Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

Nimeogopa kuongelea Ubungo na Kiembe Samaki kwasababu itabidi John Mnyika apewe ving'ora kama Rais wa Unguja! teeh tehe tehe . Mkuu znz unayodhani ni Tembo, ni panya mkuu. Huko US mkuu unashuguulika na nini.
Huku huwa nabeba mabox na kuyweka kwenye containers, nikimaliza kazi hiyo huwa naenda kazi nyingine ya kuosha vyombo kwenye hoteli moja. Weekends mara nyingi nipo na family na pia huwa nanunua vitu huku na kuvileta bongo, hasa vitu used ambavyo watu wananiagizia ..... Kwani vipi?
 
Ok hilo jambo jema kabisa. Nilikuwa naulizia maana baada ya kura ya Scotland, Washington post, Huffington Post, New times n.k. yameandika sana kuhusu mgogoro wa Bernett Formula. Naona ulikuwa busy hukupitia pitia. Ukaja moja kwa moja kuchangia kwa hisia zako.

Ahsante mkuu kazi njema, hiyo red and white stripes inashikwa na kila mmoja si, kila mtu anajua value yake isipokuwa brave tu
 
You are funny!
NIKAJA MOJA KWA MOJA WAPI? Niliyokuambia ndiyo sababu ya 4.5% na 21% nilishawahi kukujibu almost a month ago.
Labda kama unataka kunionyesha kama sijui Barnett Formula .....
Na hiyo siyo sababu ya kuuliza shughuli yangu.
 
Siku zote huwa unazusha kuwa mimi nakukimbia, mimi siwezi kumkimbia mtu pointless kama wewe. Na nimeshakujibu kuhusu 4.5% mara nyingi tu. It's based on population i.e wazanzibari ni 4.5% ya watanzania. Na kimadaraka ni 20% ya Tanzania i.e 5 regions out of 25 regions. Ndiyo maana Warioba alipendekeza bunge la Muungano liwe hivyohivyo ... GOT IT NOW????

Kwanini unalazimisha uongo? Nani Kakuambia wazanzibari ni 4.5% ya watanzania? Hiyo hesabu umeipataje? Hivi unajua formula hii asili yake ni nini kweli au unarukia tu. Unajua ilibuniwa lini na ilitakiwa kutumika kwa muda gani? Nimejadili haya Huko juu, ukipata Muda Kasome.

Na Nani Kakuambia Tanzania Ina jumla ya mikoa 25? Na hata Kama ingekuwa kweli (ingawa sio kweli), uhusiano wa idadi ya mikoa na nafasi za Ajira wapi na wapi? Yani mikoa mitano Zanzibar yenye jumla ya wakazi 1.3 million ipate 21%, na mikoa mingine yote ya bara kila mmoja ukiwa na wastani wa idadi ya wakazi wa Zanzibar nzima Kama sio zaidi, ipate 79%, huku humo humo the 1.3 million zanzibaris pia wakipewa fursa? Please! Kajipange na hoja kwanza Kabla ya kuja kudanganya Watu Hapa.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
[quote="Mchambuzi, post: 10857787" ] Kwanini unalazimisha uongo?Nani Kakuambia wazanzibari ni 4.5% ya watanzania? Hiyo hesabu umeipataje? Hiviunajua formula hii asili yake ni nini kweli au unarukia tu. Unajua ilibuniwalini na ilitakiwa kutumika kwa muda gani? Nimejadili haya Huko juu, ukipataMuda Kasome.

Na Nani Kakuambia Tanzania Ina jumla ya mikoa 25? Na hata Kama ingekuwa kweli(ingawa sio kweli), uhusiano wa idadi ya mikoa na nafasi za Ajira wapi na wapi?Yani mikoa mitano Zanzibar yenye jumla ya wakazi 1.3 million ipate 21%, namikoa mingine yote ya bara kila mmoja ukiwa na wastani wa idadi ya wakazi waZanzibar nzima Kama sio zaidi, ipate 79%, huku humo humo the 1.3 millionzanzibaris pia wakipewa fursa? Please! Kajipange na hoja kwanza Kabla ya kujakudanganya Watu Hapa

Nilipoona hajui hata nchi ina mikoa mingapi,nilijiuliza hiyo formula anaijua imepatikanaje au ! Maana hata kwa kuhisi mtuhawezi kwenda fyongo kiasi hicho. Sina uhakika kama anajua kuna mkoa Wa Manyara,Geita, Njuluma n.k.

Halafu anasema hiyo populaion ni 1.3M bado hajaeleza kuwanusu yake inaishi Tanganyika.

Tulionyesha wazi kuwa katika 21% ni wazanzibar tu, lakini pia wanaingia katika 79% kama Watanzania.
Masikini hakuweza kupata hata simple logic, mwenzetu kadandia treni ikienda. Ndio hasa sababu za kumwambia ameingia tu kwa hisia.

Huyu bwana, hatambui kuwa wazanzibar wanalalamika ajira za halamshauri, na baadhi ya wizara kama ujenzi, kilimo, afya, elimu n.k.ambazo si za muungano wafanyakazi wake ni wa muungano.
Wznz wanataka wafanyakazi hao waondolewe kwasababu ni haramu''

Wakati wakisema ni haram, wznz hao hao wanachukua 21 ya haramu, halafu wanaviazia 79 ya haramu.
Mwenzetu hilo ni kama mujiza, hana ufahamu, unconscious! Haelewi kuwa wznz ni Watanzania ndani ya 79 halafu ni wazaznibar ndani ya 21.

