Dudu Baya: Dimpoz naomba unisamehe, “nilitumia jina lako ili ujumbe ufike dunia nzima, Endelea kulinda mgongo wako

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya, leo Septemba 29, 2026 amemuomba radhi Msanii mwenzake, Omary Nyembo “Ommy Dimpoz”, kutokana na kauli aliyoitoa dhidi yake.

Akizungumza kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Dudu Baya amesema, “nilitumia jina la Ommy Dimpoz ili ujumbe ufike dunia nzima kwa sababu wewe ni maarufu, wewe ni Mdogo wangu na tunaheshimiana sana najua nilikukera, nilikuudhi, naomba uniwie radhi, nisamehe sana.”

Dudu Baya alitoa kauli hiyo dhidi ya Ommy Dimpoz wakati wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva lililofanyika Septemba 19, 2026 katika Viwanja vya General Tyre, Arusha.

Soma Pia: Dudu Baya azimiwa mic jukwaani baada ya kusema Ommy Dimpoz chakula cha watu

Dudu Baya aache utani, ujumbe wake ulifika kwa mlengwa.

Kwanini atumie jina la Dimpoz ikiwa walikuwepo wengi wengine wenye majina kwenye eneo la tukio?

Dudu atakuwa ametishwa from somewhere, kaambiwa omba radhi ama sivyo, tutalala na wewe mbele.

Inawezekana Dudu kaambiwa usipoomba radhi hatutakuita tena kwenye show zetu.
 
Sio kila mbwa mkali anabweka.Hata kama ni kweli,MAMBA amekosea kumsema mtu vibaya katika jamii.

Actually huenda hata sisi tunakosea kuwatamkia watu maneno mabaya,ila ukweli unauma asikwambie mtu.

Kama hujawahi kuongelewa vibaya omba yasikukute.
 
Mambazz 24
YBWYB

1790695797619.png
 
Msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya, leo Septemba 29, 2026 amemuomba radhi Msanii mwenzake, Omary Nyembo “Ommy Dimpoz”, kutokana na kauli aliyoitoa dhidi yake.

Akizungumza kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Dudu Baya amesema, “nilitumia jina la Ommy Dimpoz ili ujumbe ufike dunia nzima kwa sababu wewe ni maarufu, wewe ni Mdogo wangu na tunaheshimiana sana najua nilikukera, nilikuudhi, naomba uniwie radhi, nisamehe sana.”

Dudu Baya alitoa kauli hiyo dhidi ya Ommy Dimpoz wakati wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva lililofanyika Septemba 19, 2026 katika Viwanja vya General Tyre, Arusha.
Huyu habahatishi mkuu alichokisema pale stejini ni uhakika wa asilimia mia
 
Back
Top Bottom