Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

CCM NA WASHIRIKA WAOWAWEWESEKA, WAHAMISHA UTETEZI KUTOKA GHARAMA ZA SERIKALI SASA WAJIFANYA KULINDAMUUNGANO,
Back to the topic,
wakati mchakato wa katiba kwa hatua ya bunge maalumu la katiba, makada wa CCMwaliipinga sana rasimu ya tume kwa kisingizo cha muundo una gharama nyingi bilajustification kwakua tu walijua wanaongea na wajinga wanao kubali kila upuuzi unaosemwa.

Mchumi kama Mwigulu, Prof. Tibaijuka, Mwandosya, Dr. mwayembe, Migiro na wasomiwengi wa chama hicho wakijadili bila justification wala proof za kitaalam walaukidogo kuhusiana na gharama. Cha kusitisha sana watu wenye vyeo ndani ya chamakama mwenezi wao wakawa wanongea very cheap things " ukiongeza mke mwingineni gharama"
Kwa nini walifanya hayo yote kudanganya kuhusu gharama??Jibu ni rahisi wanawajua watanzania ni wajinga na watadanganyika kirahisi kwaniwao ndio wana maisha duni, sasa ukiwaambia unawaongezea mzigo inakua ni shidakwao na kwa hapo wakajua wataungwa mkono( na hasa watanganyika maana ndio wanoumia zaidi)


Mungu hamfichi Mnafiki, nini kimetokea baadae? Kama alivyoainisha mchambuzikwenye bandiko lake # 23 na Nguruvi3 kwenye mada zake za gharama za muungano,CCM wameumbuka ghafla, rasimu yao ya mafichoni inaoneka ni ya gharama kubwamara dufu ya ile rasimu ya tume ya warioba na wale wooote waliokua wanapigakelele kwamba serikali tatu ni gharama wapo kimya juu ya hili

Kiukweli hamuwezi kujibu maswali haya zaidi ya blah blah,maana kwa kuangalia tu kwenye presidential status kutoka watu watatu sasa nikama saba ( refer; Mchambuzi, bandiko # 23), bunge lenye watu karibu 400compare na Bunge la watu 75 ( hata ukichukua na bunge la tanganyka na zanzibahawawezi kuzidi 300). Na gharama kubwa zaidi za kuwabenbeleza wazanzibar
Kila nikiwaza sipati jibu juu ya mtazamo wa hawa watu naninalilia nchi yangu sana kupata viongozi wenye maono haya.

"Even the magicians can run out of tricks". Wote hawazungumzi tenamambo ya gharama za serikali sasa wanapiga kelele tu kwamba tuulinde muunganokwa gharama yoyote.

utawala wa Rumi ulipokaribia kuanguka walilazimisha mambo kwa kujiona wao niruler na wengine watawafuata kwa kila wasemacho, lakini muda uliwalazimishakukubali ukweli. Ninatamani viongozi na wanchi wasome alama za nyakati nakujiadjust accodingly, maana hata huu muungano tunaosema tunaulinda kama ni kwavisions za nmana hii ya kuwadanganya wanachi kwamba katiba sio muhimu kwao,basi Naliona anguko kubwa sana na ninafadhaika sana hatutaki kuukubali ukweli.

Niishie hapa, maana ninajisikia uchungu sana kwa namna mambo yanavyokwenda kwenyenchi yangu, i feel cryng for my country,kwa nini watu hawafunguki na kuonazaidi ya upeo wa kawaida, zaidi ya wanasiasa wetu zaidi ya wapiga ramli waongina wapotoshaji??
King, si hao tu uliowataja, hapajamvini wapo akina@MwanaDiwani, Kobello, Happy Feet Mkandara, waliosimama kidete kwanza kwa njia nyingi za kidanganyifu.

1. Walisema Warioba hakutumwa kupendekeza S3.
Tuliwawekeahadidu za rejea alizopewa na Kikwete, tume zilizoundwa na matokeo yake na watuwaliopoteza kazi kama Jumbe, wabunge waliopoteza nafasi zao kwama Njelu Kasakan.k. Tukawaonyesha kuwa Warioba hana hatia.


Wakaja na hoja ya S3 ni gharama. Tuliwauliza ni gharamakwa nani? Ukiwa na S3 ni nafuu kwa Tanganyika kwasababu haitabeba mzigo woote kwa jina la Tanzania. Wanafiki wanashindwa kusema ni mzigo kwa Zanzibar.

Tumewauliza, znz ilikuwa nchi huru, na madai ya S3 ni yao, iweje wao wawaoneehuruma? Hawakuwa na jibu


Rasimu ya CCM ya mafichoni, ambayo tuliitaja kwa majinahata kabla ya kuchomolewa tukaeleza ililenga kutoa pipi na peremende kwa wazaznibar. Ndicho hasa kilichotokea. Badala ya kupunguza gharama sasa ni mzigomzito sana wa gharama.

Kwa mfano, Rais wa znz anayechagyuliwa na wznz kwa ajiliya wznz, sasa atakuwa makamu wa Rais wa JMT.
Hii maana yake ataliipwa mshahara na JMT ambayo inasimama kwa kodi za Mtanganyika.

Hata akistaafu kama akinaMaalim Seif, Karume , Jumbe, Salimin mafao yao yanatoka hazina Dar kama kodi zaMtanganyika.


Katika wale makamu wa Rais wa znz, mishahara yao inatoka hazina.
Ni mwaka zaidi ya 10 mishahara ya SMZ ni jukumu la hazina Dar esSalaam.
Tunajua 4.5 inayotegemea makusanyo ya Tanganyika ndiyo inaendesha SMZ .


Nikupe mfano, TRA ukikamua kodi za Watanganyika ndivyo wznz wanavyopata 4.5 nene hata bila kufanya kazi.
Kibaya zaidi gharama kama za hilo bunge ni kubwa, atazibeba Mtanganyika.

Kila unachokiona ni ongezeko la gharama basi hilo ni ingezeko kwa Mtanganyika.
Ushahidi usio na shakaumeonyesha znz haina lolote au chochote inachotia zaidi ya kubembea mgongoni.


Hawa CCM na kama unavyomsoma MwanaDiwani, wameficha uovu walioutenda na sasa wanasema twende mbele ili Watanganyika wasahau hoja zao za gharama, na jinsi wanavyomtwisha Mtanganyika mzigo.

Wanataka, kuficha uhuniwalioutenda hata pale walipobaki wenyewe.
Hadi leo katibu wa bunge anahesabu kura za bunge lao tuliloambiwa limekamilika.


