Dudubaya amjibu Mwakyembe, azidi kumshukia Ruge Mutahaba

Binafsi sijaona sheria yoyote iliyovunjwa kiasi cha Mh. Mwakyembe aamuru Dudubaya akamatwe. Si lazima kila mtu amsifie marehemu. Pamoja na hayo manzuri anayosifiwa Ruge, ni ukweli ulio wazi kuwa alikuwa na mapungufu mengine ambayo yaliwakwaza baadhi ya watu. Si sahihi Mwakyembe kutaka kuuaminisha umma kuwa Ruge alikuwa malaika. Rusisahau kuwa ni Ruge huyuhuyu amefariki akiwa amepiga marufuku nyimbo za wasanii wa Wasafi kupigwa Clouds media kisa tu hawa vijana wamegoma kunyonywa. Ni Ruge huyuhuyu ambae aliendesha kampeni kubwa ya kutaka kumpoteza Diamond kwenye ramani ya muziki. Watu kama kina Lady Jaydee wanayajua vinzuri machungu waliyosababishiwa na Ruge. Tufike mahali tuache kuwa wanafiki eti kisa mtu kafa.
 
Kunadilika unamaanisha nini mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kubadilika ni kuendana na soko la muziki kwa kuzingatia wakati na mazingira. Kubadilika kuanzia mavazi, beat, style ya kuimba, , video style na uandishi. Angalia nyimbo za prof Jay, Dully Sykes, Jmo na Lady Jdee za zamani na za sasa hivi ndiyo utaona utofauti.
Afande Sele, Dudu baya na Juma Nature ni wasanii walioshindwa kubadilika kimavazi, kuimba (anaimba style hiyo hiyo), maudhui ya nyimbo ni yale yale, beat ni zile zile. Unategemea nani atamsikiliza?
 
Unamkamata Dudu Baya unamuacha Cyprian Musiba...wenye akili lazma wakushangae......
 
tulimtakia kheri osama?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni heri huyo mnafki anamtakia mema maiti anamzika baada ya hapo ndio anazungumza aliyotendewa, kwanza hata hao viongozi wenu wa dini hawajawaambia kuhusu kumsengenya maiti? marehemu ni marehemu yake yanakua yameshaisha kwa wakati huo hata wewe umtukane vipi hakuna anachosikia wala hawezi kurudi kukujibu zaidi unaowaumiza ni wapendwa wake, unasupport ujinga wa Dudubaya unasahau kua maneno yake yanaumiza wengine,

Hebu vaa viatu vya wazazi wa Ruge au vya watoto wake, umefiwa na baba yako au mama yako au mke wako halafu kabla hujampumzisha unasikia mtu/watu wanamuongelea kwa mabaya je unafurahi?

Hakuna mtu ameambiwa ahuzunike lakini kama huna huzuni kwanini usikae tu kimya kuliko kuanza kumtusi na kumkejeli marehemu?
wewe katika maisha yako umefanya mazuri tu hakuna baya hata moja? ni nani aliyekamilika chini ya jua?

PS; Mwakyembe hajakurupuka ila watu wamemuomba aingilie kati kumdhibiti huyo Dudubaya japo kwa muda tu ili kumaliza msiba.
 
Huyo dada yako Saida mwenyewe kwa kinywa chake aliweka wazi kua Ruge sie aliyemuibia bali yule meneja wake wa zamani ndio alikua anachukua hati miliki za nyimbo zake,

Ngwear!? lol, kwa hiyo Ruge ndie alikua anamvutisha madawa au?

Haya wewe ungana na Dudubaya mfe mkazikwe ili muende kumsuta vizuri huyo marehemu, maana kupiga kelele huku ni kazi bure, Hawasikiiii.
 
Hivi ile hadithi ya Vinega.... iliishiaga wapi?
 
Huyo DUDU BAYA hajuwi NGUVU ZA MAREHEMU,,anadhani KUFA NI HIYARI,,,afanye afanyavyo WATAKUTANA TU NA RUGE tena soon huko KUZIMU,,,usimdhihaki MAITI,, hujuwi safari yako LINI,,na huko uendako ni WAPI,,na mwenyeji wako ni NANI , Nina uhakika NDANI YA SIKU 90 atapata MAJIBU.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikubaliani na wewe. Haijalishi mtu ni mzima au amefariki. Osama Bin Laden alipouawa kuna watu walisikitika na kuna waliofurahi. Sadam Husein naye hivyo hivyo. Mwalimu Nyerere naye hivyo hivyo. Japokuwa ki-moral siyo vizuri lakini hakuna sheria iliyokataza mtu kutoa maoni yake kuhusu mtu aliyefariki hasa kama alikuwa public figure. Kusema ukweli hata mimi siwezi kukaa na kuanza kufuruhia kifo cha binadam mwenzangu. Lakini hili halininyimi kuzungumza ukweli kwa mtu anayeonewa bila kosa kwa sababu ya kiongozi mkurupukaji kama Mwakyembe. Unajua hawa viongozi wetu hawana kazi za kufanya ndiyo maana unaona wanapishana pishana sehemu zenye mazishi na sherehe kama fisi kwenye mzoga. Dudubaya hakufanya kosa lolote. Yeye ametoa maoni yake juu ya marehemu. Kwani ni lazima asifu? Kama Familia ya marehemu inaona kuwa amekashifiwa basi ndiyo wanatakiwa kuchukuwa hatua na si wanasiasa wadandie mambo yasiyowahusu. Halafu mbaya zaidi Mwakyembe Wizara yake haina uhusiano kabisa na jambo aliloamuru lishughulikiwe! Kama anahusika basi ni ruksa waziri wa Kilimo kuamuru mtu anayemkashifu mkulima yeyote aliyefariki akamatwe!
 
Labda huyo felician ndo THE LATE RUGE πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Kumbe wengi mnalaumu hata bila kuwa na ushahidi na mnachanganya mambo. Ruge alimtapeli wapi Saida wakati aliyemtapeli ni Felician yule wa FM studios aliye msainisha mkataba kuwa nyimbo ni mali yake.
 

Mkuu hayo maneno umeyatoa wapi eti ufanye maovu duniani halafu tukusindikize kwa mema
Yaan uwe mwizi au uuwe watu halafu ukifa tukufanye uwe mwema hiko kitu hakuna
Mnavyoongea muwe mnafikiria kabla ya kusema
Mshahara wa dhambi ni umauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…