Dullah Mbabe apoteza kwa pointi dhidi ya Eric Katompa, Arusha, Novemba 25, 2023, Dullah alalamikia Majaji

Huyu dulla amewezaje kupata jina kubwa kwenye ngumi ya Tz wakati uwezo wake ni mdogo sana?
 
Huwa siangalii ngumi, lkn pambano LA Jana nimeangalia kuanzia mwanzo mpaka mwisho.. Nimeshangaa mnoo kusikia dulla akilalamika wakati tank lake LA mafuta lilikata kuanzia round 4 tu. Muda wote alibaki kukumbatia na kufanya pambano kukosa mvuto kabisaa! Kuna wakati nilitamani lile pambano LA Sara na Tatiana lingekuwa ndiyo pambano kuu kuliko LA kina dulla.. Ukweli dulla siyo bondia kabisaa hata kupigana tu hajui anachojua ni kukumbatia tu
 
Atuache kwanza, tupo tunamsaidia dada yetu anaetaka kujinyonga.
 
Mwanaume unaliaje hivyo huku umekumbatiwa kama umefiwa?

Kuna lia ya kiume bana..
Badala ya kumuonea huruma nilicheka maana ilikuwa ni kichekesho badala yake.
Ni wapuuzi tu, wanapewa maiki hawaongei cha maana wala nini?
 
Ndiyo maana alimkumbatia na Ibra Class
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…