TIPS: JINSI YA KUANZISHA BIASHARA YA PHARMACY KWA UFUPI by
sonaderm,
Nov 23, 2015.
Maelezo kifupi namna mtu anaweza kuanzisha hatua kwa hatua biashara ya Dawa au kama inavyojulikana na wengi yaani Retail Pharmacy.
Lakini kabla sijaenda moja kwa moja kwenye hatua hizo, ni muhimu basi kuweza kujua Pharmacy ni kitu gani hasa?
Kwa mujibu wa sheria ya Famasi au PHARMACY ACT, Pharmacy ni sehemu ambayo chini ya usimamizi wa mfamasia ambaye amepewa dhamana ya uangalizi wa shughuli zake (Pharmaceutical services) itauza au kununua dawa zilizo kwenye makundi ya moto au Baridi nikiwa na maana dawa zinazohitaji uangalizi au prescription na dawa za kawaida au Over the counter medicines (OTC Medicines).
Watu wengi huchanganya kati ya Duka la dawa Muhimu (DLDM) na Pharmacy. Hivi ni vitu viwili tofauti na utofauti wake unakuja kuwa DUKA LA DAWA MUHIMU au kama yanavyojulikana kitaalamu (Accredited Drug Dispensing Outlets au ADDO) hayaruhusiwi kuuza baadhi ya dawa za moto kisheria, na ukikuta wanauza basi ujue ni kinyume na Sheria na Taratibu za Pharmacy Act na ni vyema ukatoa taarifa kwa vyombo husika au Baraza la Wafamasia.
Mtu yoyote anaweza kumiliki Famasi hata kama hana Taaluma ya Ufamasia ila atalazimika kumuajiri mfamasia kwa Part time au Full time na malipo mara nyingi hutegemea na makubaliano kati ya mmiliki na Mfamasia mwenyewe. Wengine huamua kuingia partnerships na wengine huamua kuwa huru kwa kuajiriwa kwa muda.
Hatua Ya Kwanza
Kama zilivyo biashara zingine ni vyema kwanza ukafanya utafiti binafsi kwa kuangalia
Location, economic status ya watu wanaozunguka eneo hilo na
ushindani wa kibiashara au kama kuna Famasi maeneo hayo ambayo yanaweza kukuletea ushindani mkubwa na kushindwa kufanikiwa kibiashara.
Baada ya kufanya hayo na kujiridhisha na eneo husika unalotaka kutoa huduma hiyo, mfuate mfamasia wa wilaya wa eneno hilo ili uweze kumweleza dhumuni lako na kukupa maelezo kama kuna maombi mengine yoyote ya uanzishwaji wa Famasi yaliyokwisha pelekwa kwenye eneo ulilochagua kufanya huduma hiyo.
Wengi huwa wanakurupuka kwa kulipia chumba cha biashara na baadae huingia hasara kwani wanakuta kuna mtu teyari kwenye eneo hilo ameshapeleka maombi ya kuanzisha Famasi kama yeye. Kisheria kuna umbali ambao lazima uwepo kati ya Famasi na Famasi na ili usiingie hasara hiyo ni vyema kabla hujalipia chumba cha biashara basi onana na mfamasia wa wilaya kwanza.
Ukubwa wa chumba cha Biashara pia ni kitu muhimu sana kuzingatia kwenye Biashara hii. Kama utataka kufungua Famasi ya rejareja, basi utatakiwa kuwa na chuma kisichopungua 25 meter square ili uweze kukigawa na kupata chumba cha mbele yaani counter, chumba cha kutolea dawa au Dispensing room na stoo ya dawa.
Hatua Ya Pili
Baada ya kuhakikisha eneo lako la biashara ni salama na chumba chako kina ukubwa unaotakiwa kadiri mfamasia wa wilaya alivyokushauri, basi lipia chumba chako na anza marekebisho kama utakavyoelekezwa na mfamasia wa wilaya ili pawe na muonekano wa kisasa na kuvutia kwa kuweka hizo partitioning kwa ajili ya chumba cha mbele, kutolea dawa na stoo! Wengi hupendelea kuweka partitioning za Aluminium lakini hata ceiling board na gypsum hukubalika na huokoa gharama.
Hakikisha hicho chumba kina mzunguko mzuri wa hewa kwa kuweka feni na Air conditioner! Sheria pia inataka kuwe na vigae chini ili kurahisisha usafi na kuzua maambukizi ya magonjwa au vumbi ambayo hupunguza nguvu za dawa au kuharibika. Pia unaweza kuweka mbwembwe zingine za kibiashara ili kuvutia wateja wako kama rolling adverts na vioo ukutani.
Hatua Ya Tatu
Ukishamaliza kufanya marekebisho yako na kama ulivyoshauriwa na Mfamasia wa Wilaya, unatakiwa kumwita ili aje kukukagua Jengo (Premise Inspection) na kukuandikia kibali ambacho utalazimika kulipia hizo form za ukaguzi na maombi ya kibali ambayo yakishajazwa hutumwa baraza la Famasi uweze kupewa leseni na ruhusa ya kuanzisha biashara yako (Licence and Permitt). Kwa kawaida hapa huwa kuna gharama za kulipia na gharama huongezeka kama mmiliki sio mfamasia, hulazimika kulipia professional fee ya Mwaka. Hii hatua huweza kucuhukua hata miezi mitatu au sita kukamilika au kupata kibali chako kwani Baraza la Wafamasia lazima likae vikao kupitia maombi yako.
