Dulla anapokea kipigo cha mbwa koko huko

Dulla anapokea kipigo cha mbwa koko huko

Dulla huyoooo😁😁😁😁😁🤗
FB_IMG_16338133356228578.jpg
 
Huyu Bondia Katompa Tshimanga sio mtu wa kawaida.
Ana ngumi nzito balaa kila ikifika mtu chalii.

Watu watambue Ubondia hodari sio bidii ya mazoezi pekee.
Bondia lazima azaliwe na nguvu za asili ndio ajifunze Ubondia.

Ubondia ni Kipaji pia.
Ila huenda huyu Tshimanga Katompa alipaka vumbi la Kongo,
Sio kwa migumi ile.
 
Acha apigwe,msosi wenyewe anakula kwa mudi mabiriani unategemea nini? Mkongo kashapiga vitu vyake toka msitu wa kongo ni kumpelekea tu moto!
 
Afile munu, asigale munu.
Jamaa anajifanya wa Darisalaaaaaaama,anafikiri kiongea vineno vya kizaramo ndio wapinzani wake watamuogopa,ana uwezo mdogo sana ameshindwa kabisa kocontain game,sijapenda kaidhalilisha Tanzania
 
Tatizo maneno mengi sana

Ila huyo mkongo nlipomuona mwanzoni

Nligundua physic yuko vizuri

Ova
 
Hamna bondia mle

Nimeukumbuka Uzi wako mmoja humu kuhusu Dulla Mbabe na Twaha Kiduku, nilikuona Mnoko kwenye ule uzi kumbe upo sahihi.

Sasa naamini huyu Dulla hamna Kitu, iwapo nitaandakiwa Pambano hata mimi ninayepigana Style ya Snake The Monkey Shadow basi ninamdondosha Dullah mapema tu.
 
Kuendelea kumuita "Mbabe" wakati anakalishwa chini mara 3 ni matumizi mabaya sana ya hilo neno
 
imefika kipindi sasa cha kustaafu maana anapoelekea atakuja kufa ulingoni
 
Back
Top Bottom