Ujanja unaotumika ni kuwasahaulisha Watanganyika.
Well,kwa kizazi cha sasa hilo litafanya kazi kwa muda mfupi.

In long run ni tatizokubwa sana. Huu muungano utavunjika mapema kuliko wanavyoona wao.

Hawa akinaMwanaDiwani wanashindwa kuelewa kuwa kuongelea muungano ilikuwa taboo, sasahivi siyo tena.
Hasira zilizojengeka kwa Watanganyika kuhusu jinsi wanavyoibebaznz kwa gharama kubwa ni bomu la hatari sana.


 
Comrade,
UKAWA gani hiyo unayoisema ambayo itaishi mpaka kwenye chaguzi kuu?.

UKAWA ya Maalim Seif anayetaka Mamlaka kamili kwa Zanzibar, in other word, kwa siasa za Tanzania ina maana kuvunja Muungano.

Hoja zao zimegota, kwa sasa wamebakiwa na political frustration .
Written all over their faces, I can tell by the tone of their statements.
 
Kasome hapa http://www.afrobarometer.org/files/documents/media_briefing/tan_r5_mediabriefing.pdf ukurasa wa 22.

hayo mambo ya ughaibuni na usomi ni kelele zako za kipuuzi tu ambazo hazina maana kwangu. Na hayo mambo ya bush au kuwa mjini hizo ni fikra zako za kipumbavu ambazo sina muda nazo. Go read that research, then you can decide to accept/reject it.

Mkuu, Huu ni mjadala huna sababu kutoa povu.

Wanachosemawenzako ni kuwa nchi hii ilipaswa kusaidiwa na watu wenye exposure, kwa bahatimbaya sivyo.

Ndio maana wanakuambia kuwa kabla ya kusoma Afrobarometerni lazima ufahamu Tanzania ikoje.
Mikoa ya Tanzania ilikuwa 25 miaka 20iliyopita. Sasa unapokuja na hoja kama hiyo, unawatia watu hamaki kwasababu nichini ya kiwango mkuu.

Hebu tujikite zaid katika gharama.
Siku za nyuma ulisemaS3 zitaongeza gharama, hoja hii bado unayo au umebadilika.

Kuhusu mgawao wa 4.5% acha kuongelea population maanahaikuwahi kuwa kigezo.
Kusoma ni jambo moja kuelewa ni jambo jingine. Hizotafiti unazoleta tuna appreciate hazina maana ni ukweli wote

Kule Uingereza nilikokupa reference ya Bernett formulasasa hivi wana tatizo.
Hawakutumia population pekee kama wanahesabu mazizi ya ngòmbe.
Haya mambo yanahitaji ufungue macho kidogo, hivyo nakusihi utulie kwanza,ujipange halafu tuendelee.

Na mwisho, Bunge la Warioba lilikuwa na wajumbe 75 wa JMT.Hili la Chenge 400 unasemaje mkuu!!

Na wewe unayesema tukuulize habari za senate na Congress,unaamini ule upuuzi wa Sitta hata walipobaki wenyewe. Kwamba wapo na golihakuna golikipa bado wanafanya uhuni ambao leo bado kura zainahesabiwa, kura zasms, Facebook , Yahoo n.k.

Tulitegemea watu kama wewe wasimame na kusema huu niupuuzi. Mung wangu! Eti unasema hilo limefanikiwa! Mkuu ndio maana watuwanahoji exposure na mengine. Kwa mwendo huu tutashindwa kukuuliza mambo kama ulivyoshauri
 
Sina interest na position yeyote ya siasa Tanzania na sidhani kama nina uwezo huo. Pia sina interest ya kuishi Tanzania, ila ukweli ni lazima usemwe.

Ahsante kwa kutoonyesha interest. Tulio nao wanatosha kabisakuivuruga nchi hii. Kama kutahitajika wakala, jaribu kufikiria, nchi inahitajiwataalamu wa spinning.

Mkuu ukweli upi?huu wa Tanzania ina mikoa 25. Halafuunataka vijana wetu waamini , tena ukiwashauri wakuulize maana unajua habari zasenate na Congress. Hapana! Tunawaambia vijana wawe waangalifu.

Mkuu, umepata nafasi ya kuangalia suala la gharama ukilinganisha na lile la rasimu ya Warioba?
 
Written all over their faces, I can tell by the tone of their statements.
Tena frustration hiyo kaonyesha balozi wa Uingereza, Marekani n.k. Kwakweli ina frustrate, fikiria kura za smz, yahoo, Tango. Hadi leo Kashishila anahesabu. Hivi wajumbe 400 kura zainahesabiwa wiki 2 tena wakiwa wenyewe bila uhakiki, hiyo hai frustrate kweli.


Frustration kubwa Zaidiaanyo Rais wetu. Alikubali mchakato naS3, akakataa mchakato na S3, akakubali S3 zisubiri hadi aondoke.

Kaitamabalozi, wakamwambia hawaji kushuhudia upokeaji wa upuuzi.
Sasa hapo kwelikwanini rais asiwe frustrated
 
All of the above, based on population as a major variable. Maamuzi yalifanywa na serikali zote mbili baada ya kufuata uamuzi wa IMF kwenye mgao wa BOT ('96).
Baadae (starting 2006 ) Mfumo huohuo ukafuatwa na ministry of finance kwenye mgao wa General Budget.

Formula ilitumia Population, like it or not na mgao wa ajira ulitumia regional blocks
Erasmus University Thesis Repository: Ownership on Aid, Rhetoric or Reality? The case of Zanzibar: The Semi- Autonomous State of Tanzania Chapter 3.

Kwanza haujajibu swali - je ni kweli Kwamba Tanzania Ina mikoa 25 Kama unavyodai?

Pili, usikimbilie QUALITATIVE research/statements Kama hizo Kujibu swali, haujajibu swali, umeanza kuliepa Kama kawaida yako. Swali letu ni Rahisi sana:

• Tufanyie "A QUANTITATIVE ANALYSIS", tuonyeshe kwa kufafanua, je hizi takwimu za 21% ya Ajira kwa Zanzibar, na 79% kwa Tanzania bara zimefikiwaje?