Yeye kaota formula kama ya kijana wa kidato cha nne,halafu anapulizia ubani na manukato kwa kusema aulizwe yeye yupo Marekani.
 
Nimekupa jibu murua kabisa!! .... hizo numbers hazijatoka from the air bali zime-base kwenye kitu Fulani. Now, wether it makes sense to you or not, that's another issue. Halafu kukaa Marekani ni uchaguzi tu wa mtu kuendesha maisha yake, haimaanishi kuwa ninatakiwa niwe juu kuliko let say anaekaa bongo. UNACHEMSHA!
Comrade,
Inabidi uwavumilie hawa ndugu zetu kwa sababu wao wakikosa hoja wanaanza kejeli na kuita majina kana kwamba kujua majina, maisha ya mleta hoja na kazi yake ndiyo njia ya kujenga hoja mbadala.

Niliwaambia kitambo, kutumia nguvu nyingi za hoja za nguvu na nguvu za hoja bila uhalisia wa siasa zetu ni kupoteza muda.

Tanzania iliyopo siyo hiyo wanayoidhani katika fikra na mitazamo yao, lakini kilicho cha muhimu zaidi, ni Watanzania hao hao kwa uwingi wao wanaoamua maisha yao kitaifa.

Kwa sasa hoja waliyobaki nayo eti Tanganyika itadaiwa kwa nguvu. My left foot.

Kila mara nilikuwa ninawaambia, badala ya kujenga hoja za kujiaminisha nyuma ya keyboard/keypad, ingekuwa ni vizuri wakazijongea siasa zetu kwenye political epicenter.

Bila kuufahamu ukweli, wataendelea kuwa na msongo wa jambo ambalo hawawezi kulibadilisha leo au kesho. Watanzania wengi kupitia wajumbe wa Bunge Maalum hawajawa tayari na jambo lao kama ilivyoonekana kwenye Bunge Maalum la Katiba. Hata kama kesho au kesho kutwa tukienda kwenye Kura za Maoni, jibu litakuwa kama lilivyotolewa na Bunge Maalum.

Hii ndiyo hali halisi ya Tanzania katika kioo cha siasa.

Rais Kikwete amewashauri na kuwaambia, wasipoteze muda, wasubiri hayo ya kwao katika muda wake kwa sababu kwa sasa hayakubaliwi pamoja na kwamba labda yanaweza yakawa mazuri. Haisadii kwa sasa kushupaa kwa jambo ambalo limekataliwa na Wajumbe wa Bunge Maalum kwa sababu huu siyo muda wake.
 
Nilipoona hajui hata nchi ina mikoa mingapi,nilijiuliza hiyo formula anaijua imepatikanaje au ! Maana hata kwa kuhisi mtuhawezi kwenda fyongo kiasi hicho. Sina uhakika kama anajua kuna mkoa Wa Manyara,Geita, Njuluma n.k.

Halafu anasema hiyo populaion ni 1.3M bado hajaeleza kuwanusu yake inaishi Tanganyika.
Tulionyesha wazi kuwa katika 21% ni wazanzibar tu, lakini pia wanaingia katika 79% kama Watanzania.
Masikini hakuweza kupata hata simple logic, mwenzetu kadandia treni ikienda. Ndio hasa sababu za kumwambia ameingia tu kwa hisia.

Huyu bwana, hatambui kuwa wazanzibar wanalalamika ajira za halamshauri, na baadhi ya wizara kama ujenzi, kilimo, afya, elimu n.k.ambazo si za muungano wafanyakazi wake ni wa muungano.
Wznz wanataka wafanyakazi hao waondolewe kwasababu ni ‘’haramu’’

Wakati wakisema ni haram, wznz hao hao wanachukua 21 ya haramu, halafu wanaviazia 79 ya haramu.
Mwenzetu hilo ni kama mujiza, hana ufahamu, unconscious!

Haelewi kuwa wznz ni Watanzania ndani ya 79 halafu ni wazaznibar ndani ya 21.

Yeye kaota formula kama ya kijana wa kidato cha nne,halafu anapulizia ubani na manukato kwa kusema aulizwe yeye yupo Marekani.

Kwa kuongezea, Kobello, MwanaDiwani, Tusaidieni Hapa:

Maamuzi ya 4.5% and 21% kwa mmoja ya washirika wa muungano I (Zanzibar) yalifanywa on what:

1. Economic basis?
2. Legal basis? And
3. Democratic basis?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Comrade,
Inabidi uwavumilie hawa ndugu zetu kwa sababu wao wakikosa hoja wanaanza kejelina kuita majina kana kwamba kujua majina, maisha ya mleta hoja na kazi yakendiyo njia ya kujenga hoja mbadala.

Niliwaambia kitambo, kutumia nguvu nyingi za hoja za nguvu na nguvu za hojabila uhalisia wa siasa zetu ni kupoteza muda.

Tanzania iliyopo siyo hiyo wanayoidhani katika fikra na mitazamo yao, lakinikilicho cha muhimu zaidi, ni Watanzania hao hao kwa uwingi wao wanaoamua maishayao kitaifa.

