Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Hivi wachangiaji wamechangia mawazo ya duka dogo la dawa au dispensery? maana kuna maduka yana mtaji wa laki mbili, muuzaji hata hajasomea, au vigezo havijali ukubwa wa huduma?
 
duka la dawa baridi alihitaji mfamasia,linahitaji m2 mwenye dispensing certificate n mwenye duka anatakiwa apitie course ya addo owner for a month
mtaji unaweza ukawa mil 5 for starting coz inabidi ulipie registration kwa pharmacy council kwa maelezo zaidi cheki website ya pharmacy council ili ujue full description ya addo

Asante mkuu kwa taarifa.

Sasa hapa Red Giant hembu mtupe ufafanuzi wa hizi Lugha.
Maana haya maduka yoote yanaandikwa Pharmacy
Sasa Hapa naona kwamba Duka la dawa Baridi halihitaji kuwa na mfamasia na hapo juu naona linatakiwa kuwa na mfamasia.

Hembu tuwekeni sawa hapa
 
Asante mkuu kwa taarifa.

Sasa hapa Red Giant hembu mtupe ufafanuzi wa hizi Lugha.
Maana haya maduka yoote yanaandikwa Pharmacy
Sasa Hapa naona kwamba Duka la dawa Baridi halihitaji kuwa na mfamasia na hapo juu naona linatakiwa kuwa na mfamasia.

Hembu tuwekeni sawa hapa

Kuna tofauti kati ya duka la dawa na pharmacy,pharmacy lazima uwe na frame yenye AC na liwe vyumba 2 na lazima kuwe na cheti cha mfamasia while duka la dawa sio lazima kuwa na AC na hauhitaji cheti cha mfamasia ni kibali kutoka TFDA na kuna dawa zinauzwa pharmacy tu duka la dawa hawaruhusiwi kuuza
 
Sio lazima umuweke mfamasia chukua mtu aliyesoma ado mlipe laki mbili au tatu kwa mwezi inatosha huyo wa milion achana nae unaweza kula hasara tu
 
Sio lazima umuweke mfamasia chukua mtu aliyesoma ado mlipe laki mbili au tatu kwa mwezi inatosha huyo wa milion achana nae unaweza kula hasara tu

Ukitaka kufungua pharmacy lazima uwe na mfamasia ambaye ataweka cheti chake hii hugharimu laki tisa mpaka 1.3.

Maduka ya dawa baridi haihitaji mfamasia
 
Mimi mwenyewe nataka kufungua duka la dawa baridi za wanadamu ila sasa kikwazo ni madawa yenyewe yanayohitajika naomba nitumie hayo madawa ambayo naweza kuweka dukani kwangu kwa pm pls mkuu
sio lazima ila kunakozi ya 40 days hutolewa kwa msimu na TFDA. hiyo ni lazima.
 
Mimi Najua Pharmacy Na Ninaweza Kumsaidia Ama Kumshauri Mtu Yeyote Kwa Maongezi Kupitia Simu Ama Ana Kwa Ana Akitaka Kufanya Biashara Ya Dawa Za Binadamu Vizuri. Atakayehitaji Tuwasiliane Tu Maana Kujibu Mara Kwa Mara Hapa Huwa Nashindwa
0784082847
0659528724
Nipo Temeke, Dar Es Salaam
Karibu Nikusaidie
 
Heshima zenu wakuu..
Nina capital ya 4mil nimeplan kufungua duka la madawa muhimu ya binadamu mkoani Dar es salaam..
Kwa ambaye ameshawahi kufanya naomba anielekeze procedures za kufuata ili kupata vibali!!
 
Nenda ofisi za mfamasia wa wilaya. Hapo utapata utaratibu wote.
 
Heshima zenu wakuu..
Nina capital ya 4mil nimeplan kufungua duka la madawa muhimu ya binadamu mkoani Dar es salaam..
Kwa ambaye ameshawahi kufanya naomba anielekeze procedures za kufuata ili kupata vibali!!
Hakikisha unachet cha ADDO cha umiliki na Cheti cha ADDO cha mtoa dawa.
 
Ellyson

hv vibali vyote vinalipiwa gharama kiasi gani!? je baada ya hapo nitatakiwa kwenda TRA kwa ajili ya leseni ya biashara!?
 
Last edited by a moderator:
Kwanza lazima mfamasia na timu yake wakague na kulipitisha hapo ndiyo utaanza mambo mengine ya tra na leseni. Kibali kwa sasa kinalipiwa 50,000=
 
Unaitaji uhuzulie mafunzo ya Ado, mmiliki na muuzaji wako.hizo hutolewa kila mwaka.kupata habr nenda ofisi za mfamasia wa wilaya iliyo karibu na unakotaka kufungua.atakupa maelekezo ya kina na ndo yye anatoa lesen ya biashara yako.Ni rais na faidi ipo
 
Habari wakuu!!

