Dunia imeanza kuelewa ni kwanini CHADEMA wanapigania kufa na kupona Katiba Mpya

Dunia imeanza kuelewa ni kwanini CHADEMA wanapigania kufa na kupona Katiba Mpya

Dawa ni kuingia kwa wingi kukiboresha chama hicho kilichopo ambacho atleast kimeonyesha kubadilika kila awamu...Hii ni our own style of democracy...CCM haijawahi kuwa ile ile unaona trend...Which means ndani ya CCM kuna democracy illa nje ya CCM hakuna chama kinachoweza kuizidi CCM kwa strategies na processes, CCM ni institution imara kabisa naweza kusema imara kuliko hata serikali yenyewe....CCM ilichokosa ni vijana ambao walidanganywa na vyama vilivyoundwa kwa malengo ya kutugawanya na kutu distract kwenye maendeleo hivyo kubakiza wengi ambao ni ma opportunists na wenye kuwa na God fathers...Hata hivyo trend ilibadilika alipoingia hayati JPM na kwa sasa CCM ina vijana wazuri lakini bahati mbaya fulani hivi bado wengi hawajapata strategic positions.
CCM ilishuka kutoka mbinguni? Si kilianzishwa na kujengwa tena kikiwa chama pekee. Unategemea kukijenga vipi chama cha Upinzani kama kinazuiwa kufanya mikutano hata ya ndani?
 
Hivi hata ukitumia akili ndogo tu, hayo mataifa yawasaidieni ninyi kupata katiba kwa manufaa yenu na raia wa nchi ambazo mmeona hata kupitisha sheria ya mageuzi kuhusu maliasili ilikuwa kama kutenda kosa la jinai?

Unapenda mno kupata madaraka kwa nguvu...Na kusema ukweli muombe Mungu isijetokea mimi nikawa Rais wa nchi hii, nitakuwa zaidi ya Hayati JPM....You arw so obsessed na kutwaa madaraka hata kwa gharama za maisha ya watu...Mungu na awahukumu saqasawa na dhamira zenu....I hate even being in one country na watu wa aina yenu; Wasaliti wakubwa!
Ulirudia kusoma ulichoandika kabla ya kukiposti!!?? Pole sana kwa kuwa na kichwa cha kufugia nywele.
 
Acha kulazimisha si wote bali baadhi. Mfano mimi sioni umuhimu wa katiba mpya
Ni kweli sio wananchi wote wanaona umuhimu wa katiba mpya. Lakin wananchi wote wanaojitambua, wasio wanafiki, wazalendo wa kweli na wanaolitakia mema taifa hili Kwa wakati uliopo na ujao, wanajua tumechelewa sana kupata katiba mpya. Wachache Sana ukiwamo wewe ndio hawaoni umuhimu wa katiba mpya. Tunaweza kuwaweka ktk makundi:
1. Wapumbavu, wajinga, mazezeta & the like. Mst likely umo kundi hili.
2. Wanafiki fulani wenye njaa wanaojali shibe haramu ya muda mfupi. Baadhi ya polisi wamo kundi hili. Pia viongozi wa dini baadhi.
3. Wanufaika wakubwa wa mfumo kandamizi. Humu wapo viongozi wakubwa wa ccm na familia zao.
4. .....
5. .....
 
Hivi sasa vyombo mbalimbali vya kimataifa vya habari vya nje kama vile vya CNN, Aljazeera, BBC na vingine vingi, "headlines" ya habari zao ni kukamatwa na Jeshi la Polisi nchini kwa Mbowe na "kubambikiwa" kesi ya ugaidi kwa kosa tu la kupigania Katiba mpya ya nchi hivi sasa.

Vile vile mashirika mbalimbali ya dunia kama vile Amnesty International na mengine mengi tu yanashinikiza pia Mbowe aachiwe huru, kwa kuwa ni dhahiri kuwa amefunguliwa kesi ya ugaidi kisiasa.

Ukiangalia hata zile haki za mtuhumiwa zimekiukwa kwa kiasi kikubwa Sana na Jeshi la Polisi Katika kesi hii ya ugaidi wa Mbowe kama vile kumpeleka kisiri siri mahakamani, Bila hata kuwajulisha mawakili wake, wanaomsimamia kwenye kesi yake

Ni kwanini nasema Chadema Wana kila sababu ya kupigania kufa na kupona mabadiliko ya Katiba mpya sasa na siyo wakati mwingine wowote.

