kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Wanaume wamezidi ubabe, hawakubali kujishusha kwa maslahi ya wote, tabia ambayo inailetea hasara dunia yote.
Wanaume hawaamini kama unaweza kumkosoa, kumuelekeza, kumfukuza au kumuagiza mtu bila kufokafoka kwanza.
Wanaume hawaamini kama unaweza kufanya jambo zuri la maendeleo bila mbwembwe, kujisifia sana mwenyewe na kusifiwa.
Wanawake ni kinyume chake, wanachohitaji wao ni matokeo mazuri tu basi. Wanaona aibu kwake kukiwa na hali mbaya kuliko kwa mwenzake kama yeye, kiongozi kama yeye, mzazi kama yeye, mzuri kama yeye. Hatamani kuharibu labda itokee bahati mbaya tu. Watatumia uwezo wao wote, akili yao yote na mbinu zao zote katika kufanikisha jambo lake hata kama iwe ni sherehe tu ya birthday ya mtoto. Hawapendi kutia aibu, hawavumilii aibu na hawapendi kusemwa vibaya.
Mwanamke Ni mwepesi kusamehe ili mambo yaende. Udhaifu wake ni kama ukimbeza, ukimdharau, kumdanganya, ukimtukana na kumpiga mbele za watu. Kama Akikukasirikia kwa mambo hayo ni vigumu kukusamehe.
Rais Obama nae ameliona hilo, hebu sikiliza taarifa hii.
View: https://youtu.be/HOXzORhon6g?si=1hOqHjVJCW-Ssp-o