DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
Good
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Fedha au pesa kwanza huwa haziombewi kwa wale watu wanyoofu kwa maana ya kwamba kama hauna unajisi wowote ambao umefanyiwa uliopelekea ukose zile nguvu za umiliki wa pesa basi ukiomba huwa unaomba zidisho la baraka pekee.Vipi kuhusu kutumia nguvu za ancestors katika kuomba baraka na mafanikio ya kipesa!?
sasa mkuu katka kuwaomba hao incestors upande upi ni mzuri zaidi je,ni upande wa baba au wa mama..? na pia ikiwa umewaomba incestors mfano wakunyoeshee mambo ya kifedha lakini wao incestors walipokuwa duniani walikuwa maskini hoehae shida tupu hawana fedha lakini sasa wamekuwa incestors na leo ww unaenda kuwalilia shida za kifedha ili wakufungulie njia zako za kupata pesa je,wataweza fanya unayotaka au ni lazima huyo incestors awe alijipata kifedha au kimafanikio kwa kile unachomuomba alipokuwa duniani.??Fedha au pesa kwanza huwa haziombewi kwa wale watu wanyoofu kwa maana ya kwamba kama hauna unajisi wowote ambao umefanyiwa uliopelekea ukose zile nguvu za umiliki wa pesa basi ukiomba huwa unaomba zidisho la baraka pekee.
Sasa kuna watu ambao hawana fedha lakini pia hawana unajisi wowote ambao wamewekewa ndani yao, watu hawa wapo ambao hujitahidi sana kwenye kuomba ila hawafanikiwi kifedha na mwisho huwa wanalaumu watumishi wao wa kiroho, sasa shida haipo kwenye hao watumishi wa kiroho na wala haipo kwenye maombi ila ipo kwenye mpishano wa njia kati ya yule mwenye kuhutaji fedha na fedha zenyewe.
Mambo ya kiroho huwa yanaishia rohoni kwa maana ya kwamba ile mitetemo inapotoka katika ule ulimwengu wa juu sana huwa haiji moja kwa moja hadi katika ulimwengu huu wa damu na nyama ila badala yake huwa inaishia kwenye upande wa kiroho na kutoka hapo kuja kwenye huu ulimwengu huwa ni lazima kiunganishi kiwepo sasa kiunganishi cha maombi ya fedha kutoka katika upande huo wa kiroho kuja kwenye ulimwengu wa damu na nyama huwa ni hatima yako kwa maana ya kwamba kwenye hatima ya mtu ndiko kuliko na nguvu ya umiliki wa fedha.
Hatima ni mtindo wa maisha ambao mtu amepangiwa aje auishi hapa duniani ili na yeye aweze kutoa mchango wake wa kuujenga na kuufanya ulimwengu uweze kuwa sehemu salama ya kuishi.
Kwahiyo endapo mtu ataishi maisha yaliyo nje ya hatima yake basi kuwa na hakika ya kwamba atakua anapishana na zile baraka zitokanazo na maombi ya kifedha.
Kwahiyo kabla hujaomba au kuombewa juu ya mambo haya ya kifedha ni lazima kwanza uhakikishe unajiweka mahala sahihi sio hatima inakutaka uwe daktari halafu Wewe umeamua uwe muuza nguo, hapa tayari ni mpishano.
Sasa, na katika kuomba baraka hizi huwa mtu anaouwezo wa kuziomba katika nguvu yoyote ya kiroho ambayo inayo uwezo wa kunyanyua ile mitetemo yake.
Na nilisema ya kwamba kuomba baraka kwa njia hiyo ya kutumia ancestors huwa ni rahisi na ni njia ya haraka kwa maana mtu huwa anakua na muunganiko wa moja kwa moja na hao ancestors ila sasa unatakiwa uwe na uhakika ya kwamba hayo maombi unayapeleka mahala sahihi.
Kwa maana si kila ancestor anaweza akaombwa baraka za fedha na akazifungua ingawa wapo wenye huo uwezo.
Kwasababu fedha haziombewi ila kinachoombewa ni njia ya kupitishia hizo fedha, kwa maana nyingine fedha ni matokeo ya uadilifu wa mtu katika kuishi yale maisha ambayo aliumbwa aje ayaishi hapa duniani.
Ingawa si kila mwenye fedha ni muadilifu wa kihatima ila wapo ambao wamepata pesa kwakua ni waadilifu wa kiimani katika upande wa kiroho kwa maana ameitumia ile imani inayo fungamana na yeye kubadili hatima.