Kama wafanyavyo wengine kwenye hii Forum nimeona nami leo nije kwa maelezo kifupi namna mtu anaweza kuanzisha hatua kwa hatua biashara ya Dawa au kama inavyojulikana na wengi yaani Retail Pharmacy.

Lakini kabla sijaenda moja kwa moja kwenye hatua hizo, ni muhimu basi kuweza kujua Pharmacy ni kitu gani hasa?
Kwa mujibu wa sheria ya Famasi au PHARMACY ACT, Pharmacy ni sehemu ambayo chini ya usimamizi wa mfamasia ambaye amepewa dhamana ya uangalizi wa shughuli zake (Pharmaceutical services) itauza au kununua dawa zilizo kwenye makundi ya moto au Baridi nikiwa na maana dawa zinazohitaji uangalizi au prescription na dawa za kawaida au Over the counter medicines (OTC Medicines).

Watu wengi huchanganya kati ya Duka la dawa Muhimu (DLDM) na Pharmacy. Hivi ni vitu viwili tofauti na utofauti wake unakuja kuwa DUKA LA DAWA MUHIMU au kama yanavyojulikana kitaalamu (Accredited Drug Dispensing Outlets au ADDO) hayaruhusiwi kuuza baadhi ya dawa za moto kisheria, na ukikuta wanauza basi ujue ni kinyume na Sheria na Taratibu za Pharmacy Act na ni vyema ukatoa taarifa kwa vyombo husika au Baraza la Wafamasia.

Mtu yoyote anaweza kumiliki Famasi hata kama hana Taaluma ya Ufamasia ila atalazimika kumuajiri mfamasia kwa Part time au Full time na malipo mara nyingi hutegemea na makubaliano kati ya mmiliki na Mfamasia mwenyewe. Wengine huamua kuingia partnerships na wengine huamua kuwa huru kwa kuajiriwa kwa muda.

Hatua Ya Kwanza

Kama zilivyo biashara zingine ni vyema kwanza ukafanya utafiti binafsi kwa kuangalia Location, economic status ya watu wanaozunguka eneo hilo na ushindani wa kibiashara au kama kuna Famasi maeneo hayo ambayo yanaweza kukuletea ushindani mkubwa na kushindwa kufanikiwa kibiashara.

Baada ya kufanya hayo na kujiridhisha na eneo husika unalotaka kutoa huduma hiyo, mfuate mfamasia wa wilaya wa eneno hilo ili uweze kumweleza dhumuni lako na kukupa maelezo kama kuna maombi mengine yoyote ya uanzishwaji wa Famasi yaliyokwisha pelekwa kwenye eneo ulilochagua kufanya huduma hiyo.

Wengi huwa wanakurupuka kwa kulipia chumba cha biashara na baadae huingia hasara kwani wanakuta kuna mtu teyari kwenye eneo hilo ameshapeleka maombi ya kuanzisha Famasi kama yeye. Kisheria kuna umbali ambao lazima uwepo kati ya Famasi na Famasi na ili usiingie hasara hiyo ni vyema kabla hujalipia chumba cha biashara basi onana na mfamasia wa wilaya kwanza.

Ukubwa wa chumba cha Biashara pia ni kitu muhimu sana kuzingatia kwenye Biashara hii. Kama utataka kufungua Famasi ya rejareja, basi utatakiwa kuwa na chuma kisichopungua 25 meter square ili uweze kukigawa na kupata chumba cha mbele yaani counter, chumba cha kutolea dawa au Dispensing room na stoo ya dawa.

Hatua Ya Pili

Baada ya kuhakikisha eneo lako la biashara ni salama na chumba chako kina ukubwa unaotakiwa kadiri mfamasia wa wilaya alivyokushauri, basi lipia chumba chako na anza marekebisho kama utakavyoelekezwa na mfamasia wa wilaya ili pawe na muonekano wa kisasa na kuvutia kwa kuweka hizo partitioning kwa ajili ya chumba cha mbele, kutolea dawa na stoo! Wengi hupendelea kuweka partitioning za Aluminium lakini hata ceiling board na gypsum hukubalika na huokoa gharama.

