Duh mwamba kakutwa kiwili wili tu, kichwa hakipo!

Duh mwamba kakutwa kiwili wili tu, kichwa hakipo!

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
11,191
Reaction score
35,870
Mnamo Novemba 2020, Robert Kabera alikimbilia Uganda. Mamlaka ya kijeshi ya Rwanda ilitangaza uchunguzi kuhusu madai kwamba alimnyanyasa kingono mwanafamilia wa miaka 15.

Kabera alikana mashtaka hayo, akayaita ya uwongo na ya kisiasa. Aliomba hifadhi, akitoa mfano wa mateso ya kisiasa na vitisho, na wakati mwingine alipewa hadhi ya ukimbizi akiwa na ulinzi wa polisi.

Akiwa uhamishoni, akawa mkosoaji wa serikali ya Kagame kupitia muziki na hasa chaneli yake ya YouTube.

Mnamo au karibu na Oktoba 16-17, 2026, alipokuwa katika eneo la Luwala la Wilaya ya Mpigi (karibu na Kampala), ambapo alikuwa akisimamia ujenzi wa nyumba, aliuawa na kukatwa kichwa.

Wakazi wa eneo hilo waligundua mwili wake; kichwa chake hakikupatikana. Polisi wa Uganda walithibitisha mauaji hayo na kufungua uchunguzi; jamaa (pamoja na kaka yake) walimtambua.

Mjane wake, Jeanne d'Arc Rwigema Uwizeye, alionyesha hofu kwa usalama wa familia hiyo. Serikali ya Rwanda haikuwa imetoa maoni hadharani kuhusu ripoti za awali.

Makundi ya upinzani ya uhamishoni yalitaka uchunguzi kamili, yakibainisha mtindo wa vurugu dhidi ya wakosoaji wa Rwanda walioko nje ya nchi. Hakuna nia rasmi au wahusika waliothibitishwa hadharani.
 
Paul Kagame mwanaume huwezi kumchezea. Tanzania tunahitaji Rais km bw. PK
 
nimekumbuka mbalisana vita mkwawa na mdogowake na mjerumani

mkwawa mwanzo alitaka ukiua adui kata kichwa akaone ukiua watano hakikisha vichwa idadi hiyo umempelekea aone ,ndo chimbuko la kijiji moja kinaitwa lunda matwe(matwe (kihehe) kiswahili vichwa na lunda(kukusanyapamoja) hivyo eneo hilo ndipo palikusanywa vichwa hivyo

wanajeshi wakalalamika mzigo unakua mkubwa sana ,wanakabdilishiwa kwamba ukiua adui kata kende weka kwenye uma wala mishikaki mnaelewa

Tafsiri ya huyu jamaa kutenganishwa mwili na kichwa aliyewatuma aliwapa onyo wasipoenda na kichwa inawageukia
 
Kosa lake alikimbilia uganda, uganda ni rwanda tu bora hata angekimbilia Tanzania akakae hata singida huko, mpaka wauaji wake wafike singida watakuwa wamedakwa njiani na hawatoki kurudi kwao rwanda
Kagame hana mchezo. Po pote pale duniani anakudabua. Afrika Kusini huko huwa anawadabua tu eti wengine wanajirusha kutoka ghorofa ya nane. Modus Operandi (MO) kama ya Putin. Oligarchs wengi sana wameshajirusha kutoka maghorofani.

US huko alikuwepo jamaa mtata sana anaitwa Prof. Andre Kimenyi. PK alipita naye naye kimya kimya. Hata Mchungaji Mtikila huyu wa kwetu naye alipitiwa na MOSSAD ya Rwanda. PK akikutaka huna pa kukimbilia. Akina Mange, Hilda Newton na Sarungi hawa ingekuwa PK aaaah zamaniiii angekuwa keshamalizana nao! Super dangerous!
 
Kagame hana mchezo. Po pote pale duniani anakudabua. Afrika Kusini huko huwa anawadabua tu eti wengine wanajirusha kutoka ghorofa ya nane. Modus Operandi (MO) kama ya Putin . US huko alikuwepo jamaa mtata sana anaitwa Prof. Andre Kimenyi. Naye alipita naye kimya kimya. Hata Mchungaji Mtikila huyu wa kwetu naye alipitiwa na MOSSAD ya Rwanda. PK akikutaka huna pa kukimbilia. Akina Mange, Hilda Newton na Sarungi hawa ingekuwa PK aaaah zamaniiii angekuwa keshamalizana nao! Super dangerous!
Mbona kama unasifia uharamia huu??
 
Unajificha Uganda utakuwa Una wazimu kabisa, ukienda hata South Tu Hapo lazima uliwe kichwa....Tatizo ukiwa na historia chafu halafu Huna cha Ku offer yaani Huna information za maana basi hakuna nchi makini itakukubali, ww utaishia humu humu Burundi, Kenya na mwisho Jua utakufa Tu Otherwise funga bakuli lako.
 
Kagame hana mchezo. Po pote pale duniani anakudabua. Afrika Kusini huko huwa anawadabua tu eti wengine wanajirusha kutoka ghorofa ya nane. Modus Operandi (MO) kama ya Putin. Oligarchs wengi sana wameshajirusha kutoka maghorofani.

US huko alikuwepo jamaa mtata sana anaitwa Prof. Andre Kimenyi. PK alipita naye naye kimya kimya. Hata Mchungaji Mtikila huyu wa kwetu naye alipitiwa na MOSSAD ya Rwanda. PK akikutaka huna pa kukimbilia. Akina Mange, Hilda Newton na Sarungi hawa ingekuwa PK aaaah zamaniiii angekuwa keshamalizana nao! Super dangerous!
Mtikila alikuwa na issue gani na Rwanda mkuu?
 
Mtikila alikuwa na issue gani na Rwanda mkuu?
Google Mtikila vs Kagame au Mtikila vs. Rwanda....

Wakosoaji wa serikali ya Rwanda kila wanapokimbilia hawapo salama, huwindwa na kumalizwa.

Kote walipokimbilia kama S.A jamaa wanawamalizia hotelini.

Yupo aliyewahi kuwa mwanajeshi wa RPF aliyekimbilia S.A alikiepuka kifo kama bahati tu, jamaa walipojua hoteli aliyokuwa akiishi wakapanga kummalizia chumbani anapolala.

Bahati yake siku ya tukio, kilichomuokoa ni kutoka kwake chumbani mapema kwenda chini akanywe chai, wakati huo ndio jamaa wa Rwanda wakazama chumbani kwake na kumkosa, wakapekua kote hawakumpata.

Na wakishazama ndani wakamkuta mbaya wao hawachukui chochote toka kwake zaidi ya roho yake, ni risasi moja tu ya kichwa, au kifua, kisha wanaondoka zao.

Naamini ni baadhi ya nchi za ulaya magharibi na USA pekee ndio zenye uwezo mzuri kuwalinda hao jamaa, lakini nje ya hapo hawako salama.

Hata hapa kwetu, wote waliojaribu kuonekana tishio kwa serikali ya Rwanda hawakuachwa salama,kuanzia marehemu Mvungi, Mtikila, na baadhi ya wanajeshi waliokuwa jeshi la RPF, wote walimalizwa.
 
Back
Top Bottom