Kwa sasa hoja waliyobaki nayo eti Tanganyika itadaiwa kwa nguvu. My left foot.

Kila mara nilikuwa ninawaambia, badala ya kujenga hoja za kujiaminisha nyuma yakeyboard/keypad, ingekuwa ni vizuri wakazijongea siasa zetu kwenye politicalepicenter.

Bila kuufahamu ukweli, wataendelea kuwa na msongo wa jambo ambalo hawawezikulibadilisha leo au kesho. Watanzania wengi kupitia wajumbe wa Bunge Maalumhawajawa tayari na jambo lao kama ilivyoonekana kwenye Bunge Maalum la Katiba.Hata kama kesho au kesho kutwa tukienda kwenye Kura za Maoni, jibu litakuwakama lilivyotolewa na Bunge Maalum.

Hii ndiyo hali halisi ya Tanzania katika kioo cha siasa.

Rais Kikwete amewashauri na kuwaambia, wasipoteze muda, wasubiri hayo ya kwaokatika muda wake kwa sababu kwa sasa hayakubaliwi pamoja na kwamba labdayanaweza yakawa mazuri. Haisadii kwa sasa kushupaa kwa jambo ambalolimekataliwa na Wajumbe wa Bunge Maalum kwa sababu huu siyo muda wake.
Well,nadhani hukufuatilia mjadala.

Huyo bwana alisema aulizwe kwasababu anaishiMarekani, ndicho chanzo cha kuanza kumuuliza. Lakini pia, tumemuuliza kwasbabutulizosema. Baada ya suala la Scotland, magazetui mengi ya Marekaniyamezungumzia sana hatima ya Uingereza yakigusia Bernett Formula inayotumika najinsi ahadi za Cameron na wenzake zitakavyokumbana na hoja ya England. Hivyo,huyo bwana wa Marekani iweje asiyaone hayo?

Hata ya Tanzania hayajui. Leo 2014 kama kuna mtu anaaminiTanzania ina mikoa 25 na formula ya kupata 21% ya ajira na 4.5% ya pato laTanganyika kwenda znz inategemea mgawanyo wa mikoa 25, ni out of touch na mamboya nyumbani na huko ughaibuni. Ni fact hata kama ina maumivu

Mfano wako kuhusu kauli ya Kikwete kuwa wenye kutaka S3wasubiri ni mbovu sana na una mu-expose Kikwete katika mambo haya.

1. Kwanzaalianzisha mchakato nje ya chama, halafu chama kikateka mchakato.
Katikaleadership hiyo ni kukosa vision. Hakujua mambo yataendaje au yataishaje. Kosala kwanza.

2. JK alitakiwa tafute suluhu ya tatizo la muungano kwa njiamuafaka. Kukubali znz ibadili katiba na kuwa juu ya katiba ya JMT ni kosa laRais aliyeko madarakani.

3. JK alipaswa kuanza na kura ya maoni baada ya mswadakuchanwa mbele ya John Smawel Sitta

4. JK alifanya makosa kuteua makada wa CCMna kujaza wanasiasa wengi badala ya wananchi

5. JK alikuwa kigeugeu kilaalipokutana na wapinzani dalili ya kukosa msimamo na udhaifu.

6. JK alikuwa nahabari zote kuhusu S3. Angeweza kuzuia mchakato. Wajumbe wa tume wamesemaalijua kila hatua.

7. JK alikwenda kuongea na wana CCM na kuwaambia wajiandaena S3.

7. JK akaongea na TCD na kuwaambia maoni ya wananchi yaheshimiwe.

8. JKakaenda kuvuruga bunge kwa madai jeshi litapindua nchi

9. JK akautana naWapinzani, aahidi kuahirishwa mchakato.

10. JK aenda Dodoma kupkea rasimu yafacebook n.k.

Unapotolea mfano wa kauli ya JK kama kauli za viongoziwengine unatukosea heshima.

JK hana msimamo, anayumba, dhaifu, ana unafiki nawala hana ufahamu wa kile anachosimamia.

Ni kiongozi anayeongoza kuwapendezawatu na wala si kuongoza.

Pengine ndio maana majirani wameamaua kutetenga maanamtu anayebadilika kama kinyonga huyo ni wa kuangalia sana. Hivyo kama ni rolemodel ni kwako, nina uhakika taifa hili halitamkumbuka baada ya muda wakeisipokuwa pale tu utakapotajwa uovu au mambo ya hovyo.

Kuhusu Tanganyika, hilo wala lisikutie shaka.Watanganyika wanaona na wanaelewa yanayoendelea hadi sasa.
Kwa ufupi, hakunamznz mwenye heshima tena baada ya kugundua kuwa hawana msaada, walahatuwahitaji na hatuwategemei.

Unakumbuka bungeni wameambiwa live kuwa wao ni tatizo.Hilo litaendelea kwasababu Watanganyika wamebaini yote kuhusu kunyonywa, niuongo, Wao ni kupe wakubwa sana mgongoni.

