Tofauti na Maelezo ya jaji warioba na tume ya katiba, juzi Katika hotuba yake baada ya kukabidhiwa katiba iliyopendekezwa, hatukumsikia rais wa JMT Wala kiongozi yoyote akifafanua maslahi ya Washirika wa pande zote Mbili za muungano - hasa kiuchumi na kimamlaka. Badala yake, tulichosikia kwa lugha nyepesi Kabisa ilikuwa ni maslahi ya upande mmoja tu wa muungano - Zanzibar, huku maslahi kwa upande wa Tanganyika yakipuuzwa Kama vile Tanganyika haipo, lakini muhimu zaidi, Kama vile Tanganyika haitapata athari Zozote chini ya Mfumo ndani ya katiba inayopendekezwa.
Kwa mfano, Zanzibar wameahidiwa mikopo ya nje, uhusiano wa kimataifa, kuendesha rasilimali zao za Mafuta na gesi, na muhimu, tofauti na Huko nyuma, Zanzibar sasa itavuna viongozi watano wenye hadhi ya urais huku Tanganyika ikivuna viongozi wawili tu wenye hadhi ya urais (Tena hadhi ya kinadharia tu), huku kivitendo, Zanzibar wakiwa Ndio walioshika mpini. Tutajadili masuala haya yote - moja baada ya jingine, lakini Katika Bandiko hili, ningependa kujadili suala la madaraka ya urais chini ya katiba inayopendekezwa na jinsi gani mapendekezo husika yatachochea kuvunjika kwa muungano:
Tukumbuke Kwamba hoja za kina
Nape Nnauye,
MwanaDiwani,
chama,
Kobello,
Gamba la Nyoka,
Mtanganyika,
ZeMarcopolo, na makada Mbali mbali CCM dhidi ya serikali Tatu ilikuwa ni pamoja na Kwamba serikali Tatu zitaongeza utitiri wa viongozi, hivyo kuongezea mzigo walipa kodi. Makada hawa walikebehi sana hoja zetu juu ya uwepo wa rasimu ya CCM ya mafichoni lakini Ukweli sasa upo wazi - rasimu iliyopotishwa Ina content ambayo ilishafanyiwa kazi na kina Chenge, migiro, Wassira, lukuvi, etc Kabla hata mjadala kamili bungeni haujaanza. Tulisema miezi Sita iliyopita (April 2014), na sasa Ukweli huo umesimama.
Twende moja kwa moja kwenye hoja.
Tume ya warioba ilipendekeza rais mmoja wa muungano na viongozi Wengine wawili wa kuongoza pande Mbili za muungano bila ya kujalisha Viongozi hawa watapewa majina gani ya kiutawala. Pahala ambapo palitarajiwa kuwa suala la title za viongozi wa nchi washirika lingejadiliwa lakini bila ya kuathiri Roho ya rasimu ya wananchi (serikali Tatu) ilikuuwa ni ndani ya bunge maalum la katiba. Lakini tofauti na tume ya warioba, na katiba inayopendekezwa sasa imebariki gharama kubwa zaidi kwa wananchi, hasa watanganyika. Tofauti na rasimu ya tume ya jaji warioba, rasimu ya mafichoni ya CCM Sasa imeweka wazi Kwamba Jamhuri ya muungano wa Tanzania itakuwa na viongozi SABA wenye hadhi ya URAIS. Tukianza na Upande wa Zanzibar, wao watakuwa na viongozi WATANO wenye hadhi ya urais, Kama ifuatavyo:
1. Rais wa Zanzibar (anayepigiwa kura na wazanzibari tu lakini Ana Nguvu hadi kwa wananchi ambao Hawakushirikishwa kumchagua - watanganyika).
2. Makamu wa kwanza wa rais Zanzibar ambae ni msaidizi wa rais wa Zanzibar, hivyo kuwa na mamlaka ya kukaimu mamlaka juu ya watanganyika.
3. Makamu wa pili wa rais Zanzibar (mamlaka sawa na makamu wa kwanza wa rais Zanzibar).
4. Makamu wa kwanza wa rais wa JMT (mgombea mwenza kutoka Zanzibar (Huyu yupo kuwakilisha maslahi ya wazanzibari, sio watanganyika).
