Nilisoma kitabu Cha tiputipu hakika wazungu wameficha sana historia,pia wameanikiwa kuwafanya waarabu kua watu wabaya na wapenda utumwa wakati ni tofauti na uhalisia was kipindi hiko
Hapa ndipo mnapoharibu ninyi mabwana. Waarabu hawakuwa watu wema kwa waafrika wazawa. Waliuza watumwa maelfu kwa maelfu, mbaya zaidi waliuza hadi watumwa wa kizungu.
Tukirudi kwenye mada ya
The Boss , historia kuhusu Zanzibar ipo wazi na imejaa kwenye vitabu. Tatizo ni kwamba watanzania hatupendi kusoma na kufanya tafiti. Hata kama tukisoma tunasoma ili kukidhi ajenda zetu za kidini, kikabila na kisiasa. Historia haitakiwi isomwe hivyo...
Kuhusu Zanzibar sasa, Sultani hakuishia Dar es salaam na Mombasa, alifikia sehemu nyingi za ndani. Dr Karl Jhulke wa Ujerumani alivyokuja Tanganyika ili kusaini mikataba na Lady Mbumi of Mkondokwa aliambiwa kabisa kwamba eneo lile liko chini ya Zanzibar.
Upande mwingine, Dr Karl Peters wa The Society for Germany Colonization, aliambiwa kwamba maeneo kama Arusscha (Arusha) na Kilimanjaro yalikuwa chini ya Sultani (Under Zanzibar Suzerain) baada ya machifu wa maeneo hayo kufanya mikataba na Sultani.
Ukisoma zaidi, mkataba wa chifu Mangungo unamtambua mangungo kama Sultan, na siyo Traditional Chief. Hivyo inaonesha kabisa utawala uliokuwa unafahamika maeneo hayo ulikuwa ni ule wa kinzanzibari wa kisultani, kwasababu maeneo hayo yalikuwa chini ya Zanzibari.
Ushahidi wa hili ninalolisema uko kwenye barua ambazo Sultani aliwaandikia wafalme wa Uingereza na Ujerumani baada ya mkataba wa Berlin akilalamika kwanini wamegawana maeneo yake bila yeye kushirikishwa. Tafuta hizi barua utazipata...
Binafsi, huwa nasema ni heri waarabu waliingiliwa (thwarted) mapema na wazungu katika kutawala sehemu za huku bara. Kama wasingezuiliwa, mambo mabaya sana yangefanyika huku. Mabaya mno....