Dunia ina Umri gani? Mabillioni, Mamillioni, Malaki au Maelfu?

Dunia ina Umri gani? Mabillioni, Mamillioni, Malaki au Maelfu?

Mkuu Darwin amezaliwa katika masonic family. Na ujanja wote kaupata kutoka kwa babu yake Erasmus Darwin. Huyu mzee alikuwa superintelligent. Alikuwa ni philosopher, poet, scientist na physician. Huyu ni moja ya watu waliokuwa Most informed karne ya 18. Huyu ananafasi kubwa sana katika Evolution na kile alichokiandika darwin alipokuwa kisiwani galapagos. Kabla ya kuhamia mji wa Derby 1788 alijiunga na freemasonry katika Lodge ya Cannonage kilwinning. Watoto wa huyu mzee yaani baba zake darwin 1804,1807,1808 walijiunga katika Lodge iitwayo Tryian. Huwezi kumtenga darwin na hii kitu.
Hebu fanya hiyo homework maana hili tumewahi kulijadili humu pia.

Nyundo nimekupa mfano tu Lakini Kuna maelfu ya ooparts ambazo zimejaribiwa na vyuo vingi na lab zinazoaminika. Fanya utafiti. Muda haitoshi ningekuwekea source za kutosha kutoka kwenye most respected and top University Labs na comments za HODS.

Hahahahaa naona umeleta Quote ya mzee wa upako kuhusu Dini na Location. Huo ni mtazamo wako mkuu sio lazima uwe sahihi. Paul alikuwa farisayo sugu Tena akida wa kikosi kinachosaka na kuua wafuasi wa yesu. Lakini alibadilika katikati ya mazingira yasiyowezekana.

Karibu sana.
Darwin alikuwa na akili sana toka babu yake alikuwa botanist wkati baba yake akiwa medical doctor , alipata elim nzuri pia alitembea sehemu mbali mbali za ulimwengu alikuwa ni mmoja wa binadamu wenye akili tuu.

Mzee wa upako yuko right ungezaliwa pakistan leo hii ungekuwa uko ISIS unakata vichwa vya wakristo. Kwanza huwa namkubal sana huyo jamaa ni muelewa

Lakini ni vema tungebaki na miaka hii hii bilion 4 ambayo ina include hadi yako ya 6000, hebu tuitendee haki sayansi
 
