Hayo ni mawazo yako finyu afadhali ungeuliza sababuNi kwasababu una mzigo wako humu kwenye katiba iliyopo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hayo ni mawazo yako finyu afadhali ungeuliza sababuNi kwasababu una mzigo wako humu kwenye katiba iliyopo.
Mawazo yangu finyu yanaona sababu za bunge kujaa wabunge wa NEC CCM ni hii katiba mbovu tuliyonayo. Ukiwa mpinzani sahau nafasi hata ya kuwa kiongozi wa mtaa. Anaeitetea hii katiba ni mmoja kati ya wale wachache wanaonufaika nayo.Hayo ni mawazo yako finyu afadhali ungeuliza sababu
Hivi hata ukitumia akili ndogo tu, hayo mataifa yawasaidieni ninyi kupata katiba kwa manufaa yenu na raia wa nchi ambazo mmeona hata kupitisha sheria ya mageuzi kuhusu maliasili ilikuwa kama kutenda kosa la jinai?Hivi sasa vyombo mbalimbali vya kimataifa vya habari vya nje kama vile vya CNN, Aljazeera, BBC na vingine vingi, "headlines" ya habari zao ni kukamatwa na Jeshi la Polisi nchini kwa Mbowe na "kubambikiwa" kesi ya ugaidi kwa kosa tu la kupigania Katiba mpya ya nchi hivi sasa.
Vile vile mashirika mbalimbali ya dunia kama vile Amnesty International na mengine mengi tu yanashinikiza pia Mbowe aachiwe huru, kwa kuwa ni dhahiri kuwa amefunguliwa kesi ya ugaidi kisiasa.
Ukiangalia hata zile haki za mtuhumiwa zimekiukwa kwa kiasi kikubwa Sana na Jeshi la Polisi Katika kesi hii ya ugaidi wa Mbowe kama vile kumpeleka kisiri siri mahakamani, Bila hata kuwajulisha mawakili wake, wanaomsimamia kwenye kesi yake
Ni kwanini nasema Chadema Wana kila sababu ya kupigania kufa na kupona mabadiliko ya Katiba mpya sasa na siyo wakati mwingine wowote.
Sababu kubwa ni kuwa hii Katiba ya nchi imepitwa na wakati, na ni ya mfumo wa chama kimoja kwa kuwa imempa madaraka ya ki_mungu mtu, Rais wa nchi, ambaye ni wa CCM, kiasi ambacho hakika, inadhoofisha kwa kiasi kikubwa mno kupanuka kwa demokrasia nchini
Rais wa nchi ndiyo kila kitu hapa nchini, anafanya uteuzi wa watendaji wote kwenye nafasi muhimu kwenye serikali hii.
Kwa mfano tumejionea hivi majuzi, akiwateua makada wa CCM, kutoka UV- CCM, vibinti vidogo kabisa kushika nafasi nyeti za u_DED, ambapo hao ndiyo wanategemewa kuwa "marefa" kwenye uchaguzi wa vyama vingi, kwenye maeneo waliyopangiwa!
Baada ya kelele nyingi Sana, zilizopigwa mwaka Jana na wapinzani, kwenye uchaguzi mkuu uliopita, kuwa CCM ilifanya wizi wa waziwazi kwenye uchaguzi huo, kwa kuwatumia makada hao wa CCM kwa kusaidiwa na Jeshi la Polisi, kufanya wizi huo wa kura, ndiyo kwanza anazidi kukoleza kwa kufanya uteuzi huo wa upendeleo kabisa!
Bado Rais Samia Suluhu Hassan anaendeleza teuzi hizo za "kipuuzi" kwa kuendelea kuwajaza makada wa CCM wasiokuwa na ujuzi wowote kwenye hizo nafasi za utendaji Katika majimbo yao, kwa lengo tu la kwenda kufanya "wizi" wa kura kwenye maeneo waliyopangiwa.
Sababu zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa suala hilo la uundwaji wa Katiba mpya siyo kipaumbele chake kwa sasa, kwa kuwa hivi sasa, anaujenga uchumi wa nchi, ulioanguka Sana, hazina mashiko.
Hatujasahau namna Rais aliyemtangulia, Hayati Magufuli, namna alivyokuwa akituaminisha watanzania kuwa tutembee vifua mbele, kwa kuwa nchi yetu ni tajiri Sana, hadi tunaweza kuwa "donor country" wa kuweza kuwakopesha hayo mataifa yanayojiita yameendelea!
Swali ambapo wananchi tunapaswa kumuuliza Rais Samia Suluhu Hassan, hivi uchumi wa nchi yetu umeanguka ghafla, baada ya kifo cha Magufuli?
Swali la pili, haoni kuwa uundwaji wa Katiba mpya ya nchi, unapaswa kufanywa sasa, ili kuepuka hii hali ya kumfanya Rais mungu mtu, ambaye yeye ndiye amepewa mamlaka makubwa mno ya kuteua watendaji mbalimbali wa serikali na haulizwi ni vigezo gani anatumia vya kuwateua hao watendaji wake?