Lakini pia si kila ambae hana fedha si muadilifu, wapo watu ambao ni waadilifu ila njia zao zimefanywa kuwa ngumu na watu wengine kwa maana ya kwamba wamewekewa unajisi.
Na kwa namna hiyo hiyo pia ipo hata kwenye upande wa kimungu.
Neno tumfanye mtu kwa mfano wetu pia linajumuisha mgawanyiko wa majukumu kwenye maeneo mbalimbali katika mfumo wa zile nguvu kuu nne za asili za uumbaji kwa maana ya maono, usaidizi, maarifa pamoja na uwezo wa kufanya kazi kwa bidii.
Wewe ni daktari ila mimi ni muhandisi ingawa wote tunaangukia kwenye eneo la maarifa lakini changamoto ya kidaktari nikiletewa mimi sitaweza kuitatua kama ambavyo changamoto ya kihandisi ikija kwako utakavyoshindwa kuitatua.
Kwa hiyo kwakua kinachoombewa ni njia na si pesa basi huyo ancestor ambae unatakiwa umuombe wewe ni lazima awe aliuhishwa kwakupita zile njia ambazo wewe unazipita katika upande huo wa kihatima, kwahiyo sio kila ancestor aliuhishwa kwakua aliziendea njia zake vyema katika upande huo ambao Wewe unauhudumu lakini pia ndio upande ambao wa hatima yako kwa maana ya kwamba ndani yake ndimo baraka zako za umiliki zinamo tembea.
Wacha niiweke tena namna hii...
Mimi na Wewe wote tulikua na shahuku ya kuinyanyua ile nguvu ya maarifa ambayo ililala ndani yetu na tukafuata utaratibu wa kunyanyua nguvu hiyo kwakuziendea zile njia zifaazo kunyanyua nguvu hiyo kwa weledi kwa maana ya kukaa darasani na kufuata zile taratibu za kidarasa zilizosaidia tuweze kudumu darasani hadi kufikia mwisho ambapo wote tuliuhishwa yaani kutunukiwa kulingana na maarifa tuliyo yanyanyua ndani yetu, licha ya kwamba wote tunamaarifa ila sehemu tunazohudumu ni tofauti tofauti kwahiyo ancestors hawapokei kila ombi ila kila ombi lafaa liende kwa yuLe anaehusika na mambo hayo.
Ufupisho wa maneno yote hayo ni kwamba huwezi kuwa na swali la hesabu ukaenda kuomba mwalimu wa kiswahili akusaidie kulisolve.
Pande zote mbili zinamuingiliano na wewe Kwahiyo unaweza kuomba upande wowote kati ya hizo mbili (na hapa nitapaandikia ili niweke msisitizo fulani ila kwa sasa baki na hilo).sasa mkuu katka kuwaomba hao incestors upande upi ni mzuri zaidi je,ni upande wa baba au wa mama..? na pia ikiwa umewaomba incestors mfano wakunyoeshee mambo ya kifedha lakini wao incestors walipokuwa duniani walikuwa maskini hoehae shida tupu hawana fedha lakini sasa wamekuwa incestors na leo ww unaenda kuwalilia shida za kifedha ili wakufungulie njia zako za kupata pesa je,wataweza fanya unayotaka au ni lazima huyo incestors awe alijipata kifedha au kimafanikio kwa kile unachomuomba alipokuwa duniani.??
kwa nilivyokusoma tangu umeanza naamini hakuna aliyezaliwa kuja kuwa maskini bali ni kushindwa kusoma code tu kuijua hatima yako ila wengi ndio hivyo hatuzijui hatima zetu maana ni ngumu kwa kutumia akili za kawaida.na kuhusu ancestors umetolea mfano wa picha kwenye maduka ya wahindi nimejiuliza swali ikiwa wanafamilia watatu wenye hatima toafauti lakini wakafanikiwa kimaisha kupitia biashara moja iliyoasisiwa na babu inamaana hao watoto au wajukuu zake wamefanana hatima na huyo babu.? na baada ya kuindeleza biashara kwa pamoja ikakua mara tatu ya babu hali ya kuwa hatima zao ni tofauti, hapa wanafanikiwaje wote wanakuwa maisha ya ukwasi..kwanini asiwe mmoja katika warithi wa hiyo biashara ya babu au kuna namna wanafanya kiasi kwamba hata sisi waswahili tukifanya pia tunakuwa kama wao kiuchumi?Pande zote mbili zinamuingiliano na wewe Kwahiyo unaweza kuomba upande wowote kati ya hizo mbili (na hapa nitapaandikia ili niweke msisitizo fulani ila kwa sasa baki na hilo).
