompa tena hata wilaya LAKINI MZEE unazo zile nafasi za wabunge wa kuteuliwa (nafikiri zinakua 10) tafadhali tunakusihi, jicho lako limgeukie tena huyu Bwana Paulo sio kama utakuwa unarudisha mpira kwa kipa hapana ila kijana wako Paulo alikua mtiifu sana kwako achilia mbali ndoto zake mwenyewe kama kiongozi za kuhakikisha anakusaidia wewe kufikia ile nchi ya ahadi, basi ikikupendeza umuweke tena katika wale 'wanao' kumi wa ziada pale mjengoni ili wakati anapigania kutimiza ndoto zake hizo na sisi tunufaike na uongozi wake na kusonga mbele Pamoja.

Wako mtiifu!
Mzee hapangiwiiiii! hapo ndio unamwambia amtupe kabisaaaa. Au umeamua kumharibia?
 
Uwepo wa Makonda Na Thamani Yake Dhidi ya:
1.Panya Road
2.Mihadarati na madawa ya kulevya
3.Uzururaji
4.Utelekezaji Watoto
5.Uvivu
6.Ukataji Tamaa
7.Upigaji na njia za mkato kimaisha
8.Miundombinu mibovu jijini Dar
9.Usahaulifu wa maendeleo kwa vijana.
10.Usahaulifu wa vipaji vya vijana.
 
Back
Top Bottom