Dunia ya Mungu vitu vya mzungu? Wabongo tunatengeneza nini?

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Yaani Bongo bado sana, hivi hatushtuki? nguo za mzungu, viatu vya mzungu, mpaka chandarua uliyolalia ni ya mzungu! simu ya mzungu, Sisi tunatengeneza nini?

Shule zenyewe tunazosoma ni mfumo wa mzungu, tunakaririshwa madudu ambayo hayatusaidii kupata hata ugali wa kila siku bila kuomba ajira kwa huyo huyo mzungu.
Biblia ya mzungu, Kurani ya huko huko... yaani mpaka namna ya kusema na Mungu wetu tumepangiwa! Hatuna chetu? Hatuna asili? Kila kitu lazima kiidhinishwe na mtu wa nje ndio tuone kina baraka, .

Mpaka kondomu ni za mzungu. Yaani hata ulinzi wa afya yako na starehe yako ya ndani kabisa inategemea kiwanda cha mzungu? Bila mzungu huwezi hata kufurahia maisha yako ya siri? Huu ni utumwa wa kiwango cha lami!

Bongo tumefika mwisho wa reli Unaambiwa Dini zilitokea huko, basi unaanza kudharau asili yako na mizizi yako ya Kiafrika.

Dada zangu, mnatia aibu mpaka basi! Yaani mpaka shape na kuongeza makalio mnataka ya mzungu? Mnakimbilia kununua madawa ya mzungu, mnafanya upasuaji wa mzungu, ili mradi tu mfanane.
Mungu amekupa weusi wako, amekupa umbo lako la asili la Kiafrika, lakini wewe unajiona huna thamani mpaka uwe na "mchina" au shape ya kizungu. Huu ni ugonjwa wa akili, siyo urembo!.

Barabarani unadunda na gari la mzungu, mafuta yenyewe yanatoka huko huko. Sisi huku ni fundi gereji tu wa kurekebisha screpa zao, hatuna uwezo wa kuunda hata baiskeli ya kueleweka!.

Ukiumwa kidogo, unakimbilia dawa za mzungu. Mpaka panadol ni ya mzungu! Yaani bila maabara za mzungu sisi huku tunakufa wote? Tumesahau kabisa mizizi yetu, tumetupa mitishamba yetu, tunasubiri mzungu atuambie "kunywa hii" ndio tuone tumepona..

Unasoma kwa bidii ili upate cheti cha mzungu, uende ukaajiriwe kwenye kampuni ya mzungu. Yaani akili yako yote imewekwa kwenye box kwamba mafanikio ni kumtumikia mzungu!.

Yesu alizaliwa huko, Dini zilitokea huko, Bustani ya Edeni iko huko... Hivi hatujiulizi kwa nini kila kitu kizuri tunaambiwa kiko huko na sisi huku tulikuwa tunafanya nini? Tumeshikwa akili, tumepofushwa macho!
Bongo bado sana! Inabidi tushtuke, tuache ushamba wa kuiga kila kitu na kuanza kuthamini uasili wetu na akili zetu wenyewe!.

Unajidai unajua muda, lakini saa ni ya mzungu. Muda wenyewe unauhesabu kwa mfumo wa mzungu! Yaani bila majira yao sisi hatujui hata lini jua linazama?.
Umekaa mbele ya TV ya mzungu, unaangalia tamthilia za mzungu, unasikiliza biti za mzungu. Mpaka namna ya kutikisa kichwa unamuiga mzungu! Unaimba mistari ya kizungu huku hujui hata maana yake, mradi tu uonekane unaenda na wakati.

Kwenye sherehe zetu sasa, hapo ndio utacheka upate kilema! Unafungua champagne ya mzungu, unakunywa whisky ya mzungu, unavaa shela la kizungu. Hivi harusi zetu za asili zilienda wapi? Tumeshakuwa copy paste kiasi kwamba hata furaha yetu lazima ifanane na ya Ulaya!

Tiles za mzungu, rangi ya kuta ya mzungu, mpaka choo unachokalia ni cha mzungu! Yaani hata haja yako huwezi kuitoa bila kutumia teknolojia ya mzungu? Huu ni utumwa mpaka chooni, dah nachoka mimi!.
 
Ila imesahau neno moja kubwa sana ambalo ni

" INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN"

Maana yake "Hakika sisi sote ni wa Mungu na kwa hakika kwake YEYE tutarejea"

Mungu anahekima kubwa sana kuwapa wazungu elimu na uvumbuzi wa vitu vingi sana vya kidunia. Yeye anajua kwanini alimtunuku Mzungu na akamnyima babu yako huko mpitimbi.
 
Sisi tunatengeneza nini?
Vitu vingi vya Plastic ni Made in Tanzania, vitu vingi vya Glass ni Made in Tanzania, vitu vingi vya sanaa michoro, vinyago, nk vinavyouzwa duniani ni Made in Tanzania, bila kusahau tunatengeneza mimba pia tumezaa na wajapan, wahispania, wamarekani, wafaransa, waturuki hadi Waisrael tumewapiga mimba kwa hio hatuko nyuma ya dunia unayoiona wewe
 
Pengine elimu ya uvumbuzi ungepewa wewe basi isingeweza kusambaa kuwafaa watu wote duniani.Uhalisia tunauona jinsi gani waafrika tusivyowaps heshima wasomi na wavumbuzi wetu
 
Hata kwenye kuteua mitume, Mungu hakumfanya kila mwanadamu awe mtume...Why?

Anajua strength ya kila mmoja wetu katika kuibeba elimu
 
PhD za mchongo , kelele nyingi kazi kushambulia serikali wala hawana ugunduzi.
Tanzania unashangaa kumuona kiongozi kila siku yupo kwenye ziara na majukumu ya kiserikali ila inafika november unamuona mlimani city pale akitunukiwa phd na chuo kikuu...unajiuliza huo muda wa kusoma alikuwa anaupata wapi?
 
Yaani Bongo bado sana, hivi hatushtuki? nguo za mzungu, viatu vya mzungu, mpaka chandarua uliyolalia ni ya mzungu! simu ya mzungu, Sisi tunatengeneza nini?

Shule zenyewe tunazosoma ni mfumo wa mzungu, tunakaririshwa madudu ambayo hayatusaidii kupata hata ugali wa kila siku bila kuomba ajira kwa huyo huyo mzungu.
Biblia ya mzungu, Kurani ya huko huko... yaani mpaka namna ya kusema na Mungu wetu tumepangiwa! Hatuna chetu? Hatuna asili? Kila kitu lazima kiidhinishwe na mtu wa nje ndio tuone kina baraka, .

Mpaka kondomu ni za mzungu. Yaani hata ulinzi wa afya yako na starehe yako ya ndani kabisa inategemea kiwanda cha mzungu? Bila mzungu huwezi hata kufurahia maisha yako ya siri? Huu ni utumwa wa kiwango cha lami!

Bongo tumefika mwisho wa reli Unaambiwa Dini zilitokea huko, basi unaanza kudharau asili yako na mizizi yako ya Kiafrika.

Dada zangu, mnatia aibu mpaka basi! Yaani mpaka shape na kuongeza makalio mnataka ya mzungu? Mnakimbilia kununua madawa ya mzungu, mnafanya upasuaji wa mzungu, ili mradi tu mfanane.
Mungu amekupa weusi wako, amekupa umbo lako la asili la Kiafrika, lakini wewe unajiona huna thamani mpaka uwe na "mchina" au shape ya kizungu. Huu ni ugonjwa wa akili, siyo urembo!.

Barabarani unadunda na gari la mzungu, mafuta yenyewe yanatoka huko huko. Sisi huku ni fundi gereji tu wa kurekebisha screpa zao, hatuna uwezo wa kuunda hata baiskeli ya kueleweka!.

Ukiumwa kidogo, unakimbilia dawa za mzungu. Mpaka panadol ni ya mzungu! Yaani bila maabara za mzungu sisi huku tunakufa wote? Tumesahau kabisa mizizi yetu, tumetupa mitishamba yetu, tunasubiri mzungu atuambie "kunywa hii" ndio tuone tumepona..

Unasoma kwa bidii ili upate cheti cha mzungu, uende ukaajiriwe kwenye kampuni ya mzungu. Yaani akili yako yote imewekwa kwenye box kwamba mafanikio ni kumtumikia mzungu!.

Yesu alizaliwa huko, Dini zilitokea huko, Bustani ya Edeni iko huko... Hivi hatujiulizi kwa nini kila kitu kizuri tunaambiwa kiko huko na sisi huku tulikuwa tunafanya nini? Tumeshikwa akili, tumepofushwa macho!
Bongo bado sana! Inabidi tushtuke, tuache ushamba wa kuiga kila kitu na kuanza kuthamini uasili wetu na akili zetu wenyewe!.

Unajidai unajua muda, lakini saa ni ya mzungu. Muda wenyewe unauhesabu kwa mfumo wa mzungu! Yaani bila majira yao sisi hatujui hata lini jua linazama?.
Umekaa mbele ya TV ya mzungu, unaangalia tamthilia za mzungu, unasikiliza biti za mzungu. Mpaka namna ya kutikisa kichwa unamuiga mzungu! Unaimba mistari ya kizungu huku hujui hata maana yake, mradi tu uonekane unaenda na wakati.

Kwenye sherehe zetu sasa, hapo ndio utacheka upate kilema! Unafungua champagne ya mzungu, unakunywa whisky ya mzungu, unavaa shela la kizungu. Hivi harusi zetu za asili zilienda wapi? Tumeshakuwa copy paste kiasi kwamba hata furaha yetu lazima ifanane na ya Ulaya!

Tiles za mzungu, rangi ya kuta ya mzungu, mpaka choo unachokalia ni cha mzungu! Yaani hata haja yako huwezi kuitoa bila kutumia teknolojia ya mzungu? Huu ni utumwa mpaka chooni, dah nachoka mimi!.
Uzuzu umezidi! Mpaka dini ni za wazungu! Mf. Mungu wa Israel, Mungu wa weusi ni yupi?
 
Back
Top Bottom