Suala la uundwaji Katiba mpya ni hitaji la sasa la wananchi wa nchi hii na hakuna sababu zozote zenye mashiko, za kuendelea kufanya "delaying tactics"
Kumbe mnalilia vyeo?Mawazo yangu finyu yanaona sababu za bunge kujaa wabunge wa NEC CCM ni hii katiba mbovu tuliyonayo. Ukiwa mpinzani sahau nafasi hata ya kuwa kiongozi wa mtaa. Anaeitetea hii katiba ni mmoja kati ya wale wachache wanaonufaika nayo.
Kwa kweli inashangaza mno, namna CCM wanavyoshupalia shingo wanaposikia Chadema, wakipigania kufa na kupona uundwaji wa Katiba mpya.Duniani kurekebisha na kubadilisha katiba ni kitu cha kawaida. Watu wote wanawashangaa CCM kuwa mbogo wakisikia mabadiliko ya katiba.
Tatizo siyo kupata Katiba lakini noa ya hao wanaopigania katiba....Kwao katiba inahusu kuingia madarakani na wala siyo welfare ya watanzania...Wameshakuwa chama kikuu cha upinzani kwa zaidi ya muongo moja watuonyeshe walichowahi kukifanya chenye tija zaidi ya kupinga tu kila kitu na kugeukageuka kama vinyonga katika hoja zao....CCM ikilegea na kukabidhi nchi kwa watu wa jinsi hii, vizazi vyetu havitawasamehe!Kwa kweli inashangaza mno, namna CCM wanavyoshupalia shingo wanaposikia Chadema, wakipigania kufa na kupona uundwaji wa Katiba mpya.
Wananchi tunajiuliza hivi kuna nini hadi hawa maccm yakatae uundwaji wa Katiba mpya??
Kwani nyinyi mna hati miliki ya nchi hii?Kumbe mnalilia vyeo?
Wewe bado unaishi kwa shemeji yako mme wa dadako unashinda sebureni ukiangalia tamthilia na usiku unalala sebureni huku ukisikiliza dadako anavyomkatikia mme wenu chumbani huwezi kujua chochote kuhusu maisha.Acha kulazimisha si wote bali baadhi. Mfano mimi sioni umuhimu wa katiba mpya
Una uhakika gani na una hiki sema? Kama kwa miaka 60 chama tawala kimeshindwa kuisimamia serikali ili hata kupata maji kila kijiji na nyumba bora kwa raia tutegemee ni nini zaidi?Tatizo siyo kupata Katiba lakini noa ya hao wanaopigania katiba....Kwao katiba inahusu kuingia madarakani na wala siyo welfare ya watanzania...Wameshakuwa chama kikuu cha upinzani kwa zaidi ya muongo moja watuonyeshe walichowahi kukifanya chenye tija zaidi ya kupinga tu kila kitu na kugeukageuka kama vinyonga katika hoja zao....CCM ikilegea na kukabidhi nchi kwa watu wa jinsi hii, vizazi vyetu havitawasamehe!
Nina uhakika na zaidi kwakua I was once with these people!Una uhakika gani na una hiki sema? Kama kwa miaka 60 chama tawala kimeshindwa kuisimamia serikali ili hata kupata maji kila kijiji na nyumba bora kwa raia tutegemee ni nini zaidi?
Dawa ni kuingia kwa wingi kukiboresha chama hicho kilichopo ambacho atleast kimeonyesha kubadilika kila awamu...Hii ni our own style of democracy...CCM haijawahi kuwa ile ile unaona trend...Which means ndani ya CCM kuna democracy illa nje ya CCM hakuna chama kinachoweza kuizidi CCM kwa strategies na processes, CCM ni institution imara kabisa naweza kusema imara kuliko hata serikali yenyewe....CCM ilichokosa ni vijana ambao walidanganywa na vyama vilivyoundwa kwa malengo ya kutugawanya na kutu distract kwenye maendeleo hivyo kubakiza wengi ambao ni ma opportunists na wenye kuwa na God fathers...Hata hivyo trend ilibadilika alipoingia hayati JPM na kwa sasa CCM ina vijana wazuri lakini bahati mbaya fulani hivi bado wengi hawajapata strategic positions.Una uhakika gani na una hiki sema? Kama kwa miaka 60 chama tawala kimeshindwa kuisimamia serikali ili hata kupata maji kila kijiji na nyumba bora kwa raia tutegemee ni nini zaidi?
Very trueMawazo yangu finyu yanaona sababu za bunge kujaa wabunge wa NEC CCM ni hii katiba mbovu tuliyonayo. Ukiwa mpinzani sahau nafasi hata ya kuwa kiongozi wa mtaa. Anaeitetea hii katiba ni mmoja kati ya wale wachache wanaonufaika nayo.
UmelaaniwaHivyo vyombo siku hizi ni sawa na nagazeti ya udaku na ushilawadu tuu si kama zamani
Kwakuwa unakula Mali za watanzania bila kutoa jasho huku ukiwakandamiza bila hurima,huwezi on a umuhimuAcha kulazimisha si wote bali baadhi. Mfano mimi sioni umuhimu wa katiba mpya
Huna sababu,hata ukiwa nazo zipo kwa kulinda wizi wako na maccm wenzakoHayo ni mawazo yako finyu afadhali ungeuliza sababu
Mnasubiri Nini kuanzisha fukutoKatiba mpya ni takwa la kitaifa, hata sisi CCM tunaitaka ila tumezibwa midomo