Sababu kubwa ni kuwa hii Katiba ya nchi imepitwa na wakati, na ni ya mfumo wa chama kimoja kwa kuwa imempa madaraka ya ki_mungu mtu, Rais wa nchi, ambaye ni wa CCM, kiasi ambacho hakika, inadhoofisha kwa kiasi kikubwa mno kupanuka kwa demokrasia nchini

Rais wa nchi ndiyo kila kitu hapa nchini, anafanya uteuzi wa watendaji wote kwenye nafasi muhimu kwenye serikali hii.

Kwa mfano tumejionea hivi majuzi, akiwateua makada wa CCM, kutoka UV- CCM, vibinti vidogo kabisa kushika nafasi nyeti za u_DED, ambapo hao ndiyo wanategemewa kuwa "marefa" kwenye uchaguzi wa vyama vingi, kwenye maeneo waliyopangiwa!

Baada ya kelele nyingi Sana, zilizopigwa mwaka Jana na wapinzani, kwenye uchaguzi mkuu uliopita, kuwa CCM ilifanya wizi wa waziwazi kwenye uchaguzi huo, kwa kuwatumia makada hao wa CCM kwa kusaidiwa na Jeshi la Polisi, kufanya wizi huo wa kura, ndiyo kwanza anazidi kukoleza kwa kufanya uteuzi huo wa upendeleo kabisa!

Bado Rais Samia Suluhu Hassan anaendeleza teuzi hizo za "kipuuzi" kwa kuendelea kuwajaza makada wa CCM wasiokuwa na ujuzi wowote kwenye hizo nafasi za utendaji Katika majimbo yao, kwa lengo tu la kwenda kufanya "wizi" wa kura kwenye maeneo waliyopangiwa.

Sababu zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa suala hilo la uundwaji wa Katiba mpya siyo kipaumbele chake kwa sasa, kwa kuwa hivi sasa, anaujenga uchumi wa nchi, ulioanguka Sana, hazina mashiko.

Hatujasahau namna Rais aliyemtangulia, Hayati Magufuli, namna alivyokuwa akituaminisha watanzania kuwa tutembee vifua mbele, kwa kuwa nchi yetu ni tajiri Sana, hadi tunaweza kuwa "donor country" wa kuweza kuwakopesha hayo mataifa yanayojiita yameendelea!

Swali ambapo wananchi tunapaswa kumuuliza Rais Samia Suluhu Hassan, hivi uchumi wa nchi yetu umeanguka ghafla, baada ya kifo cha Magufuli?

Swali la pili, haoni kuwa uundwaji wa Katiba mpya ya nchi, unapaswa kufanywa sasa, ili kuepuka hii hali ya kumfanya Rais mungu mtu, ambaye yeye ndiye amepewa mamlaka makubwa mno ya kuteua watendaji mbalimbali wa serikali na haulizwi ni vigezo gani anatumia vya kuwateua hao watendaji wake?

Suala la uundwaji Katiba mpya ni hitaji la sasa la wananchi wa nchi hii na hakuna sababu zozote zenye mashiko, za kuendelea kufanya "delaying tactics"
Samia amekuwa mpuuzi kama mtangulizi wake
 
Katiba iliyopo inatutesa sana ,nimda mwafaka kubadili katiba mpya haraka iwzekanavyo!
 
Ni kweli sio wananchi wote wanaona umuhimu wa katiba mpya. Lakin wananchi wote wanaojitambua, wasio wanafiki, wazalendo wa kweli na wanaolitakia mema taifa hili Kwa wakati uliopo na ujao, wanajua tumechelewa sana kupata katiba mpya. Wachache Sana ukiwamo wewe ndio hawaoni umuhimu wa katiba mpya. Tunaweza kuwaweka ktk makundi:
1. Wapumbavu, wajinga, mazezeta & the like. Mst likely umo kundi hili.
2. Wanafiki fulani wenye njaa wanaojali shibe haramu ya muda mfupi. Baadhi ya polisi wamo kundi hili. Pia viongozi wa dini baadhi.
3. Wanufaika wakubwa wa mfumo kandamizi. Humu wapo viongozi wakubwa wa ccm na familia zao.
4. .....
5. .....
Acheni kutumia neno WOTE. Tumia neno wengi etc. Ni upumbavu kudhani iwapo wewe una mtizamo fulani basi WOTE tuna mtizamo husika.
 
