Dudu Baya: Kinachofanya Tanzania itulie tofauti na jirani zetu ni kuwa sisi tumenyimwa elimu ya haki zetu. Wenzetu wanayo

Na kama Mahakama hazifanyi kazi yake ipasavyo yaani inasikiliza upande mmoja kwa upendeleo utafanyaje?
Mahakama kazi yake kusikiliza hoja na ushahidi dhahiri mahakama haifanyi kazi kwa dhana tu unaweza kuwa umeonewa lakini ukashindwa kudhihirisha kwa ushahidi. Mbona kuna kesi nyingi tu watu wameshinda dhidi ya serikali ila nyinyi mkishindwa kesi ndio umeonewa. Mahakama ziko level tofauti kutoa nafasi ya kukata rufaa. Hili la kusema mahakama haijatenda haki kwa kigezo gani unatumia? umeshindwa kesi jipange. Kwa hiyo kila anayeshindwa kesi aingie barabarani kufanya fujo? basi itakuwa kila siku nchi nzima wako barabarani kupinga hukumu.
 
😀😀😀😀😀😀
 
Inavyoonekana aidha huelewi chochote unajiongelesha tu au unaongea kachama zaidi. Ngoja tukupe dalasa kidogo

Kamwe usije kujidanganya kudhani kwamba Sheria za nchi ni perfect as long as Sheria wenyewe zimetungwa na wanadamu tena wanadamu wenyewe wanasiasa, ulisha msikia magufuli akisema mkataba wa bandari ya bagamoyo ni kichaa pekee ndo angeweza kukubaliana nao!!

Mwalim Nyerere aliwahi kukiuka Sheria za serikali ya mkoloni alipoona ni kandamizi kwa hiyo inapotokea Sheria imetungwa hata kama imeputishwa kama ni kandamizi raia wanatakiwa kupaza sauti ili ibadilishwe Wala sio dhambi hata wewe ni mnufaika wa baadhi ya watu ujasiri waliosimama imara kuhakikisha jambo fulani linabadilishwa
 
Na hapa ndipo unathibitisha uhalisia wa madai ya dudubaya maana mada inasema watanzania wamenyimwa elimu ya haki zao wewe unasema huna shida
 
Inferiority complex aka kupumbazwa akili,ogopa sana hii kitu,wkt wauchaguzi wanawaza mgombea gani ametoa vitenge/hela/pombe iliwamchague wkt hizo gharama akifanikiwa kupata km ni ubunge huo nimshahara wake mmoja wa mwezi gharama zote zimerudi
 
Kumbe unajuwa hakuna kitu perfect sasa unataka kudai nini wakati unajuwa hakuna perfect na umesema binadamu hajawahi kuweka sheria perfect, sasa nikupe elimu wewe hata vitavu vya dini vimoja lakini humo humo tunaelewa tofauti na tunatofautiana na vitabu vimoja. Wewe kumtaja JPM tu nimekuelewa ni wale watu wanaishi na chuki baada ya JPM. JPM alikuwa mtu mzuri na alifanya aliyoweza kufanya miaka yake aliyotawala ila kwa sasa tumuache apumzike kwa amani.

JPM alifanya yake na mengine aliyakataa ni jukumu lake kama Rais lakini hakuwa mkamilifu pia ndio katika utawala wake ajira zote zilisimama, hakuwahi kuongeza mishahara pamoja na madai yote tumefunga mianya ya rushwa, hakuna kusafiri, hakuna bandari ya Bagamoyo lakini pamoja na yote hakuwahi kuajiri wala kuongeza hata cent tano hujiulizi kwanini? Hizi haki unazotaka kwenda kuandamana ni JPM alivunja kila kifungu kwenye katiba ulikuwa wapi kuongelea haki za raia? Mimi nakubaliana na kitu kimoja, nchi hii inahitaji Rais kama JPM tough na kuwachapa watu bila huruma ndio watu wanakaa kwa adabu kinyume cha hapo ndio watu kama nyinyi mnatokea kujifanya haki za raia. Mlikuwa wapi wakati wa JPM?
 