“Mwanzo” ni Lini?
Masimulizi ya kitabu cha Mwanzo yanaanza kwa taarifa hii sahili lakini yenye kujaa maana: “Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.” (Mwanzo 1:1) Wasomi kadhaa wa Biblia wanakiri kwamba taarifa hiyo inafafanua jambo tofauti na mambo yaliyofanywa katika zile siku za uumbaji zinazozungumziwa kuanzia mstari wa 3. Yaani, kulingana na maneno ya ufunguzi ya Biblia, tayari ulimwengu, kutia ndani Dunia yetu, ulikuwako kwa muda usiojulikana kabla ya siku za uumbaji.
Wanajiolojia wanakadiria kwamba dunia imekuwako kwa muda wa miaka bilioni 4, nao waastronomia hukadiria kwamba huenda ulimwengu umekuwako kwa muda wa miaka bilioni 15. Je, mavumbuzi hayo—na mengine yatakayovumbuliwa wakati ujao—yanapingana na Mwanzo 1:1? Hapana. Biblia haitaji muda hususa ambao “mbingu na dunia” zimekuwako. Sayansi haipingani na mambo yanayosemwa katika Biblia.
Mungu angewezaje kutokeza nuru katika siku ya kwanza kama hakuwa amefanya mianga hadi siku ya nne? Neno la Kiebrania linalotafsiriwa ‘fanya’ katika mstari wa 16 si sawa na neno ‘umba’ linalotumiwa katika Mwanzo 21, sura ya 1, mstari wa 1, 21, na 27. “Mbingu” ambazo zilitia ndani mianga ziliumbwa muda mrefu kabla ya “siku ya kwanza” kuanza. Lakini nuru ya mianga hiyo haikuwa imefika kwenye uso wa dunia. Katika siku ya kwanza, “kukawa na nuru” kwa sababu nuru ilipenya mawingu mazito na kuonekana duniani. Hivyo, dunia iliyokuwa inazunguka ikaanza kuwa na vipindi vya mchana na usiku. (Mwanzo 1:1-3, 5) Bado vyanzo vya nuru hiyo havikuonekana kutoka duniani. Hata hivyo, katika kipindi cha nne cha uumbaji, badiliko muhimu lilitokea. Sasa, jua, mwezi, na nyota zilifanywa ‘ziangaze dunia.’ (Mwanzo 1:17) ‘Mungu alizifanya’ katika maana ya kwamba sasa zingeweza kuonekana kutoka duniani.
Mungu angewezaje kutokeza nuru katika siku ya kwanza kama hakuwa amefanya mianga hadi siku ya nne? Neno la Kiebrania linalotafsiriwa ‘fanya’ katika mstari wa 16 si sawa na neno ‘umba’ linalotumiwa katika Mwanzo 21, sura ya 1, mstari wa 1, 21, na 27. “Mbingu” ambazo zilitia ndani mianga ziliumbwa muda mrefu kabla ya “siku ya kwanza” kuanza. Lakini nuru ya mianga hiyo haikuwa imefika kwenye uso wa dunia. Katika siku ya kwanza, “kukawa na nuru” kwa sababu nuru ilipenya mawingu mazito na kuonekana duniani. Hivyo, dunia iliyokuwa inazunguka ikaanza kuwa na vipindi vya mchana na usiku. (Mwanzo 1:1-3, 5) Bado vyanzo vya nuru hiyo havikuonekana kutoka duniani. Hata hivyo, katika kipindi cha nne cha uumbaji, badiliko muhimu lilitokea. Sasa, jua, mwezi, na nyota zilifanywa ‘ziangaze dunia.’ (Mwanzo 1:17) ‘Mungu alizifanya’ katika maana ya kwamba sasa zingeweza kuonekana kutoka duniani
 
hoe-oud-de-aarde.jpg

???????

Swali hili ni Muhimu sana hasa dunia ya leo maana limeigawa katika vipande viwili ambavyo havina ukaribu wala ufanano hata chembe.

1:Wanaoamini Dunia iliumbwa(Creationists) - Dunia ina umri wa miaka takribani 6000 (maelfu).Pia kunadhana ndogondogo zinazoendana na hii.

2:Wanaoamini Dunia iliibuka (Evolutionists) - Dunia iliibuka Takribani miaka Bilioni 4.6 na maisha kuanza miaka Billioni 3.5 iliyopita.Pia kuna dhana takribani saba za uibukaji.

Haya ndio Matokeo ya Hii mitazamo miwili.
1: Kama dunia ni changa (Miaka kama 6000) Basi Dhana ya uibukaji EVOLUTION inakufa hapohapo. Somo kwamba tulitokana na Sokwe linafia hapo hapo.​

2: Kama Dunia imezeeka na inaumri wa miaka Billioni 4.6 basi, Dunia haikuumbwa na chochote kuhusu uumbaji ni stori zisizo sawa. Na ikumbukwe bila tukio hili ktuokea kwa mabillioni ya miaka tena kidogo kidogo hii dhana inakufa rasmi.
Vipimo Vya miaka.
1: EVOLUTION; Hapa wanatumia Carbon dating au Radiometric Dating (Ni njia ambazo ili zifanye kazi inabidi ujumuishe na MAKISIO/ASSUMPTIONS), Yawezekana kuna mengi zaidi pia.

2:CREATION; Hapa inatumika Umri wa watu hasa waliozaliwa baada ya adam,Historia,Utafiti na nyaraka za kale na kwenda hadi kufika leo tulipo.Yawezekana kuna mengi zaidi pia

Karibuni kwa changamoto fikirishi,
always am a Winner Kiranga gasgas Nyani Ngabu CHARMILTON tejateja Apollo Iceman 3D UHURU JR Kikwajuni One Behaviourist Stefano Mtangoo Hb wa Ilala Kahtan Ahmed Vivax Warrior faiz MALCOM LUMUMBA na wengine wengi...

