Dudu Baya: Kinachofanya Tanzania itulie tofauti na jirani zetu ni kuwa sisi tumenyimwa elimu ya haki zetu. Wenzetu wanayo

Akizungumza kwenye moja ya blog za mitandaoni msanii huyo mkongwe amesema kuwa inayoitwa amani tuliyonayo Tanzania ni kwa vile tu wananchi wamenyimwa elimu ya haki zao.

Amesema kwa mtanzania akiwasha runinga akaona kipindi kinaongelea mambo ya katiba anahamisha hiyo chanel haraka sana atatafuta mipira au mziki ama tamthilia ila kuongelea mambo yanayohusu mustakabali wa maisha yao wanaona hayawahusu.

Amesema hicho ndo tunatofautiana na jirani zetu kwa wenzetu asilimia kubwa ya raia wanaelewa haki zao hivyo ikitokea zinachezewa hawataki masihara kabisa.
Kumbe Dudu baya sometimes una akili eh. 😀😀
 
mifano ya dudu baya ndio hii
Sasa wewe si chukuwa family yako ingia barabarani mfuate Dudu baya. Tz kama kuna mjinga jiangalie wewe wa kumsikiliza Dudu baya mtu ambaye kujiongoza tu kama yeye kashindwa ndio akili za kibongo, tafuta pesa acha hasira hakuna shortcut kwenye maisha.
 
Mahakama zipo pia kumbuka unaweza kuwa wewe hujawachagua ila kuna watu wamewachagua kwa hiyo wana mandate ya kuongoza. unashida mahakama zipo sio kuleta fujo barabarani kuna watu wako busy kutafuta pesa.
Wewe inaonekana una changamoto ya kuelewa historia ya mapambano ya kupigania haki
 
Fujo maana yake ni nini?
Maandamano ya amani wewe kwa kiwango chako cha ufahamu unachukulia ni fujo ?
Hivi nyinyi mnakazi za kufanya? au mnaandamana jumapili. nchi ina chaguzi ukifika chagua unayemtaka baada ya hapo tafuta pesa tu.
 
Sasa wewe si chukuwa family yako ingia barabarani mfuate Dudu baya. Tz kama kuna mjinga jiangalie wewe wa kumsikiliza Dudu baya mtu ambaye kujiongoza tu kama yeye kashindwa ndio akili za kibongo, tafuta pesa acha hasira hakuna shortcut kwenye maisha.
Haya ni mawazo potofu. Ukikandamiza sana haki za wengi the least of your problems itakuwa watu kuingia barabarani.
 
Iko haja ya kupata regime itakayobalansi vizuri haya mambo mijadala ya burudani Ina nguvu sana kuliko mijadala ya mustakabali wa taifa letu
Hiyo regime runaipataje sasa? Yaani ulichosema ni sawa na kusema "Ipo haja ya Dar kuwa kama Tokyo". Issue ni tunaipataje hiyo regime?
 
Sasa wewe si chukuwa family yako ingia barabarani mfuate Dudu baya. Tz kama kuna mjinga jiangalie wewe wa kumsikiliza Dudu baya mtu ambaye kujiongoza tu kama yeye kashindwa ndio akili za kibongo, tafuta pesa acha hasira hakuna shortcut kwenye maisha.
Hoja sio kuingia barabarani pekee hoja ni kutambua haki ya raia. Alichoongea ni kwamba watanzania uwezo wa kutambua haki zao upo chini.
Wengi wetu huishia kuonewa na kupotezea
 
Akizungumza kwenye moja ya blog za mitandaoni msanii huyo mkongwe amesema kuwa inayoitwa amani tuliyonayo Tanzania ni kwa vile tu wananchi wamenyimwa elimu ya haki zao.

Amesema kwa mtanzania akiwasha runinga akaona kipindi kinaongelea mambo ya katiba anahamisha hiyo chanel haraka sana atatafuta mipira au mziki ama tamthilia ila kuongelea mambo yanayohusu mustakabali wa maisha yao wanaona hayawahusu.

Amesema hicho ndo tunatofautiana na jirani zetu kwa wenzetu asilimia kubwa ya raia wanaelewa haki zao hivyo ikitokea zinachezewa hawataki masihara kabisa.
Upole ni hulka ya watanzania kabla hata ya uhuru kupatikana. Akumbuke kuwa hawa Gen Z ni wajukuu wa wale askari wa MAUMAU waliouawa kwa wingi na uhuru ukaja kupatikana baada ya damu nyingi kumwagika.

Kijana wa Kenya hawezi kufanana na kijana wa Tanzania. Yule wa Kenya ni mjukuu wa mwanaharakati aliyepata uhuru kwa kuuchukua kutoka kwa Muingereza. Huyu wa Tanzania kaupata uhuru kwa namna ya kukaa mezani na kujenga hoja zenye kueleweka pia kuna suala la haki ya Tanzania kupewa uhuru baada ya kupita miaka kadhaaa.

Naamini tofauti ya Tanzania na Kenya ni ya miaka mingi nyuma. Hata hizo haki tungekuwa tunazifahamu bado huwezi kukwepa mchango wa hulka zetu za upole zenye kututofautisha na majirani wa kaskazini.
 
Haki inapatikana kisheria na mahakama zipo.
Ni mara ngapi kwenye ziara za viongozi wetu unakuta haki za watu zimechezewa kwa makusudi kabisa mpaka viongozi waje waingilie kati!?