Shida sio kufanikiwa kifedha ila shida ni njia alizozipita ndio njia unazozipita wewe? Kwa maana ya ile hatima yake ilikua inafanana na wewe?
Kwa maana kinachoombewa si fedha ila ni njia ya kupitishia hizo fedha Kwahiyo kama unaemuomba alifanikiwa kifedha kwakua alikua mkulima na wewe unamuomba ufanikiwe kifedha lakini wewe ni muuza duka la vifaa vya umeme ni ngumu kufanikiwa kwa maana maombi yako yatakapofika kwenye ile mitetemo ya juu huwa yanarudi kwenda kwenye ile njia ya hatima sio kwenye fedha.
Kwahiyo kama hatima aliyouhishwa nayo ni kilimo basi baraka zipatikanazo kwake zinaenda kwenye kilimo Kwahiyo ili ukutane nazo basi yakupasa uwe na hatima inayofungamana na yeye.
Ukizunguka kwenye maduka ya wahindi unaweza ukakutana na picha ya babu yao ambae ndio muanzilishi wa hiyo biashara wanayoifanya, Kwahiyo wanaunganisha mitetemo ya yule aliyepo dukani na ya muasisi wa biashara hiyo ili hata kama yeye hayupo kimwili aweze kuwepo hapo kiroho.
Na mwisho niseme kwamba huwezi kuomba kiatu kwa mtu ambae alizaliwa hana miguu lakini pia swali la hesabu liende kwa mwalimu wa hesabu na swali la history liende kwa mwalimu wa history.
Yeah umesoma kwa kuelewa, ni kweli nguvu ya umiliki iko kwa kila mtu.kwa nilivyokusoma tangu umeanza naamini hakuna aliyezaliwa kuja kuwa maskini bali ni kushindwa kusoma code tu kuijua hatima yako ila wengi ndio hivyo hatuzijui hatima zetu maana ni ngumu kwa kutumia akili za kawaida.na kuhusu ancestors umetolea mfano wa picha kwenye maduka ya wahindi nimejiuliza swali ikiwa wanafamilia watatu wenye hatima toafauti lakini wakafanikiwa kimaisha kupitia biashara moja iliyoasisiwa na babu inamaana hao watoto au wajukuu zake wamefanana hatima na huyo babu.? na baada ya kuindeleza biashara kwa pamoja ikakua mara tatu ya babu hali ya kuwa hatima zao ni tofauti, hapa wanafanikiwaje wote wanakuwa maisha ya ukwasi..kwanini asiwe mmoja katika warithi wa hiyo biashara ya babu au kuna namna wanafanya kiasi kwamba hata sisi waswahili tukifanya pia tunakuwa kama wao kiuchumi?
Bila shaka nililizungumza hapo juu kwamba kuna watu wako timilifu katika ile mitetemo ya mfumo nyota wao na wengine si watimilifu na kikawaida wale watimilifu huwa wanawaambukiza wale ambao sio watimilifu kwahiyo kama umeoa mwanamke ambae ni mtimilifu basi kila mnaposhiriki tendo ile mitetemo inahama kutoka kwake kuja kwako.mkuu Thecoder kuna swali linanitatiza ni kuhusu Ndoa kwamba unakuta baadhi ya watu kabla ya ndoa wana maisha ya kawaida tu ya shida na dhiki nyingi wanaunga unga tu kitaa lakini baada ya ndoa maisha hayo yanabadilika ndani ya miaka mitano tu ana biashara kubwa,gari,pesa nyingi na amejenga nyumba..ukimuulizi vp atakujibu ni ndoa imemletea baraka hizo.! wakati kuna wengine wana hizo ndoa miaka kibao na watoto wengi lakini maisha yao ufakara na shida muaka yote..swali langu ni je,kuna sir gani hapa kwenye kuchagua mwenza wa ndoa ambae atakuwa sumaku au njia na mkondo wa kupitisha hizo baraka za mafanikio hadi kwako je,ufanye au uangalie nini kipindi unatafuta mwenza wa ndoa.? je,kuna dalili au ishara zozote kwa mwanamke au mwanaume ambazo ukiziona utajua huyu ana kitu kitakachokukamilsha ambacho kwa pamoja mkiingia kwenye ndoa mtajipata na mtafanikiwa sana kimaisha..sasa,utazijuaje hizo code kabla/baada kuingia ndani ya ndoa hata kwa dalili tu.