Na Tatu, the 4.5% formula ya BOT haikuja 1996 but 1994. That said and done, formula ya BOT haikuhusu fedha za bajeti au fedha za maendeleo, Bali mgao wa dividends zake baina ya pande Mbili za muungano I, na huko juu tumejadili hili. Miaka karibia kumi baadae, yani Mwaka 2003, tume ya pamoja ya fedha (JFC) ikabeba formula hii in a copy and paste fashion, bila any economic, legal or democratic basis. Swali letu kwako:

•Kwanini JFC na hazina zili copy and paste the 4.5% formula ya BOT? On what economic grounds?

Na nadhani Unafahamu Kwamba the 4.5% BOT formula ilikuwa ni ya kutumika kwa miaka mitano tu, lakini ikalazimishwa kukaa hadi Leo, kwa misingi ya kisiasa kuliko kiuchumi, na athari zake ni nyingi kuliko faida.

Mkuu, Just like the Barnett formula in the UK, it's about time sasa Tanzania kuja na formula ambayo:

1. It's need driven - inayoangalia mahitaji ya wananchi kuendana na hali zao za kiuchumi.
2. Transparent, and
3. With strong legal, democratic and economic grounds. Sio formula za kisiasa na za kisera zinazoishi kwenye mafaili ya mwigulu hazina.




Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwanza haujajibu swali - je ni kweli Kwamba Tanzania Ina mikoa 25 Kama unavyodai?

Pili, usikimbilie QUALITATIVE research/statements Kama hizo Kujibu swali, haujajibu swali, umeanza kuliepa Kama kawaida yako. Swali letu ni Rahisi sana:

• Tufanyie "A QUANTITATIVE ANALYSIS", tuonyeshe kwa kufafanua, je hizi takwimu za 21% ya Ajira kwa Zanzibar, na 79% kwa Tanzania bara zimefikiwaje?

Na Tatu, the 4.5% formula ya BOT haikuja 1996 but 1994. That said and done, formula ya BOT haikuhusu fedha za bajeti au fedha za maendeleo, Bali mgao wa dividends zake baina ya pande Mbili za muungano I, na huko juu tumejadili hili. Miaka karibia kumi baadae, yani Mwaka 2003, tume ya pamoja ya fedha (JFC) ikabeba formula hii in a copy and paste fashion, bila any economic, legal or democratic basis. Swali letu kwako:

•Kwanini JFC na hazina zili copy and paste the 4.5% formula ya BOT? On what economic grounds?

Na nadhani Unafahamu Kwamba the 4.5% BOT formula ilikuwa ni ya kutumika kwa miaka mitano tu, lakini ikalazimishwa kukaa hadi Leo, kwa misingi ya kisiasa kuliko kiuchumi, na athari zake ni nyingi kuliko faida.

Mkuu, Just like the Barnett formula in the UK, it's about time sasa Tanzania kuja na formula ambayo:

1. It's need driven - inayoangalia mahitaji ya wananchi kuendana na hali zao za kiuchumi.
2. Transparent, and
3. With strong legal, democratic and economic grounds. Sio formula za kisiasa na za kisera zinazoishi kwenye mafaili ya mwigulu hazina.




Sent from my iPhone using JamiiForums
Administratively, Zanzibar ni mikoa 5 na Bara ni mikoa 20. 5 ni 20% ya 25.
Kuhusu hazina ku-kocopy formula ya IFM, kuna ubaya gani kama ni makubaliano kati ya serikali mbili na DPs?

Kama unaona Barnett formula ni outdated, jaribu kuwashauri waingereza waje na formula unayoitaka wewe. Waingereza siyo kwamba ni wajinga, no! wanajua hilo ila hakuna political will. Same as in Tanzania, kama kuna political will, basi itarekebishwa. And that's what matters.

Ila usiaminishe umma kuwa kuna mtu alilala akaota halafu akaja na 4.5% au 21%. It's based on something, now wether you like it or not that's another issue.

It must be a good arithmetic model at that time, kukubaliwa na pande zote.Na IMF ina actuarists wake, ila kama unapingana nao that's okay ila usidhani imeokotwa tu jalalani.
 
Sina interest na position yeyote ya siasa Tanzania na sidhani kama nina uwezo huo. Pia sina interest ya kuishi Tanzania, ila ukweli ni lazima usemwe.

For the first time and maybe in your entire life, you have admitted something that is not only true but makes some sense as to why you are pro status quo and that is...you don't give a damn what takes place in Tanzania, shamba la bibi. You have no interest of living in Tanzania and why should you? Ukishachuma kwa nini usitokomee? Tofauti yetu na ninyi iko hapo! Tanzania ikichomwa mkuki, damu tunavuja sisi ambao hatujawazia kulipa mgongo taifa letu.

Tunapohangaika juani (ugenini), tunawafikiria na kuwakumbuka ndugu zetu, wazazi wetu, watoto wetu, wajukuu zetu, ndugu na marafiki; tunaota ndoto za siku tutakapoungana nao; tutakapoweza kujumuika tena nao na kula pamoja kivulini (nyumbani) Kikwete doesn't care, Chenge doesn't care, Sitta doesn't care, Kinana doesn't care...why should they? Kwani pesa zao zinakaa bongo?

Muundo wa Serikali mbili ndio umetumiwa kama daraja na watawala wajanja katika kuwaibia Watanganyika kwa sababu hakuna wa kuwauliza wala kuwawajibisha. Wakishajificha kwenye koti la Muungano nani atawahoji? Ni hao hao wanaamua watumie vipi mali ya Watanganyika kuendeshea mambo ya Muungano...wengi wao wakiwa ni watu wale wale walioteuliwa na Raisi huyo huyo mwenye madaraka ya kimungu!

Halafu anakuja Jaji Warioba kuwakilisha rasimu inayotaka kuziba mianya hiyo ya wizi na kuhakikisha kwamba mipaka imechorwa mambo ya Muungano yanapoanzia na kuishia wapi na vivyo hivyo kwa Tanganyika, thubutu! Waliozoea vya bwerere vya kutunishia mifuko yao kwenye mabenki ya nje kama Chenge eti ndio hao hao wanaongoza kamati za kututungia Katiba huku akina Kobello na MwanaDiwani wakishangilia, ptyuuu!
 
Ahsante kwa kutoonyesha interest. Tulio nao wanatosha kabisakuivuruga nchi hii. Kama kutahitajika wakala, jaribu kufikiria, nchi inahitajiwataalamu wa spinning.
Mkuu ukweli upi?huu wa Tanzania ina mikoa 25. Halafuunataka vijana wetu waamini , tena ukiwashauri wakuulize maana unajua habari zasenate na Congress. Hapana! Tunawaambia vijana wawe waangalifu.

