Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

Nguruvi nadhani unakosea sana unaposema mimi ni sehemu ya Katiba ya Chenge, kusema kweli mimi si sehemu ya katiba ya Warioba wala Chenge. Nimeipinga katiba ya Warioba sababu ilijaa ego na makorokoro ambayo wengi mlikuwa mnafumbia macho sababu tuu ilikuwa na serikali tatu, mambo kama haki za vijana, mambo kama ukomo wa ubunge (ubaguzi wa hali ya juu), sijui watu kufanya referendum kama hawamtaki kiongozi, matokeo ya ile katiba hata na hiyo serikali tatu ingeleta political gridlock.

Tofauti yangu mimi na wewe kama nilivyosema mwanzo nawake maono yangu bayana, nilishasema tangu awali kwamba kama mnataka muungano wa serikali zaidi ya moja( mimi ni mmoja ya wanaosema serikali moja au VUNJA muungano/gawa mbao) basi hakuna budi kuwabeba Zanzibar, sababu hawana uwezo wa kifedha, hawako katika jeografia nzuri na mengine. Nyinyi mpo nyuma ya pazia, hamuutaki muungano lakini mnaona fedhea kuja mbele na kusema Muungano na ukome. Mimi huko sipo naaita sinia sinia na sio sahani kubwa.

Hoja ya II

Kuhusu rasimu ya Warioba, wengine tulisema kilichofanyika nikukusanya maoni na kuyaweka katika mpangilio. Bunge la katiba ndilo lilipaswakuchambua kwa lengo la kuboresha.

Mfano, ukomo wa Wabunge ni maoni ya wananchi.Je, walikuwa na mantiki, na kwanini waseme hivyo.
Hilo ndilo lilipaswakujadiliwa.

Rasimu ya Warioba hatujasema ni msahafu au bibilia, tulisema ni mwongozo wa wapi tunakwenda. Hoja namba III (Kuvunja muungano).

Kama unatusoma vema tumesema na ninaendelea kusema, muungano maana yake ni maridhiano yenye kuleta unafuu kwa wananchi.

Muungano si maridhiano ya kibaguzi ya kumbebesha mwingine mzigo.
Kama ni kubebeshana mzigo basi ni afadhali tuvunje jahazi tugawane mbao.Nipo katika rekodi.

Mfano, znz si kuwa inabebwa, ni tatizo kubwa sana la uchumiwa Tanganyika.
Zanzibar peke yake inachukua mapato yanayotoka Tanganyika kulikomapato yanayokwenda katika halmshauri 54 za Tanganyika.

Swali, ni kwanini kuwena ubaguzi huu, tukijua wazi znz haina mchango wowote wa maana katika huumuungano ukilinganisha na wilaya moja kama ya Mpanda.

Kwanini wanakuwa special.Tuna invest ili iwe tupate return gani.

Pamoja na investment hiyo znz inakuwani tatizo la malalamiko.
Katika hali hiyo kuna nini cha kufanya Zaidi yakugawana mbao.

Ninaposema tuvunje jahazi, nina maana ‘tumechoka na znz'' nakwamba hatuna sababu za kuwabeba na kisha kuvuna lawama na matusi.

Wewe unashuri tuwavumilie kwasababu ya muungano.
Ni kuulize huo muungano unaomuumiza Mtanganyika una return gani kiasi cha kusema tuwavumilie. Kibaya Zaidi wznz wanapanda mbegu mbaya sana ya ubaguzi. Wana kitu kinaitwa narcissism, wana ego n.k.

Katika mazingira waliyobebwa,hawakupaswa kufungua vinywa. Wewe unashuri tuwavumilie, hebu niambie kwa return gani tunayotegemea kwa uwepo wa znz.

Ninachosema hapa ni kuwa znz, ikiwa sehemu ndogo sana haiwezi kuwa na umuhimu kuzidi sehemu kubwa za taifa hili zenye umuhimu zaidi.

Hatuwezi kuelekeza rasilimali zetu katika eneo tusilotegemea return ya aina yoyote, huoni ujinga. Hivyo znz wanapaswa, kwanza, kuwa na adabu, pili kujitambua wapo mgongoni na tatu kukubalikuwa hata siku moja hawatakuwa kama Tanganyika.

Kama haiwezekani tuvunje jahazi, ni upuuzi kumpa kupe hadhi ya ng'ombe.
Hakuna ushirika wa kupe na ng'ombe. Ni ima kupe atulie mgongoni au adondoke chini, ndio kuvunja
 
Mkuu , umeongea hoja nyingi naomba nizirejee bila mpangilio.
Hoja ya I (Tatizo la Tanzania si katiba)
Kwanza, tatizo la Tanzania ni katiba.

Huwezi kwenda au kutenda jambo ukiwa huna muongozo.
Hiyosocial engineering unayosema lazima ijengwe katika taratibu za nchi,ihakikishwe ipo katika taratibu na sheria na inakidhi haja na matamanio ya ummakutokana na dira yao.

Rushwa, ubadhirifu na mengine ni matokeo ya kuwa na mfumombaya wa utawala na uendeshaji wan chi.
Mfumo hujengwa kwa taratibu na sheria watuwaliojiwekea, ambao ni Katiba ya nchi inayozaa sheria zote zinazotumika nchini

Tazama mataifa kama India, Marekani, Canada, Australia auJapan kwa uchache, utaona miongozo yao inawalinda bila viongozi. Kwa mfano,katika miaka 7 iliyopita Japan imekuwa na mawaziri wakuu Zaidi ya 5.
Nchi ipo imara kwasababu ina mwongozo na si mtu.

India iliwahi kuwepo kwa miezi 3 bila waziri mkuu, haikuyumba kwasaabu ina mwongozo na viongozi.

Sisi tuna viongozi hatuna mwongozo. Ndio maana Rais anawezakuficha madhambi chini ya kapeti, akakumbatia wahalifu na sasa ndio wanamfanyiakazi ya kuandika mwongozo na maadili ya taifa.

Hivi kweli mhalifu anaweza kuandika sharia itakyomzuia yeye kufanya uhalifu?

Hoja ya pili....