Hakikisha hicho chumba kina mzunguko mzuri wa hewa kwa kuweka feni na Air conditioner! Sheria pia inataka kuwe na vigae chini ili kurahisisha usafi na kuzua maambukizi ya magonjwa au vumbi ambayo hupunguza nguvu za dawa au kuharibika. Pia unaweza kuweka mbwembwe zingine za kibiashara ili kuvutia wateja wako kama rolling adverts na vioo ukutani.

Hatua Ya Tatu

Ukishamaliza kufanya marekebisho yako na kama ulivyoshauriwa na Mfamasia wa Wilaya, unatakiwa kumwita ili aje kukukagua Jengo (Premise Inspection) na kukuandikia kibali ambacho utalazimika kulipia hizo form za ukaguzi na maombi ya kibali ambayo yakishajazwa hutumwa baraza la Famasi uweze kupewa leseni na ruhusa ya kuanzisha biashara yako (Licence and Permitt). Kwa kawaida hapa huwa kuna gharama za kulipia na gharama huongezeka kama mmiliki sio mfamasia, hulazimika kulipia professional fee ya Mwaka. Hii hatua huweza kucuhukua hata miezi mitatu au sita kukamilika au kupata kibali chako kwani Baraza la Wafamasia lazima likae vikao kupitia maombi yako.

Tukumbuke pia hii biashara ni tofauti na biashara zingine kwani ni huduma pia kwa jamii na ni ya kitaalamu. Mikataba ya ajira ya wataalamu kama Dispensing Nurse,Pharmaceutical Technician au Mfamasia wako lazima iwepo wakati wa ukaguzi na ujazaji wa form za leseni za Baraza la Wafamasia. Hii ina maana kwamba kama huna Medical background kwenye dawa utalazimika kuajiri hao watu muhimu ambao ni kati ya mfamasia au technician ili aweze kukusaidia kutekeleza majukumu ya utoaji huduma za dawa.

Hatua Ya Nne

Wengi wakishakaguliwa hukurupuka kwa kwenda kununua mzigo (Dawa) na kuziweka au kuzipanga stoo)!Cha msingi hutakiwi kuwa na papara, subiri vibali vyote vya baraza la Famasi umepata na leseni ya biashara kutoka kwa Afisa Biashara wa wilaya ndio ujihakikishie kuanza kununua dawa kutoka kwa whole salers au distributors.

Hatua Ya Tano

Hatua hii ni ya kufungua Famasi yako na teyari kwa kuanza huduma, kumbuka siku zote biashara ni ubunifu hivyo basi hakikisha wahudumu wako ni competent na wana ueledi wa kutosha kwenye kutoa maelezo sahihi ya dawa na matumizi yake!Hakikisha pia wahudumu muda wote ni wenye lugha nzuri kwa wateja wa rika zote na tabasamu muda wote!
Kama unajiweza kifedha ni vyema wahudumu wakawa na uniforms au makoti ya kitabibu(Medical coat) ili kuonekana professional zaidi na kuwavutia wateja.

Inashauriwa pia uwe na Water dispenser ili wateja wenye uhitaji wa lazima kuanza kunywa dawa papo hapo waweze kupata huduma hiyo bila kusahahu kipimo cha uzito kiwepo kuwawezesha wahudumu kutoa dozi za dawa sahihi kwa wateja hasa watoto chini ya miaka mitano.

Cha Kuzingatia

Kama zilivyo biashara zingine ni muhimu kujiandaa kwa fedha japo si lazima kiasi kikubwa (At least 20M), na biashara hii utalazimika kumuajiri mfamasia ili akusimamie Famasi yako na kwa sasa wafamasia hutoza si chini ya Tsh. 1,000,000/ kwa mwezi na huyo ni wa part time tu, hivyo basi ni vyema ukawa na kiasi cha kuanzia cha kutosha kwa ajili ya kumlipa advance hata ya miezi sita kabla biashara yako haija stabilize au kuzoeleka na kufanya vizuri.

Kwa sasa pia kuna makampuni au Distributors wanaokopesha dawa kwa wateja wake, hivyo unaweza pia kujihusiha na haya makampuni ili waweze kukukopesha dawa na kulipia baadae.

Ni hayo tu machache niliyoona niwashirikishe, wengi wana pesa lakini hawajui waifanyie nini, hivyo basi kama umeelewa vizuri biashara hii kwa maelezo hapo juu nakushukuru na nikutakie upambanaji wenye kheri..Pamoja sana!
 
Safi sana kwa mwongozo wako mzuri....pia ni vizuri mhusika akafanya utafiti wa mahali atakapokuwa akichukulia mzigo wa kuuza. awajue wazabuni na pia aanzishe mahusiano ya kibiashara ya karibu.
 
Back
Top Bottom