Dondosha hapa chochote unachoamini au kujua kuhusu haya mawili. Ninaamini hakuna ambaye yuko pande zote mbili kwani hazichangamani.

Ukitoa na reference, illustrations, Quotes, links, chochote kile Kumtetea Adam au Homosapiens na makazi yake tutashukuru
Masimulizi ya kitabu cha Mwanzo yanaanza kwa taarifa hii sahili lakini yenye kujaa maana: “Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.” (Mwanzo 1:1) Wasomi kadhaa wa Biblia wanakiri kwamba taarifa hiyo inafafanua jambo tofauti na mambo yaliyofanywa katika zile siku za uumbaji zinazozungumziwa kuanzia mstari wa 3. Yaani, kulingana na maneno ya ufunguzi ya Biblia, tayari ulimwengu, kutia ndani Dunia yetu, ulikuwako kwa muda usiojulikana kabla ya siku za uumbaji.

Wanajiolojia wanakadiria kwamba dunia imekuwako kwa muda wa miaka bilioni 4, nao waastronomia hukadiria kwamba huenda ulimwengu umekuwako kwa muda wa miaka bilioni 15. Je, mavumbuzi hayo—na mengine yatakayovumbuliwa wakati ujao—yanapingana na Mwanzo 1:1? Hapana. Biblia haitaji muda hususa ambao “mbingu na dunia” zimekuwako. Sayansi haipingani na mambo yanayosemwa katika Biblia.
 
Haya mengine yooote mi sijui ila nachoamini mwisho wa dunia ni pale mtu anapokufa basi,tena yawezekana nikikufa kesho basi kesho kutwa ntazaliwa Donad Trump.so hatuna mwanzo wala mwisho,na dunia haina mwanzo wala mwisho
 
Nawapenda wapumbavu wanaoamini wanachoambiwa na kukataa wanachoambiwa. Biblia inasema mpumbavu amesema moyoni mwake kwamba hakuna Mungu. Sasa naongea na hao wapumbavu.
1. Biblia sio scientific book. Mpumbavu angetaka biblia ijieleze kisayansi wakati lengo la biblia ni mpaka mwenye uelewa mdogo amuelewe Mungu.sasa biblia ingeandikwa kisayansi wsngapi wangeisoma?
2. Mpumbavu anafikiri Biblia imekuja na majibu mepesi. Ingekuwa hivyo Mungu sio mpumbavu wa kudumaza akili za wanadamu. Mungu alimuumba mwanadamu katika kiwango bora kabisa na alimuachia kazi ya kustimulate uwezo wa kufikiri.
3. Mpumbavu anasifia kazi iliyofanywa na mwanadamu kwa kile ambacho ni haki ya mwanadamu kukifanya.
Kuhusu miaka ya Dunia
Kwa Mungu priority haikuwa kuleta habari za kiuchunguzi Bali ilikuwa kuleta mahusiano na yeye na kuleta ustaarabu kwa Dunia.
Hitimisho
Mwalimu akikuachia homework halafu ukaikamilisha INA maana huyo MWALIMU ni mjinga?
Aliyekuachia Homework na wewe uliyefanya yupi anastahili sifa?
 
Kuna nyayo mpya imegundulika hapa kwetu Tanzania kwamba binadamu wa kale aliishi miaka million tatu iliyopita. Kwa mantiki hiyo binadamu hawa waliishi Tanzania miaka 1000 kabla ya Kristo Yesu.

Yawezekana mambo haya ni kweli:-

1. Bado hatujajua huu mfumo mzima wa solor umejitengeneza kwa miaka mingapi? na Je kipi kilifanyika mpaka kila kitu kikawa automated. kwa mfano Namna dunia inavyojuzungusha yenyewe, kwa nini isisimame kwa muda au itokee hitilafu iache kuzunguka?

2. Binadamu wa kale alikuwa Mweusi ama Mweupe? Kwa nini sisi wanadamu kama tulitokana na kitu kimoja kwa nini tunatofautiana? wachina, wazungu, waafrica ???

