Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Nataman sana kufungua duka ilo na pia mazingira nilipo panaruhusu sana ila nakosa utaalam fani yng haiusian na mambo ya dawa but kama kuna mtu anaweza saidia utaalam itakua kher tujinasue na uchumi tegemezi
kunamtu yeyote au ndugu yako anahusika na mambo hayo?
 
Tafadhali nitafute 0762208190, whatsup, call au sms ili tufanye kazi, kuna shida ya hiyo kitu, tunaweza Fanya kazi TANGA HANDENI. I am serious in business
Mtafute Mfamasia wa Wilaya yako, ama Mganga Mkuu wa Wilaya. Ndio hao wahusika wakuu.
 
mm nataka kufungua duka la madawa ya binadamu nahitaji mnitumie list ya madawa na nini cha kufanya kwa huduma hii ya duka la dawa jimmyfoxxgongo
Duka la dawa muhimu(dldm) au pharmacy?

Kuhusu DLDM
Kwanza kama upo dar nenda kwa mfamasia wa wilaya uliyoko wewe mueleze unataka kufungua duka la dawa muhimu(dldm) atakupa maeneo yaliyoruhusiwa na serikali kufungua maduka ya dawa muhimu mfano wilaya ya kinondoni eneo ni changanyikeni, bunju n.k (ukumbuke kuchukua na fomu ya kujaza please) utaenda eneo utakalotajiwa kufanya survey ukiridhika tafuta frem eneo hilo ukipata iandae fremu yako hakikisha iwe na tiles chini, kama kuna uwezekano wanataka iwe na choo karibu, iwe na sink la maji japo wengi tunatumia ndoo yenye cork, weka shelves za kioo, weka mlango wa kioo, weka store ni lazima iwepo ukiweka vyote hivyo tafuta muuzaji awe na cheti cha addo. Jaza fomu yako sehemu ya kwanza na ya mwisho mkataba wako na muuzaji, ukimaliza kujaza sehemu ya kwanza peleka fomu yako ofisi ya serikali za mitaa kwa afisa mtendaji wa sehemu unapofungulia atakuja kukagua na timu yake akimaliz atasaini na kuweka muhuri ataipeleka kwa afisa afya wa eneo hilo pia watakuja kukagua shelves ndani wanao muongozo wa nini wakague ila moja wapo ni choo, sink la maji, stoo, tiles na mengineyo wakimaliza utalipa ada kidogo ya ukaguzi nadhani ni 50. Watakupa fomu zako utazipeleka kwa mfamasia wa wilaya nao watakuja kukagua wakimaliza utalipa ada ya ukaguzi 50 pia halafu utapewa account namba ukalipie kibali ukimaliza utapewa muda lini itakuwa kibali tayari, watakuita kuchukua utaenda na risiti ya benk uliyoenda kulipia ada na utabeba cheti org cha muuzaji wako ambacho ni addo utapewa kibali na orodha ya dawa zinazoruhusiwa kuuzwa kwa level ya dldm basi utaenda nunua utaanza kazi pia unaweza weka dawa ukishakaguliwa tuu na mfamasia wa wilaya maana unaweza chelewa kupata kibali
Nadhani umepata mwanga kidogo pls kama una swali pia uliza tuu maana mimi kwasasa nasubiria kibali tuu hatua zote tyr hizo
 
Kwa mwenyeji wa ilala naomba anisaidie kupitia kata zilizopendekezwa n eneo gani lenye population ya watu wenye uhitaji wa duka la dawa muhimu
 
ni mtaji kiasi gani?vifaa gani niwe navyo?ikiwa Mimi ninao utaalamu huo.
naomba kusaidiwa
Sidhani kama upo makini mkuu maana unapokuwa na uelewa wa jambo hilo ina maana ulikuwa unafanyia kazi vifaa hivyo kwa majaribio sasa iweje leo uullize swali la aina hiyo hapa?
 
Habarini wapendwa,

Naomba mtu anisaidie kujua ni madawa gani ya binadamu yanatakiwa kuwekwa kwenye duka la dawa kwani nataka kuifanya biashara hiyo ila sina experience nayo nataka kumuweka mtaalaamu pindi nitakaponunua dawa hizo na kufungua duka hilo.

Mwenye uelewa au anayefahamu anisaidie kwa kuni pm kunitumia list ya madawa.


Asanteni sana
 
habarini wapendwa naomba mtu anisaidie kujua ni madawa gan ya binadamu yanatakiwa kuwekwa kwenye duka la dawa kwani nataka kuifanya biashara hiyo ila sina experience nayo nataka kumuweka mtaalaamu pindi nitakaponunua dawa hizo na kufungua duka hilo mwenye uelewa au anayefahamu anisaidie kwa kuni pm kunitumia list ya madawa


asanteni sana
Dah naona wataalamu wameingia mitini...hiyo biashara inalipa sana...kwa kukushauri japo mie sifanyi hiyo biashara..kaonane na wazoefu wa hiyo biashara japo ni wachache watakaokupa siri ya mafanikio si unajua watz na kiroho cha wivu..badae onana na madaktari wa dispensary/health center/ Hospital zilizo karbu na location utakayofungua duka, waulizie magonjwa yanayosumbua sana hilo eneo na possible drugs, badae ukiweza onana na mphamasia wa wilaya atakupa mchongo wa dawa zinazoruhusiwa...kila lakheri na Mungu akutangulie
 
habarini wapendwa naomba mtu anisaidie kujua ni madawa gan ya binadamu yanatakiwa kuwekwa kwenye duka la dawa kwani nataka kuifanya biashara hiyo ila sina experience nayo nataka kumuweka mtaalaamu pindi nitakaponunua dawa hizo na kufungua duka hilo mwenye uelewa au anayefahamu anisaidie kwa kuni pm kunitumia list ya madawa


asanteni sana
Niliwahi kukujibu lakinikuna thread iliandikwa biashara ya maabara ya binadam nilikupa mwanga sijui kama uliusoma maana hata swali hukuuliza nikajua haupo serious ungekuwa serious ningekusaidia kufahamu kupitia mimi hapa ila sasa itabidi uje na maswali pm nitakupa mwongozo maana siwezi andika hapa sio vizuri ila kama ni ushauri tafuta hiyo thread ya biashara ya maabara utakuta nimefafanua kwa kirefu ok fanya kwa faida yako
 
Niliwahi kukujibu lakinikuna thread iliandikwa biashara ya maabara ya binadam nilikupa mwanga sijui kama uliusoma maana hata swali hukuuliza nikajua haupo serious ungekuwa serious ningekusaidia kufahamu kupitia mimi hapa ila sasa itabidi uje na maswali pm nitakupa mwongozo maana siwezi andika hapa sio vizuri ila kama ni ushauri tafuta hiyo thread ya biashara ya maabara utakuta nimefafanua kwa kirefu ok fanya kwa faida yako
hakuwahi kunijibu mkuu labda ulimjibu mwingine naona utakuwa umechanganya labda niwe nimesahau mm niko serious sana na nina nia ya kufungua duka la dawa ninachokuomba nipe mwongozo na nipe list ya madawa mkuu pls kama utojali
 
Back
Top Bottom