Dubai, China, Uturuki, au South Africa?

Dubai, China, Uturuki, au South Africa?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kama unataka kufanya ziara ya kuangalia fursa za kibiashara, hasa kuangalia bidhaa za kuzileta nchini, ni nchi ipi inaweza ikawa sahihi zaidi kuitembelea? Muda wa ziara ni wiki mbili!

Nchi ipi kati ya hizi? DUBAI, CHINA, UTURUKI, au SOUTH AFRICA?

Kwa nini?
 
China bidha bei chini ingawa mbali.Dubai bei kidogo ghali ila karibu. Uturuki sijawahi kwenda ,sina cha kushauri.wala Sauzi
 
China bidha bei chini ingawa mbali.Dubai bei kidogo ghali ila karibu. Uturuki sijawahi kwenda ,sina cha kushauri.wala Sauzi
Kuna mtu alikuwa akipasifia Uturuki kuwa pako vizuri kwa nguo na samani (furniture)
 
Ndugu nenda uchina hutajuta...Pia usiangakie bidhaa tu,angalia na namna wanavyo duplicate...
 
Muondoe South Afrika hapo, hao wengine ndo kuna bishara kwa sasa.

Uturuki ni nguo quality, makapeti mazito, mapazia na vito vya samani.

Dubai kama unataka simu used, laptops, spea za magari used, mashuka makubwa nk huko panakufaaa sana plus ni karibu.

China ndo baba lao, everything ni cheap, sema tu ni umbali.
 
Back
Top Bottom