Na sheria za mitaani zitakapoanzakutumika, wewe na CCM wenzako mtaelewa tulionya kitu gani.
Prof Kabudi kasemaWatanganyika wana yao vifuani, siku yakiioka. Kuhusu hoja, mbona tuna hoja nyingi hambazo wewe nawenzako hamzijibu?
1. Hebu tuambie je, mumuweza kujibu hoja za Tanganyika kuvaakoti
2. Mumeweza kujibu hoja za Watanganyika kubeba muungano.
3. Mumewezakujibu hoja za Tanganyika kulipia gharama za SMZ na watu wake?

Na hapa nakuja kwako specific
1. Hebu tueleze, kama ardhini ya muungano na mafuta na gesi ya znz si ya muungano, hayo mafuata na gesiyapo katika ardhi ya nchi gani?

2. Kwanini mafuta na gesi ya Tanganyika yawe yamuungano yale ya znz yawe ya znz

3. Gharama za Tanganyika kwa 4.5 zipo katikaformula gani? Rejea swali la mchambuzi hapo juu

4. Je, suala la ajira hiyo 21%ya ajira za Tanganyika kwa znz inapatikana kwa utaratibu gani na formula gani.Na je 79 ni ya Tanganyika au ni ya Tanzania. Kama ni ya Tanzania mznaznbiaranaruhusiwa pia.

5. Kuna uhalali gani mwanafunzi wa Tanganyika asome kwamkopo katika nchi yake, yule wa nchi jirani ya znz asome bure

6. Tuambie gharama za S2 na zile za S3 ya warioba zipi kubwakwa rasimu ya Chenge na Sitta

Hebu tuanza hapa kwanza, Kumbuka hatutajadili rasimu ya Chenge bila kurejea ubovu na uozo wa facebook kule Dodoma. Hivyo jiandae kwa hilo.Hatutajadili haramu tunajadili mambo yaki taifa.
 
MwanaDiwani, #66 :

Nilisha kueleza Kwamba hauna uelewa Katika masuala haya ya mabadiliko ya katiba zaidi ya uelewa wa kupuliziwa kwenye akili Kama upepo wa Tairi Gereji na CCM. Tazama jinsi gani hoja zako zilipwaya Katika Uzi wako wa "siasa za Zanzibar na hatima ya Tanzania". Katika Uzi ule, ulionyesha bayana jinsi gani usivyojua siasa za Zanzibar kwani to you, siasa hizi ni synonymous to siasa za ASP na TANU. Ni kutokana na uelewa wako finyu, that thread failed to cover much mileage. Uzi ukafeli kutimiza Malengo yake.

Nikirudi kwenye hoja ya msingi ambapo unaendelea kukipamba chama cha mapinduzi Kwamba kimelipatia taifa katiba murua kwa wananchi, Ni wazi Kabisa Kwamba rais Kikwete na CCM waliingia Katika mchakato wa katiba kwa Shingo upande bila ya utashi wa kisiasa. Katiba mpya haikuwa agenda au msimamo wa rais au wa chama cha mapinduzi, Bali shinikizo nje ya CCM na serikali yake. Ushahidi juu ya hili upo wazi, lakini nitajadili kwa uchache:

Wasaidizi wa rais serikalini - mwanasheria mkuu wa serikali (werema) na waziri mwenye dhamana wa Wakati ule - waziri wa Sheria (Kombani), historia tayari imeshawaandika wote Kwamba walikwishatoa maoni Yao ambayo yalikuwa ni maoni ya serikali ya CCM ya Kupinga umuhimu wa taifa Kupata katiba mpya. Sasa Leo unapata wapi Nguvu za kusifia mchakato Ambao CCM na serikali yake ziliuvamia kwa Shingo upande na bila ya utashi wa kisiasa? Sio wewe Wala viongozi wa CCM wenye moral authority Katika hili.

Historia itakuja andika Kwamba Haiwezekani Kwamba mwanasheria mkuu wa serikali na waziri wa Sheria wakurupuke na matamshi Yao Kupinga haja ya taifa Kupata katiba mpya, Bali walifanya hivyo baada ya kujiridhisha Kwamba uongozi wa nchi na uongozi wa chama cha mapinduzi hawataki katiba mpya, na hapo ndipo wakatoa kauli zao Kupinga wazo la katiba mpya.
MwanaDiwani, CCM iliparamia Taratibu za mchakato wa katiba mpya, na uparamiaji huu ulianza kwa Mara ya kwanza baada ya Sheria ya mabadiliko ya katiba namba "8" kuwasilishwa bungeni (bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania). Ndani ya bunge lile kulikuwa na vuta nikuvute baina ya wabunge wa CCM na wabunge wa upinzani, lakini pia upinzani na serikali ya CCM. Wabunge wa CCM wakashirikiana na serikali Yao kuhakikisha Kwamba kinachopitishwa na bunge ni Kile tu ambacho kitalinda maslahi Yao, na sio maslahi ya wananchi. Huu ulikuwa ni utekelezaji wa Kile kilichoamriwa Katika kikao cha halmashauri kuu ya taifa (NEC) kilichofanyika Dodoma mwezi Mei, 2012. Ni Katika kikao Hiki, CCM Ndio ilifanya uamuzi Rasmi nini kiingizwe Katika katiba mpya na nini kiachwe.