Mkuu, umepata nafasi ya kuangalia suala la gharama ukilinganisha na lile la rasimu ya Warioba?



Kwa kuwa mikoa inaongezwa, haimaanishi kuwa maamuzi nayo ni lazima yabadilishwe. Zanzibar ina mikoa mitano na Tanzania inayo 20. That is a basic model.

Kama mikoa itaongezeka au kupunguzwa, hiyo haiharibu hoja.

Nirudi ughaibuni. Katiba ya US ilipitishwa na States 13, sasa hivi zipo 50. Does that ring the bell?

Rasimu ya Warioba inaleta gharama zaidi. Hata yeye mwenyewe anajua hilo, wewe ndiye unayeleta marais saba, lol!
 
For the first time and maybe in your entire life, you have admitted something that is not only true but makes some sense why you are pro status quo and that is...you don't give a damn what takes place in Tanzania, shamba la bibi. You have no interest of living in Tanzania and why should you? Ukishachuma kwa nini usitokomee? Tofauti yetu na ninyi iko hapo! Tanzania ikichomwa mkuki, damu tunavuja sisi ambao hatujawazia kulipa mgongo taifa letu. Tunapohangaika juani (ugenini), tunawafikiria na kuwakumbuka ndugu zetu, wazazi wetu, watoto wetu, wajukuu zetu, ndugu na marafiki; tunaota ndoto za siku tutakapoungana nao; tutakapoweza kujumuika tena nao na kula pamoja kivulini (nyumbani) Kikwete doesn't care, Chenge doesn't care, Sitta doesn't care, Kinana doesn't care...why should they? Kwani pesa zao zinakaa bongo?
Sijachuma hata senti tano Tanzania. Sijawahi kufanya kazi Tanzania, labda field nikiwa chuoni.
Naomba mjadala kati yangu na wewe uishie hapa, tunaweza kutukanana na kukashifiana kwa mambo ya kiimani tu, maana siuoni ukweli unaousimamia. Umeniuliza data na nimekupa.

Kinachofuata kwa mtu mstaarabu ni ku-dispute au kukubali au angalau kuwa kimya. You did none of those.
 
Kobello[/B] na MwanaDiwani wakishangilia, ptyuuu!

Mkuu, tena mijizi illiyokubuhu inayojulikana Interpol ndioimepewa kazi na CCM kuandika maadili ya taifa. Eti inaandika tunu za taifa.

Hivi kweli Watanzania tumefika mahali hatuna watu hadi tuwashangilie wezi.
MwanaDiwani kuna moral authority hapo!!!

Halafu wezi wale wale Rais aliowawajibisha ndio wameenda Dodoma kumkabidhi rasimu ya CCM, Chenge na Sitta. Na Rais kapokea. Majuzi tu kuna secret service' mmoja kule Marekanialiongozana na Obama katika elevator. Kumbe ana historia ya ''criminal offense''.

Hilo limekuwa kubwa magazeti na vyombo vyote vya habari vinaongelea.
Mkuu wa itifakikibarua kipo katika chaki Tanzana, rais anakabidhiwa nyaraka nyeti ya taifa na wezi.

unaambiwa sasat wende mbele. Hata kama ni kusonga, tukikumbuka highschool yaSamwel Sitta ambayo hadi leo wanahesabu wabunge kwakweli inasikitisha bado kunawanaume wanashangilia.
Wana suruali zao zina upanga na mkanda! Hata chembe ya soni hawana.
 
Last edited by a moderator:
Barubaru,

Sioni mantiki ya kumjadili mbunge a nkasi, Kessy Kama mfano wa watanganyika wote kushindwa kumalizia the last mileage ya kudai Tanganyika Yao. Alichofanya Nguruvi3 ni kumtumia mfano bwana kessy Kama mtanganyika bungeni na Mwana CCM ambae na yeye sasa anaona hoja zetu Zipo wapi, basi. Suala la yeye Kupiga kura ya kuunga Mkono rasimu ya CCM halina maana Kama suala Kwamba wapo wabunge na wana CCM wengi ambao wanaona Ukweli upo wapi lakini kinachowazuia ni vitisho, Tena kwa mfano, kwa kessy, sio vitisho kutoka kwa CCM bara tu, Bali hata waZanzibari. Turudi kwenye mada.


Sent from my iPhone using JamiiForums

Hata mimi nimemtumia Keissy kama mfano katika kujenga hoja yangu kuwa waTGk ni waoga na hawajiamini na hilo ndilo linalosababisha kujenga khofu ya kuanzisha Sirikali yao Tanganyika.

Na kama utanisoma vizuri nilisherehesha kwa kusema hata Nguruvi3 angekuwepo mjengoni basi angenung'unika sana lakin mwisho wa siku angepiga kura ya NDIO kwa vifungu vyote vya katiba ya Sitta.

Tumpe pongeza sana Mwanasharia mkuu wa Znz kwa kuwa muwazi na mkweli na hilo limemuweka huru katika nafsi yake.

Pole mkuu ila unapoitazama shilingi basi itazame pande zote sio upande mmoja kwani kwa kufanya hivyo watu wanaweza kusema una makengezaa.

Mwisho namaliza kwa kukwambia waarabu tuna usemi mmoja '' UKIMUONA MTU MZIMA NA AKILI ZAKE TIMAMU ANATEMA ASALI NA KUTAMANI PILIPILI, UJUE KUNA JAMBO HAPO'' Usimbeze.
 
MwanaDiwani , kuna tetesi kuwa Zakhia Meghji amepiga kurakama mjumbe wa Zanzibar.

Inasemekana hayupo katika orodha ya wajumbe wakuteuliwa wa znz na wala si mbunge.

Mkuu unaweza kutuweka sawa kuhusu ukweli auauongo wa hii jambo? Pili, kuna habari mbunge wa NCC hakupiga kura, lakiniimeonekana yake ni ya ;NDIYO''

Sasa mkuu, wewe na ZeMarcopolo mnaposema katibaimeshapitishwa mna maana gani? Tunajaribu kupata ufafanuzi tu wa haya walahakuna tatizo na rasimu ya CCM. Tusaidieni
 
MwanaDiwani CCM walisema takwimu za Warioba zilikuwa chache. Tunaomba utueleze hapa, SawmwelSitta alipewa nguvu na sheria gani ya nchi hii kujiteua kama tume ya kukusanyamaoni?
Pili, iweje CCM itumie watoa maoni takribani 30waliohojiwa na Sitta na kuyaingiza katika katiba ikiwa, yale 18,000 ya Wariobahayakuwa yanatosha?
Ndugu Nguruvi3
Wakati mwingine nikisoma hoja zako huwa ninadhani unachokifanya hapa ni sarcasm and whimsical!

