Dudubaya amjibu Mwakyembe, azidi kumshukia Ruge Mutahaba

Dudubaya amjibu Mwakyembe, azidi kumshukia Ruge Mutahaba

kwanza,kabla ya kurekodi kile kipindi cha yule mama kichaa kwamba kazaa na gwajima mlionekana na DAB kwenye parking ya clouds mkichukua kibahasha inasemekana ni 200,000, mkala hela ya watu na kipindi hakikuruka ilihali hadi raia namba moja wa nchi the very same week alitangaza kwamba shilawadu ndicho kipindi anachokipenda akiwa ikulu
The same week zikaachiwa cctv footages zikionyesha uvamizi na nyinyi mtaani mlikiri kwa washkjai wenu kwamba mlikula mitama heavy
*muelewe kwamba downfall ya DAB kutoka kupendwa hadi kuchukiwa ilianzia pale na sijui kama truly kasemehe moyoni mwake maana hadi magazeti ya nje ya nchi hadi leo yana refer lile tukio in a negative way
*Baadaye zikavuja habari kwamba bwana DAB alishawahi kukataa rushwa kutoka kwa marehemu ili kum favour rafiki yake aendelee kupewa contracts za kujenga mabarabara mabovu ya dsm kama ile ya akachube,kwa hiyo inaonekana jamaa kwenye ile issue ya cctv sio kwamba alisimamia maadili bali ilikuwa ni kisasi chake lakini naye mwishoni alipigwa na bumbuwazi kama sisi wote baada ya kugundua kwamba jamaa hata afanye makosa ya aina gani hatoki kwenye kile cheo
*ndugu zangu naona bado mnachukua vinahasha na kugeuza kipindi kiwe personal vendetta ,shauri zenu bana...maana consipracy theories kuhusu SUMU wenyewe mnaziona,mjue tu balaaa lilianzia ile issue ya kumuhiji mama kichaa kwamba kazaa na gwajima
*Ikaja issue ya mwandada yule kumkimbia marehemu na kwenda kuolewa jamaa akiwa iringa kikazi,inasemkana GAVANA alitoa mamiliioni kufanikisha harusi ili kumkomoa jamaa,masikini ya Mungu siku ya mwisho kampigia mwandada kaishiwa kurekodiwa akilia na kusambazwa mitandaoni
*mnakumbuka issue ya sudi,maua sama,ben na shafiih walivyolala polisi jamaa akapost kuna mtu katekeleza magari manne mabovu ,yaani jamaa alikuwa hoi kitandani bado anadhihakiwa
*mnaona jinsi wasafi media ilivyochanua baada ya ile scandal yenu?
****KUWENI MAKINI MADOGO MAANA NA NYIE UJINGA WENU UNAJULIKANA KUTOKA ISSUE ZA LGBT HADI KU SNIFF PELE..kuweni makini mno sasa hivi hamna mtetezi,mtapotezwa ,anzeni tu kumsifia jamaa maana hata baada ya ile scandal mlimrushia vijembe ananuka miguu na mdomo
 
Kama MTU alikuwa mbaya atasemwa kwa mabaya yake hata akiwa marehemu,mbona idd amin anasemwa hadi kesho kwa mabaya yake!!?
Mtu anapoondoka huwa tunamtakia kheri ktk safari yake ya mwisho haijarishi duniani aliishi vipi eidha kwa kheri au kwa ubaya kwani ni mmoja peekee anayetoa hukumu ya haki, vilevile sisi sote ni wadhambi hakuna aliyekamilika bali ni Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema mwenye
Kurehema, let him Rest In Peace

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent by Diaspora
 
'social reject' lazima atafight,ila soon atatulia na kujiona alivyo mjinga,.........….alivyokua anapiga wenzake na kuogopwa anadhania anaweza kuwaogopesha watu wote hata serikali….
 
Oil chafu ukiigusa unachafuka.

Nakupenda tu! Vile ulivyo nakupenda tu! Mimeno kama ngiri
Nakupenda tu! Vile ulivyo nakupenda tu! Pua kama ngumi.

Krii! Krii! Unatoa unga! Ukitema mate yanadundaaa!!
 
Kwani Ruge hana mabaya? Mbona tunataka kumfanya malaika? Halafu ubishani unavyokuwa ndo anasemwa hata kwa yale ambayo si yake sasa!

Mi nafkiri mwenyekujua mabaya yake aseme na mwenyekujua mazuri yake aseme.

Wasionekane wale wanaosema mabaya ni wabaya na hali huyu hakuwa malaika.
Anasemwa baba wa taifa semebuse Ruge jamani. Ingawa hawa wanaomsema wangeacha kwanza wenye majonzi wakaomboleza au hata angalau kumaliza msiba kwanza lakini huwezi kuzuia watu kusema hata siku moja.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Kabla ya hiyo ngoma miaka ya tisini mwishoni alitoa dude na album ya DEGE LA JESHI .... Hatari sana .... Inawezekana tunaongea na vijana waliozaliwa 2000s kama yuleeee aliyemmis Alicios eti alikuwa anamsikkia mama take akiimba
Mkuu hapo mwishoni sasa yaani kuna mtu alikuwa anamsikia mama yake akiimba ya bolingo hahaaaaa

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Aisee,kwa namna mnavyofunguka acha niendelee kusoma na ku-like coments zenu.....!!
 
Dudubaya amezidi kumshukia Ruge mutahaba na kusema kuwa alikuwa akiwanyonya wasanii aliokuwa anasema anawainua
Dudubaya ameendelea kusena kuwa Ruge ndio alisababisha Studio ya Bongo Records kuanguka kutokana na kutaka fedha kutoka kwa producer huyo na wasanii aliokuwa akiwarekodia

Amesema yupo tayari kwenda polisi ambako ameitwa kwenda kesho


Huyu jamaa ni FALAsi mkubwa
 
Kwani Ruge hana mabaya? Mbona tunataka kumfanya malaika? Halafu ubishani unavyokuwa ndo anasemwa hata kwa yale ambayo si yake sasa!

Mi nafkiri mwenyekujua mabaya yake aseme na mwenyekujua mazuri yake aseme.

Wasionekane wale wanaosema mabaya ni wabaya na hali huyu hakuwa malaika.
Anasemwa baba wa taifa semebuse Ruge jamani. Ingawa hawa wanaomsema wangeacha kwanza wenye majonzi wakaomboleza au hata angalau kumaliza msiba kwanza lakini huwezi kuzuia watu kusema hata siku moja.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
Poa. Na nyie tunawasubiri siku akifa Dudu baya mje hapa na mazuri yake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rest in peace kivipi.....mangapi kayafanya huyu mhaya yasiyo na chembe ata ya Huruma....alimtapeli mpaka Dada yetu Said a karoli...mm kiukweli naungana na Dudu Baya na na hii kwangu haijaanza leo....huyu MTU unadhani ni wangapi aliwaharibia maisha yako kupitia mziki....Ngwea,Hide,Sugu n.k
Kumbe wengi mnalaumu hata bila kuwa na ushahidi na mnachanganya mambo. Ruge alimtapeli wapi Saida wakati aliyemtapeli ni Felician yule wa FM studios aliye msainisha mkataba kuwa nyimbo ni mali yake.
 
Dead men tale no tales

Sent using Jamii Forums mobile app
Lady Jay Dee aliandika kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii. Ilikuwa siku ya Jumatano, tarehe moja mwaka 2013.

WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.

Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE
 
Back
Top Bottom