Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Huwa nashangaa kweli watu tukishukuru Wazazi hasa Mama eti kwa kukuleta duniani.
Kuna kipi hasa cha maana huku duniani mpaka uwashukuru hao wazazi?
Yani tumetengeneza kitu kwamba huko ulikokuwepo hapakuwa sehem nzuri kuliko dunian.
Kama dunia kwako imejaa Mateso kwanini isiwe Lawama kwao? Hivi kwanza uliwaomba hao wazazi wakuzae?
Mi naona hakuna haja ya kushukuru mzazi yoyote katika hili. Kwasababu hamkukubaliana kukuleta duniani, walifanya kwa malengo yao, hivyo wao ndio walipaswa kukunyenyekea kukuleta huku.
Maisha hayana maana yoyote ile kwani mwisho wa siku kuna kufa, baada ya kufa kila ulichokifanya hakina maana tena kwako.
Unaonaje ukirudi ulikotoka? Kama haiwezekani basi hata wao walishindwa kuzuia uwepo wako. Nao wapo kwa style hiyo hiyo yako.
Shukrani wanapaswa kupewa kwa matunzo yaani kukufanya u-survive. Ila shida nyingine za duniaini zinaletwa na mpangilio wa maisha mfano kama public policy ni mbovu, poverty juu, then maisha magumu na wengine kukimbilia kwenye maisha magumu.
Mengine yapo juu ya uwezo wao na pia wewe inabidi upigane na kutumia fursa vizuri mara zinapojitokeza.