Ni mara ngapi tumesikia wenye mamlaka ya kuhakikisha haki imetendeka wamepindisha haki?
Ni mara ngapi tumesikia Hadi viongozi wakubwa wanatumbuliwa kwa sababu walibariki na kulinda mifumo ovu chini yao!?
 
Hoja sio kuingia barabarani pekee hoja ni kutambua haki ya raia. Alichoongea ni kwamba watanzania uwezo wa kutambua haki zao upo chini.
Wengi wetu huishia kuonewa na kupotezea
Sasa nikuulize kama nchi limetuletea nini kama taifa kwa tabia zetu hizi, maana tujifananishe na jirani zetu mnaowasifia nini wamepata na sisi nini tumepata. Kwa tabia zetu hizi za kupuuza kimaisha sisi na wao hatuna tofauti ila sisi tumewazidi tabia, tunapendana, tuna amani hatuna history ya violence hata uhuru tumepata kwa kuongea. wala sio tabia mbaya kupuuza baadhi ya mambo lakini sio kwamba watu wajinga au hawajui, ndio maana tuna kesi nyingi mahakamani kila siku dalili watu wanadai haki zao njia sahihi. USA wana system bora kabisa duniani lakini bado kuna watu hawatendewi haki, wako wanafungwa bila makosa na wako wanauliwa bila makosa.
 
Ni mara ngapi kwenye ziara za viongozi wetu unakuta haki za watu zimechezewa kwa makusudi kabisa mpaka viongozi waje waingilie kati!?

Ni mara ngapi tumesikia wenye mamlaka ya kuhakikisha haki imetendeka wamepindisha haki?
Ni mara ngapi tumesikia Hadi viongozi wakubwa wanatumbuliwa kwa sababu walibariki na kulinda mifumo ovu chini yao!?
Kama walitumbuliwa basi mfumo unafanya kazi. Ndugu yangu hata nchi zilizoendelea kwa mifumo bado wana issue nyingi sana na ndio maana unaona wameanza kuwagawanyika wenye kufuata mlengo wa kulia na wako kushoto. Mimi sisemi hakuna matatizo nchini lakini pia hakuna nyumba isiyokosa matatizo ila watu wanaongea na maisha yanaenda na kama nchi tutaongea na tutaenda ila tusitake kuiga tabia mbaya za majirani. wameshauwana sana tena sana imewasaidia nini kama mwananchi, zaidi ya wana siasa tu.
 
Kinachosemwa hapa sii kuiga tabia mbaya bali uelewa wa kutambua haki zetu upo chini kuliko wenzetu na ujasiri wa kuzidai pia upo chini kuliko wenzetu Hilo ni la kubisha mkuu!?
 
Unaweza kuwa kweli wala sibishi lakini naukuuliza wao wamefaidika na nini kwa hilo na sisi tumefaidika na nini kwa tabia zetu hizi. Sisi wa Tanzania ni watu tunapenda raha shida basi tu zinakuja lakini raha tunapenda ndio ina reflect maisha yetu. Tunapenda kupuuza kwa mambo yatakayo tukosesha raha hizi ndio tabia zetu na nzuri. kuna wakati ukitaka amani lazima upuuze baadhi ya mambo ukiwa serious na maisha utakosa amani. Tunapenda raha na ibaki hivyo.
 
😂😂😂 We jamaaa bhana tuna hatari ya kutengeneza kizazi kisichojua kuhoji na hivyo hao waliozoea mivutano wakachukua mahali petu!!
 
Wana tatizo la ardhi majirani zetu, sehemu kubwa ya nchi yao ni jangwa kule kaskazini pote ni sawa na Somalia, pakavu na hapafai kwa kilimo.

Kitendo cha wachache kuishi kama wapo peponi na wengi wakizaliwa katika tabaka la kunyonywa ni lazima siku moja hao wanaoonewa watakuja kusomesha watoto wao na wakikua tegemea balaa kwenye nchi.

Mwalimu Nyerere alikuwa anaona mbali sana, alihakikisha anasomesha bila ya kuwepo kwa madaraja ya mkubwa na mdogo na imesaidia sana huko kwenye ajira kukutana na wasomi wenye uelewa kwamba elimu waliyoipata iliwekwa katika mfumo wa utawanyaji wa haki kwa kila mtu kuweza kuipata.

Mwigulu Nchemba anajiita mtoto wa mkulima, angekuwa ni Mkenya angekuwa ni sawa na hawa Gen Z. Kuna mawaziri na wakurugenzi na makatibu wakuu wengi tu wenye kufanana na Mwigulu na hawa wanaitofautisha Kenya na Tanzania.
Kabisa mkuu sisi na jirani ni vitu viwili tofauti mazingira ya sehemu ina reflect tabia za jamii. Amani haiji kama mvua kuna mambo lazima mkubali kuyapuuza ili amani itawale. Hao wa Kenya ndani ya mioyo yao wanatamani tunavyoishi tuko simple na tunapenda raha tu shida hatupendi. Uhuru wa kupitiliza una madhara yake pia lazima uweke limit.
 
😂😂😂 We jamaaa bhana tuna hatari ya kutengeneza kizazi kisichojua kuhoji na hivyo hao waliozoea mivutano wakachukua mahali petu!!
Wenye kujuwa kuhoji wamepata nini sisi hatuna, sana sana wamezika watu kwa ujinga tu mwisho wa siku serikali ni ile ile maisha ni yale yale ni wamepata. Ndio maana ziko chaguzi ni wakati wa kuchagua unayemtaka ukishindwa basi heshimu majority.
 
Back
Top Bottom