Historia itakuja andika Kwamba - Ni msimamo huu wa serikali Ndio uliosababisha Sheria ya mabadiliko ya katiba kurudishwa bungeni zaidi ya Mara tano Katika kipindi cha miaka miwili ikiwa ni pamoja na tarehe 11 march 2011, November 18 2011, February 9, 2012 na September 6, 2013.

Historia itakuja andika Kwamba - Eneo kubwa ambalo wengi walipinga lilihusiana na rais kukabidhiwa jukumu la kuteua wajumbe wa BLK. Hoja ya msingi ikawa Kwamba kwa kumpa rais madaraka ya aina hii, bunge husika halitakuwa na uhuru wa Kuandaa katiba mpya kufuatana na maoni Yao kwa tume ya jaji warioba. Hakuna aliyesikilizwa, lakini Leo mnatafuta credit kwa Jambo ambalo mlishalivuruga. Mlishatanguliza maslahi ya CCM na maslahi yenu binafsi tangia Mei 2012. Matokeo yake, waliokuja kuteuliwa Kama wajumbe wa BLK, wengi wao wakawa ni makada wa CCM. Idadi Yao kamili ilishajadiliwa kwahiyo tusipoteze muda Katika hili.

Historia itakuja andika Kwamba - Bunge la katiba likageuka kuwa mkutano mkuu wa CCM bila ya kujali Kwamba rasilimali zinazotumika kuendesha bunge lile ni za watanzania wote milioni 45, sio za wanachama wa CCM milioni 5 (na hata hii idadi sio ya kweli). Hadi Hapa tunaona Kwamba CCM ilikuwa tayari Ina katiba yake kichwani, lakini pia ilikuwa inafanya kazi ambayo hawakuipenda.

Katika uteuzi wa wajumbe 201, CCM iliamua kupuuza historia, CCM ilikataa kukumbuka kilichotokea Mara ya kwanza bungeni na kupeleka muswaada huo kurudishwa bungeni Mara tano. CCM haikutaka kujikumbusha Kwamba muswaada wa mabadiliko ya katiba uliwasishwa bungeni kwa hayo ya dharura 15 Aprili 2011 na ukapingwa kila kona, na hata Samuel Sitta alichomewa muswaada huo Mbele yake Kule unguja. Serikali ikaamriwa na spika Anna Makinda Kwamba iondoe muswaada huo kutoka Katika hayo ya dharura na badala yake uingizwe Katika utaratibu wa kawaida. Makinda pia akatoka amri Kwamba muswada huo uchapishwe kwa lugha ya Kiswahili, utangazwe kwenye media zote na pia sehemu yake ya utangulizi iwekwe vizuri ili wananchi waelewe kwa lugha Rahisi Kabisa juu ya kilichomo mle. Hata hivyo, Kama vile historia itakavyokuja kuandika, hakuna hata agizo moja ambalo lilitekelezwa. Kilichokuja kuitwa "muswada mpya" hakikuwa na tofauti na kilichoondolewa bungeni.

Yaliyofuatia baada ya hapo sote tunajua, na historia itaweka wazi - yani kuanzia kuvunjwa kwa tume ya katiba bila utaratibu, tovuti ya tume kufungwa nje ya utaratibu, uchakachuaji wa Sitta wa kanuni ambao ulimruhusu rais kuja kuhutubia BLK baada ya jaji warioba as if rais ni mmoja wa wajumbe wa bunge lile, lakini Mbaya zaidi kuweka msimamo wa CCM ili wajumbe wa BLK watekeleza Yale ambayo CCM inataka yatekelezwe.

Sio hivyo tu, BLK likajipa mamlaka nje ya Sheria husika na Kuanza kuondoa maoni ya wananchi, kubandikwa sura mpya na uchakachuaji mwingine. Mchakato wa katiba ulitarajiwa kupitia hatua kuu nne:

1. Kukusanya maoni.
2. Kuboresha rasimu ya kwanza kupitia mabaraza ya katiba kwenye kata.
3. Kujadiliwa ndani ya BLK.
4. Kupigiwa kura ya maoni.

Popote pale, inapoundwa tume ya katiba, bunge maalum (constituent assembly) haiwezi kujigeuza kuwa tume ya katiba. Kwa Tanzania, CCM imefanya kituko Hiki. Bunge maalum halipaswi Kabisa kuita wakulima, wafugaji, wavuvi, wahunzi ili watoe maoni Yao. Kufanya hivyo ni Kinyume cha Sheria, na katiba inayopitia hatua Kama hii ni katiba haramu. Bunge la katiba halitakiwi kujitwisha mamlaka ya Mahakama kutafsiri Sheria. BLK halipaswi kung'oa ibara za rasimu na kuingiza ibara mpya. Badal yake, kazi ya BLK ni kuboresha rasimu tu, kwisha.

Kuchakachua maoni yaliyowasilishwa na tume haikuwa tu CCM kudharau kazi za wananchi na tume ya warioba, Bali hata CCM kujipa jukumu la kuvunja muungano. Muungano uliundwa na TANU na ASP, na muungano utavunjwa na chama cha mapinduzi (CCM). Historia itakuja wahukumu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
MwanaDiwani CCMwalisema takwimu za Warioba zilikuwa chache. Tunaomba utueleze hapa, SawmwelSitta alipewa nguvu na sheria gani ya nchi hii kujiteua kama tume ya kukusanyamaoni?

