Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Hivi sasa vyombo mbalimbali vya kimataifa vya habari vya nje kama vile vya CNN, Aljazeera, BBC na vingine vingi, "headlines" ya habari zao ni kukamatwa na Jeshi la Polisi nchini kwa Mbowe na "kubambikiwa" kesi ya ugaidi kwa kosa tu la kupigania Katiba mpya ya nchi hivi sasa.
Vile vile mashirika mbalimbali ya dunia kama vile Amnesty International na mengine mengi tu yanashinikiza pia Mbowe aachiwe huru, kwa kuwa ni dhahiri kuwa amefunguliwa kesi ya ugaidi kisiasa.
Ukiangalia hata zile haki za mtuhumiwa zimekiukwa kwa kiasi kikubwa sana na Jeshi la Polisi Katika kesi hii ya ugaidi wa Mbowe kama vile kumpeleka kisiri siri mahakamani, bila hata kuwajulisha mawakili wake, wanaomsimamia kwenye kesi yake
Ni kwanini nasema Chadema Wana kila sababu ya kupigania kufa na kupona mabadiliko ya Katiba mpya sasa na siyo wakati mwingine wowote.
Sababu kubwa ni kuwa hii Katiba ya nchi imepitwa na wakati, na ni ya mfumo wa chama kimoja kwa kuwa imempa madaraka ya ki_mungu mtu, Rais wa nchi, ambaye ni wa CCM, kiasi ambacho hakika, inadhoofisha kwa kiasi kikubwa mno kupanuka kwa demokrasia nchini
Rais wa nchi ndiyo kila kitu hapa nchini, anafanya uteuzi wa watendaji wote kwenye nafasi muhimu kwenye serikali hii.
Kwa mfano tumejionea hivi majuzi, akiwateua makada wa CCM, kutoka UV- CCM, vibinti vidogo kabisa kushika nafasi nyeti za u_DED, ambapo hao ndiyo wanategemewa kuwa "marefa" kwenye uchaguzi wa vyama vingi, kwenye maeneo waliyopangiwa!
Baada ya kelele nyingi Sana, zilizopigwa mwaka Jana na wapinzani, kwenye uchaguzi mkuu uliopita, kuwa CCM ilifanya wizi wa waziwazi kwenye uchaguzi huo, kwa kuwatumia makada hao wa CCM kwa kusaidiwa na Jeshi la Polisi, kufanya wizi huo wa kura, ndiyo kwanza anazidi kukoleza kwa kufanya uteuzi huo wa upendeleo kabisa!
Bado Rais Samia Suluhu Hassan anaendeleza teuzi hizo za "kipuuzi" kwa kuendelea kuwajaza makada wa CCM wasiokuwa na ujuzi wowote kwenye hizo nafasi za utendaji Katika majimbo yao, kwa lengo tu la kwenda kufanya "wizi" wa kura kwenye maeneo waliyopangiwa.
Sababu zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa suala hilo la uundwaji wa Katiba mpya siyo kipaumbele chake kwa sasa, kwa kuwa hivi sasa, anaujenga uchumi wa nchi, ulioanguka Sana, hazina mashiko.
Hatujasahau namna Rais aliyemtangulia, Hayati Magufuli, namna alivyokuwa akituaminisha watanzania kuwa tutembee vifua mbele, kwa kuwa nchi yetu ni tajiri Sana, hadi tunaweza kuwa "donor country" wa kuweza kuwakopesha hayo mataifa yanayojiita yameendelea!
Swali ambapo wananchi tunapaswa kumuuliza Rais Samia Suluhu Hassan, hivi uchumi wa nchi yetu umeanguka ghafla, baada ya kifo cha Magufuli?
Swali la pili, haoni kuwa uundwaji wa Katiba mpya ya nchi, unapaswa kufanywa sasa, ili kuepuka hii hali ya kumfanya Rais mungu mtu, ambaye yeye ndiye amepewa mamlaka makubwa mno ya kuteua watendaji mbalimbali wa serikali na haulizwi ni vigezo gani anatumia vya kuwateua hao watendaji wake?
Suala la uundwaji Katiba mpya ni hitaji la sasa la wananchi wa nchi hii na hakuna sababu zozote zenye mashiko, za kuendelea kufanya "delaying tactics"