Jee tatizo ni muongozo au tatizo ni wanao ongoza? Katiba ina weka misingi ya juu kabisa, ila sheria ambazo hutungwa na bunge zinakuwa ni focal point ya kuongoza. So, tuseme 100% katiba ya Warioba ingepita, jee hilo lingeondoa tatizo? Sidhani, sababu katiba inakupa 360 approach, lakini bunge linatunga sheria za kuongoza. Sasa hawa hawa wezi (politician) ndio tungewategemea watunge sheria za kuisaidia katiba jee unadhani wangetunga sheria hizo? Umegusia kwamba raisi ana uwezo wa kukumbatia waharifu, lakini ata utunge katiba ya aina gani waarifu bado watakuwa wanabanwa na sheria ambazo bunge itatunga, na kama hao hao waarifu ndio wanatunga sheria jee unadhani watajifunga?

Ndio maana nasema kwamba hiii JF ni chemchem na chimbuko la maono na fikra pevu, kwenye hili la katiba nadhani tumetanguliza kamba kwenye kisima bila Kata, hatuwezi chota maji. Tatizo is more complex and more complicated, lazima approach iwe beyond katiba. Ndio maana nimekuwa nikiuliza hili swali "Jee Tanzania inaitaji katiba sasa ivi"?

Umezungumzia nchi kama Marekani, jee ni katiba peke yake ambayo inasababisha Marekani kuwa hapa ilipo katika uongozi bora? au ni pamoja na maono na fikra pevu za viongozi wao? Sikatai katiba inatoa muongozo wa juu (guideline) lakini katiba peke yake sio chimbuko la maendeleo, kwani wamarekani wengi hawajui hata nini kipo ndani ya katiba yao, sema mfumo wa sheria za nchi yao na maisha ndani ya kuheshimu utawala wa sheria ndio yamewafikisha hapo walipo.

Kenya wameiga katiba ya USA, wametanguliza kamba bila kata, lakini mpaka sasa kichwa kinawauma, hakuna linalofanyika katika bunge lao sababu ya political gridlock. Ninacholia mimi ni kwamba tatizo sio wao, bali tatizo ni sisi wote.
 
Mkuu mtanganyika , katiba ni mwongozo na kama ulivyosema ni focal pointya sharia zingine. In other words sharia nyingine zitatengenezwa kwa reflectionya katiba. Kwa mfano, katiba ya 1977 ina maungufu makubwa ya maadili ya viongozi.

Ndio maana wamekaa wakaunda tume ya maadili na kujiwekea utaratibu wa kutaja mali wakiingia wakitoka haiwahusu. Sheria mama haiwabani, waogope nini?

Ukisoma Rasimu ya Warioba, mambo mengi sana yaliwekwa katika mizani ya watu kutochezea nchi. Kulikuwa na checks and balance hasa katika madaraka ya viongozi wakubwa.

Utaona Rais alikuwa anawajibishwa, tofauti na sasa ambapo Rais anaweza kugeuka kituko na akaitwa Rais.

Ni kweli Wamarekani wanaweza kutojua nini kipo katika katiba yao, lakini wanajua wakitaka kukipata kipo wapi.
Sisi hata ukitaka hakipo.Huoni tofauti hiyo mkuu

Kuhusu nchi zilizoendelea, nimekupa mifano tu ya kukuonyeshakuwa Japan inabadili mawaziri wakuu kama nguo na bado inabaki kuwa 3 economy ya dunia.

India imewahi kuishimiezi 3 bila kiongozi lakini mwongozo uliwaongoza.
Uingereza imekaa wiki 3 wala watu hawakujua kuwa kuna tatizo la uchaguzi kwasasa taratibu zao walizojiwekea zinawaongoza.

Marekani, Rais Clinton allikutwa ofisini akijinafasi na Monie. Almanusura kibarua kiote majani. Tanzania Rais anakabidhiwa nyaraka ya serikali na wahalifu wa Interpol, hakuna tatizo.

Yeah, hakuna tatizo kwasabau muongozo wetu haumlazimishi au kumwajibisha rais. Yeye ni kamfalme kasiko nakofia tu ya kifalme. Kuna uhusiano mkubwa sana wa stability and development na katiba.
 
Hoja ya II

Kuhusu rasimu ya Warioba, wengine tulisema kilichofanyika nikukusanya maoni na kuyaweka katika mpangilio.
.Bunge la katiba ndilo lilipaswakuchambua kwa lengo la kuboresha.

Mfano, ukomo wa Wabunge ni maoni ya wananchi.Je, walikuwa na mantiki, na kwanini waseme hivyo.
Hilo ndilo lilipaswakujadiliwa.

Rasimu ya Warioba hatujasema ni msahafu au bibilia, tulisema ni mwongozo wa wapi tunakwenda.

Hoja namba III (Kuvunja muungano).

Kama unatusoma vema tumesema na ninaendelea kusema, muungano maana yake ni maridhiano yenye kuleta unafuu kwa wananchi.

Muungano si maridhiano ya kibaguzi ya kumbebesha mwingine mzigo.
Kama ni kubebeshana mzigo basi ni afadhali tuvunje jahazi tugawane mbao.Nipo katika rekodi.

Mfano, znz si kuwa inabebwa, ni tatizo kubwa sana la uchumiwa Tanganyika.
Zanzibar peke yake inachukua mapato yanayotoka Tanganyika kulikomapato yanayokwenda katika halmshauri 54 za Tanganyika.

Swali, ni kwanini kuwena ubaguzi huu, tukijua wazi znz haina mchango wowote wa maana katika huumuungano ukilinganisha na wilaya moja kama ya Mpanda.

Kwanini wanakuwa special.Tuna invest ili iwe tupate return gani.

Pamoja na investment hiyo znz inakuwani tatizo la malalamiko.
Katika hali hiyo kuna nini cha kufanya Zaidi yakugawana mbao.

Ninaposema tuvunje jahazi, nina maana ‘tumechoka na znz'' nakwamba hatuna sababu za kuwabeba na kisha kuvuna lawama na matusi.

