Kwa Tanzania hakuna tofauti ya msomi na ambaye hajaenda shule, tofauti ipo kwenye uchapa kazi na vipawa toka kwa Mungu. Nchi yetu toka imeanza inaongozwa na wasomi, lakini bado nchi ni masikini. Kibaya zaidi hata hao wasomi hawajui kwanini sisi ni masikini! Tafuta dongo lingine maana hili halikutoi.
Na kwa taarifa yako elimu yetu ni mbovu kupita maelezo, kiasi kwamba inazalisha wajanja wajanja, na watu wenye uwezo duni, matokeo yake watu wanaishi kwa kujipendekeza zaidi kwani ndio kinga ya wenye uwezo mdogo, na mavyeti ya kukariri. Najuta hata nilienda chuo kikuu kufuata nini kwa aibu ninayoona toka kwa tunaojiita wasomi.