Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
Kama Kiongozi kamwe usiwe katikati, chagua upande ambao utaona unakufaa na uende mazima siyo nusu nusu, nusu nusu itakufaa tu kama kila kitu kiko sawa, lkn kikinuka hauna msaada wowote na wanakushukia kama mwewe.
Mfano Erdogan wa Uturuki mwaka 2016 kama asingekuwa rafiki wa kweli wa Putin ilikuwa ntolee tayari, aliponea chupu chupu kupigwa coup d’tat Putin akamtip na kumuokoa, juzi kati pia Kazakhstan kilishanuka lkn kwa kuwa nchi za huko zina ushirikiano na Urusi Putin akazima Mapinduzi, Syria pia bila ya urafiki wa ukweli na wa kuaminiana na Urusi sasa hivi Assad asingekuwepo, hata Irani anakingiwa kifua pia.
Mara nyingi USA au Urusi huwa wanajua kinachotokea Dunia nzima hivyo kama ukiwa rafiki yao wa kweli wanakulinda kama umafia unatokea kwa mmoja wao.
Lakini ukiwa nusu nusu huku unataka kule unatamani pia kama, kikinuka uko peke yako, ndicho kilichomponza Gadafi kwa mtazamo wangu alikuwa huku kwa Amerika, Ufaransa na akina Tony Blair anakula hapo hapo pia alijiweka na Urusi, kilivyonuka Putin alikaa pembeni ingawaje walijua kila kitu lkn alikuwa vugu vugu na mtu vugu vugu haaminiki, hata Sadamu Husein pia alikuwa vugu vugu huku anatumika na Amerika hapo hapo pia anajipendekeza kwa Urusi, Amerika ilivyokinukisha Urusi kakaa pembeni.
Hata sijui…