5. Makamu wa pili wa rais wa JMT (ambae pia Ana kofia nyingine ya urais wa Zanzibar).
Hapa tusisahau Kwamba katiba ya Zanzibar (2010) imepora mamlaka ya katiba ya JMT.
Kwa Upande wa Tanganyika, wao watakuwa na viongozi WAWILi tu kati ya marais Saba wanaoridhiwa na katiba inayopendekezwa:
1. Rais wa JMT - Huyu tumeshaona jinsi gani katiba ya Zanzibar (2010) ilivyompora mamlaka. Kwa maana nyingine, rais wa JMT chini ya katiba inayopendekezwa atakuwa ni rais wa Muungano kinadharia tu, huku akiwa sio lolote kivitendo. Kwa maana nyngine Rahisi, rais wa muungano will become "a toothless dog" Katika uongozi wake wa jamhuri ya "muungano". Ukweli huu utazidi kujitokeza siku sio nyingi kwani Kama alivyojadili
Nguruvi3 Hapa au kwingineko, Zanzibar hawawezi kurudi nyuma na kubadili katiba Yao kwa manufaa ya Tanganyika iliyovaa koti la muungano.
2. Rais wa pili kutoka wa Tanganyika atakuwa ni waziri mkuu wa JMT ambae vituko vya katiba inayopendekezwa vimempa wadhifa wa "makamu wa TATU" wa rais!
Hii inafanya uwepo wa marais SABA Katika mazingira ya katiba inayopendekezwa - Zanzibar ikitoa watano, Tanganyika ikitoa wawili, huku marais wa upande wa Zanzibar wakiwa Ndio wenye mamlaka makubwa zaidi kiutawala (rejea mgongano wa kikatiba) lakini pia kirasilimali (kwani chochote cha Tanganyika ni cha muungano kwa vile haina serikali yake). Hali hii inafanya cha Zanzibar Kiwe cha Kwao, na cha Tanganyika Kiwe cha wote - watanzania. Licha ya soko moto kote hili, bado Gharama zote za kuhudumia marais hawa Saba wakiwa madarakani na wakienda kustaafu zitakuwa ni za mtanganyika. Mwezi Aprili mwaka huu, Hamad rashid alipinga sana rasimu ya tume Kwamba itapelekea uwepo wa marais watatu ambao watakuwa ni mzigo kwa walipa kodi. Katika Hili la marais Saba sijui atakuwa na mtazamo gani. Tatizo letu ni Kwamba hatuna waandishi wa habari Mahiri kufuatilia mambo Kama haya.
Kama alivyojadili
Nguruvi3, muungano umefikia Katika hatua ya hatari kuliko kipindi chochote Kile. Kwa mfano Katika suala jamhuri ya muungano, miaka 50 baadae, JMT imekuwa ni nchi Mbili Zenye serikali Mbili, na marais Saba,lakini Watu bado Hawaoni Kwamba hili ni bomu la mtego (timing bomb).
Chini ya Katiba inayopendekezwa, CCM inapendekeza kwamba – Rais wa Zanzibar afanywe kuwa Makamu wa Rais wa Muungano bila ya kujalisha Rais wa Muungano anatokea upande upi wa Muungano. Kwa kufanya hivyo, CCM inadai kwamba – hali hii itamwongezea Rais wa Zanzibar - "madaraka na hadhi" ndani ya serikali ya Muungano na pia nje ya nchi. Huku ni kupandikiza mbegu ya machafuko na hatimaye kuvunjika kwa muungano kwa sababu:
Mkataba wa Muungano (1964) uliweka utaratibu ambao – Rais wa Muungano wa NCHI Moja, alikuwa na wasaidi wake wakuu wawili – Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar (Marehemu Karume), na Makamu wa Pili wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanganyika (Marehemu Kawawa).
LAKINI chini ya katiba inayopendekezwa, CCM haisemi iwapo Rais ni MMOJA wa nchi MOJA, badala yake Inasema tu kutakuwa na rais wa JMT, na hao Wengine Sita.
