Dudu Baya: Kinachofanya Tanzania itulie tofauti na jirani zetu ni kuwa sisi tumenyimwa elimu ya haki zetu. Wenzetu wanayo

Dudu Baya: Kinachofanya Tanzania itulie tofauti na jirani zetu ni kuwa sisi tumenyimwa elimu ya haki zetu. Wenzetu wanayo

Akizungumza kwenye moja ya blog za mitandaoni msanii huyo mkongwe amesema kuwa inayoitwa amani tuliyonayo Tanzania ni kwa vile tu wananchi wamenyimwa elimu ya haki zao.

Amesema kwa mtanzania akiwasha runinga akaona kipindi kinaongelea mambo ya katiba anahamisha hiyo chanel haraka sana atatafuta mipira au mziki ama tamthilia ila kuongelea mambo yanayohusu mustakabali wa maisha yao wanaona hayawahusu.

Amesema hicho ndo tunatofautiana na jirani zetu kwa wenzetu asilimia kubwa ya raia wanaelewa haki zao hivyo ikitokea zinachezewa hawataki masihara kabisa.
Huyu nae dudu baya mpumbavu mbona enz za jiwe hakua akiyazungumza haya kaongea ukweli ika mtu mnafiki hua simkubali dudu ana jnafiki wa kinge*** sana enzi za jiwe sikuwah nsikia akitoa hizi kauki
 
Wamenyimwa na nani? Mbona kwenye mfano wake kuna vipindi vya luninga vinavyohusu mambo ya katiba (utawala na maamuzi) na watanzania walio wengi ndio hawapendi.
Wanachukuliwa watu wa Lumumba hapo wakajadili maswala ya katiba nani awasikilize ? Wale huwa ni makada watupu wa ccm ambao wamevaa nguo za kiraia
 
KOnki, konki, konki master is back!!!

Alindwe kwa gharama yoyote.
 
Huyu nae dudu baya mpumbavu mbona enz za jiwe hakua akiyazungumza haya kaongea ukweli ika mtu mnafiki hua simkubali dudu ana jnafiki wa kinge*** sana enzi za jiwe sikuwah nsikia akitoa hizi kauki
Kwani ukimsikia kipindi hiki unaumia masikio?Pata ujumbe wake na uache kulalamika.Ungewasikia wangapi?
 
Haiondoi ukweli tribalism ilishamiri sana enz za jiwe na hata huyu hakuwah kosoa zaid ya kuwananga upande ule ni wabaya
Ndicho kinakufanya ushindwe kuelewa anachoongea leo?Halafu,enzi za huyo aliyetoroka kuishi,ni vyombo gani vya habari vilikua huru kurusha/kuandika taarifa za kumpa changamoto?
 
Yaah ni kweli, na hii inaanzia ngazi ya familia.
Baba na mama kutwa kucha busy na simba na yanga. Kina baba wa siku hizi hawa hata hivyo vipindi hawaangaliagi ni mpira na tamthilia tu.
Wanawajua sana akina Etugrubey na akina Pasha wa Uturuki 😂😅👍
 
Kumbe Dudu baya kuna wakati akili zake zinakuwa timamu hivi!
Hongera sana kwa kuona hili, kumbe wewe una akili na ufahamu tofauti kabisa na akina baba level na mwijaku!
 
Back
Top Bottom