Tukumbuke pia hii biashara ni tofauti na biashara zingine kwani ni huduma pia kwa jamii na ni ya kitaalamu. Mikataba ya ajira ya wataalamu kama Dispensing Nurse,Pharmaceutical Technician au Mfamasia wako lazima iwepo wakati wa ukaguzi na ujazaji wa form za leseni za Baraza la Wafamasia. Hii ina maana kwamba kama huna Medical background kwenye dawa utalazimika kuajiri hao watu muhimu ambao ni kati ya mfamasia au technician ili aweze kukusaidia kutekeleza majukumu ya utoaji huduma za dawa.
Hatua Ya Nne
Wengi wakishakaguliwa hukurupuka kwa kwenda kununua mzigo (Dawa) na kuziweka au kuzipanga stoo)!Cha msingi hutakiwi kuwa na papara, subiri vibali vyote vya baraza la Famasi umepata na leseni ya biashara kutoka kwa Afisa Biashara wa wilaya ndio ujihakikishie kuanza kununua dawa kutoka kwa whole salers au distributors.
Hatua Ya Tano
Hatua hii ni ya kufungua Famasi yako na teyari kwa kuanza huduma, kumbuka siku zote biashara ni ubunifu hivyo basi hakikisha wahudumu wako ni competent na wana ueledi wa kutosha kwenye kutoa maelezo sahihi ya dawa na matumizi yake!Hakikisha pia wahudumu muda wote ni wenye lugha nzuri kwa wateja wa rika zote na tabasamu muda wote!
Kama unajiweza kifedha ni vyema wahudumu wakawa na uniforms au makoti ya kitabibu(Medical coat) ili kuonekana professional zaidi na kuwavutia wateja.
Inashauriwa pia uwe na Water dispenser ili wateja wenye uhitaji wa lazima kuanza kunywa dawa papo hapo waweze kupata huduma hiyo bila kusahahu kipimo cha uzito kiwepo kuwawezesha wahudumu kutoa dozi za dawa sahihi kwa wateja hasa watoto chini ya miaka mitano.
Cha Kuzingatia
Kama zilivyo biashara zingine ni muhimu kujiandaa kwa fedha japo si lazima kiasi kikubwa (At least 20M), na biashara hii utalazimika kumuajiri mfamasia ili akusimamie Famasi yako na kwa sasa wafamasia hutoza si chini ya Tsh. 1,000,000/ kwa mwezi na huyo ni wa part time tu, hivyo basi ni vyema ukawa na kiasi cha kuanzia cha kutosha kwa ajili ya kumlipa advance hata ya miezi sita kabla biashara yako haija stabilize au kuzoeleka na kufanya vizuri.
Kwa sasa pia kuna makampuni au Distributors wanaokopesha dawa kwa wateja wake, hivyo unaweza pia kujihusiha na haya makampuni ili waweze kukukopesha dawa na kulipia baadae, pia ni vizuri mhusika akafanya utafiti wa mahali atakapokuwa akichukulia mzigo wa kuuza. awajue wazabuni na pia aanzishe mahusiano ya kibiashara ya karibu. Kama zilivyo biashara nyingine si vyema kuanza na mzigo wa bei kubwa au quantity nyingi za items!mame sure kwa kila item zisizidi 5 kama sehemu ya kufanya utafiti wa kujua fast and slow moving items!ukishajua fast moving utaongeza quantity!pia hicho kiasi kinategemea na kodi ya pambo au chumba chenyewe cha biashara maana renovation inakula sana pesa kama chumba cha biashara kimechoka..hivyo mimi nilianza na hicho kiasi na nimefanikiwa. Kama zilivyo biashara zingine,changamoto hazikosekani!Cha kuzingatia ni kuwa smart na kufanya vitu bila kukurupuka, location siku zote huwa ni kitu muhimu sana kwenye hii biashara bila kusahau ubunifu!faida utaiona tu mkuu.
Kama unaanza biashara,ni vyema kuwa na varieties ya items au dawa!ni muhimu uwe na kila aina ya dawa japo kwa uchache au small quantities!hii itakurahisishia kupunguza hasara hasa kwa zile dawa ambazo hazitatoka na zenye short expiry dates! List ya wholesalers,importers au distributors kwa TZ ni ndefu na kila mmoja ana advantage yake!cha msingi ni kuhakikisha unafanya ka utafiti kadogo ka kupeleleza supplier mzuri kwenye registered medicines na price.Muhimu ni kuandaa item list ya dawa unazotaka kuanza nazo na kuzunguka kwa hao suppliers wakupe bei zao baada ya hapo utaweza kuwa na uamuzi sahii wa kuchagua!kiwango cha kuanzia kwenye mzigo inategemea pia na item list yako ni kubwa kiasi gani lakini kama famasi yako ni ya nje ya mji 10M inaweza kutosha kwa kuanzia kwenye dawa pekee...kumbuka varieties ni muhimu!
Ni hayo tu machache niliyoona niwashirikishe, wengi wana pesa lakini hawajui waifanyie nini, hivyo basi kama umeelewa vizuri biashara hii kwa maelezo hapo juu nakushukuru na nikutakie upambanaji wenye kheri..Pamoja sana!