Katiba inayopendekezwa haisemi ni kiongozi gani ndiye atakayesimamia Mawaziri watakaokuwa wanasimamia mambo ya Tanzania Bara katika mfumo huu wa serikali mbili "ulioboreshwa". Katika mikakati yake ya kuuza kwa umma katiba inayopendekezwa, CCM haina Maelezo juu ya ufafanuzi wa masuala muhimu (kiutekelezaji), kwa mfano, - katika mazingira ya Zanzibar kuwa ni "nchi" kamili, yenye "mamlaka" kamili, katiba, amiri jeshi mkuu, Wimbo wa taifa, ikitokea kwamba Rais wa Muungano anatokea upande wa pili wa muungano (Zanzibar), JE:
· Rais huyu kutoka nchi jirani ya "Zanzibar" atasimamia masuala yasiyo ya muungano - ya upande unaoitwa "Tanzania Bara", ndani ya Jamhuri ya Muungano, kwa mamlaka yepi?
· Iwapo Rais wa Muungano atatokea panapoitwa "Tanzania Bara", Rais huyu wa Muungano atakuwa na mamlaka yepi ya kusimamia mambo ya "Tanzania Bara" wakati yeye atakuwa amechaguliwa na wananchi wa pande zote mbili za muungano - Tanganyika na Zanzibar?
· Zipo wapi ‘pande mbili' za muungano bila ya kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika?
Katika haya, CCM haina uwezo wa kufafanua Hali ambayo itazidi kuudhoofisha muungano. Kwa vyovyote vile, Katiba inayopendekezwa haitaboresha muungano bali itajenga mazingira ya kuvunja muungano. Tuendelee kufafanua hili:
Kwa mfano, iwapo Rais wa Muungano atatokea upande wa nchi jirani ya "Zanzibar", ambaye kwa Mujibu wa katiba inayopendekezwa, Rais wa Zanzibar pia atakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano. CCM inapendekeza kuwa rais wa nchi Jirani ya Zanzibar moja kwa moja awe ni makamu wa rais wa muungano (Tanganyika) hata Kama hakuna mtanganyika hata mmoja aliyempigia kura. Kwa maana nyingine, rais wa Zanzibar pia atakuwa ni rais wa watanganyika kwa njia ya uteuzi. Hiki ni kituko cha mwaka - watanganyika kuwa na marais wawili, mmoja waliyempigia kura, mwingine aliyepigiwa kura nchi Jirani (Zanzibar) kisha kuteuliwa kuwa rais wao watanganyika, Tena akiwa na katiba (ya Zanzibar)ambayo Ipo juu kimamlaka kuliko Ile ya watanganyika/muungano.
Mbali ya athari hizi, Ipo nyingine kubwa. kwa mfano, Kitendo cha rais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais wa muungano bila kujalisha Rais wa Muungano atatokea upande upi wa Muungano kitatupeleka Katika Hali ifuatayo:
• Siku moja, Rais wa Muungano na Makamu Wa Rais Wa Muungano, wote watakuwa wametokea nchi jirani ya "Zanzibar". Kwa maana hii, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, CCM inajenga mazingira ambayo Zanzibar hawataweza tena kutoa Rais wa Muungano. Hii ni kwa sababu:
Hali hii itaamsha watanganyika kwani kwa maana ya Kwamba - Kama tulivyoona, chini ya rasimu inayopendekezwa na CCM, Rais wa Zanzibar "automatically", atakuwa pia ni Makamu wa Rais wa Muungano. Sasa ikitokea Siku CCM ikasimamisha mgombea Urais wa Muungano kutokea nchi jirani ya "Zanzibar", nchi ambayo pia automatically itatoa makamu wa Rais wa Muungano, chini ya mazingira ya sasa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, wapiga kura kutoka upande wa inayoitwa "Tanzania Bara", upande ambao una wapiga kura zaidi ya 90% ya wapiga kura wote wa Jamhuri ya Muungano, HAKIKA, wengi ya wapiga kura hawa kutoka "Tanzania Bara", hawatakubali kumchagua mgombea wa urais (CCM) kutokea nchi ya Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake pia anatokea huko huko "nchini" Zanzibar. Kwa maana nyingine, wananchi wa tangangika siku moja watakataa mgombea wa aina hii atakayependekezwa na CCM.