Pili, iweje CCM itumie watoa maoni takribani 30waliohojiwa na Sitta na kuyaingiza katika katiba ikiwa, yale 18,000 ya Wariobahayakuwa yanatosha?

Tueleze, ni sheria au kanuni gani ziliruhusu wabunge 2kupiga kura, na kwavile CCM walisema ni kura ya wazi, kwanini Sitta ameficha

Tueleze, mahujaji waliwezaje kupiga kura wakiwa katikaIbada yao. Nani alihakiki kura za facebook na fax, yahoo na google

Tueleze kwanini Sitta alikataa uwakilishiw wakati wakuhesabu kura

Tufahamishe iweje hadi leo katibu wa bunge anajadiliwaliopiga kura na wasiopiga kura. Hiyo 2/3 ya BMK-CCM ilipataikana vipi? Tueleze, mwanasheria mkuu wa znz amefukuzwa kazi kwa kosala kura yake. Je, uwepo wake ulikuwa kama mwanasheria au kama mjumbe. Na kamani mwanasheria, kitendo cha yeye kupinga rasimu kinamaanisha nini katika uzaniwa kisiasa. Tueleze, Rais Kikwete aiposema S3 zisubiri hadi aondoke,ili hali akijua kila kilichoendelea katiaka tume, alikuwa na maana gani nakwanini alaicha mchakato ukaendelea.

Na mwisho tueleze, ni lini suala la katiba limekuwa hojaya CCM. Liliingizwa katika vikao kwa utaratibu gani. Kumbuka maji ukiyavulia nguo.
 
Last edited by a moderator:
barubaru, kwa mtazamo wangu wazanzibar ndio wenye tatizo hilo la unafiki kuliko wabara, wao wakiwa Zenji watakuambia ni nchi kamili na wengi wanataka NKataba, wakivuka maji tu kuja nchi jirani ya Tanganyika watakuambia Zanzibar sio nchi ni sehem ya JMT, mfano halisi hata raisi wao kauonyesha juzi wakati wa makbidhiano ya rasimu ya CCM pale Dodoma, katamka wazi Zanzibar ni sehem ya JMT na sio nchi, kiukweli Zanzibar inaihitaji zaidi Tanganyika than Tang. Needs Zanzibar.

Tatizo la Watanganyika ambalo basically ndio linawatesa ni uoga wao kulidai jina la Tanganyika kwa uhuru na kuongea wazi kwamba tunaotaka kupumua ni Watanganyika maana nchi jirani ya Zenji wanatutegemea na kutunyonya kwenye mengi kuanzia Kiuchumi, ulinzi, Elimu na mengi neyo.

Ahali yangu sisi tunaamini wazi mwanaume kamili au wanywezi wanasema NYANDA jilili ni yule anayezungumza hadhwarani na sio yule anayejificha chooni na kupaza sauti.

Kumbuka waZnz wamezungumza pale mjengoni dodoma ugenini mbele ya waziri mkuu wenu kuwa iwe nkataba au 3 au hata moja LAKIN LAO NI KUTAKA ZNZ YENYE MAMLAKA KAMILI yaani wajitawale kwa kila nyanja na sio mpaka kwa ihsani ya Tgk.

Jiulize ni Mtgk gani mwenye kwenda Znz na kuthubutu kusema yale ya Keissy kule Znz. Nafikiri uliona hata Keissy aliporopoka walitaka kumshushia kipigo pale pale kwake Dodoma na hakuna Mtgk aliyethubutu kumsaidia zaidi ya doula kumlinda.

Hivi ukiliona DUME LINANUNG'UNIKA CHOONI utalionaje?

Kumbuka Znz wanataka mamlaka kamili na sio lingine. na ndio hilo wanalopigania.

Pole sana
 
Barubaru,

Sioni mantiki ya kumjadili mbunge a nkasi, Kessy Kama mfano wa watanganyika wote kushindwa kumalizia the last mileage ya kudai Tanganyika Yao.

Alichofanya Nguruvi3 ni kumtumia mfano bwana kessy Kama mtanganyika bungeni na Mwana CCM ambae na yeye sasa anaona hoja zetu Zipo wapi, basi. Suala la yeye Kupiga kura ya kuunga Mkono rasimu ya CCM halina maana Kama suala Kwamba wapo wabunge na wana CCM wengi ambao wanaona Ukweli upo wapi lakini kinachowazuia ni vitisho, Tena kwa mfano, kwa kessy, sio vitisho kutoka kwa CCM bara tu, Bali hata waZanzibari. Turudi kwenye mada.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Wanaotaka Tanganyika ni wachache zaidi ya ambao hawajali uwepo wake. Watanzania bara wengi hawajali haya mambo ya serikali tatu kama mnavyoaminishwa.
Kobello, alianza Kinana na dai kwamba kwa Watanzania wengi uwepo wa Katiba mpya si kipaumbele chao kwani wanachojali zaidi ni maendeleo yao. Akaja Nape Nnauye akasema Watanzania wengi hawahangaishwi na swala la Katiba mpya, wanachojali ni barabara na upatikanaji wa maji. Leo na wewe ume join the band wagon kwamba wanaotaka Tanganyika ni wachache zaidi ya ambao hawajali uwepo wake na kwamba Watanzania bara wengi hawajali haya mambo ya serikali tatu kama tunavyoaminishwa.

