Msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya, leo Septemba 29, 2026 amemuomba radhi Msanii mwenzake, Omary Nyembo “Ommy Dimpoz”, kutokana na kauli aliyoitoa dhidi yake.
Akizungumza kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Dudu Baya amesema, “nilitumia jina la Ommy Dimpoz ili ujumbe ufike dunia nzima kwa sababu wewe ni maarufu, wewe ni Mdogo wangu na tunaheshimiana sana najua nilikukera, nilikuudhi, naomba uniwie radhi, nisamehe sana.”
Dudu Baya alitoa kauli hiyo dhidi ya Ommy Dimpoz wakati wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva lililofanyika Septemba 19, 2026 katika Viwanja vya General Tyre, Arusha.