Una muda mrefu hapa kwenye jukwaa la siasa na lazima unafahamu majibu ya hoja unazozileta na kuuliza maswali!.

Kwanza, CCM tulikuwa specific kwenye hoja zetu kuhusu Muungano na hii inatokana na majibu yaliyokuwa yanatolewa na Jaji Warioba. Majibu kuhusu msingi uliopelekea kwa Tume ya Jaji Warioba kuhusu Muungano ndiyo yaliyowafanya siyo CCM peke yake bali hata wananchi wengine kuzihoji takwimu zilizokuwa zinajengewa hoja na Tume ya Jaji Warioba. Jaji Warioba kwenye andiko lake alidai sababu za kupendekeza Serikali tatu ni idadi ya watu ''wengi'' waliopendekeza mfumo wa Serikali tatu. Wananchi wakataka kufahamu, wananchi ''wengi'' katika mantiki ipi na katika msingi gani.

CCM haikuwahi kusema takwimu zote zilizopelekea kuandikwa kwa Rasimu ya Pili ya Katiba zilikuwa ni chache. Usiilishe CCM maneno yako.

Pili, Hakukuwepo na CCM kwenye Bunge Maalum bali kulikuwepo na Wajumbe wa Bunge Maalum ambao walikuwa wanawakilisha wananchi kupitia makundi mbali mbali kama yalivyokuwa yameainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sehemu ya Tano, Ibara ya 22(1).

Kuanza kujenga hoja za kichama katika mtazamo wako hakuwezi kuifanya hoja yako kuwa valid katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83.

Kwa sasa unaendelea kuonyesha kuwa kila siku hoja zenu zinabadilika kutokana na upepo wa hoja. Ni ninyi mliokuwa mnadai CCM walienda na Rasimu mliyokuwa mnaita ya mfukoni, lakini kwa sasa unataka tena kutuaminisha Samwel Sitta alichukua maoni ya watu 30. Guys, where's your consistency?. Awe na Rasimu ya Mfukoni halafu tena achukue maoni ya wananchi!. Gimme a break!

By the way, kuna mdau mmoja alienda Mahakamani akitumia hoja kama yako na Mahakama ilijibu kwa kutoa hukumu ambayo nakala yake ni hii hapa chini. Soma kwa faida yako ili usiendelee kuuliza swali kama hili kila mara!

attachment.php

attachment.php


Tueleze, ni sheria au kanuni gani ziliruhusu wabunge 2kupiga kura, na kwavile CCM walisema ni kura ya wazi, kwanini Sitta ameficha.
Hakuna kanuni iliyosema wabunge waliopiga kura ya siri basi watatangazwa hadharani. Zinazotangazwa ni kura zao. ndivyo ilivyofanyika.

Kikundi inachojiita UKAWA ndiyo kilishupaa kutaka wabunge waruhusiwe kupiga kura ya siri ambapo maridhiano yalifanyika na kukubaliwa kuwa, kama kuna mjumbe anataka kupiga kura ya siri, basi atapiga kura ya siri. Kama kuna mjumbe anataka kupiga kuwa ya wazi basi atapiga kura ya wazi.

Kanuni iliyoongoza upigaji kura ni hii,
38.-(1) Utaratibu wa kupiga kura ya wazi au ya siri utaelekezwa na Mwenyekiti kwa kushauriana na Katibu.
(1A) Katibu atakuwa Msimamizi Mkuu wa Upigaji kura katika Bunge Maalum.
(1B) Katika kutekeleza mamlaka yake kwa mujibu wa fasili ya (1A), Katibu anaweza kumteua mtu yeyote kufanya kazi za usimamizi wa upigaji kura kwa niaba yake".