Wewe unashuri tuwavumilie kwasababu ya muungano.
Ni kuulize huo muungano unaomuumiza Mtanganyika una return gani kiasi cha kusema tuwavumilie.

Kibaya Zaidi wznz wanapanda mbegu mbaya sana ya ubaguzi.
Wana kitu kinaitwa narcissism, wana ego n.k.

Katika mazingira waliyobebwa,hawakupaswa kufungua vinywa.
Wewe unashuri tuwavumilie, hebu niambie kwa return gani tunayotegemea kwa uwepo wa znz.

Ninachosema hapa ni kuwa znz, ikiwa sehemu ndogo sana haiwezi kuwa na umuhimu kuzidi sehemu kubwa za taifa hili zenye umuhimu zaidi.

Hatuwezi kuelekeza rasilimali zetu katika eneo tusilotegemea return ya aina yoyote, huoni ujinga.

Hivyo znz wanapaswa, kwanza, kuwa na adabu, pili kujitambua wapo mgongoni na tatu kukubalikuwa hata siku moja hawatakuwa kama Tanganyika.

Kama haiwezekani tuvunje jahazi, ni upuuzi kumpa
kupe hadhi ya ng'ombe.
Hakuna ushirika wa kupe na ng'ombe. Ni ima kupe atulie mgongoni au adondoke chini, ndio kuvunja
jahazi

Kama nguvu ya Bunge la Katiba ni pamoja na Kuboresha kama ulivyo sema hapo awali, basi kubadili serikali tatu kwenda mbili ni kuboresha pia. Au unaposema kazi yake ilikuwa kuboresha unamaanisha kuna sehemu wao walipewa ruhusa kuboresha na kunasehemu wao waliambia usiguse, " No room for improvement" kwenye section hii? Kama unakubaliana na kwamba rasimu ya Warioba sio kamusi wala bibilia, basi unafungua mjadala kwamba kuboreshwa ni pamoja na maono mbadala ya wabunge wa bunge la katiba.

Kuhusu swala la muungano, mimi nimekuwa shabiki namba moja wa muungano ambao ni "cost effective" na moja na namba mia moja. Ukiangalia maandiko yangu ya miaka ya nyuma nimekuwa shabiki wa kuomba referendum vote kwa pande zote kuuliza jee tunataka muungano au hatutaki muungano. Na nimelia kwamba kabla hata hatujawaza herufi K katika neno Katiba basi tuitishe kura ya kuwauliza wananchi kama wanataka muungano au lahasha. Sababu kwa miaka mingi sana nimekuwa nikisikia neno Kero za Muungano. Tumeona UK wamekuwa wakiwakimbia Scotland for years kuwapa nafasi ya kujitoa katika muungano, mpaka juzi wananchi walipoulizwa wakasema wao wanautaka muungano. Kwa nini na sisi tusiwaulize wananchi?

Sasa basi, nafahamu uhalisia uliopo ni pamoja na pressure kutoka kwa donor countries kama USA na UK kwamba Zanzibar ni potential threat wa insecurity katika zone kama itaachwa yenyewe. Na ni hawa mabwana ambao wanasababisha hata wazo la kura ya maoni isiwepo. Sasa kujibu swali lako moja kwa moja ni kwamba neither serikali mbili no tatu itapunguza gharama za kuendesha serikali ya Muungano katika that level. Na hili tulilijadili kwa kutumia budget forecast na other metrics.

Jee tunaweza kufanya maridhiano tukawa na something in between kuridhisha mnaotaka serikali tatu, na wale wanao taka mbili na sisi tunaotaka Moja?. Yes, lakini tumekuwa busy kusaka nani atashinda wao, ama sisi, mwisho wa siku hakuna linalofanikiwa zaidi ya kutengeneza msiba mwingine.

Ukweli ni kwamba kama tangu mwanzo tungekubali kwamba tofauti ni kubwa baina ya makundi haya, basi tunatafuta maridhiano ambayo yatawapa kidogo kidogo makundi yote bila kuondoa misingi. Hiyo ndio approach ambayo kama Jaji warioba na Jakaya wangekuwa viongozi bora wangetupatia, lakini walicholeta ni kuigawa nchi kwenye makundi. Mwisho wa siku katiba imegawa nchi zaidi ya kuunga nchi jambo ambalo katiba yoyote inatakiwa kufanya kuunganisha na sio kugawa.
 
Mkuu

Mtanganyika ,labda ungeniambia kuna tatizo la wasomi wa jamii yetu ningeweza kufikiriakukuelewa. Kwa mfano, unapotuambia January Makamba ana model nzuri nashangaa.Unless upo pembeni na ngoma au debe.

Huyu J, alikuwa na JK kama myeka 24hr. Ndiye alikuwaanamwandikia hotuba ambazo leo tunajua zilikuwa za kuficha uhalifu tu. Ni huyuJM ambaye ni naibu waziri ameshindwa kutatua katatizo kadogo tu ka kodi za simuwizarani kwake. Huyu JM hana rekodi yotote unayoweza kutuonyesha.

Leo unatuonyesha model yake. Haya si ndiyo yale ya nichagueniniwaletee maendeleo' kana kwamba maendeleo ni tenga la ubuyu kutoka Comoro.

In other words, huyu yupo kwenye system na hana track recordyoyote ile, leo anawezaje kutuwekea model tuone anafaa.
 
Mkuu @Mtanganyika ,labda ungeniambia kuna tatizo la wasomi wa jamii yetu ningeweza kufikiriakukuelewa. Kwa mfano, unapotuambia January Makamba ana model nzuri nashangaa.Unless upo pembeni na ngoma au debe.
Huyu J, alikuwa na JK kama myeka 24hr. Ndiye alikuwaanamwandikia hotuba ambazo leo tunajua zilikuwa za kuficha uhalifu tu. Ni huyuJM ambaye ni naibu waziri ameshindwa kutatua katatizo kadogo tu ka kodi za simuwizarani kwake.
Huyu JM hana rekodi yotote unayoweza kutuonyesha.
Leo unatuonyesha model yake. Haya si ndiyo yale ya ‘nichagueniniwaletee maendeleo' kana kwamba maendeleo ni tenga la ubuyu kutoka Comoro.
In other words, huyu yupo kwenye system na hana track recordyoyote ile, leo anawezaje kutuwekea model tuone anafaa.
Nguruvi nadhani umechukua neno January out of content, nilichosema mimi ni kwamba at least amekuwa akisema kwamba tatizo sio uongozi bora peke yake but culture (utamaduni) mzima wa wananchi. Hii alone nakubaliana nae asilimia 100. Now is he a good leader or does his leadership style is what needed? nadhani that can be debatable muda mwingine.

