Duh! Huyu baba ni jeuri na katili sana. Tusaidiane kumkemea

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Huyu baba ana watoto wengi sana, lakini hajali kuwatunza. Anadai ana mapesa mengi na mali nyingi. Lakini watoto wake wakiugua hawaambii waende hospitali, badala yake anawahimiza waende kwa waganga wa kienyeji.

Amewaajiri watoto wake wamsaidie kufanya kazi zake lakini ajabu hawapi mshahara.

Watoto wake waliooa na kuolewa, akisikia wana migogoro katika ndoa, badala ya kuwashauri wayamalize kwa upendo, anawaambia wapeane talaka au watoane roho.

Huyu baba hapendi amani. Anafurahia kuona watoto wake wakigombana na majirani. Anachekelea wakitukanana na watu mitandaoni.

Watoto wake wakipata mafanikio, badala ya kuwashauri wawe wema na wanyenyekevu, anawatia moyo wajivune, wajisifu, na kuwaonea wengine.

Baadhi ya watoto wake wanapitia changamoto kubwa za maisha. Badala ya kuwasaidia wajikwamue, eti anawaambia wanywe sumu wafe au wajiue kwa kujinyonga!

Wengine anawasukuma wavute bangi au wanywe pombe eti ndio njia ya kusahau shida zao. Pamoja na ubaya huo wanaotendewa, watoto wake wanakubali tu kuendelea kukaa na baba huyu.
 
Ndugu yangu, huyu baba unamfahamu. Ni shetani. Na watoto wake ni wale wanaoishi katika dhambi bila kutubu. Biblia inasema:

"Ninyi ni watoto wa baba yenu, ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli, maana hamna kweli ndani yake. Anaposema uongo, yeye husema lugha yake ya asili kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.”
— Yohana 8:44

"Yeye atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo...”
— 1 Yohana 3:8
 
Shetani ni mwizi. Lengo lake ni kukuibia afya yako, furaha yako na mafanikio yako. Hana mema anayoweza kukupa. Yesu anamwita shetani mwizi. Na anaeleza kuwa kazi za shetani ni kuiba, kuua na kuangamiza.
“Mwizi huja ili aibe, aue na aangamize. Mimi nimekuja ili wapate uzima, kisha wawe nao tele.”
— Yohana 10:10

Leo tumepata ufunuo huu. Shetani ni baba wa uongo. Hatuna haja ya kumtii baba huyu mwovu. Yesu alikuja kutuondoa katika mikono ya mtesi huyu:
1 Yohana 3:8b
"...Mwana wa Mungu alikuja duniani kuziharibu kazi za Ibilisi.”
 
Tumpinge huyu baba wa uongo. Tusimame pamoja, tumkemee huyu baba mwovu.
"Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia." —Yakobo 4:7

Tumuombe Mungu atupe macho ya rohoni, tuzitambue hila na mitego ya shetani na kukataa kazi za huyu baba dhalimu.

Tusikubali kamwe kuwa watoto wake tena. Tugeuke tumfuate Yesu.

Jihoji sasa, jichunguze. Je uko chini ya baba yupi? Kama unatenda dhambi ujue uko chini ya baba mkatili huyu(shetani). Leo ni siku yako ya kumkataa na kuachana naye. Tubu dhambi zako, na kumpokea Yesu leo, uanze kuishi chini ya Baba wa kweli, ambaye ni Mungu wa mbinguni.

Ukikataa ushauri huu, nakusikitikia kwakuwa shetani atakufanya utumbukie katika moto wa milele.
 