(2) Wakati wa kupiga kura ya siri, kila Mjumbe atapiga kura ya "Ndiyo" au "Hapana", kwa kutumia karatasi ya kupigia kura itakayokuwa imeandaliwa na Katibu kwa ajili hiyo.
(3) Upigaji kura ya siri utakuwa ni kwa Mjumbe baada ya kupewa karatasi ya kupigia kura, kuweka alama ya vema (") kwenye moja ya kisanduku pembeni ya namba ya ibara husika au pembeni ya maneno "Rasimu ya Mwisho ya Katiba" sanjari na maneno "Ndiyo" au "Hapana", kwa jinsi yeyé binafsi anavyoona inafaa.
(4) Mjumbe ambaye ataharibu karatasi yake ya kupigia kura atairudisha karatasi hiyo iliyoharibika kwa Katibu na atapewa karatasi nyingine ya kupigia kura.
(5) Mjumbe ambaye atakuwa na mahitaji maalum au atakuwa anahitaji usaidizi katika zoezi la kupiga kura, atapatiwa mahitaji hayo na usaidizi huo kwa utaratibu ulioandaliwa na Katibu kwa ajili hiyo.
(6) Baada ya kila Mjumbe anayestahili kupiga kura ya siri kupiga kura, kura hizo zitakusanywa na kuwekwa kwenye masanduku ya kura na kupelekwa kwenye chumba maalum kitakachokuwa kimeandaliwa kwa ajili ya kuhesabu kura mbele ya mawakala walioteuliwa kwa ajili ya kusimamia kura hizo.
(7) Kwa Mjumbe anayetaka kupiga kura ya wazi utaratibu utakaotumika utakuwa ni kwa kuitwa jina na Katibu au mtu yeyote aliyeidhinishwa na Katibu na Mjumbe kutamka kwa sauti maneno "Ndiyo" au "Hapana" kuhusu ibara husika au Rasimu ya Mwisho ya Katiba.
(8) Utaratibu wa kupiga kura ya siri au ya wazi kwa Mjumbe anayepiga kura nje ya Maeneo ya Bunge Maalum utaelekezwa kwa maandishi na Katibu baada ya kushauriana na Mwenyekiti.
(9) Mjumbe yeyote aliye nje ya maeneo ya Bunge Maalum kwa ruhusa ya maandishi ya Mwenyekiti anaweza kupiga kura kwa njia ya nukushi, mtandao au njia nyingine yoyote itakayoelekezwa na Katibu baada ya kushauriana na Mwenyekiti na kura hizo zitajumuishwa pamoja na kura nyingine zilizopigwa chini ya Kanuni hizi.
(10) Kwa madhumuni ya fasili ya (9) ruhusa ya Mwenyekiti maana yake ni ruhusa ya maandishi kwa Mjumbe kutoka nje ya eneo la Bunge Maalum na ruhusa ya kupiga kura akiwa nje ya maeneo ya Bunge Maalum.
(11) Baada ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa Kanuni hii kuhesabiwa, Katibu atatangaza matokeo ya kura ambayo yataingizwa katika Taarifa Rasmi.
Tueleze, mahujaji waliwezaje kupiga kura wakiwa katikaIbada yao. Nani alihakiki kura za facebook na fax, yahoo na google
Kanuni ya 38(1) ndiyo iliyoruhusu wajumbe walioko nje ya Bunge kupiga kura zao. Kanuni inasema hivi,
38A.-(1) Mjumbe yeyote aliye nje ya maeneo ya Bunge Maalum anaweza kupiga kura mbele ya Afisa aliyethibitishwa kwa maandishi na Katibu wa Bunge kuwa msimamizi wa upigaji wa kura kwa masharti yafuatayo:
(a) awe ameruhusiwa kwa maandishi kuwepo nje ya ukumbi wa Bunge Maalum na Mwenyekiti; na
(b) awe ameomba kwa Mwenyekiti na kuruhusiwa kwa maandishi kupiga kura yake akiwa nje ya ukumbi wa Bunge Maalum, Isipokuwa Mwenyekiti anaweza kumruhusu Mjumbe aliyeomba ruhusa ya mdomo kupiga kura nje ya maeneo ya Bunge Maalum iwapo Mwenyekiti ataridhika kuwa Mjumbe huyo yupo katika hali au mazingira yasiyomuwezesha kuomba ruhusa kwa maandishi.
(2) Afisa aliyeteuliwa na Katibu wa Bunge Maalum kwa madhumuni ya fasili ya (1), mara baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika, atawasilisha Taarifa kwa Katibu wa Bunge Maalum inayojumuisha pamoja na mambo mengine, rejista la Wajumbe waliopiga kura litakaloainisha:
(a) majina ya Wajumbe waliopiga kura za siri;
(b) majina ya Wajumbe waliopiga kura za wazi;
(c) tarehe ambayo Mjumbe alipiga kura; na
(d) majina ya Wajumbe waliojiorodhesha kupiga kura lakini hawakupiga kura.
(3) Kwa madhumuni ya Kanuni hii, Afisa aliyeteuliwa na Katibu kusimamia upigaji kura maana yake, ni mtumishi wa Bunge Maalum, au mtu yeyote aliyeteuliwa na Katibu kwa madhumuni hayo.
Tueleze kwanini Sitta alikataa uwakilishiw wakati wakuhesabu kura
Nani alikuambia Mhe. Sitta alikataa uwakilishi kwenye kuhesabu kura wakati Kanuni zinaeleza wazi?
Kwa taarifa yako, wajumbe sitta walichaguliwa kwenda kusimamia zoezi la kuhesabu kura kama ilivyobainishwa kwenye Kanuni 38(6) kinachosema,
38(6) Baada ya kila Mjumbe anayestahili kupiga kura ya siri kupiga kura, kura hizo zitakusanywa na kuwekwa kwenye masanduku ya kura na kupelekwa kwenye chumba maalum kitakachokuwa kimeandaliwa kwa ajili ya kuhesabu kura mbele ya mawakala walioteuliwa kwa ajili ya kusimamia kura hizo.
Tufahamishe iweje hadi leo katibu wa bunge anajadiliwaliopiga kura na wasiopiga kura. Hiyo 2/3 ya BMK-CCM ilipataikana vipi?
Nimeisha sema, hakukuwepo na CCM kwenye Bunge Maalum bali kulikuwepo na Wajumbe wa Bunge Maalum.
2/3 ilipatikana kwa njia ya upigaji wa kura kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 38 na 39 ya Bunge Maalum. Zisome hizo kanuni hapo juu!
Tueleze, mwanasheria mkuu wa znz amefukuzwa kazi kwa kosala kura yake. Je, uwepo wake ulikuwa kama mwanasheria au kama mjumbe. Na kamani mwanasheria, kitendo cha yeye kupinga rasimu kinamaanisha nini katika uzaniwa kisiasa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amepewa madaraka kikatiba na kisheria ya kumfukuza Kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar bila kuhojiwa sababu ya kufanya hivyo.

Kama unataka kufahamu zaidi, unaweza kumtafuta aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe, Othman Masoud Othman kwa maelezo zaidi!
Tueleze, Rais Kikwete aiposema S3 zisubiri hadi aondoke,ili hali akijua kila kilichoendelea katiaka tume, alikuwa na maana gani nakwanini alaicha mchakato ukaendelea.

Rais Kikwete hajawahi/hakuwahi kusema Serikali Tatu zisubiri mpaka aondoke bali alisema, hataruhusu vulugu za kijeshi nchini zinazosababishwa na ulegevu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wakati akiwa Madarakani labda wanaotaka kufanya hivyo na kuvunja Muungano inabidi wasubiri mpaka atoke.
Na mwisho tueleze, ni lini suala la katiba limekuwa hojaya CCM. Liliingizwa katika vikao kwa utaratibu gani.
Labda na wewe nikuulize, Ni lini hoja ya Katiba imekuwa exclusive right ya baadhi ya watu, kikundi au chama cha siasa.
Kabla hujajibu naomba uelewe kuwa suala la Katiba ni hoja ya kitaifa iliyoletwa na serikali inayotumikia wananchi kitaifa. Ndiyo maana hata Bunge Maalum la Katiba halikuwa na vyama bali makundi yanayowakilisha wananchi wa Tanzania.

Kama wewe ulikuwa unadhani kwenye Bunge Maalum kulikuwa na vyama, basi hizo ni fikra zako na mtazamo wako.
Kumbuka maji ukiyavulia nguo…
-huna budi kuyaoga!

CCM imeyaoga na sasa Katiba inayopendekezwa imepatikana. CCM kwa sasa iko kwenye ajenda ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kura ya maoni.

Mchanganuo wa upatikanaji wa Katiba Inayopendekezwa tunawaachia wale wanaotegemea ajenda za CCM kuendesha siasa zao.
 
