Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

sababu dawa ziuzwazo ni kama 160.

Red Giant heshima mbele sana mkuu,

Hapo unamaanisha nini mkuu, je ni aina ya dawa ambazo ndiyo zenye matumizi kwa wingi?. na je madawa yanapatikana wapi kama ukiamua kujikita kwenye huduma hii ili kusaidia ndugu zetu walio pembezoni.

Na nini zaidi mtoa huduma anahitaji kujua kabla ya kuanzisha huduma hii?
 
Hizi dawa wameweka zile ambazo matumizi kwa wingi kama za malaria, maumivu ,za fangasi za kupaka, antibiotic kama fragyl na amoxicillin na dawa za minyoo. madawa unapata kwenye famasi za jumla.

Mambo ya kuzingatia ni kuwa na mtu aliyepitia mafunzo ya dawa muhimu na kuhakikisha eneo lako linaruhusiwa kuwa na DLDM.
 
Nasikia biashara hii inalipa sana hasa ukiiweka eneo ambalo hakuna ushindani mkubwa hasa vijijini ambako unakuta hakuna huduma za afya za karibu
 
Mimi sina uzoefu sana na madawa ila Tuna system kwa ajili ya pharmacy. Katika kuwasaidia wateja kuingiza stock na kuseti system naona. Ukiwa na eneo zuri biashara inalipa sana maana huwa naangalia bei ya jumla na jinsi tunavyo Uziwa reja reja tofauti Ni kubwa. Pia mwenye duka mmoja alishaniambia kuwa biashara Ni Nzuri sana
 
Mimi nimethubutu nimeanzisha kijijini kisumba manispaa s/wanga ila mtoa dawa sijampata bado
 
hapo kidogo pagumu. inatakiwa uwe na chati cha mfamasia wa kusimammia utayemlipa kama 1m kwa mwezi, uwe na fremu ya vyumba viwili,, AC na friji. pia jamaa wanakaagua eneo kama linafaa na ukijenga pia wanakuja kucheki ili wakupe kibali.

Hayo mengine si neno sana, lakin hapo kwa Mfamasia, si unaweza kukubaliana naye tu ukatumia cheti chake halafu unamlipa part time anakuwa anakuja mara moja moja, au anatakiwa kuwa full time?
 
Hayo mengine si neno sana, lakin hapo kwa Mfamasia, si unaweza kukubaliana naye tu ukatumia cheti chake halafu unamlipa part time anakuwa anakuja mara moja moja, au anatakiwa kuwa full time?
Kumuweka mfamasia fulltime ujipange kuanzia 2.5m. mkataba wa usimamizi unamtaka kuhudhuria 15hrs kwa wiki.
 
kumuweka mfamasia fulltime ujipange kuanzia 2.5m. mkataba wa usimamizi unamtaka kuhudhuria 15hrs kwa wiki.

Mimi sijaelewa vizuri hapa. Huyu mfamasia anasimamia nini hasa. Mtaani kuna maduka ya dawa madogo sidhani kama watakuwa na uwezo wa kuzalisha faida ya kulipa kiasi hicho kwa mfamasia.
 
Mkuu kama upo dsm na unataka kuweka medical store! subiri kwanza maana tarehe 31 mwezi huu wamiliki wote wa dawa baridi watakuwa na kikao na waziri wa afya ili kujuwa atma yao, maana yanatakiwa yafungwe yote au yaruhusiwe offical!!!

Kama yakikatazwa lazima uwe na mfamasia ili uweze kufunguwa duka, wakijakubali hakuna aja ya mfamasia maana ukiweka mfamasia utapata hasara.
Wafamasia wapo wengi, kuna wa part time ni lakin 7-9 kwa mwezi na mwezi mzima anaweza asije.
 
Habari za wakati huu.
Naomba fahamu taratibu za kufungua duka la dawa za binadamu.
Karibuni kwa michango mbalimbali ndugu zangu.
 
Ili kufungua DUKA LA DAWA MUHIMU masharti ni kama ifuatavyo;

Endapo duka linafunguliwa maeneo ya Kijijini linatakiwa kuwa umbali wa Mita 200 kutoka duka lingine, endapo lipo Mjini
umbali ni Mita 300.

Mahitaji
- Uwe na vyumba viwili Chumba cha kwanza (duka lenyewe): Ukubwa ft 10x10 urefu ft 9 na Chumba cha pili (stoo): ft 4x8 urefu ft9
- Mmilikii na muuzaji wapate mafunzo ya TFDA (wasiliana na halmashauri husika ili kujua ratiba za mafunzo)
- Jaza fomu za maombi ambazo zinapatikana wilayani; zinapitishwa kitongoji, kata, wilaya.

ANGALIZO: KAMA UNATAKA KUANZISHA PHARMACY INA MASHARTI TOFAUTI NA DUKA LA DAWA MUHIMU. FIKA OFISI ZA WILAYA ONANA NA MFAMASIA WA WILAYA AKUPE DETAILS ZA KUTOSHA
 
Asante kwa maelezo mazuri!,Yametusaidia wengi hapa.
 
Duka la dawa baridi alihitaji mfamasia,linahitaji m2 mwenye dispensing certificate n mwenye duka anatakiwa apitie course ya addo owner for a month
mtaji unaweza ukawa mil 5 for starting coz inabidi ulipie registration kwa pharmacy council kwa maelezo zaidi cheki website ya pharmacy council ili ujue full description ya addo.
 
Back
Top Bottom