Shetani ni mwizi. Lengo lake ni kukuibia afya yako, furaha yako na mafanikio yako. Hana mema anayoweza kukupa. Yesu anamwita shetani mwizi. Na anaeleza kuwa kazi za shetani ni kuiba, kuua na kuangamiza.
“Mwizi huja ili aibe, aue na aangamize. Mimi nimekuja ili wapate uzima, kisha wawe nao tele.”
— Yohana 10:10

Leo tumepata ufunuo huu. Shetani ni baba wa uongo. Hatuna haja ya kumtii baba huyu mwovu. Yesu alikuja kutuondoa katika mikono ya mtesi huyu:
1 Yohana 3:8b
"...Mwana wa Mungu alikuja duniani kuziharibu kazi za Ibilisi.”
CCM Ni mashetani
 
CCM Ni mashetani
balibabambonahi jifunze kuuzuia ulimi wako usinene mabaya (1 Petro 3:10-12).
Halafu inakuwaje mambo ya siasa unayaleta hapa? Ukipigwa 'bani' utamlaumu nani?

Anyway, nadhani pia haya Maandiko hujawahi kuyasoma:
Warumi 13:1-7 BHN
"Kila mtu anapaswa kuwatii wenye mamlaka katika serikali; maana mamlaka yote hutoka kwa Mungu; nao wenye mamlaka wamewekwa na Mungu. Anayepinga mamlaka ya viongozi anapinga agizo la Mungu; nao wafanyao hivyo wanajiletea hukumu wenyewe. Maana, watawala hawasababishi hofu kwa watu wema, ila kwa watu wabaya. Basi, wataka usimwogope mtu mwenye mamlaka? Fanya mema naye atakusifu; maana yeye ni mtumishi wa Mungu anayefanya kazi kwa faida yako. Lakini ukifanya mabaya, basi, huna budi kumwogopa, maana anao kweli uwezo wa kuadhibu. Yeye ni mtumishi wa Mungu, kuwaonesha ghadhabu yake wale watendao maovu. Kwa hiyo ni lazima kuwatii wenye mamlaka, si tu kwa sababu ya kuogopa ghadhabu ya Mungu, bali pia kwa sababu dhamiri inadai hivyo. Kwa sababu hiyohiyo nyinyi hulipa kodi; maana viongozi hao humtumikia Mungu ikiwa wanatimiza wajibu wao. Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliye heshima, heshima."
 
Kiongozi ambaye huua wake naye hutoka kwa Mungu? Amri ya Mungu inaamuru "usiue" wewe unaua,je umetoka kwa Mungu? No Reform No election.CCM ni mashetani
 
balibabambonahi jifunze kuuzuia ulimi wako usinene mabaya (1 Petro 3:10-12).
Halafu inakuwaje mambo ya siasa unayaleta hapa? Ukipigwa 'bani' utamlaumu nani?

Anyway, nadhani pia haya Maandiko hujawahi kuyasoma:
Warumi 13:1-7 BHN
"Kila mtu anapaswa kuwatii wenye mamlaka katika serikali; maana mamlaka yote hutoka kwa Mungu; nao wenye mamlaka wamewekwa na Mungu. Anayepinga mamlaka ya viongozi anapinga agizo la Mungu; nao wafanyao hivyo wanajiletea hukumu wenyewe. Maana, watawala hawasababishi hofu kwa watu wema, ila kwa watu wabaya. Basi, wataka usimwogope mtu mwenye mamlaka? Fanya mema naye atakusifu; maana yeye ni mtumishi wa Mungu anayefanya kazi kwa faida yako. Lakini ukifanya mabaya, basi, huna budi kumwogopa, maana anao kweli uwezo wa kuadhibu. Yeye ni mtumishi wa Mungu, kuwaonesha ghadhabu yake wale watendao maovu. Kwa hiyo ni lazima kuwatii wenye mamlaka, si tu kwa sababu ya kuogopa ghadhabu ya Mungu, bali pia kwa sababu dhamiri inadai hivyo. Kwa sababu hiyohiyo nyinyi hulipa kodi; maana viongozi hao humtumikia Mungu ikiwa wanatimiza wajibu wao. Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliye heshima, heshima."
Na mtu wa kulindwa uhai wake alindwe.We submitted our freedoms in return of protection.What should we do when the sorvereign not only does not protect our freedoms and property but she bocomes a monister against us?
 
Back
Top Bottom