Duh, walokole mnatuchosha - mnatuboa na mada zenu!

Duh, walokole mnatuchosha - mnatuboa na mada zenu!

Atakaye abudu anachojua yeye kuwa ndiye mungu anakuwa na lengo la kuudhi? Ustaadh akija kuweka maspika hapo kwako kila ijumaa anaita majini kwa kiarabu zitakuwa si kelele sababu hana lengo la kuudhi?

Mungu unayemuabudu wewe si MUNGU wa imani ya kila mtu.

Ni kelele. Kelele ni kelele hata zisiposemwa.
Ndio sababu nimehoji kwanini watu wanakuwa biased? Mashabiki wa mpira uwanjani na walevi kwenye baa za mitaani wakipiga kelele, hakuna anayelalamika, lakini walokole wakiimba nyimbo za kumsifu Mungu wanaambiwa wanapiga kelele. Kulikoni?
 
Kama walioacha uzinzi, umalaya, ufisadi, ujambazi, rushwa, uuaji, matusi, ulaghai, uonevu, baada ya kumwamini Yesu, wamepagawishwa; je, wanaofanya matendo hayo maovu tuwaiteje?
Ungetafakari kwanza hilo, usingewabeza wanaomcha Mungu na kutenda yaliyo safi na ya haki.
Kuendekeza "dini" na udini sio kumcha Mungu.
 
Ndio sababu nimehoji kwanini watu wanakuwa biased? Mashabiki wa mpira uwanjani na walevi kwenye baa za mitaani wakipiga kelele, hakuna anayelalamika, lakini walokole wakiimba nyimbo za kumsifu Mungu wanaambiwa wanapiga kelele. Kulikoni?
Kutolalamika kwao haibadilishi kuwa ni makelele.
 
Mtu anakutahadharisha usiende motoni unamuona kero. Haya, kuna siku habari hizi njema hamtazisikia tena. Yesu akija atawanyakua watakatifu tu na neema itafungwa. Wenye dhambi tu ndo watabaki duniani wakiteseka. Mtatamani kuwasikia walokole lakini hamtawaona tena. Itakuwa kilio na kusaga meno.
cocastic tubu dhambi zako na umpokee Yesu, kabla wakati huo haujafika.
Mkuu samahani. Huko mbinguni watakuwa wanafanya kazi gani ?
 
Back
Top Bottom