Sasa na mimi nauliza; ni kwa tafiti zipi mnatoa haya madai ya kipuuzi? What's wrong with you guys? Kwamba bila haya wala soni unaweza kutetea mambo ya kilaghai, kihuni na kipuuzi yanayotendeka nchini kama tulivyoshuhudia ndani ya kinachoitwa Bunge Maalum La Katiba? Halafu mtu anajiita msomi akidai ameishi ughaibuni muda mrefu...talk of taking an African out of the bush but never taking the bush out of him, that's what! Kobello, je unadhani CCM wanaweza kuthubutu kuruhusu level playing field wakati wa kampeni ya for and against Katiba ya CCM (Chenge/Sitta) kwenye kura ya maoni?
 
Mkuu Mag3, kina Kobello wa ughaibuni Ndio hawa waliokuwa na balozi wao Ombeni Sefue pale Washington. Sefue karudi hapa na kukwea ukatibu kiongozi lakini ameshindwa kuonyesha uwezo wake wa kiuongozi. Kwa mfano, kwa mantiki Kama hizi za Kobello na wenzao wa ughaibuni, Sefue anatetea uharibifu wa kina Sitta na Chenge bungeni na kudai Kwamba ni sahihi kuweka Kando mjadala wa muundo wa muungano kwasababu eti suala hili limeligawa taifa. Sefue akaendelea kusema Kwamba "muundo wa sasa utabaki Kama ulivyo sasa kwa kuwa bunge limeshindwa Kupata maridhiano juu ya Jambo Hilo". Swali letu kwa Sefue na wenzake akina kobello ni hili:

• ikiwa serikalini hakuna muafaka Katika muundo wa serikali Tatu, upo wapi muafaka wa serikali Mbili? Makubaliano yake yanatokana na nini? Hoja Zipi? Hoja za Nani? Lini na wapi?

• iwapo hakuna muafaka juu ya muundo wa muungano, kuna muafaka Katika masuala ya tunu za taifa? Maadili na miiko? Muundo wa bunge? Mapato ya serikali ya muungano?

Cc chama, MwanaDiwani, ZeMarcopolo.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuongezea, Kobello, MwanaDiwani, Tusaidieni Hapa:

Maamuzi ya 4.5% and 21% kwa mmoja ya washirika wa muungano I (Zanzibar) yalifanywa on what:

1. Economic basis?
2. Legal basis? And
3. Democratic basis?

Sent from my iPhone using JamiiForums
All of the above, based on population as a major variable. Maamuzi yalifanywa na serikali zote mbili baada ya kufuata uamuzi wa IMF kwenye mgao wa BOT ('96).
Baadae (starting 2006 ) Mfumo huohuo ukafuatwa na ministry of finance kwenye mgao wa General Budget.

Formula ilitumia Population, like it or not na mgao wa ajira ulitumia regional blocks
Erasmus University Thesis Repository: Ownership on Aid, Rhetoric or Reality? The case of Zanzibar: The Semi- Autonomous State of Tanzania Chapter 3.
 
Mkuu Mag3, kina Kobello wa ughaibuni Ndio hawa waliokuwa na balozi wao Ombeni Sefue pale Washington. Sefue karudi hapa na kukwea ukatibu kiongozi lakini ameshindwa kuonyesha uwezo wake wa kiuongozi. Kwa mfano, kwa mantiki Kama hizi za Kobello na wenzao wa ughaibuni, Sefue anatetea uharibifu wa kina Sitta na Chenge bungeni na kudai Kwamba ni sahihi kuweka Kando mjadala wa muundo wa muungano kwasababu eti suala hili limeligawa taifa. Sefue akaendelea kusema Kwamba "muundo wa sasa utabaki Kama ulivyo sasa kwa kuwa bunge limeshindwa Kupata maridhiano juu ya Jambo Hilo". Swali letu kwa Sefue na wenzake akina kobello ni hili:

• ikiwa serikalini hakuna muafaka Katika muundo wa serikali Tatu, upo wapi muafaka wa serikali Mbili? Makubaliano yake yanatokana na nini? Hoja Zipi? Hoja za Nani? Lini na wapi?

• iwapo hakuna muafaka juu ya muundo wa muungano, kuna muafaka Katika masuala ya tunu za taifa? Maadili na miiko? Muundo wa bunge? Mapato ya serikali ya muungano?

Cc chama, MwanaDiwani, ZeMarcopolo.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mchambuzi, hakuna Mtanzania mwenye akili timamu ambaye yuko ughaibuni kwa jitihada zake mwenyewe ambaye kwa namna yoyote ile anaweza akatetea ujinga, uhuni, ulaghai na upuuzi unaofanyika nchini. Wote wanaofanya hivyo ni ama ni kwa tamaa, ulafi, utumwa au unafiki; sifa ambazo zimewaganda kama kupe kwa sababu tu ya kutegemea fadhila za hilo genge la mafia lililokamata madaraka.

Hao akina Kobello ndio hao hao; wanaishi kwa kuwalamba miguu watawala wasije wakawasahau huko mbele ya safari; mtu uliyebahatika kupata exposure ya kushuhudia tawala za kistaarabu zinavyofanya kazi utateteaje uendeshaji wa mambo kihovyohovyo kama tunavyoshuhudia kila kukicha? Wengi ama ni ndugu, washikaji au washirika wao na wanao wajibu wa kutetea status quo...hiyo kwao ni amri.
 