HOJA ZISIZO NAMAJIBU
TUNASHAURIWA TUMEZE BILA KUTAFUNA

WATANGANYIKA TUNASEMA ‘NI NGUMU KUMESA''


WATETEZI HOI,WAMWACHA WARIOBA KAMA ALIVYO,WASEMA TWENDENI TU

Kobello, mikoa haikuwa kigezo cha 4.5%. Mchambuzi kaonyeshahadi tarehe za lini 4.5 ilianza kutumika na ilikusudiwa kuisha lini. Kamtembezayule ndugu yetu wa tovuti ya JFC hajarudi tena.

Naomba upitie bandiko laMchambuzi. Mikoa ilikuwa Zaidi ya 25 wakati 4.5 inawekwa.
Leo Tanzania hainamikoa 25 kama unavyoelewa.[/COLOR]


Nilikupa dondoo kuhusu Bennet formula inavyoleta tabuUingereza kwa sasa. Hiyo ilikuwa ya kisayansi.

Unapotumia population ya mikoa,mkuu unakosea. Mkoa mmoja wa znz ni sawa na kata ya mzimuni.
Hilo tu linaelezakuwa 4.5 kwa vigezo vyako ni kitu kisichowezekana.
Huhitaji simple calculator,logic inaweza kukusaidia.


Mkuu Mag3 , kuna hoja ya gharama za muungano. Nimemuuliza KobelloMwanaDiwani kuwa kama ya Warioba (S3) ilionekana ni mzigo, tunaombawatuonyeshe hii ya Chenge/Sitta na CCM ina unafuu gani?
Kobello hana jibuanachosema ''Ya Warioba ni ghali'' hajaweza kuandika Zaidi ya mstari huo


Kuna swali linguine linalohitaji majibu kutoka kwa@MwanaDiwani Kobello .
Tuliambiwa kuwa rasimu ya Warioba , serikali kuuinaelea haina vyanzo vya uhakika vya mapato.

Swali: Kwa mujibu wa rasimu yenuna Sitta/Chenge vyanzo vya uhakika vya mapato ni vipi?
Ya Wariobna tumeonatayari, tunahitaji yenu


Mchambuzi , kuna hoja umegusia wanaposema muungano ni bainaya pande mbili.
Hivi unapokuwa na Tanzania ambayo znz imo, na upande mwingineznz peke yake, hapo kuna pande mbili?


King Suleiman , kuna mahali umeomba uonyeshwe weakness yarasimu ya Warioba na strength ya rasimu ya Sitta/CCM/Chenge etc.

Sijui kama kuna aliyewahi kufanya hivyo.Ninasoma mabandiko yanasema ‘tusonge mbele rasimu imepitishwa'' hatuambiwiuliyouliza.


Na swali la mwisho, hivi hao marais 5 kutoka znz ambaokikatiba wanaruhusiwa kutawala Tanganyika, watalipwa mishahara yao kwa kigezogani na nani?

Kama ni JMT iweje Mtanganyika abebe zigo la samadi bila sababu


(Tutamalizia sehemu y mwisho inayohusu vongozi wa dini)
 
Last edited by a moderator:
Ahsante kwa kutoonyesha interest. Tulio nao wanatosha kabisakuivuruga nchi hii. Kama kutahitajika wakala, jaribu kufikiria, nchi inahitajiwataalamu wa spinning.
Mkuu ukweli upi?huu wa Tanzania ina mikoa 25. Halafuunataka vijana wetu waamini , tena ukiwashauri wakuulize maana unajua habari zasenate na Congress. Hapana! Tunawaambia vijana wawe waangalifu.

Mkuu, umepata nafasi ya kuangalia suala la gharama ukilinganisha na lile la rasimu ya Warioba?
Ndugu Nguruvi3
Kwa sasa ninachokiona hapa ni kutafuta sababu ambazo kimantiki haziko ndani ya msingi wa hoja na kuanza kuzishikia bango ili kuondoka katika msingi wa hoja ili uonekane kma ni mshindi!.

Nini kinachokushangaza kwa mwanadamu kukosea idadi ya Mikoa iliyoko kwa sasa lakini idadi hiyo ndiyo ilikuwa kabla ya mabadiliko na kuongezwa mikoa mingine. Nini kitakushangaza kama atatokea mwananchi hafahamu idadi ya wilaya za Tanzania achilia mbali Kata zake.

Let's stick to our main topic!.

Hatufanyi mashindano bali tunaelimishana na kupashana habari.
 
MwanaDiwani, nitajibu hoja zako lakini nianze na hii yarasimu ya mfukoni.
Ni kweli kuna bandiko linlozungumzia rasimu ya CCM yamfukoni.
Bandiko hilo tulilitoa mwezi April hapa duru. TuliwatajaChenge, Asha, Sitta kama vinara wa rasimu hiyo.

Tulieleza rasimu ililenga kutoa pipi na peremende kwawazanzibar.
Tukasema hakuna kinachobadilika isipokuwa kutungua rasimu yaWarioba ili ile ya mafichoni ya CCM itoke. Nadhani unajua kamati ya uandishiilikuwa na akina nani na wznz wamepewa marais 5 kwa gharma za Mangayika

Kuhusu Sitta kukusanya maoni, hilo nalo tumesema hapa duru.
Tukasema kuwa anachokifanya ni kujaribu kuonyesha kuwa CCM wamesikiliza maoniya wananchi ili kutoa uhalali wa rasimu ya mfukoni kutoka nje.

Ni mbinu ile ile iliyotumika kusema UKAWA wanapiga simu etiwamezuiwa.
Hilo lilikuwa kujenga mazingira ya kupata wajumbe 2 ambao Sitta pekeyake ndiye anawajua.
Wewe umepewa kazi ya publicity tu.

Hivyo kuna hoja mbili, rasimu ya mafichoni ambayo imetokakama tulivyoonyesha na ukitaka mabandiko tutakuwekea kipengele kimoja hadi kingine.Pili, kuna la Sitta kuita watu 30 na kusema ni maoni ya wakulima na wafugaji.

Hilo linazaa maswali haya. Kwanza, endapo unaamini katika sheria iliyounda BMK,ni kifungu gani kimempa mamlka Sitta kujiteua kuhoji watu. Mamlaka hayo kayapata wapi hadi yaingie katika rasimu ya CCM.

Anna Tibaijuka ni CCM na alisimama mbele akisema ili takwimuzilete maana at least 30% ya watu ingetumika. Nape alisema Warioba kahoji watu18,000 wakati CCM ina wanachama milioni 5.
Na hoja kubwa ilikuwa takwimu zaWarioba si za kisayansi.

