Dunia ya Soka impe Luka Modric heshima yake

Dunia ya Soka impe Luka Modric heshima yake

Bila kumung'unya maneno wanazi na wazandiki wa soka duniani hawamtendei haki Luka Modric. Wamekuwa wakimu-underrate na kumuona mchezaji wa kawaida.

Lakini kwa misimu kama mitatu Luka yupo katika ubora wa kipekee aking'arisha vilivyo safu ya kiungo ya Real Madrid.

Ila bahati mbaya, wazandiki wa soka wanawasifia viungo wa kawaida kama Pogba, Fabregas, Kroos, na Rakitic.

kikosini Real Madrid, wachezaji wanaosujudikiwa ni Ronaldo, Marcelo, Sergio Ramos na Casemiro. Wanamsahau mtu ambaye yuko nyuma ya pazia ya mafanikio ya hao wengine.

Kwanini dunia ya soka haimpi heshima yake Luka?

Mkuu...ningependa nikuweke sawa apo unaposema kroos ni kiungo Wa kawaida kumlinganisha eti na pogba na fabregas unakosea...sasa Huyo jamaa ndo kabisa huwa uwepo wake kwenye match ni kama vile hayupo ila akitolewaga tu utagundua dimba pale kati limepwaya...hii ilijidhihirisha baada ya kroos kutolewa na sub katika 2nd-leg ya atletico kwenye ligi ambapo game iliisha 1-1,so far pale kati dimbani Madrid kuna viungo Wa maana si mchezo...tukianza na Kroos ni Master pass na penetration kuntu(HUYU NI MZURI ZAIDI TIMU IKIWA INASHAMBULIA),MODRIC ni mmiliki mzuri wa mpira na hutuliza pressure ya mpira pale dimbani(HUYU NI MZURI ZAIDI TIMU INAPO POSSESS MPIRA)...Pia kuna CASEMIRO huyu ni mkabaji makini(HUYU NI MUHIMU SANA TIMU IKIWA INASHAMBULIWA)...Na kila mmoja ana umuhimu wake kwa mfano Casemiro akitokaga na timu ikiwa inashambuliwa lazima Ramos adungwe RED...tafsiri yake mabeki wameelemewa na pale kati kumekuwa uchochoro,Modric asipokuwepo utaona kabisa midfilders za timu pinzani wanamiliki Mpira kuliko madrid na mipira mingi huwa inapotea sana pale kati(hapa naona Isco sherehe hii ya kumiliki Mpira pale kati anaweza ifanya vyema sikuizi isipokuwa tatizo lake huwa anapoza sana mipira anayopewa na wenzie maana hadi afanye udambwi wake ule ndo atoe Pasi...muda mwengine hii hukata morale ya timu) na Kroos asipokuwepo utagundua utoaji wa pasi za mwisho na penetration ni ovyo ila Kroos huwa sio mzuri pale Ramos anapopataga RED ambapo Casemiro inamlazimu arudi pale nyuma kumsaidia varane/nacho na hivyo inawalazimu Kroos na modric kubaki pale kati...apa mzigo huwa unamwelemea sana modric kwa kuwa Kroos si mkabaji kivile bora modric na kwa kuwa timu haipandi kama awali Kroos anashindwa kufanya kazi yake anayoifanyaga ya kutoa pasi za mwisho(katika situation kama hii kroos anakuwaga mzigo na huchoka vibaya kwa kuwa dimba huchafukwa na wao pale kati wapo Wawili tu yeye na luka...ukizingatia kukaba sana sio haiba yake...na apa mara nyingi sub inayoingia badala yake utaona ni Kovacic ana afadhali kwenye kukaba kuliko Kroos).
 
Mkuu naomba nitie neno hapo kidogo...unaposema luka alikuwa tegemezi spurs kulinganisha madrid unakosea sana kwa kuwa kitendo cha yeye kuanza kwenye 1st-eleven za Madrid ni kiashiria tosha cha kutegemewa...luka huanza venginevyo labda awe majeruhi...kingine kwenye timu kama Madrid mastaa ni wengi na hii ndo hufanya baadhi ya wachezaji kuonekana kawaida...na pale Madrid mchezaji unaweza kuwa fundi lakinii namba lazima uipiganie.
Naunga mkono mtazamo wako lakini naomba nikumbushe tu mtazamo wangu umetokana na mada husika iliyopo.
Si kwamba dunia hampi heshima yake modric bali ni kitendo chake cha kukimbilia timu yenye nyota wengi kiasi kwamba yeye pia kuonekana ni wakawaida tu.
 
tatzo wa Madrid wengi matahira wanamsifia anaelishwa ananenepa bila kumjua mtafutaji
Kumshabikia ronaldo sio utaahira wewe,ronaldo dunia nzima wewe wale wanaompigia kula ashinde balon dor mashabiki wa Madrid wale?

Luka machine ila mbele ya ronaldo na messi watasubiri wengi
 
Mchezaji wa kulazimisha sifa mi simtaki sifa huwa zinakuja tu hazilazimishwi
 
Luka kuna kipindi majeruhi yalimuandama sana, nadhani sasa hivi ametulia tulia. Tatizo la Madrid ni kumuona ronaldo ndie kila kitu, akiondoka pale hawa wengine wataanza kuheshimiwa.

Sijawahi kumpingaga huyu bwana ndani ya uwanja ila kroos namuona ni wa kawaida ila Modric na Casemiro ni wa pekee.

Aisee acha maneno yako. Achanana Toni Kroos, hiyo ni mashine ya kijerumani isiyokuwa na mfano. Kama wewe ni mnazi na mshabiki wa juujuu tuu huwezi kuiona kazi ya Kroos.

Toni kroos ana uwezo wa kupiga pasi zaidi ya 100 kila mechi huku akiwa na accuracy ya zaidi ya 90%. Na siyo pasi tuu ilimradi, bali ni pasi zizazohamisha uwanja. Kama ulikuwa hujui, Toni kroos ndo injini ya madrid
 
Bila kumung'unya maneno wanazi na wazandiki wa soka duniani hawamtendei haki Luka Modric. Wamekuwa wakimu-underrate na kumuona mchezaji wa kawaida.

Lakini kwa misimu kama mitatu Luka yupo katika ubora wa kipekee aking'arisha vilivyo safu ya kiungo ya Real Madrid.

Ila bahati mbaya, wazandiki wa soka wanawasifia viungo wa kawaida kama Pogba, Fabregas, Kroos, na Rakitic.

kikosini Real Madrid, wachezaji wanaosujudikiwa ni Ronaldo, Marcelo, Sergio Ramos na Casemiro. Wanamsahau mtu ambaye yuko nyuma ya pazia ya mafanikio ya hao wengine.

Kwanini dunia ya soka haimpi heshima yake Luka?
Maneno yako kweli ila kumbuka haya matuzo ni kibiashara zaidi na huwa wadhamini wanacheza big role, hebu fikiria wakati wa Xavi Barca jamaa ndio alikuwa machine sijawahi kumuona enzi zaki akipoteza mipira lakini eti hajawahi kuwa mchezaji bora sifa zote Ronaldo au Messi. Hata wakati wa Scholes ilikuwa ni Beckham tu iko mifano mingi sana kuna watu wanacheza sana tu lakini bidhaa haziuzi mpira ni biashara zaidi haya makampuni yanachagua mpaka wachezaji bora ila wauze bidhaa zao.
 
Mzee mm pale madrid bila kupepesa Macho, wachezaji wangu bora n Marcelo na Ramos a.k.a The Gladiator, Modrick kiukweli sipingi wala sikatai mana sijamshuhudia sana
 
Bila kumung'unya maneno wanazi na wazandiki wa soka duniani hawamtendei haki Luka Modric. Wamekuwa wakimu-underrate na kumuona mchezaji wa kawaida.

Lakini kwa misimu kama mitatu Luka yupo katika ubora wa kipekee aking'arisha vilivyo safu ya kiungo ya Real Madrid.

Ila bahati mbaya, wazandiki wa soka wanawasifia viungo wa kawaida kama Pogba, Fabregas, Kroos, na Rakitic.

kikosini Real Madrid, wachezaji wanaosujudikiwa ni Ronaldo, Marcelo, Sergio Ramos na Casemiro. Wanamsahau mtu ambaye yuko nyuma ya pazia ya mafanikio ya hao wengine.

Kwanini dunia ya soka haimpi heshima yake Luka?
Modric anaheshimika Spain kama vile Kante anavyoheshimika England wala hakuna mtu anayemu-underrate. Umesikia mkuu?
 
tatzo wa Madrid wengi matahira wanamsifia anaelishwa ananenepa bila kumjua mtafutaji
Modric ni kiungo matata sana duniani. Anaheshimiwa na kila mtu isipokuwa haters msioitakia Madrid yetu mafanikio.
 
tatzo wa Madrid wengi matahira wanamsifia anaelishwa ananenepa bila kumjua mtafutaji
Wewe Ni Tahira zaidi ambapo nia yako ni kuwaponda tu mashabiki wa Madrid lakini umesahau hata Messi alikuwa anakusanya Tuzo alizostahili Iniesta..
 
MODRIC NI BORA MARA 1000 YA KROOS..

LAKINI HII HAIMAANISHI KROOS NI MBOVU..
MKUMBUKE NDIO ANA PASS ACURACY KUBWA KULIKO WACHEZAJI WOTE KWENYE LA LIGA..

Na pia mkumbumbuke Madrid walikuwaga na Midfield mbovu sana iliyokuwa haiwezi kumiliki mpira,kazi zote alikuwa anazifanya Modric..
Mpaka aliponunuliwa KROOS ndio Madrid sahiv wanaanza kurud kwenye ulee mpira wao wa kipindu kileee..
 
Fans wa Madrid wamelewaa ujinga wanaolishwa na marefa wao kwa huyo mbebwaji wao anaetengebezewa magoli

Ronaldo kama uwanjan hakuna bale wala benzema
Magoli anayaskia tu kwa wenzie
Bale pia hapewi heshma
Yake

Waache uzandik waangalie

Wanaoitendea haki tim
Bale na luka
 
Back
Top Bottom