The notion that sababu natofautiana vision na someone basi all his ideas are bogus nadhani haipo balance. Mfano: Mimi na udogo wangu natofautiana na maono mengi sana ya mwalimu Nyerere, lakini I still believe kwamba kuna maeneo mengine mengi amekuwa na idea zenye mashiko.
 
Mtanganyika , ndio maana tunasema umejificha lakini wewe nichange taratibu true color zinajitokeza. Kuna construction na renovation. Hivi ni vitu viwili tofautikabisa.

Kuboresha ni improvement lakini haina maana ya kubadili msingi wa hoja.Unapofanya renovation unakuwa katika framework ya asili. Unapokuwa naconstruction unafanya kitu tofauti. Nikupe mfano wa mtaani.
Unapofanya maboresho ya degree yamedicine unaweza kuongeza somo la sociology, forensic, criminal n.k. ikabaki kuwa MD

Huwezi kufanya maboresho ya degree ya medicine kwa kuondoa anatomy,Physiology na Biochem ambayo ndiyo moyo wa course uka replace na sociology na hortculure .

Hiyo si medicine tena, ni kitu kinachofanana na medicine kwa jina lingine, na hapo hujafanya maboresho umefanya tengenezo la degree nyingine inayofanana medicine kwa baadhi ya mambo megine Moyo wa Rasimu nzima ya Warioba umenyongwa ndio maana CCMhawakujadili muundo.
Wamekwepa kwasababu wangejadili muundo na kuweka serikali2, wangekuwa wamefanya kitu kingine. Na kwasaabu wameua moyo wa rasimu ndio maana wamefumua vifungu vyote.

Hapowamefanya construction na si renovation waliyoambiwa. Hii ya Kwenu na Chengeni kitu kipya, ya Warioba ipo kaburini siku nyingi. Ndio maana nasisitiza kuwa wasomi wetu ni tatizo sana.Tatizo si wananchi, ni wasomi na hasa nakataa wazo la social engineering.

Kinachotakiwa ni program ya kuwafanya wasomi wajitambue
 
@Mtanganyika , ndio maana tunasema umejificha lakini wewe nichange taratibu true color zinajitokeza.
Kuna construction na renovation. Hivi ni vitu viwili tofautikabisa.

Kuboresha ni improvement lakini haina maana ya kubadili msingi wa hoja.Unapofanya renovation unakuwa katika framework ya asili. Unapokuwa naconstruction unafanya kitu tofauti.

Nikupe mfano wa mtaani.
Unapofanya maboresho ya degree yamedicine unaweza kuongeza somo la sociology, forensic, criminal n.k. ikabaki kuwa MD

Huwezi kufanya maboresho ya degree ya medicine kwa kuondoa anatomy,Physiology na Biochem ambayo ndiyo moyo wa course uka replace na sociology na hortculure .

Hiyo si medicine tena, ni kitu kinachofanana na medicine kwa jina lingine, na hapo hujafanya maboresho umefanya tengenezo la degree nyingine inayofanana
medicine kwa baadhi ya mambo megine

Moyo wa Rasimu nzima ya Warioba umenyongwa ndio maana CCMhawakujadili muundo.
Wamekwepa kwasababu wangejadili muundo na kuweka serikali2, wangekuwa wamefanya kitu kingine.

Na kwasaabu wameua moyo wa rasimu ndio maana wamefumua vifungu vyote.
Hapowamefanya construction na si renovation waliyoambiwa.

Hii ya Kwenu na Chengeni kitu kipya, ya Warioba ipo kaburini siku nyingi.

Ndio maana nasisitiza kuwa wasomi wetu ni tatizo sana.Tatizo si wananchi, ni wasomi na hasa nakataa wazo la social engineering.

Kinachotakiwa ni program ya kuwafanya wasomi wajitambue

Kwa hiyo ukiini wa Rasimu ya Warioba ni serikali tatu? Awali umesema kuna nafasi ya kuboresha niliposema katiba ya Warioba ilikuwa ina vimelea vingi kama Wabunge wawe na ukomo, sijui nafasi za upendeleo kwa vijana, sijui watu kama hawakutaki wanaweza kukufuza ubunge all this "sintofahamu" zina ruhusa ya kuboreshwa ambapo ni pamoja na kuzi futilia mbali, lakini swala la serikali tatu acha kama lilivyo.

Nadhani mfano wa medicine hauko sawa, unless useme katiba ilikuwa inajengwa katika misingi ya muungano wa serikali tatu kwanza na mengine yote badae. Lakini kama tulikuwa tunataka katiba ya haki sawa kwa wote, miiko ya uongozi na n.k basi tusinge ibebesha jina la kipengele na kufanya either ni serikali tatu au hakuna katiba sidhani kama hapo tupo kwenye fairness.

Kufanya the whole argument iwe iko base on number of serikali sidhani kama ni valid argument sababu to my opinion kuna almost same au zaidi ya watu wanapinga serikali tatu idea.
 
Mtanganyika,

Kuhusu suala la social engineering, naungana na Nguruvi3 Kwamba sio sahihi hata Kidogo kulaumu wananchi, wa kulaumiwa ni wasomi wanaogeuza siasa kuwa miradi Yao to manipulate wananchi. Katika jamii yoyote, kiongozi huwa ni mfano wa kuigwa.

Kama mtu anapata uongozi kwa njia za ulaghai au uhuni, Kama viongozi hawatimizi wajibu wao, njia pekee ya wananchi kurekebisha haya ni kupitia Nguvu ya umma kwa Amani - kupitia Sheria mama ya nchi, katiba itokanayo na wao wenyewe, au Nguvu ya umma kwa shari. Au Mnataka Waende kwenye Shari?

