Wana tatizo la ardhi majirani zetu, sehemu kubwa ya nchi yao ni jangwa kule kaskazini pote ni sawa na Somalia, pakavu na hapafai kwa kilimo.
Kitendo cha wachache kuishi kama wapo peponi na wengi wakizaliwa katika tabaka la kunyonywa ni lazima siku moja hao wanaoonewa watakuja kusomesha watoto wao na wakikua tegemea balaa kwenye nchi.
Mwalimu Nyerere alikuwa anaona mbali sana, alihakikisha anasomesha bila ya kuwepo kwa madaraja ya mkubwa na mdogo na imesaidia sana huko kwenye ajira kukutana na wasomi wenye uelewa kwamba elimu waliyoipata iliwekwa katika mfumo wa utawanyaji wa haki kwa kila mtu kuweza kuipata.
Mwigulu Nchemba anajiita mtoto wa mkulima, angekuwa ni Mkenya angekuwa ni sawa na hawa Gen Z. Kuna mawaziri na wakurugenzi na makatibu wakuu wengi tu wenye kufanana na Mwigulu na hawa wanaitofautisha Kenya na Tanzania.