Je athari yake ni nini?
Ni kwamba – chini ya katiba inayopendekezwa na CCM, ni muhimu sasa waZanzibari waanze kujiandaa kisaokolojia Kwamba watanganyika Kamwe hawatomchagua kwenye Sanduku la kura mgombea urais mzanzibari kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Watanganyika watakuwa wamefanya uamuzi sahihi lakini Kitachofuatia kwa upande wa Zanzibar ni Kwamba wazanzibari wataanza kulalamika kwamba wanabaguliwa, wanaonewa, wananyimwa haki ndani ya Jamhuri ya muungano, kwahiyo waachwe "Wapumue". And interestingly enough, watakaongoza katika kutoa hoja hizi ni wale wale wazanzibari ambao Islaml Jusa alisema kwamba walipofika Dodoma "Waliufyata". Ni wale wale ambao leo wanapinga kwamba wao sio "wasaka tonge". Katika kundi hili, hatutashangaa kuja kuona viongozi kama Balozi Seif Iddi, Mohamed Seif Khatib, nahodha, kificho,Hamad Rashid Mohamed, na wengine wakija kugeuka na kusema Kwamba Tanganyika inafanya Zanzibar kuwa koloni. Baadae tutaona jinsi gani ruksa kwa Zanzibar kukopa, kuwa na uhusiano wa kimataifa n.k bado hayatamaliza Dhana ya ukoloni.Hakuna mamlaka kamili kwa Zanzibar kwa Jambo lolote bila ya uwepo wa Tanganyika.
• Je kwa upande wa viongozi wa CCM bara, watakuja Lamba matapishi yao?
Kwa upande wa inayoitwa "Tanzania Bara", iwapo Mgombea Urais wa Muungano atatokea nchi jirani ya Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake "automatically" pia atatokea Zanzibar, watakaoongoza katika kupinga hali hii haitakuwa watu wengine bali wale wale makada wa CCM ambao ndani ya bunge la katiba walijiita kwa majigambo Kwamba wao Ndio wenye "Maoni ya Walio Wengi", ambao wamepitisha katiba inayopendekezwa kwa vigele gele na
Vifijo. Fitina zilizomkumba Dr. Salim Ahmed Salim alipokuwa anawania urais hazitafua dafu kwa fitina zitakazojitokeza katika mazingira tunayojadili hapa. Wana CCM ambao watakuwa katika makundi ya kutafuta Rais wa Muungano wataendesha kampeni kubwa kupinga uongozi wa Muungano kwenda kwa "nchi jirani katika kofia zote mbili za juu – Rais wa Muungano na Makamu wa Rais wa Muungano.
Kuna haja ya wazanzibari na watanganyika kuungana kuzuia hatari iliyopo Mbeleni. Ujumbe muhimu kwa wazanzibari ni Kwamba wanachoambiwa na CCM ndani ya rasimu inayopendekezwa ni kwamba:
• "Kuanzia sasa, wazanzibari wajiandae tu kisaikolojia kuwa ni "wasindikizaji" tu wa Uongozi" katika Jamhuri ya Muungano."
Pia CCM nayo ijiandae kutupiwa lawama na malalamiko mapya juu ya Ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar. Mbegu ya kuvunjika kwa muungano sio tu imeshapandwa, Bali pia imeanza kuchepuka.
Itaendelea ambapo tutajadili athari za katiba inayopendekezwa - athari Katika maeneo mengine ya uchumi, rasilimali, bunge, Mahakama, mikopo, uhusiano wa kimataifa n.k, hoja ikiwa ni jinsi gani maeneo haya yataathirika chini ya katiba inayopendekezwa, na jinsi gani yatazidi kuudhoofisha muungano wa serikali Mbili na hatimaye muungano huo kuvunjika.
Cc
Dingswayo,
Mag3,
EMT,
Mkandara,
Barubaru,
Bongolander,
ukwelikitugani,
happyfeet,
Pasco,
Jasusi,
JokaKuu,
MTAZAMO,
Mwigulu Nchemba,
Ezekiel Maige,
MJINI CHAI,
gfsonwin Mimibaba Zakumi
Sent from my iPhone using JamiiForums