huyu wa sasa hajaelewa siasa za ulimwengu zinakoelekea, magu alifeli vibaya alikuja kugundua kadri muda ulivyoenda, zile siasa na uongozi wake wa vitisho ni njia za kizamani mno, hazikuwa ngeni duniani, hazikuwahi shinda, mwishoni alionekana hata kwa sura na kauli kwamba amekwama. sasa huyu bado haelewi mipango yake na kuondoka nayo....vijana tanzania ccm bado hawana mchango kabisha bado kunahitajika combination wa experienced and long service people to create successors. epuka ambao hata kwa matendo na kauri zao tu sio za kujenga bali kufanya ili kuzima mambo ili muda wao wa kutumikia upite kama kina siro, kina mwigulu ambao ndumilakuwili, ndungai kanyaga twende ziroziro,.......achana na ya mtangulizi wako ambayo yalikuwa ya ovyo hata mjinga aliona ila aliogopa vitisho
 
itachukua miaka zaidi ya 30 watanzania kufanikisha kuipata katiba mpyaa
 
Samia amekuwa mpuuzi kama mtangulizi wake
Kwa kumweka ndani Mbowe, jambo ambalo hata mtangulizi wake hakuthubutu kulifanya, kwa maana hiyo this woman is more worse, than her prodecessor!
 
Hivi hata ukitumia akili ndogo tu, hayo mataifa yawasaidieni ninyi kupata katiba kwa manufaa yenu na raia wa nchi ambazo mmeona hata kupitisha sheria ya mageuzi kuhusu maliasili ilikuwa kama kutenda kosa la jinai?

Unapenda mno kupata madaraka kwa nguvu...Na kusema ukweli muombe Mungu isijetokea mimi nikawa Rais wa nchi hii, nitakuwa zaidi ya Hayati JPM....You arw so obsessed na kutwaa madaraka hata kwa gharama za maisha ya watu...Mungu na awahukumu saqasawa na dhamira zenu....I hate even being in one country na watu wa aina yenu; Wasaliti wakubwa!
😂😂😂😂😂!!!

Wakisaidia kupaaza sauti Kwenye Katiba- Wasaliti

Wakisaidia kutoa chanjo za mgawo- wahisani... Washirika!

Mzungu mzungu Ka'mkubwa!
 
Mimi naishi ughaibuni, nina access ya TV numbani na hata kwenye ofisi na nina access nzuri ya mitandaoni, Habari ya kukamatwa Mheshimiwa Mbowe haiko kwenye Headlines.

Inasikitisha sana kuona kuwa nchi za magharibi tunazitegemea sana na kuziona ni wakombozi lakini sio kweli, bali ni wanafiki, wabaguzi na wakandamizi. Wanawatumia wanasiasa wetu wa upinzani kwa maslahi yao na kuwatumia kwa manufaa yao tuu.

Hebu tuangalie utawala wa Magufuli, hawakumpenda basi waliingilia sana mitandaoni, luniga na kila njia kupaza habari za wapinzani na hali zao, leo hatuyasikii hayo.

Tukiangalia hali ya corona inavyowakabili WaAfrika, watu wanakufa kwa wingi, Afrika haitajwi kama ipaswavyo, Asia iko habarini kila la dakika, Serekali za kiafrika haziruhusiwi kununua chanjo kulingana na umati wao, ila wanaambiwa mtapewa kwa mgao, hawakubali kutupa ruhusa ya kutengeneza chanjo zetu wenyewe, kwani wao ndio wanaoruhusiwa, ukitumia chanjo za kichina ama Urusi hawazitambui na wanaanzisha siasa ya kutomruhusu kuingia ulaya mtu asiyepiga chanjo zao.
Alafu sisi kila kitu tunawaangalia wao.

Kwa sasa Mbowe hana faida kwao, wamehakikishiwa mambo ni mazuri na kipenzi chao Kikwete.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom