Duniani hakuna haki! Nimeibiwa simu na pesa na kupigwa chupa ila bado nikashitakiwa

Aisee umenikumbusha Visa viwili ambavyo vimenipa funzo sana maisha mwangu.
Kisa Cha kwanza nimeingia Bar ambayo huwa ndio bar tunayokutania. Sasa nimekaa na mshkaji wangu ni mwanasheria alafu mtu mzima Ila alikua ameshachangamka kidogo. Pembeni kuna jamaa kutoka Rombo walikuwa na kikao chao na huku wanagonga vyombo. Wakati wa bili wale jamaa wakamzingua muhudumu kumlipa mpaka akawa analia. Kile kitendo kilimkera jamaa yangu akaingilia Kati ili kumsaidia binti asizulumiwe pesa yake. Kosa kubwa alilofanya aliwaambia hii baa ni ya wachaga ti na warombo waondoke maana ni wase...ng tu. Aisee wale warombo walimaindi mbaya na Mimi kwa kuona vile nikawa namtoa mshkaji nje ili kuepusha shari Ila kitendo cha kusimama tu ili nimtoe jamaa ilitumwa chupa moja ya bia haijafunguliwa ikatua katikati ya mgongo wangu, nilishuka mdogo mdogo mpaka chini kwa maumivu na wiki nzima sikuweza kutumia choo cha kuchuchumaa
 
Najua ni ngumu kwa peke yako na ndio maana nimezungumzia company kutoka kwa masela hapo
mwanangu huku chini its possible...huwezi kua na taaluma,una jamii inakuangalia watoto ..familia kazi..then unaenda bar unaanza tukanana na mhudumu na kurusha ngumi...sababu iliyofanya mdada ampige chupa za kutosha ni kwakua mdada hana cha kupoteza...tulivyokua sekondari chuo tulikua hatuna cha kupoteza .,...au labda kwakua humu tunatofautiana miaka..imagine meneja wa bank unakutwa selo au umepasuka chupa kisa ulikua na masela mnagombania chenji yenu ya buku 10...kwanza sina masela .ukinizingua nakufunga tu
 

Pole sana
Naamini umejifunza tayari sina haja ya kukwambia mengi
 
ulifanya vizuri pia kuaga maana hapo ungejifanya kidume chupa ingeishia kichwani
 

Hiyo ya 3 ni utumbo.kama unabisha soma tena.
 
pole bro ukienda baa tambua kuna watu hawana cha kupoteza
pia wanawake wanatetewa ata km wao ndio wenye makosa
 
Lakini nilichojifunza hawa wanao behave kama hawana chakupoteza na kuwa wagomvi kwa wengine mara nyingi hawajawahi kukutana na kichapo kikali

Mimi nipigwe chupa tatu za kichwa nipotezee, hivi huyo demu atanichukuliaje yani?

Sasa si anaweza hata kunivunjia heshima mbele ya familia yangu na watoto, kunichukulia mi kibonde kua siwezi nika fight back kwa hiyo wewe kwa mazingira hayo utachuna utamuacha akutie vyupa vingine mbele ya watoto?

Mzee kila mtu na anavyo pima mambo, kwa situation kama hiyo wewe unaona ni fair kumuacha demu akunyuke na chupa kwasababu haitaleta picha nzuri kwa heshima yako ambayo umejijengea mtaani ni aibu kukutwa upo cello kwa hatia ya kumpiga mtu ambaye kimsingi alikua mkorofi

Kwangu mimi hiyo naona haija kaa njema, kwasababu kama lengo ni kuiaminisha jamii kua wewe ni mtu fulani mwenye heshima zako basi utakubaliana na mimi kwamba hiyo heshima lazima uilinde na uitetee usikubali mtu mwingine aivunje heshima yako kwa kukuchezea. Sitaki kuamini kwamba maana ya heshima unayoikusudia wewe ni "uzembe"

Hata sheria zina ruhusu kujitetea pale ambapo unashambuliwa (self defense) Kama unaogopa kwenda cello kwasababu ya kujibu shambulizi kumbuka jamaa pamoja na kuwa mhanga wa kupigwa chupa, kuibiwa simu, hela lakini mchizi ndio aliyeenda jela
 
Ulijitakia.
Kumbe pombe hunywi bar ulienda kufanya Nini?
Kama hunywi pombe epuka sehemu walipo walevi.
Ndio maana hata polisi walijua wewe Ni mlevi mgomvi
 
Bro umeongea point kabisa lakini ki ukwel km wale jamaa wasingenishika basi sasa hv tungekuwa tunaongea mengine maana na mimi chupa nilishika ila nilizuiwa kikamilifu kama ningepata nafasi basi ningeweza hata kumaliza kila kitu pale pale
 
kampani yangu ilikuja imechelewa bro ndio ilionitoa apo kituoni
Asije kukudanganya mtu maisha ya kitaa yanaendeshwa kitaa, mtaani huku kila mtu niga na bado tunapeana respect kwasababu hata uwe miraba minne utaishia kuwavutia mashori ila kwa vibopa unakalishwa tu kwasababu likishafikia swala la ugomvi hakuna u-solo

Hao jamaa wangefanya tukio hilo huku mitaa yetu na tena kama ulivyoeleza kua kuna kiosk, basi hata isingekua shida kwenye mapatano ya bei maana kungekua na malupulupu mengi hapo
 
Ugomvi wa bar ni balaa

Kuna siku tulikuwa wadada 3 sehemu tunakunywa na mkaka mmoja hivi

Kuna dada akaanzisha zengwe pale nadhani kusudi ni Kama kilichokutokea

Ila bahati mbaya akakutana na wadada wamevurugwa kichapo kilitembea Ile Timu yake ikaanza kurusha chupa

Yule kaka akingilia akachapa ngumi za kutosha,

Mi nikakwea boda nikakimbia Uzuri wale wapiganaji walinikabidhi vitu vyote so upande wa wapiga sachi haukufanikiwa lolote

Hapo nilikuwa nasoma uzi fulani humu unazungumzia kukaa mbali na hatari

Nikahepa nikaacha watu wanapigana chupa na kusachiana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…