Ngumi jiwe, kasema kweli kabisa. Hao ndiyo Watanzania halisi. Maadui zetu sisi ni vijana wanaoishabikia ccm, kwa maslahi yao, ya kutaka uongozi ndani ya chama na bunge. Hawa wanarudisha nyuma, juhudi za kukichomoa hiki chama kongwe Tz.
Mimi na wewe tunatofautiana kwenye mambo ya Yanga tu, kwingine aaahh
 
Hizi hoja zako za chuki dhidi ya magufuli sijajua ulikozitoa nilichofanya mimi ni kukupa mf kuwa watunga Sheria wetu kuna wakati hutunga kwa kuumiza maslahi ya wengi hivyo hata kama hiyo Sheria imeputishwa kihalali kama raia ni haki na wajibu wetu kuipinga kwa njia zozote ila wewe hutaki nadhani kwa kuendekeza maslahi yako binafsi
 
Wapi mimi nimemsema JPM, ni wewe umemleta kwa hoja yako JPM asingekubali mkataba wa bandari na nimekwambia hakuna kiongozi mkamilifu hata JPM alikuwa na mazuri yake na mapungufu yake lakini tunakumbuka mazuri yake ndio muhimu sasa unashindwa nini kuchukua mazuri tu ya serikali hii mpaka utake kuandamana.

Sasa swali specific usilete ujumla haki zetu, ungesema ni haki ipi unaongelea labda ungependa iwe sheria au sheria ipi unadhani haifai ingeondolewa badala ya kuleta ujuma HAKI ZETU, ni zipi hizo? maana ziko sheria nyingi nzuri tu taja wewe unayo ona ni mbaya. Kuhusu ubinafsi yes natizama maslahi yangu mimi sio mjamaa maslahi ya wote kazi ya viongozi maana huwezi hata wewe kunisaidia kwenye shida zangu.
 
Yuko sahihi
Hajui sisi Watanzania tunaakili
Huwa hatupambanii mtu angie madrakani
Hao nirani zetu ni mazezeta tu
Uwezo wa kujua ya jayo hawana
Mm siwezi kuandamana eti mtu fulani awe kiongozi ni unwege
 
Mbona umehamisha mjadala maana mimi sijajadili makosa ya mtu lkn nimekupa mf wa namna mfumo unaweza kuwaingiza chaka kwa kutolea mfano hicho kipande wewe umegeuza jpm na madhaifu/ mazuri yake ndio mada kuu.
Mimi sipo huko mimi napinga kwamba eti kwa kuwa jambo lipo kisheria basi lazima liwe sahihi sii kweli! Ndio maana kama raia tukiona jambo linabinya uhuru na utu wa mwanadamu lazima lipingwe ila kwa kuwa elimu ya haki za kiraia ipo chini ndio maana hata wewe hujaona haki yoyote uliyonyimwa sasa utaonaje wakati hujui chochote.
 
Sheria nani anatunga? Bunge linatunga sheria na watu wanawakilisha ni wale waliochaguliwa na wananchi hatuwezi sisi sote watu million 60 tukatunga sheria. Tool ya kutumia mwananchi ni wale tunaowachagua kutuwakilisha na jukumu lao moja nikutunga sheria, sheria inaweza kutungwa na kubadilishwa wakati wowote. Serikali iliyochaguliwa na sisi wanapeleka mapendekezo bunge linajadili kupitisha au kupinga mwisho ni Rais ana sign kama sheria, hawa wote wamechaguliwa na sisi.

Ndio maana nimekuuliza swali jepesi tu ni sheria ipi kwa maoni yako inabidi ibadilishwe au sheria zipi ili tuanzie hapo. Kujuwa haki zako haikupi mamlaka ya kubadili sheria kuna system inatumika kutunga au kutungua sheria. Silaha kuu uliyonayo ni kura yako sio fujo.
 
Sasa wewe si chukuwa family yako ingia barabarani mfuate Dudu baya. Tz kama kuna mjinga jiangalie wewe wa kumsikiliza Dudu baya mtu ambaye kujiongoza tu kama yeye kashindwa ndio akili za kibongo, tafuta pesa acha hasira hakuna shortcut kwenye maisha.
bado ujasema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…