Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #121
Nguruvi nadhani unakosea sana unaposema mimi ni sehemu ya Katiba ya Chenge, kusema kweli mimi si sehemu ya katiba ya Warioba wala Chenge. Nimeipinga katiba ya Warioba sababu ilijaa ego na makorokoro ambayo wengi mlikuwa mnafumbia macho sababu tuu ilikuwa na serikali tatu, mambo kama haki za vijana, mambo kama ukomo wa ubunge (ubaguzi wa hali ya juu), sijui watu kufanya referendum kama hawamtaki kiongozi, matokeo ya ile katiba hata na hiyo serikali tatu ingeleta political gridlock.
Tofauti yangu mimi na wewe kama nilivyosema mwanzo nawake maono yangu bayana, nilishasema tangu awali kwamba kama mnataka muungano wa serikali zaidi ya moja( mimi ni mmoja ya wanaosema serikali moja au VUNJA muungano/gawa mbao) basi hakuna budi kuwabeba Zanzibar, sababu hawana uwezo wa kifedha, hawako katika jeografia nzuri na mengine. Nyinyi mpo nyuma ya pazia, hamuutaki muungano lakini mnaona fedhea kuja mbele na kusema Muungano na ukome. Mimi huko sipo naaita sinia sinia na sio sahani kubwa.
Hoja ya II
Kuhusu rasimu ya Warioba, wengine tulisema kilichofanyika nikukusanya maoni na kuyaweka katika mpangilio. Bunge la katiba ndilo lilipaswakuchambua kwa lengo la kuboresha.
Mfano, ukomo wa Wabunge ni maoni ya wananchi.Je, walikuwa na mantiki, na kwanini waseme hivyo.
Hilo ndilo lilipaswakujadiliwa.
Rasimu ya Warioba hatujasema ni msahafu au bibilia, tulisema ni mwongozo wa wapi tunakwenda. Hoja namba III (Kuvunja muungano).
Kama unatusoma vema tumesema na ninaendelea kusema, muungano maana yake ni maridhiano yenye kuleta unafuu kwa wananchi.
Muungano si maridhiano ya kibaguzi ya kumbebesha mwingine mzigo.
Kama ni kubebeshana mzigo basi ni afadhali tuvunje jahazi tugawane mbao.Nipo katika rekodi.
Mfano, znz si kuwa inabebwa, ni tatizo kubwa sana la uchumiwa Tanganyika.
Zanzibar peke yake inachukua mapato yanayotoka Tanganyika kulikomapato yanayokwenda katika halmshauri 54 za Tanganyika.
Swali, ni kwanini kuwena ubaguzi huu, tukijua wazi znz haina mchango wowote wa maana katika huumuungano ukilinganisha na wilaya moja kama ya Mpanda.
Kwanini wanakuwa special.Tuna invest ili iwe tupate return gani.
Pamoja na investment hiyo znz inakuwani tatizo la malalamiko.
Katika hali hiyo kuna nini cha kufanya Zaidi yakugawana mbao.
Ninaposema tuvunje jahazi, nina maana ‘tumechoka na znz'' nakwamba hatuna sababu za kuwabeba na kisha kuvuna lawama na matusi.
Wewe unashuri tuwavumilie kwasababu ya muungano.
Ni kuulize huo muungano unaomuumiza Mtanganyika una return gani kiasi cha kusema tuwavumilie. Kibaya Zaidi wznz wanapanda mbegu mbaya sana ya ubaguzi. Wana kitu kinaitwa narcissism, wana ego n.k.
Katika mazingira waliyobebwa,hawakupaswa kufungua vinywa. Wewe unashuri tuwavumilie, hebu niambie kwa return gani tunayotegemea kwa uwepo wa znz.
Ninachosema hapa ni kuwa znz, ikiwa sehemu ndogo sana haiwezi kuwa na umuhimu kuzidi sehemu kubwa za taifa hili zenye umuhimu zaidi.
Hatuwezi kuelekeza rasilimali zetu katika eneo tusilotegemea return ya aina yoyote, huoni ujinga. Hivyo znz wanapaswa, kwanza, kuwa na adabu, pili kujitambua wapo mgongoni na tatu kukubalikuwa hata siku moja hawatakuwa kama Tanganyika.
Kama haiwezekani tuvunje jahazi, ni upuuzi kumpa kupe hadhi ya ng'ombe.
Hakuna ushirika wa kupe na ng'ombe. Ni ima kupe atulie mgongoni au adondoke chini, ndio kuvunja