3. Nini kilifana sayari ya dunia ikawa na uhai na nyingine zikakosa?

4. Jua lilijitengenezaje kuwa na madini yanayomulika bila kuisha miaka mabillioni kwa mabilioni?

5. Nguvu ya Uvutano yaani Gravitation force ipo wapi? nguvu hii ndiyo inafanya sisi na vyote vilivyopo juu ya dunia visiporomoke angani

GO9G5289.JPG




 
4.Kwa kuwa Watu waliumbwa kutokana
na udongo, ni material yepi yaliyotumika
kuumba viumbe wengine kama wanyama
na mimea? Mbona watu wanafanana sana
na hawa viumbe wengine?



aliendika hiyo na yy anajiita great thinker .....daaa ndugu yangu ww sijui.ni wa 2000
 
Naona huu uzi ulikuwa mchachu kwa baadhi ya watu humu
 
Toka Adamu mpaka wakati WA gharika ya Nuhu ni miaka 2000, toka Yesu Hadi kuzaliwa Yesu miaka 2000, toka Yesu Hadi sasa miaka 2017
 
19 Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
 
Mimi moja kwa moja napingana na CREATIONISM kwa maana haina mantiki.Nasema haina mantiki kwa sababu inatuachia maswali yasiyo na majibu na kutulazimisha tuiamini badala ya kuielewa.Mimi nina maswali yafuatayo kuhusu CREATIONISM.

1.Kama watu wote walitokea sehemu moja(mf.Mashariki ya kati), ni technologia ipi iliyotumika kusambaza watu kutoka mashariki ya kati kwenda maeneo mbalimbalina ya Dunia kama Chile, Madagascar n.k?
walivukaje bahari? Kama walisafiri, kwa nini wasingekuwa wanawasiliana kwa safari za mara kwa mara? Kwa nini kina V.Da Gama, C.Columbus wawe wagunduzi wa maeneo mengine? ina maana waliamini Dunia ni maeneo walimoishi pekee?

2.Kama tumetokana na Baba na Mama mmoja, kwa nini watu tunatofautiana sana? nini sababu na mechanism iliyosababisha wawepo watu weupe na weusi? Miaka 6000 inatosha kuruhusu mabadiliko makubwa tunanoyashuhudia ya tofauti miongoni mwa jamii za watu wa hii Dunia?

3.Kwa nini kuna mabaki ya kale yenye umri zaidi ya miaka milioni? kwa nini hayo mabaki hayapatikani nje ya Africa? Kwa nini fossils zinaonesha 'Life complexity' inaongezeka kutoka matabaka ya chini kuja matabaka ya juu ya miamba?

4.Kwa kuwa Watu waliumbwa kutokana na udongo, ni material yepi yaliyotumika kuumba viumbe wengine kama wanyama na mimea? Mbona watu wanafanana sana na hawa viumbe wengine?

5.Ukowapi ushahidi/mabaki ya bustani ya Eden, masalia/makaburi ya Adam na Eva?
Yako wapi masalia ya safina ya Nuhu? Mbona Palaeontology haioneshi kama mafuriko ya Dunia nzima yamewahi kutokea na kuua watu?

6.Kwa nini vitabu vya dini havizungumzii uwepo wa sayari nyingine?, Kama hizo Sayari ziliumbwa na Mungu, ni za kazi gani?

7.Kama Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu, kwa nini aumbe viumbe hatarishi kwa watu wake kama vile; Virus, bacteria na Fungus wenye kusababisha magonjwa na vifo kwa watu? Mungu mwenye upendo wote anaweza kuumba vyanzo vya matatizo kwa watu wake?

8.Kwa nini miili ya viumbe vya Mungu iwe na vestigial organs?

9.Kwa nini Mungu aumbe Dunia yenye majanga asilia kama matetemeko ya nchi, mafuriko, vimbunga na milipuko ya volcano? Intelligent designer anaweza kuumba dunia yenye majanga kama hii ya kwetu?

10.Kwa nini Mungu alisikitika na kuhuzunika baada ya kumuumba Binadamu(Mwa.6:5-8)? Mungu gani mjuzi wa yote afanye jambo la kumsikitisha na kumhuzunisha siku za mbeleni?
Maswali ya msingi haya
 
Back
Top Bottom