Wananchi wametoa maoni Yao juu ya ukomo wa ubunge, jinsi ya kumfanya mbunge awajibike zaidi, juu ya umuhimu wa kurudisha maadili ya uongozi, lakini hao role models wako wanashirikiana na CCM kufuta maoni ya wananchi, yet mnasimama na kujenga hoja za social engineering, huo ni upuuzi. Ni bora umeomba Kwamba hiyo debate tuiache. Ni vizuri usiilete tena.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Jamii yoyote duniani ni taswira ya viongozi. Huwezi kusema kuna disconnection kati ya nasaba za viongozi na wanaongozwa. It is impossible. Unapong'ania kwamba wasomi tuu ndio wakuchukua lawama na si wananchi nadhani haupo sahihi.

Kama kila mwanchi ni mla rushwa kwa nini viongozi wasiwe walarushwa? Kama wanchi wengi ni wabinafsi wasio jali utaifa kwa vipi viongozi wao watakuwa tofauti.

Hii idea Kwamba viongozi ni monsters kutoka Kwenye sayari ya Pluto sio kweli. Ni kutoka baina yetu. Kutibu Juu ni sawa kabisa lakini kukomesha ni kutibu chimbuko na hapa ndio social reengineer inakubalika. Mwalim alifanya Jambo hilo
 
Wananchi ni wala rushwa kwasababu wamechoka kuwa waaminifu na watiifu. Huwezi kuwa na kundi la watu wachache likichota mabilioni bila hatua halafu ukamlaumu hakimu wa mahakama ya mwanzo kuchukua vijisenti.

Lazima uelewe tofauti ya corruption na bribery. Hizi tunazoona mitaani si rushwa ni njaa tu. Hata hivyo zinakuzwa kwasababu ya rushwa ya viongozi. Kwa mfano, mzee aliyekabidhi rasimu inasemekana ana vijisenti ulaya ambavyo ni sawa na bajeti ya wizara. Hivi huyu unamweka katika mizani na trafiki anayechukua sh 5,000 kwamba wote ni wala rushwa?

Taid lolote lililofanikiwa kupiga vita rushwa, linaanza kuwa na viongozi safi.
Huwezi kuzuia rushwa kama hujipigi vita rushwa kwa kuonekana.

Hapa kwetu kuna 10% nyingi za kashfa mbali mbali, utashangaa viongozi wamekalia mafaili wakilindana.
Leo unataka trafiki awajabishwe, kwa lipi hasa. Huyu trafiki anaweza kudhibitiwa na sheria za kazini kwake tu, I mean IGP anaweza kabisa kukomesha hali hiyo.

Kwasasa haiwezekani, ukimkamata trafiki tutakuuliza vipi kuhusu bilioni 200 za Escrow na makando kando mengine? Kama huna jibu basi huna nguvu za kukemea rushwa.

Rasimu ya Warioba iliziba mianya hiyo, wale inayowagusa akina Chenge wakaamua kuondoa kwasababu tu ya klinda masilahi yao. Halafu unawalaumu wananchi!

Pengine tungewalaumu wananchi kwa kukubali watu kama Chenge kuingia katika bunge achilia mbali kuandika katiba kutoka mifukoni na mafichoni mwao.
 
Nguruvi, notion kwamba wananchi ni Watawa na viongozi ndio watenda dhambi sio kweli hata kidogo. Ni nani anae chagua hawa viongozi? Si sisi wananchi? Chenge amechaguliwa na nani? Juzi juzi Ridhiwani kashinda kwa asilimia zaidi ya 80 jee ni nani aliyemchagua? You can't justify kwamba ni okay wachini kutofuata sheria na viongozi ndio wanatakiwa wafuate sababu 10% yao ni kubwa kuliko 10,000/= anayotaka daktari ili amtibu mgonjwa muhimbili ambae hana matokeo yake anafariki dunia. Hakuna dhambi ndogo, haipo.

Rasimu ya Warioba haikuziba mwanya, sababu tatizo sio sheria tatizo ni mfumo. Huwezi weka sheria kwenye mfumo ambao umekiuka sheria, lazima ubadili kwanza mfumo.

Kama kweli jamii yetu ni hiyo ambayo mnajaribu kuinasabisha nayo, basi wapinge katiba ya Sitta. Wasimame na kusema hapana. Tuone kama hilo litatokea.
 
Nilifahamu utasema hayo na hivyo nina majibu. Hakuna justifications za kuvunja sheria kama zipo iwe kwa mkubwa au mdogo. Hilo lipo wazi.

Ninachokisema hapa ni kuwa viongozi hawawezi kusimamia sheria hizo kwasbabu wao ndio sehemu ya uozo tunaouona?
Mfano, kama kiongozi kaingia madarakani kwa njia za rushwa, uwezo wa kuwashughulikia wala rushwa ataupata wapi?

Nikutolee mfano, nchi ina vyombo vyote vya dola, hivi kwanini Scotland yard au interpol watoe majibu tofauti na serikali. Kwanini tutegemee interpol na si Polisi wetu. Kwanini kuna kesi za grand corruption hazina majibu hadi leo.
Jibu ni kuwa rushwa ipo miongoni mwa hao viongozi na hawawezi kuihughulikia kwasbabu wao ni sehemu ya rushwa.

Kwavile wamefungwa mikono tayari na kamba za rushwa, vivyo hivyo hawezi kushughulikia rushwa za chini au ndogo.
Nimetoa maelezo ya bribery na corruption. Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa. Usilinganishe. Hapa tunaongelea corruption kwanza ambalo ni tatizo kubwa kuliko bribery.

Bribery ya karani haina madhara mazito kwa taifa kama 10% ya mradi wa IPTL. Leo tunalipa umeme wa juu kufidia corruption ya viongozi. Hiyo haina maana kuruhusu uvunjaji wa sheria, ninachosema hapa ni kuwa kama huwezi kudhibiti corruption ni tatizo kubwa kwasababu linagusa mfumo zaidi ya individual. Narudia hakuna dhambi ndogo, chanzo cha bribery ni kutokana na kuenea kwa corruption ambayo ipo miongoni mwa wananchi.