Tunauliza, sayansi gani imetumika kwa watu 30 aliohoji Sittaakiwa hana mamlaka hata ya kanuni za bunge kuchukua maoni hayo.

Lakini pia lazima utueleze, kama S3 ni gharama, tuonyesheunafuu wa rasimu yenu ya mafichoni.

Na mwisho, hebu tuambie vyanzo vya uhakika vya mapato yaserikali kuu, na pia utueleze pande mbili za muungano ni zipi.

Halafu nitarudi kupitia mstari mmoja hadi mwingine wa hojazako. Kwanza tujibu yanayokuhusu.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza nashukuru,umekiri makosa na si kung'ang'ania makosa kama Kobello. Chkua fusa hi =I kumweleza awe msikivu, hapa tunongelea Tanzania yunayijua, tunaishi, tunafanya kaz na tnapata kipatoNi nchi tunayoililia kwasaab ni yetu.

Pili, mbona bado tupokatika main topic? Maswali yetu huyajibu na ni haya


  1. Unafuuwa rasimu ya CCM ni upi ukilinganisha na ile ya Warioba kwa gharama

  2. Pandembili za muungano ni zipi ikiwa Tanzania, znz imo pia
  3. Vyanzovya uhakika vya mapato vya rasimu ya Chenge ni vipi (serikali kuu)
  4. Rasimuya CCM ni ya wananchi au ni ya kujibu madai ya wazanzibar(marais 5)

    Hebu tuanzie hapo (ninkutahadhrisha kuwa hatutajadili vipengele vya rasimu, tunaangalia weakness na strength baina ya Warioba na Chenge/ccm)

    Narudia hatutajdili haramu kwasababu kufanya hivyo ni kutoa uhalali kwa mzoga. Mzoga unabaki na hadhi yake.
 
Mkuu Nguruvi3, kwanza pole kwa kudisturb mtiririko wako wa uchambuzi, karibu kwa sehem inayofuata ya viongozi wa dini, interfearence zetu ni kutaka kuelimishana na pia kurekebisha kila upotoshaji unaofanywa na watu wenye hila kutetea mambo yao yapite kwa " funika kombe mwanaharamu apite", wakumbuke hizi ni zama za uwazi na ukweli, hakun kitu kitajificha.

Mimi ningependa makada wa CCM na pro Katiba ya Sitta/Chenge hususan Mwanadiwani, Kobelo, Mkandara nawengineo. Mtuonyeshe japo kwa muktasari udhaifu wa rasimu ya tume kwa data na stregnth za rasimu hii ya CCM, mtuonyeshe quantitative na qualitative ubora wa katiba hii pendekezw dhidi ya ile ya maoni ya wananchi nchi chini ya tume. Pia mtuonyeshe kisayansi mmefikia vipi conclusion ya katib mnayoitetea na methodology zipi zilitumika bila ulaghai mpaka kufika hapa ilipo.

Tukiweza kuonyeshana facts hizo nadhani mjadala utakwend vizuri na mtatufumbua macho na kutuelimisha wengi, maana naon wengi mna bit around the bush na kukwepa vitu au point za msingi

Mag3, Mchambuzi na Nguruvi wamekuja na data zao na kuzionyesha kipengele kwa kipengele, tungependa na nyie wenzetu akina Kobbelo na mwanadiwani ntuonyeshe uhalisia, maana mpaka sasa tunachoamini ni kwamba kwenye katiba hii kuna mazingaombwe na ulaghai mwingi tu.
 
King Suleiman,

Upo sahihi Kabisa Kwamba rasimu haramu ya Chenge inayonadiwa na kina mwanadiwani, sio tu imejaa mazingaombwe, Bali pia utapeli hata kwa vijana.

Kina mwanadiwani wanajenga hoja za ovyo Kabisa Kwamba katiba mpya imezingatia mahitaji ya vijana kwa kuingiza Haki zao, baraza la vijana la taifa etc. Ukweli ni hivi:

Vijana wengi hawajui Kwamba wanaingizwa Mjini, watatumiwa kupitisha rasimu hii haramu na kisha kuja kujuta baadae. Ni wajibu wetu kuelimisha vijana wakata rasimu hii ya CCM. Nitafafanua utapeli upo wapi:

Sura ya tano:

Haki za binadamu, wajibu wa Raia, jamii na mamlaka za nchi.

51 Haki na wajibu wa vijana.
(1) "kila kijana Ana Haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu Katika shughuli za maendeleo ya jamhuri ya muungano na kwa mantiki hiyo, serikali ya jamhuri ya muungano na jamii zita hakikisha kuwa vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa Raia wema na Kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu Katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni."

Utapeli upo kwenye kipengele cha pili cha ibara hiyo ya (52):

(2) "kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), bunge litatunga Sheria itakayosimamia pamoja na mengine, uanzishwaji, muundo,majukumu na uendeshaji wa baraza la vijana la taifa."

Kwa maana hii, vijana Hawana Haki yoyote na Wala hakuna fursa Zozote ndani ya rasimu ya Chenge. Rasimu hii haisemi vijana watadai Haki na fursa husika kwa Mujibu wa Sheria Zipi. Rasimu Inasema bunge Ndio litakuja kutunga Sheria husika. Na Kama tunavyojua, bunge la CCM limeshajipanga kuja kuwapa vilio vya mwaka vijana pale muswada wa baraza la vijana la taifa utakapowasilishwa bungeni. Iwapo kina Chenge wangekuwa na nia ya Dhati
Juu ya Hili, wangeainisha ndani ya rasimu Yao Sheria ambazo zitakuja kulinda vijana, sio kusubiri kuja Waliza vijana baada ya kuwatumia kupitisha rasimu hii haramu.

Kwa majirani zetu Kenya kwa mfano, katiba Yao haina blah blah Kama katiba ya Chenge inayouzwa na kina mwanadiwani na wenzao. Katiba ya Kenya Inasema wazi Kabisa idadi ya wabunge vijana watakaoteuliwa - senate and National Assembly, lakini muhimu zaidi, katiba ya Kenya inatamka kwa Uwazi Kabisa kisheria jinsi gani vijana watadai Haki zao iwapo hazitatekelezwa.

Vijana wana kila Haki ya kuikataa rasimu hii kwenye kura ya maoni. Ni wajibu wetu kuwafungua macho sasa.


Cc MwanaDiwani, chama, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, Pasco, EMT, JokaKuu, Jasusi, Mtanganyika, Dingswayo, Mag3, Ritz, ZeMarcopolo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom