Huyo mtoto Haramu haitaji kula, kutunzwa, kwenda shule, kulelewa. Vile vile huyo mtoto Haramu ni kiumbe cha nani kama si cha Mungu. Dunia inasonga mbele, binadamu kwa asili si watakatifu, kila mmoja wetu anafanya makosa mengi yasiyoonekana na wengine- ingawa Mungu anatuona. Tusijidai eti ni wasafi mbele za watu na wengine ni haramu. Mungu pekee ndiye anayehukumu- Acha kutumia vitabu vya Mungu kuthibitisha udhaifu wako- Huna upendo kwa jirani yako (mtoto wa kike aliyepata mimba katika umri mdogo)
Ni wapi nimesema mtoto akiwa haramu haruhusiwi kula, kuvaa, kusoma na kupata mahitaji yake yote ya msingi??
Ni wapi nimesema mimi ni msafi sana na wengine ni wachafu?
Ni wapi katika hoja yangu nimehukumu mtu?
Tena ni wapi nimesema mtoto haramu au aliyezaa nje ya ndoa achukiwe na jamii?
Hivi unaelewa maana ya neno "haramu"???
Nafikiri hoja yangu ilikuwa kukukumbusha kuwa kuzaa au binti kupata ujauzito ni jambo linaloruhusiwa isipokuwa tu pale utaratibu husika unapofuatwa.
MUNGU aliweka uataratibu wa ndoa ili wanaotaka kuzaa wazae wakiwa ndani ya ndoa.
Kufanya tendo la ngono nje ya ndoa ni uasherati au uzinzi na mtoto anayezaliwa kwa uzinzi au uasherati, mbele za MUNGU mtoto huyo ni "haramu" sababu ametokana na tendo chafu. Uzinzi na uasherati vinahesabiwa mbele za MUNGU kama matendo machafu.
Mtoto anayezaliwa kwa njia hizi chafu, yeye kama yeye hana hatia kwasababu sio kosa lake kuzaliwa haramu. Lakini wanaobeba hatia ni hao waliomzaa.
Ili kuepusha hayo, ndiyo maana jamii iliyostaarabika, yenye kuishi kwa kufuata misingi bora iliyowekwa na MUNGU, imekuwa ikiwasisitiza sana Mabinti na vijana kujiepusha kabisa na vitendo vya uzinzi na uasherati vinavyoweza kuwasababishia kupata ujauzito kabla ya ndoa.
Na Tanzania sababu tunaamini katika MUNGU na ndiyo maana hata katika wimbo wetu wa Taifa tunamtambua MUNGU kwa kumtaja, tukimwomba aibariki nchi yetu na atubariki sisi pia, Je, si vyema tukiwa kama Taifa lenye kumtambua MUNGU tukiishi kwa kufuata kanuni, taratibu, na miongozo ya MUNGU??
Kwanini tusiweke nguvu kubwa kuwazuia watoto wasifanye zinaa, badala yake tunaweka nguvu kubwa kuwagharamia masomo waliopata mimba nje ya utaratibu??
Je, kwa kufanya hivyo huoni kama tunahamasisha zinaa kwa watoto wetu?
Maana kuwasomesha waliopata mimba na kuzaa ni sawa na kutuma ujumbe kwa wengine kuwa hata wao wakizaa nje ya utaratibu hakuna shida.
Like seriously? What kind of a future generation are we raising?