Last edited by a moderator:
Sasa na mimi nauliza; ni kwa tafiti zipi mnatoa haya madai ya kipuuzi? What's wrong with you guys? Kwamba bila haya wala soni unaweza kutetea mambo ya kilaghai, kihuni na kipuuzi yanayotendeka nchini kama tulivyoshuhudia ndani ya kinachoitwa Bunge Maalum La Katiba? Halafu mtu anajiita msomi akidai ameishi ughaibuni muda mrefu...talk of taking an African out of the bush but never taking the bush out of him, that's what! Kobello, je unadhani CCM wanaweza kuthubutu kuruhusu level playing field wakati wa kampeni ya for and against Katiba ya CCM (Chenge/Sitta) kwenye kura ya maoni?
Kasome hapa http://www.afrobarometer.org/files/documents/media_briefing/tan_r5_mediabriefing.pdf ukurasa wa 22.

hayo mambo ya ughaibuni na usomi ni kelele zako za kipuuzi tu ambazo hazina maana kwangu. Na hayo mambo ya bush au kuwa mjini hizo ni fikra zako za kipumbavu ambazo sina muda nazo. Go read that research, then you can decide to accept/reject it.
 
Mkuu Mag3, kina Kobello wa ughaibuni Ndio hawa waliokuwa na balozi wao Ombeni Sefue pale Washington. Sefue karudi hapa na kukwea ukatibu kiongozi lakini ameshindwa kuonyesha uwezo wake wa kiuongozi. Kwa mfano, kwa mantiki Kama hizi za Kobello na wenzao wa ughaibuni, Sefue anatetea uharibifu wa kina Sitta na Chenge bungeni na kudai Kwamba ni sahihi kuweka Kando mjadala wa muundo wa muungano kwasababu eti suala hili limeligawa taifa. Sefue akaendelea kusema Kwamba "muundo wa sasa utabaki Kama ulivyo sasa kwa kuwa bunge limeshindwa Kupata maridhiano juu ya Jambo Hilo". Swali letu kwa Sefue na wenzake akina kobello ni hili:

• ikiwa serikalini hakuna muafaka Katika muundo wa serikali Tatu, upo wapi muafaka wa serikali Mbili? Makubaliano yake yanatokana na nini? Hoja Zipi? Hoja za Nani? Lini na wapi?

• iwapo hakuna muafaka juu ya muundo wa muungano, kuna muafaka Katika masuala ya tunu za taifa? Maadili na miiko? Muundo wa bunge? Mapato ya serikali ya muungano?

Cc chama, MwanaDiwani, ZeMarcopolo.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kisheria, ukitaka kubadili mfumo wa muungano au kipengele chochote cha katiba unaweza kwa kupitia bunge.

Nadhani solution nzuri ni kupata wabunge wengi wa UKAWA 2015 na kujaribu kubadili katiba. CCM haiwezi na haina interest, and you know that. Plus you guys failed to pressure CCM kwa sababu hamna support ya wananchi.

What I'm trying to say here is ...... " I dare you! "
 
Mchambuzi, hakuna Mtanzania mwenye akili timamu ambaye yuko ughaibuni kwa jitihada zake mwenyewe ambaye kwa namna yoyote ile anaweza akatetea ujinga, uhuni, ulaghai na upuuzi unaofanyika nchini. Wote wanaofanya hivyo ni ama ni kwa tamaa, ulafi, utumwa au unafiki; sifa ambazo zimewaganda kama kupe kwa sababu tu ya kutegemea fadhila za hilo genge la mafia lililokamata madaraka.

Hao akina Kobello ndio hao hao; wanaishi kwa kuwalamba miguu watawala wasije wakawasahau huko mbele ya safari; mtu uliyebahatika kupata exposure ya kushuhudia tawala za kistaarabu zinavyofanya kazi utateteaje uendeshaji wa mambo kihovyohovyo kama tunavyoshuhudia kila kukicha? Wengi ama ni ndugu, washikaji au washirika wao na wanao wajibu wa kutetea status quo...hiyo kwao ni amri.
Sina interest na position yeyote ya siasa Tanzania na sidhani kama nina uwezo huo. Pia sina interest ya kuishi Tanzania, ila ukweli ni lazima usemwe.
 
Kisheria, ukitaka kubadili mfumo wa muungano au kipengele chochote cha katiba unaweza kwa kupitia bunge.
Nadhani solution nzuri ni kupata wabunge wengi wa UKAWA 2015 na kujaribu kubadili katiba. CCM haiwezi na haina interest, and you know that. Plus you guys failed to pressure CCM kwa sababu hamna support ya wananchi.
What I'm trying to say here is ...... " I dare you! "

Comrade,
UKAWA gani hiyo unayoisema ambayo itaishi mpaka kwenye chaguzi kuu?.

UKAWA ya Maalim Seif anayetaka Mamlaka kamili kwa Zanzibar, in other word, kwa siasa za Tanzania ina maana kuvunja Muungano.

Hoja zao zimegota, kwa sasa wamebakiwa na political frustration.
 
Back
Top Bottom