Umezungumzia wananchi kuwachagua akina Chenge. Well, hivi hutambui kuwa corruption ndiyo inawapa pesa akina Chenge kununua wananchi! Katika nchi masikini unategemea nini tofauti kutoka kwa wananchi?
 
Wanaduru nafatilia duru kwa ukaribu sana. Katika suala la muungano nimependa na swali alilouliza Nguruvi3 kwamba muungano unahusu nchi zipi? swali hili sina hakika kama kuna mwanasiasa mtetezi wa muungano aliyewahi kulitolea ufafanuzi.

Wananchi hawana elimu ya kutosha kuhusu wapi wametoka na wapi wanaenda, nguvu ya propaganda inayofanywa na watetezi wa katiba ya 6 kupitia media inapoteza umakini wa watu kuona ukweli ulivyo.
Nini sababu ya kuifanya znz ing'ang'aniwe na tanganyka, tena kwa gharama kubwa?
 
Last edited by a moderator:
Leo nilikuwa nimejipa kazi ndogo ya kupita maeneo mbalimbali ya jiji la dsm na pia vijijini vya karibu karibu, kujaribu kuelewa ni kitu gani ambacho kinawapa wananchi (hasa wanachama na mashabiki wa chama cha mapinduzi) misimamo juu muundo wa muungano.

Nilichojifunza ni Kwamba wananchi walio wengi wanasikiliza kwanza viongozi wao wanasema nini Kabla ya kufanya maamuzi, hasa kiongozi wao wa kitaifa. Hilo ni suala la utiifu na uaminifu kwa CCM. Wananchi wengi niliokutana nao wanasema Kwamba uongozi wa nchi Ukisema sasa serikali Mbili muda wake umekwisha, sasa ni muda wa serikali Tatu, wananchi hao watakuwa tayari kuunga Mkono serikali Tatu bila hata ya Maelezo ya kina juu ya kwanini serikali Tatu, na bila ya kujalisha mwalimu nyerere alipendelea Mfumo gani kwani mwalimu alikuwa ni mtu wa kubadilika na Wakati. Huu sio utafiti scientific, na Sijafanyia uchambuzi mrejesho huu lakini naamini Kwamba tunapata picha japo kwa Mbali juu ya nini kinaendelea ndani ya jamii.

Pengine wataalam wa social engineering, akina Mtanganyika ambao wana amini Kwamba tatizo la Tanzania ni wananchi na sio viongozi, watakuja kutupatia elimu zaidi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Leo nilikuwa nimejipa kazi ndogo ya kupita maeneo mbalimbali ya jiji la dsm na pia vijijini vya karibu karibu, kujaribu kuelewa ni kitu gani ambacho kinawapa wananchi (hasa wanachama na mashabiki wa chama cha mapinduzi) misimamo juu muundo wa muungano. Nilichojifunza ni Kwamba wananchi walio wengi wanasikiliza kwanza viongozi wao wanasema nini Kabla ya kufanya maamuzi, hasa kiongozi wao wa kitaifa. Hilo ni suala la utiifu na uaminifu kwa CCM. Wananchi wengi niliokutana nao wanasema Kwamba uongozi wa nchi Ukisema sasa serikali Mbili muda wake umekwisha, sasa ni muda wa serikali Tatu, wananchi hao watakuwa tayari kuunga Mkono serikali Tatu bila hata ya Maelezo ya kina juu ya kwanini serikali Tatu, na bila ya kujalisha mwalimu nyerere alipendelea Mfumo gani kwani mwalimu alikuwa ni mtu wa kubadilika na Wakati. Huu sio utafiti scientific, na Sijafanyia uchambuzi mrejesho huu lakini naamini Kwamba tunapata picha japo kwa Mbali juu ya nini kinaendelea ndani ya jamii.

Pengine wataalam wa social engineering, akina Mtanganyika ambao wana amini Kwamba tatizo la Tanzania ni wananchi na sio viongozi, watakuja kutupatia elimu zaidi.
Sent from my iPhone using JamiiForums
My two cents...kabla ya yote ninayo maswali kwa Mtanganyika;

  • Je umewahi kujiuliza ni sababu zipi zilisababisha utaratibu katika uzinduzi wa BMLK ubadilishwe ili Raisi aweze kulihutubia bunge hilo baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Warioba kuwasilisha rasimu?
  • Je umewahi kujiuliza hali ingekuwaje iwapo utaratibu wa kawaida wa uzinduzi ungefuatwa! Je Raisi angeyasema aliyoyasema kuhusu rasimu?
  • Je unadhani, kwa mfano, kama Raisi angekubaliana na muundo wa Muungano kama ulivyopendekezwa kwenye rasimu, angeweza kutokea mwana CCM kupinga msimamo wake huo?
  • Je kwa nini jitihada kubwa zinafanyika kuwa demonize wote wasiokubaliana na msimamo wa CCM kuhusu muundo wa Muungano kama wahuni na watu wanaotaka kuleta vurugu nchini?
  • Je unadhani kampeni kabla ya kura ya maoni zitaendeshwa kwa haki na uhuru kwa kuwapa fursa sawa watetezi wa muundo wa serikali tatu waweze kuwafikia wananchi?
  • Je unaamini vyombo vya dola havitatumika kuminya uhuru wa kujieleza kwa wananchi ambao wataoonesha kutoikubali Katiba kama ilivyopitishwa na wajumbe wa BMLK.
Mwisho Mtanganyika, unaweza ukawalaumu wananchi lakini kuna misimamo inayohitaji ujasiri na ni kwa bahati mbaya wengi wanakosa uthubutu wa kufanya hivyo, tumefanikiwa sana katika kujenga taifa la wanafiki. Ninavyojua kwa mwana CCM, neno ama maoni ya Raisi na Mwenyekiti wa Chama, ni amri...leo hii Kikwete akibadilisha msimamo kesho pongezi zitamiminika kutoka kwa wale wale waliokuwa wanaunga mkono msimamo wake wa awali; naam, ndivyo tulivyo...msimamo wa viongozi ndio dira ingawa kwa sasa tupo wachache wetu tunaoanza kupata ujasiri wa kuhoji na pole pole namba inaongezeka kila kukicha.
 
