Dunia imeanza kuelewa ni kwanini CHADEMA wanapigania kufa na kupona Katiba Mpya

Dunia imeanza kuelewa ni kwanini CHADEMA wanapigania kufa na kupona Katiba Mpya

Mimi naishi ughaibuni, nina access ya TV numbani na hata kwenye ofisi na nina access nzuri ya mitandaoni, Habari ya kukamatwa Mheshimiwa Mbowe haiko kwenye Headlines.

Inasikitisha sana kuona kuwa nchi za magharibi tunazitegemea sana na kuziona ni wakombozi lakini sio kweli, bali ni wanafiki, wabaguzi na wakandamizi. Wanawatumia wanasiasa wetu wa upinzani kwa maslahi yao na kuwatumia kwa manufaa yao tuu.

Hebu tuangalie utawala wa Magufuli, hawakumpenda basi waliingilia sana mitandaoni, luniga na kila njia kupaza habari za wapinzani na hali zao, leo hatuyasikii hayo.

Tukiangalia hali ya corona inavyowakabili WaAfrika, watu wanakufa kwa wingi, Afrika haitajwi kama ipaswavyo, Asia iko habarini kila la dakika, Serekali za kiafrika haziruhusiwi kununua chanjo kulingana na umati wao, ila wanaambiwa mtapewa kwa mgao, hawakubali kutupa ruhusa ya kutengeneza chanjo zetu wenyewe, kwani wao ndio wanaoruhusiwa, ukitumia chanjo za kichina ama Urusi hawazitambui na wanaanzisha siasa ya kutomruhusu kuingia ulaya mtu asiyepiga chanjo zao.
Alafu sisi kila kitu tunawaangalia wao.

Kwa sasa Mbowe hana faida kwao, wamehakikishiwa mambo ni mazuri na kipenzi chao Kikwete.
Wewe unasema kuwa habari za Mbowe hazimo Katika headlines zao.

Hivi unaona ni sahihi kwa TV ya Taifa ya TBC kutangaza habari za uongo kabisa kwa lengo la kuisaidia CCM, eti vijana wa Chadema mkoa wa Arusha, wanaunga mkono Katiba iliyopo?
 
Katiba mpya sawa ila “Dunia “?!
Itakuwa tuna tafsiri tofauti ya hilo neno.
Yaani na Uviko huu, Dunia inafikiria Chadema na katiba mpya ya Tanzania!
 
Hivi sasa vyombo mbalimbali vya kimataifa vya habari vya nje kama vile vya CNN, Aljazeera, BBC na vingine vingi, "headlines" ya habari zao ni kukamatwa na Jeshi la Polisi nchini kwa Mbowe na "kubambikiwa" kesi ya ugaidi kwa kosa tu la kupigania Katiba mpya ya nchi hivi sasa.

Vile vile mashirika mbalimbali ya dunia kama vile Amnesty International na mengine mengi tu yanashinikiza pia Mbowe aachiwe huru, kwa kuwa ni dhahiri kuwa amefunguliwa kesi ya ugaidi kisiasa.

Ukiangalia hata zile haki za mtuhumiwa zimekiukwa kwa kiasi kikubwa sana na Jeshi la Polisi Katika kesi hii ya ugaidi wa Mbowe kama vile kumpeleka kisiri siri mahakamani, bila hata kuwajulisha mawakili wake, wanaomsimamia kwenye kesi yake

Ni kwanini nasema Chadema Wana kila sababu ya kupigania kufa na kupona mabadiliko ya Katiba mpya sasa na siyo wakati mwingine wowote.

Sababu kubwa ni kuwa hii Katiba ya nchi imepitwa na wakati, na ni ya mfumo wa chama kimoja kwa kuwa imempa madaraka ya ki_mungu mtu, Rais wa nchi, ambaye ni wa CCM, kiasi ambacho hakika, inadhoofisha kwa kiasi kikubwa mno kupanuka kwa demokrasia nchini

Rais wa nchi ndiyo kila kitu hapa nchini, anafanya uteuzi wa watendaji wote kwenye nafasi muhimu kwenye serikali hii.

