Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
-
- #41
Wanaume wa daslam ukipigana nao kwa maneno huwawez kuwashinda hapo wanachukua had kombe la dunia ila mvute kati kwenye ulingo mpige jab 1, left-hook 1, Right-hook 1, overhand Right 1 alaf mmalizie na uppercut 1 anaanguka chali miguu juu haamki tena.
Zile kelele za sijui "niling'atwa na mbuzi" zinaishia hapo
Dulla Mbabe kelele nyiingi kumbe uwanjani sifuri.
Aibu sana yaani anapigwa ngumi tatu yeye anarudisha moja tena isiyo na macho mpaka mwisho anaamua kukimbia kimbia tu ili walau ashindwe kwa points. Lol.
Dulla ni bondia mzuri tu, ila ukweli ni kwamba hamuwezi twaha hata kama yatapigwa mapambano 10, labda aotee knockout kama ilivyotaka kutokea round ya kwanza.
Tatizo kubwa dulla ni mrefu lakini anamruhusu twaha arushiane naye ngumi wakiwa karibu so anashindwa kukunjuka mikono yake na kuguard. Watu wanasema mikono yake Haina nguvu, lakini ukweli ni kwamba anashindwa kuvuta ngumi vizuri. Watu warefu wanawaeka mabondia wafumbi mbali sana na wanakuwa wanatupa ngumi wakiwa mbali tu.
Kitu Cha pili dula anashindwa kabisa kuguard. Twaha kiduku akiweka mikono haachi nafasi katikati ya mikono yake, lakini dulla anaiacha nafasi sana kwasababu ni mrefu na twaha ni mfupi, so Kila ngumi ikitumwa inapenya.
Wote waliopigana ni wazaramo....kwa hiyo Dar es Salaam haijapoteza kituYule mpembavu katutia aibu sisi wanaume wa dar,leo gari limeondoka ipo siku hata wakezetu wataondoka kwa stahili hii[emoji24][emoji24]
Acha masihara kidunda ni shughuli ngumu!Kidunda hatamaliza Raundi Saba atapigwa.
Kidunda ni mbishi lakini akipata mchezaji mzuri anayeshambulia wakati wote hatoboi
Kweli dulla kumpiga KO ni ngumu sana, ila hatokaa ashinde pambano dhidi ya kiduku bila KOUmesema vizuri Sana.
Dulla pia ni kikomazi, mvumilivu na anajua kustahimili Ngumi. Angekuwa bondia mwingine Kwa Ngumi zile wala asingefika Raundi ya 7.
Na Kama Twaha ndio angekuwa anapigwa vile nakuhakikishia Pambano lingeisha mapema Sana.
Kweli dulla kumpiga KO ni ngumu sana, ila hatokaa ashinde pambano dhidi ya kiduku bila KO
Acha masihara kidunda ni shughuli ngumu!
Jamaa wa tanga alisema kiduku siyo level yakeHuyu kijana wa Morogoro aliyeshinda hivj wamewahi pigana na yule kijana wa Tanga?
Wazee wa kiyepe yai!! Huku wakishushia na alkasusu!!Pigo Kwa wanaume wa Dar.
Mwakinyo anaogopa mziki wa KidukuJamaa wa tanga alisema kiduku siyo level yake
Yeye analinda branddd๐๐
Ova
Ndio Swahiba. ๐Swahiba kumbe nawe umekesha kuangalia ngumi
Safi,namtaka mwakinyo vs kiduku now,wadigo,wazigua,wasambaa n.k mko tayari kijana wenu apambane na kiduku ๐คฃ,maana kijana mwenyewe hataki ๐๐Ndio Swahiba. ๐
Herehoa!
Leo nimeiangalia hii mechi ya hawa mabondia waliozoea kutambiana, nimefurahi kuona sijapoteza usingizi wangu bure.
Pambano lilikuwa zuri Sana. Waandaaaji walijipanga kufanikisha hili, hivyo nawapongeza Sana.
Lakini Kwa vile Mimi nami naishi Mkoa wa Morogoro Kwa kweli najisikia furaha Kwa USHINDI wa Twaha Kiduku ambaye amemtwanga Dulla.
Sasa hakuna ubishi tena kuwa Kati ya Twaha Kiduku na Dulla mbabe Nani kidume Kwa mwenzake.
Kitu pekee nilichojifunza kwenye Pambano hili kutoka Kwa Twaha Kiduku ni Kama ifuatavyo;
1. Usiwe mjivuni.
Twaha Kiduku, sio mjivuni, ninamfahamu Kwa kumuona, na Kwa vile Maeneo anayofanyia mazoezi ni karibu na ofisi yangu, ninaweza Kueleza hili pasipo shida.
Twaha Hana ujivuni, hajisikii na yupo simple Sana.
Hiyo ni akiwa huku kitaa.
Kwa upande wa akiwa ulingoni pia Twaha sio mtu wa ujivuni. Hana mbwembwe, Hana sifa Kama Sisi kina Taikon tunapenda misifa.
Kwenye mechi hii Kwa walioangalia wataungana na Mimi kuwa Twaha tangu anaingia kwenye ukumbi Hana ujivuni, tofauti na Dulla ambaye anapenda mbwembwe na mikwala.
Hii inatufundisha kuwa ajishushaye hukwezwa, ajikwezaye hushushwa.
2. Sio muoga.
Unajua watu wengi hutishwa na mikwala ya Adui zao. Dulla mbabe licha ya mikwala yake isiyoisha, mbwembwe za kuingia ulingoni, na sapoti kubwa aliyonayo bado haikumfanya Twaha amuogope.
Unajua Kwa mtu muoga ni rahisi kutishwa na mambo madogo Kama hayo.
Mechi ya leo inatufundisha kuwa tusitishwe na maneno ya Adui yetu.
3. Ufanisi na Weledi
Twaha kapigana Kwa weledi mkubwa Sana.
Kashambulia kuanzia raundi ya pili mpaka ya mwisho Kwa ufanisi wa Hali ya juu.
Twaha alitumia mbinu ya kushambulia zaidi pasipo kumpa nafasi Dulla mbabe,
Ingawaje raundi ya Kwanza Dulla
akiishambulia zaidi, alimpigaa Jab,/Ngumi Jinni ambayo ilimpeleka chini Twaha na ilibaki kidogo mchezo uishie pale na kuwa TKO.
Kwa Pambano hili, wote walioangalia wataungana na Mimi kuwa Dulla hamuwezi Twaha Kiduku, yaani kampiga Kama mtoto mdogo. Licha ya Dulla kujifanya anafurukuta.
Kesho wanamorogoro tutaandamana kuanzia Mikese mpaka Morogoro mjini, tukiwa na Crown yetu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro.
Ha ha ha haNimeng'atwa na mbuzi.
Baba sasa ndio kumekucha.