Mchambuzi,asante kwa kipande hicho na kweli kwa viongozi kama wa kwetu waliokubuhu kwaunafiki, usanii na ulaghai hizo tabia ndizo chimbuko la dai la kipuuzi kwambamuundo wa serikali tatu eti ni kumkejeli Mwalimu.
Mwalimu alisomavizuri alama za nyakati na alitabiri yote tunayoyashuhudia hivi leo lakini watukama MwanaDiwanini mifano halisi ya malimbukeni, upepo wa mageuzi ulipoanza kuvuma na jinsi CCMwalivyojipanga kuupiga vita mfumo wa vyama vingi na bila Mwalimu kuingilia katina kuonya, leo hii sijui tungekuwa katika hali gani.
Nakumbuka majina waliyopewa wanamageuzi; hayakuwa tofautisana na majina wanayopewa wanaopinga kuendelea na mfumo wa muundo wa Muunganowa serikali mbili ambao ndio umetufikisha hapa tulipo.

Mwalimu alianza kuhoji mambo mengi tu kuhusu huu Muungano; nakumbukaalivyoifananisha serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Raisi wake SalminAmour na mtoto mdogo aliyepakatwa lakini haachi kulalama hadi anamnyea aliyempakata.Nina hakika Mwalimu angekuwepo hangenyamazia tendo la kihaini la uvujwajiwaziwazi wa Katiba kwa Zanzibar kujitangazia uhuru ndani ya Muungano.

Leo hii mtu aliyepewa jukumu la kuilinda na kuitetea hiyoKatiba eti anadai kumuenzi Baba wa Taifa huku akibariki uhuni kamatulivyoshuhudia ukitendeka ndani ya kilichoitwa Bunge Maalum La Katiba. Mwalimualianza kuwa na mashaka makubwa kwa chama alichokianzisha na kuna wakatialitishia hata kukihama ikibidi baada ya kuona imepoteza muelekeo na kukosa dirakuonesha inakoelekea. Hapana, muundo tofauti haungekuwa kejeli kwaMwalimu...angeukaribisha kama njia mbadala ya kuuokoa Muungano!

Mwalimu alikuwa na mashaka na Kikwete, leo miaka 15 tunaona.
In fact alimkataa akijua mbele ya safari kutatokea wenye uwezo.

Mwalimu aliwahi kusema mkianza kuchezea katiba ya nchi mtavurugana kweli'' Aliyeruhusu katiba ya nchi kuvunjwa na wazanzibar ni Kikwete, akitoa baraka asionekane mtu mbaya.

Ukiisoma katiba ya znz 2010utashangaa Kikwete akisema ana muenzi mwalimu. Ana muenzi vipi kwa kuvunja muungano!

Katiba ya znz 2010 tayari imeshavunja muungano kimantiki,leo Kikwete anatumia jina la Nyerere kwenye muungano alioshuhudia ukivunjwa.Tena bila hata chembe ya aibu Kikwete anasema tungekuwa na S3 tungesema nini siku ya mwalimu'' Kama mwalimu angepewa nafasi ya kuuliza kuhusu muungano kutoka kaburini, majina ya watu angalipenda kuwaliza ni akina Salim Ahmed, Butiku,Warioba n.k.

Hao kwa kutumia maono na busara za old school ya mwalimu wameona hatari, leo Kikwete ambaye mwalimu alimuona tu kwenye maandamano anasifa zipi za kumuenzi mwalimu zaidi ya Butiku Na siku alipopewa katiba ya CCM, nadhani wapo wakiogeuka makaburini kwa hasira.
Mwalimu aliwahikusema Ikulu si pango la wezi.

Leo wezi wa Interpol ndio wanaandika nyaraka ya Ikulu tena wakiambiwa wana muenzi mwalimu. Jina la mwalimu linatumiwa kuziba ombwe la hoja.

Hakuna utetezi wa hoja za gharama, sasawanamtumia Mwalimu ktisha watu.
 
Wanaduru nafatilia durukwa ukaribu sana. Katika suala la muungano nimependa na swali alilouliza Nguruvi3kwamba muungano unahusu nchi zipi? swali hili sina hakika kama kuna mwanasiasamtetezi wa muungano aliyewahi kulitolea ufafanuzi.

Wananchi hawana elimu ya kutosha kuhusu wapi wametoka nawapi wanaenda, nguvu ya propaganda inayofanywa na watetezi wa katiba ya 6kupitia media inapoteza umakini wa watu kuona ukweli ulivyo.
Nini sababu ya kuifanya znz ing'ang'aniwe na tanganyka, tena kwa gharamakubwa?

Hilo swali la serikali 2. Tunaambiwa muungano ni wa nchi mbilibaasi! Ukiuliza ni zipi hawatoei jibu. Ndio maana bungeni wameacha kujadilimuundo wa muungano. Wangejaribu tu tungepata jibu, na wao hawataki tupatemajibu.

Swali lako kuwa kwanini tunafanya investment kubwa sanaznz na ni kwa return gani, ni swali litakaloulizwa muda si mrefu. Kwavile hakuna majibu, litatafutwa jibu laharaka, hakuna maana vunja. Ndiko Tunakoelekea muda fupi sana ujao.