Kwa mfano tumejionea hivi majuzi, akiwateua makada wa CCM, kutoka UV- CCM, vibinti vidogo kabisa kushika nafasi nyeti za u_DED, ambapo hao ndiyo wanategemewa kuwa "marefa" kwenye uchaguzi wa vyama vingi, kwenye maeneo waliyopangiwa!

Baada ya kelele nyingi Sana, zilizopigwa mwaka Jana na wapinzani, kwenye uchaguzi mkuu uliopita, kuwa CCM ilifanya wizi wa waziwazi kwenye uchaguzi huo, kwa kuwatumia makada hao wa CCM kwa kusaidiwa na Jeshi la Polisi, kufanya wizi huo wa kura, ndiyo kwanza anazidi kukoleza kwa kufanya uteuzi huo wa upendeleo kabisa!

Bado Rais Samia Suluhu Hassan anaendeleza teuzi hizo za "kipuuzi" kwa kuendelea kuwajaza makada wa CCM wasiokuwa na ujuzi wowote kwenye hizo nafasi za utendaji Katika majimbo yao, kwa lengo tu la kwenda kufanya "wizi" wa kura kwenye maeneo waliyopangiwa.

Sababu zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa suala hilo la uundwaji wa Katiba mpya siyo kipaumbele chake kwa sasa, kwa kuwa hivi sasa, anaujenga uchumi wa nchi, ulioanguka Sana, hazina mashiko.

Hatujasahau namna Rais aliyemtangulia, Hayati Magufuli, namna alivyokuwa akituaminisha watanzania kuwa tutembee vifua mbele, kwa kuwa nchi yetu ni tajiri Sana, hadi tunaweza kuwa "donor country" wa kuweza kuwakopesha hayo mataifa yanayojiita yameendelea!

Swali ambapo wananchi tunapaswa kumuuliza Rais Samia Suluhu Hassan, hivi uchumi wa nchi yetu umeanguka ghafla, baada ya kifo cha Magufuli?

Swali la pili, haoni kuwa uundwaji wa Katiba mpya ya nchi, unapaswa kufanywa sasa, ili kuepuka hii hali ya kumfanya Rais mungu mtu, ambaye yeye ndiye amepewa mamlaka makubwa mno ya kuteua watendaji mbalimbali wa serikali na haulizwi ni vigezo gani anatumia vya kuwateua hao watendaji wake?

Suala la uundwaji Katiba mpya ni hitaji la sasa la wananchi wa nchi hii na hakuna sababu zozote zenye mashiko, za kuendelea kufanya "delaying tactics"
Wananchi wa wapi ?mbona Mimi sijahitaji katiba mpya ,unapotoa hoja usijumuishe kila mtanzania ,umemuuliza baba ,mama ,shangazi ,mjomba ,mke, mtoto nk kwamba wanahitaji katiba mpya?
 
Katiba mpya sawa ila “Dunia “?!
Itakuwa tuna tafsiri tofauti ya hilo neno.
Yaani na Uviko huu, Dunia inafikiria Chadema na katiba mpya ya Tanzania!
Tumepata taarifa kuwa wawikilishi 4 kutoka UN wanategemea kuhudhuria kesi hiyo.

Bado kwa maoni yako hiyo haijawa Dunia?
 
Tumepata taarifa kuwa wawikilishi 4 kutoka UN wanategemea kuhudhuria kesi hiyo.

Bado kwa maoni yako hiyo haijawa Dunia?
Nenda huko Duniani uone sehemu nyingine ilivyoshida kuwapata watu wanaoijua nchi Tanzania na mahali ilipo. Nimeelewa point yako ila chumvi ilizidi kidogo.
 
IMG-20211123-WA0024.jpg
 
Wakati mwingine tutakapoamua kuandika katiba mpya tume ya katiba iundwe na wataalamu tu wa katiba na sheria wenye umri kuanzia miaka 45 kutoka ndani na nchi za mbali zilizo na demokrasia ya juu.

Watu aina ya Polepole na Bashite wasihusike kuandika katiba tunayotegemea itatupeleka miaka 100 mbele. Tutafute magenius wa katiba na sheria.
 
Back
Top Bottom