Herehoa!
Leo nimeiangalia hii mechi ya hawa mabondia waliozoea kutambiana, nimefurahi kuona sijapoteza usingizi wangu bure.
Pambano lilikuwa zuri Sana. Waandaaaji walijipanga kufanikisha hili, hivyo nawapongeza Sana.
Lakini Kwa vile Mimi nami naishi Mkoa wa Morogoro Kwa kweli najisikia furaha Kwa USHINDI wa Twaha Kiduku ambaye amemtwanga Dulla.
Sasa hakuna ubishi tena kuwa Kati ya Twaha Kiduku na Dulla mbabe Nani kidume Kwa mwenzake.
Kitu pekee nilichojifunza kwenye Pambano hili kutoka Kwa Twaha Kiduku ni Kama ifuatavyo;
1. Usiwe mjivuni.
Twaha Kiduku, sio mjivuni, ninamfahamu Kwa kumuona, na Kwa vile Maeneo anayofanyia mazoezi ni karibu na ofisi yangu, ninaweza Kueleza hili pasipo shida.
Twaha Hana ujivuni, hajisikii na yupo simple Sana.
Hiyo ni akiwa huku kitaa.
Kwa upande wa akiwa ulingoni pia Twaha sio mtu wa ujivuni. Hana mbwembwe, Hana sifa Kama Sisi kina Taikon tunapenda misifa.
Kwenye mechi hii Kwa walioangalia wataungana na Mimi kuwa Twaha tangu anaingia kwenye ukumbi Hana ujivuni, tofauti na Dulla ambaye anapenda mbwembwe na mikwala.
Hii inatufundisha kuwa ajishushaye hukwezwa, ajikwezaye hushushwa.
2. Sio muoga.
Unajua watu wengi hutishwa na mikwala ya Adui zao. Dulla mbabe licha ya mikwala yake isiyoisha, mbwembwe za kuingia ulingoni, na sapoti kubwa aliyonayo bado haikumfanya Twaha amuogope.
Unajua Kwa mtu muoga ni rahisi kutishwa na mambo madogo Kama hayo.
Mechi ya leo inatufundisha kuwa tusitishwe na maneno ya Adui yetu.
3. Ufanisi na Weledi
Twaha kapigana Kwa weledi mkubwa Sana.
Kashambulia kuanzia raundi ya pili mpaka ya mwisho Kwa ufanisi wa Hali ya juu.
Twaha alitumia mbinu ya kushambulia zaidi pasipo kumpa nafasi Dulla mbabe,
Ingawaje raundi ya Kwanza Dulla
akiishambulia zaidi, alimpigaa Jab,/Ngumi Jinni ambayo ilimpeleka chini Twaha na ilibaki kidogo mchezo uishie pale na kuwa TKO.
Kwa Pambano hili, wote walioangalia wataungana na Mimi kuwa Dulla hamuwezi Twaha Kiduku, yaani kampiga Kama mtoto mdogo. Licha ya Dulla kujifanya anafurukuta.
Kesho wanamorogoro tutaandamana kuanzia Mikese mpaka Morogoro mjini, tukiwa na Crown yetu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro.