Dunia imeanza kuelewa ni kwanini CHADEMA wanapigania kufa na kupona Katiba Mpya

CCM ilishuka kutoka mbinguni? Si kilianzishwa na kujengwa tena kikiwa chama pekee. Unategemea kukijenga vipi chama cha Upinzani kama kinazuiwa kufanya mikutano hata ya ndani?
 
Ulirudia kusoma ulichoandika kabla ya kukiposti!!?? Pole sana kwa kuwa na kichwa cha kufugia nywele.
 
Acha kulazimisha si wote bali baadhi. Mfano mimi sioni umuhimu wa katiba mpya
Ni kweli sio wananchi wote wanaona umuhimu wa katiba mpya. Lakin wananchi wote wanaojitambua, wasio wanafiki, wazalendo wa kweli na wanaolitakia mema taifa hili Kwa wakati uliopo na ujao, wanajua tumechelewa sana kupata katiba mpya. Wachache Sana ukiwamo wewe ndio hawaoni umuhimu wa katiba mpya. Tunaweza kuwaweka ktk makundi:
1. Wapumbavu, wajinga, mazezeta & the like. Mst likely umo kundi hili.
2. Wanafiki fulani wenye njaa wanaojali shibe haramu ya muda mfupi. Baadhi ya polisi wamo kundi hili. Pia viongozi wa dini baadhi.
3. Wanufaika wakubwa wa mfumo kandamizi. Humu wapo viongozi wakubwa wa ccm na familia zao.
4. .....
5. .....
 
Samia amekuwa mpuuzi kama mtangulizi wake
 
Katiba iliyopo inatutesa sana ,nimda mwafaka kubadili katiba mpya haraka iwzekanavyo!
 
Acheni kutumia neno WOTE. Tumia neno wengi etc. Ni upumbavu kudhani iwapo wewe una mtizamo fulani basi WOTE tuna mtizamo husika.
 
huyu wa sasa hajaelewa siasa za ulimwengu zinakoelekea, magu alifeli vibaya alikuja kugundua kadri muda ulivyoenda, zile siasa na uongozi wake wa vitisho ni njia za kizamani mno, hazikuwa ngeni duniani, hazikuwahi shinda, mwishoni alionekana hata kwa sura na kauli kwamba amekwama. sasa huyu bado haelewi mipango yake na kuondoka nayo....vijana tanzania ccm bado hawana mchango kabisha bado kunahitajika combination wa experienced and long service people to create successors. epuka ambao hata kwa matendo na kauri zao tu sio za kujenga bali kufanya ili kuzima mambo ili muda wao wa kutumikia upite kama kina siro, kina mwigulu ambao ndumilakuwili, ndungai kanyaga twende ziroziro,.......achana na ya mtangulizi wako ambayo yalikuwa ya ovyo hata mjinga aliona ila aliogopa vitisho
 
itachukua miaka zaidi ya 30 watanzania kufanikisha kuipata katiba mpyaa
 
Samia amekuwa mpuuzi kama mtangulizi wake
Kwa kumweka ndani Mbowe, jambo ambalo hata mtangulizi wake hakuthubutu kulifanya, kwa maana hiyo this woman is more worse, than her prodecessor!
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!!!

Wakisaidia kupaaza sauti Kwenye Katiba- Wasaliti

Wakisaidia kutoa chanjo za mgawo- wahisani... Washirika!

Mzungu mzungu Ka'mkubwa!
 
Mimi naishi ughaibuni, nina access ya TV numbani na hata kwenye ofisi na nina access nzuri ya mitandaoni, Habari ya kukamatwa Mheshimiwa Mbowe haiko kwenye Headlines.

Inasikitisha sana kuona kuwa nchi za magharibi tunazitegemea sana na kuziona ni wakombozi lakini sio kweli, bali ni wanafiki, wabaguzi na wakandamizi. Wanawatumia wanasiasa wetu wa upinzani kwa maslahi yao na kuwatumia kwa manufaa yao tuu.

Hebu tuangalie utawala wa Magufuli, hawakumpenda basi waliingilia sana mitandaoni, luniga na kila njia kupaza habari za wapinzani na hali zao, leo hatuyasikii hayo.

Tukiangalia hali ya corona inavyowakabili WaAfrika, watu wanakufa kwa wingi, Afrika haitajwi kama ipaswavyo, Asia iko habarini kila la dakika, Serekali za kiafrika haziruhusiwi kununua chanjo kulingana na umati wao, ila wanaambiwa mtapewa kwa mgao, hawakubali kutupa ruhusa ya kutengeneza chanjo zetu wenyewe, kwani wao ndio wanaoruhusiwa, ukitumia chanjo za kichina ama Urusi hawazitambui na wanaanzisha siasa ya kutomruhusu kuingia ulaya mtu asiyepiga chanjo zao.
Alafu sisi kila kitu tunawaangalia wao.

Kwa sasa Mbowe hana faida kwao, wamehakikishiwa mambo ni mazuri na kipenzi chao Kikwete.
 
Reactions: Ame
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…