Mizimu ni roho ambazo zimeuhishwa na nilikwambia uwe makini kwasababu roho zinauhishwa katika pande zote mbili kwa maana ya ule upande wa nuru lakini pia upande wa giza na kwa ujumla wake roho hizo huitwa Mizimu.Mkuu kwanza nikupe hongera Kwa somo nzuri sana!! Mungu akufidie, kwanza umetumia muda mwingi kufundisha!! na Bado unaendelea kujibu maswali yetu. Hongera sana!
Sasa nina maswali machache
katika mada ya Dunia ni uwanja wa vita ya hatima.kuna mahali umesema.
Ni rahisi kujibiwa kama utaomba Kwa kujiungamani na asili yenu, yaani kuomba Kwa mababu. Kuliko kuomba Kwa kutumia jina la Yesu, lakini ukatoa angalizo kuwa, uombe Kwa mizimu kama unauhakika hio mizimu iliishi Kwa kutenda mema hapa duniani. Lasivyo utavaa miroho ya hatari.
1> Sasa wakati unamjibu madu mmoja kuhusu kuwepo au kutowepo Kwa moto wa milele, umefanunua vizuri kuhusu kuzaliwa na kufa. Na unasema Kuna Roho ambazo uhuwishwa na kuvishwa uzima wa milele, Roho ambazo zilifikia hatima Yao vizuri!! Sasa inakuwaje ziwe mizimu na wakati umesema kuwa , Kuna mizimu wazuri na mizimu wabaya!! na umesema Kuna Roho ambazo uharibiwa!! Kuna mahali umenipiteza!! Mizimu ni zipi? Na Roho zinaharibiwa ni zipi?
Vipi kama mtaona wote mkiwa na alam M inakuwaje? Mfano M ya mwanamke inaonekana vizuri zaidi kuliko ya mwanaume?Bila shaka nililizungumza hapo juu kwamba kuna watu wako timilifu katika ile mitetemo ya mfumo nyota wao na wengine si watimilifu na kikawaida wale watimilifu huwa wanawaambukiza wale ambao sio watimilifu kwahiyo kama umeoa mwanamke ambae ni mtimilifu basi kila mnaposhiriki tendo ile mitetemo inahama kutoka kwake kuja kwako.
Sasa kuna njia kadhaa za kujua yupi ni yupi ila njia rahisi ni ile ya alama zilizomo kwenye viganja vya mikono.
Kuna alama kadha wa kadha nikipata wasaa nitaziweka hapa ili uweze kujua kwamba alama ipi na ipi inaonesha utimilifu ila katika alama hizo nyingi za kuonesha utimilifu alama maarufu ambayo wengi wanaitambua ni ile ya M.
Watu wengi wenye alama hii huwa ni watimilifu kwa maana kwamba wanaweza kuwahamishia mitetemo watu wengine ambao wako na alama tofauti.
Siku nitaandika kipande kirefu kuongelea hizi alama pamoja na kuzichambua kwamba ipi ni ipi na ipi inaendana na ipi.
Nimekuelewa vizuri Sasa!! tuendelee.Mizimu ni roho ambazo zimeuhishwa na nilikwambia uwe makini kwasababu roho zinauhishwa katika pande zote mbili kwa maana ya ule upande wa nuru lakini pia upande wa giza na kwa ujumla wake roho hizo huitwa Mizimu.
Roho zilizoharibika ni zile ambazo zimetoka kwenye mfumo wa uumbaji kwa maana hazirudi tena duniani na wala haziuhishwi kuwa katika mamlaka za mbingu bali zinatolewa kabisa kama mbegu mbovu yaani zilizooza na mkulima.
Nakushukur kunionesha haya Madini Sister!! Ubarikiwe na Usichoke Kutuonesha maana jukwaa kubwa hiliSomo limeeleweka bro, endelea....
Umechange Id?Nakushukur kunionesha haya Madini Sister!! Ubarikiwe na Usichoke Kutuonesha maana jukwaa kubwa hili
NdioUmechange Id?
Okay sawa, hii shule ndefu....ila pitia kuna vitu utajifunza, possible hata ile biashara unatumia nguvu sana kumbe hata sio hatma yako.😹Ndio