Salaam Wakuu,
Tangu kilichoitwa uchaguzi wa 29 Oktoba 2025 kumalizika, Samia Suluhu ameshindwa eti kufanya kazi zake sababu ya unyanyasaji kijinsia. Inadaiwa watanzania wanamsononiesha kwa kumzushia mambo ambayo hajawahi fanya.
View attachment 3539165
Martha Mlata Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida
Kwamba Watanzania wamemnyima ushirikiano kama waliokuwa wanawqpa Marais wengine.
Watanzania wanamzuia Samia kufanya kazi. Hata aliposema watu wapande Miti, ni watanzania wachache walijitokeza wakati ni kwa mannufaa yao.
Bado mnaendelea kuzungumzia mauaji ya 29 Oktoba 2025, akisikia eti ni sawa na kumtonesha kidonda hivyo hataki tuzungumzie mauaji.
Yeye anadai hajawahi kuua ta sisimizi🤣
Sasa kaenda kwa Wajomba zake Huko Uarabuni.. Atasema yote hata mlivyochongea kwa nchi za Magharibi hata wakakata misaada. Kila ubaya mliomfanyia kaunoti kwenye Notebook.
Sasa tusubiri Warabu watunyoshe. Tumewachokozea Mtoto🤣🤣..
View attachment 3539166
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Mtawala wa Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, kando ya Mkutano wa Dunia (WGS2026) Dubai, Jumatano, Februari 04, 2026.
MyTAKE
Leo atatema nyongo..
Soon tunaletewa Tende na Halua kama pole. 🤣🤣
Hapo alikuwa anazugumzia dili ya dhahabu aliyompelekea!! Mwanamke huyu ataifilisi nchi ; Mungu tuhurumie sie waja wako kutoka kwa mikono ya huyu fisadi.