Kumbe unajuwa hakuna kitu perfect sasa unataka kudai nini wakati unajuwa hakuna perfect na umesema binadamu hajawahi kuweka sheria perfect, sasa nikupe elimu wewe hata vitavu vya dini vimoja lakini humo humo tunaelewa tofauti na tunatofautiana na vitabu vimoja. Wewe kumtaja JPM tu nimekuelewa ni wale watu wanaishi na chuki baada ya JPM. JPM alikuwa mtu mzuri na alifanya aliyoweza kufanya miaka yake aliyotawala ila kwa sasa tumuache apumzike kwa amani.
JPM alifanya yake na mengine aliyakataa ni jukumu lake kama Rais lakini hakuwa mkamilifu pia ndio katika utawala wake ajira zote zilisimama, hakuwahi kuongeza mishahara pamoja na madai yote tumefunga mianya ya rushwa, hakuna kusafiri, hakuna bandari ya Bagamoyo lakini pamoja na yote hakuwahi kuajiri wala kuongeza hata cent tano hujiulizi kwanini? Hizi haki unazotaka kwenda kuandamana ni JPM alivunja kila kifungu kwenye katiba ulikuwa wapi kuongelea haki za raia? Mimi nakubaliana na kitu kimoja, nchi hii inahitaji Rais kama JPM tough na kuwachapa watu bila huruma ndio watu wanakaa kwa adabu kinyume cha hapo ndio watu kama nyinyi mnatokea kujifanya haki za raia. Mlikuwa wapi wakati wa JPM?