Maboso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 5,164
- 5,762
Binafsi sijaona sheria yoyote iliyovunjwa kiasi cha Mh. Mwakyembe aamuru Dudubaya akamatwe. Si lazima kila mtu amsifie marehemu. Pamoja na hayo manzuri anayosifiwa Ruge, ni ukweli ulio wazi kuwa alikuwa na mapungufu mengine ambayo yaliwakwaza baadhi ya watu. Si sahihi Mwakyembe kutaka kuuaminisha umma kuwa Ruge alikuwa malaika. Rusisahau kuwa ni Ruge huyuhuyu amefariki akiwa amepiga marufuku nyimbo za wasanii wa Wasafi kupigwa Clouds media kisa tu hawa vijana wamegoma kunyonywa. Ni Ruge huyuhuyu ambae aliendesha kampeni kubwa ya kutaka kumpoteza Diamond kwenye ramani ya muziki. Watu kama kina Lady Jaydee wanayajua vinzuri machungu waliyosababishiwa na Ruge. Tufike mahali tuache kuwa wanafiki eti kisa mtu kafa.