Propaganda ya akina Sitta imewakumba wasomi pia. Hapa JFkuna watu wanaamini eti kuna nchi ya Tanzania bara iliyoungana na Zanzibar. Niwatu wana elimu na exposure nzuri sana, kwabahati mbaya matumizi ya maarifa nikidogo sana.Cc Bongolander Mkandara Happy Feet Alinda
 
Last edited by a moderator:
My two cents...kabla ya yote ninayo maswali kwa Mtanganyika;

  • Je umewahi kujiuliza ni sababu zipi zilisababisha utaratibu katika uzinduzi wa BMLK ubadilishwe ili Raisi aweze kulihutubia bunge hilo baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Warioba kuwasilisha rasimu?
  • Je umewahi kujiuliza hali ingekuwaje iwapo utaratibu wa kawaida wa uzinduzi ungefuatwa! Je Raisi angeyasema aliyoyasema kuhusu rasimu?
  • Je unadhani, kwa mfano, kama Raisi angekubaliana na muundo wa Muungano kama ulivyopendekezwa kwenye rasimu, angeweza kutokea mwana CCM kupinga msimamo wake huo?
  • Je kwa nini jitihada kubwa zinafanyika kuwa demonize wote wasiokubaliana na msimamo wa CCM kuhusu muundo wa Muungano kama wahuni na watu wanaotaka kuleta vurugu nchini?
  • Je unadhani kampeni kabla ya kura ya maoni zitaendeshwa kwa haki na uhuru kwa kuwapa fursa sawa watetezi wa muundo wa serikali tatu waweze kuwafikia wananchi?
  • Je unaamini vyombo vya dola havitatumika kuminya uhuru wa kujieleza kwa wananchi ambao wataoonesha kutoikubali Katiba kama ilivyopitishwa na wajumbe wa BMLK.
Mwisho Mtanganyika, unaweza ukawalaumu wananchi lakini kuna misimamo inayohitaji ujasiri na ni kwa bahati mbaya wengi wanakosa uthubutu wa kufanya hivyo, tumefanikiwa sana katika kujenga taifa la wanafiki. Ninavyojua kwa mwana CCM, neno ama maoni ya Raisi na Mwenyekiti wa Chama, ni amri...leo hii Kikwete akibadilisha msimamo kesho pongezi zitamiminika kutoka kwa wale wale waliokuwa wanaunga mkono msimamo wake wa awali; naam, ndivyo tulivyo...msimamo wa viongozi ndio dira ingawa kwa sasa tupo wachache wetu tunaoanza kupata ujasiri wa kuhoji na pole pole namba inaongezeka kila kukicha.

Mag3, nitakupa majibu kutokana na maono yangu ambayo kwa kukupa ufafanuzi hayaambatani na CCM wala hayafungamani na chama chochote bali ni maono huru.

1. Nadhani utakubaliana na mimi haingii akilini kwamba Jaji Warioba apewe kiti kuzungumza baada ya Raisi, ukiangalia leadership protocol boss ndio anakuwa mzungumzaji wa mwisho. So, hili likuwa na more logical lakini wana siasa wame spin kuonyesha kwamba intention ilikuwa kuvunjavunja katiba ya jaji warioba.

2. Jakaya kama sehemu ya jamii alikuwa na haki ya kusema yake ya moyoni. Kwani Azimo la Arusha si lilikanwa mwalimu akiwa hai?

3. Tatizo la namba za serikali limeigawa Tanzania katika makundi, nadhani Jaji Warioba na kundi lake walishindwa kutumia utashi kuangalia njia mbadala ya kuridhisha pande zote yaani serikali mbili, tatu na sisi wa serikali moja. Kama warioba angejua hilo leo tusinge kuwa hapa tulipo. Instead wao walichotumia ni kuja na statistics ambazo mungu ndio anajua walipo zitoa na kutaka kusokomeza mzigo wa serikali ambao ungejaa mabwanyenye. Nadhani cha muhimu ingekuwa kutengeneza reconciliation panel ambayo ingefanya maridhiano kati ya wanao taka tatu na wale wa mbili na sisi wa moja. Hii ingepunguza makali, instead wamekwenda kwenye Medieval age playbook na kurudi na yaleyale

4. CCM wanatumia political tactique sababu wao sera yao kichama ni serikali mbili, sasa kama vile Ukawa wavyotumia mchezo wa kwamba serikali tatu ndio suluhu. Tofauti ni kwamba CCM wapo more organized, wanajua nini wanataka na UKAWA ni genge tuu ambalo bado halijajua linataka nini. That is a difference, hawa wako more organized na hawa wengine wapo wapo tuu. Leo wanaitwa TCD wanakwenda behind doors wanakubaliana na mchakato uendelee wakija kwenye majukwaa wanasema tumegomea, wapo kama kuku aliyekatwa kichwa, focus less. So, CCM wanatumia old playbook ambayo ni dirty politics always works.

5. Mkuu kampeni za nini tena? Katiba isambazwe wananchi wasome mwenye kuipenda aseme ndio ambae anaikataa aseme hapana. Unataka tena kampeni za nini?

6. Tatizo kubwa ni moja mkuu walio upande wa pili wa sarafu ambao wana tetea serikali tatu wapo very disorganized, hawafamiki nini wanataka, mara wanagomea mara wanakutana na JK, hawajitambui. Sidhani tatizo lipo kwa vyombo vya usalama.

Mimi nakataa kabisa kusema kwama kunaitajika ujasiri wakati unapiga kura ya siri. Hakuna ujasiri katika kusimama katika yale unayo amini. Mkubwa nadhani katika mikoa ya watu wenye uweleo na utashi Dar es Salaam iko juu sana, jee unaweza kuniambia kwa nini CCM wanashinda Dar es Salaam. Hawa watu wapo more inform labda kushinda mikoa yote ya Tanzania, lakini bado CCM wanaweka magoigoi na wanashinda. Unataka kuniambia kwamba hapa tusiseme kwamba sumu yetu ni sisi wenyewe.

Wachache wenye kuhoji uhalisia walikuwepo tangu wakati wa Mwalimu Nyerere, watu kama Kambona na wengine. Tatizo lilopo ni moja mfumo wa elimu na maisha unajenga wananchi wasio jitambua. Labda tufanye mapinduzi ya kifikra ndio tunaweza kushinda, vinginevyo hizi ni sauti za mwangu hazimtishi mpiga mbiu.
 
Mtanganyika,

Hivi kweli unajua hoja ya serikali Tatu ilizaliwa lini ndani ya muungano wa serikali Mbili? Unapwaya sana na hoja zako Kwamba serikali Tatu ni ubunifu wa jaji warioba, hata watoto wadogo wanaona upotoshaji wako kwani hata maandishi ya kwenye vipande vya magazeti vilivyoviringisha mihogo yao ya kukaanga vinakukana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom